Hotuba za viongozi

Mchaga

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,378
204
Hivi ni sahihi kusema marehemu mwalimu nyerere au hayati mwalimu nyerere.

Katika hotuba yake ya mbio za mwenge mwanza leo, dr shein anamtaja baba wa taifa kama marehemu mwalimu nyerere, mimi nadhani ni sahihi angemtambulisha kwa utangulizi wa hayati.

Ni vyema waandishi wa hotuba za viongozi wakawa makini katika kuandika hizi hotuba.

Baba wa taifa na mwasisi wa mbio za mwenge hawezi kutajwa kama marehemu hili ni kosa kubwa sana, hata kama ni marehemu lazima apewe heshima yake ya pekee na atajwe kama hayati baba wa tiafa...:(

au ndio zile dalili za kumchoka na kuchoka mambo aliyoyaasisi.
 
Hotuba haina jipya ndefu mambo mengi na mengi ya kisiasa kwa sasa anazungumzia mauji ya albino...
 
Tuwalinde na kuwaenzi ndugu zetu maalbino...anaendelea, serikali imechukuwa hatua mbalimbali kama vile kukusanya sensa ya maalbino kwa kulinganisha na idadi ya vifo
 
Back
Top Bottom