Hotuba ya Zitto Kabwe Bungeni Juni 15, 2011 - Bajeti Mbadala

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA FEDHA MHE.KABWE ZUBERI ZITTO (MB) KUHUSU MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya njema na kuweza kusimama hapa mbele ya Bunge hili, kuwasilisha Maoni na Mapendekezo ya Kambi ya Upinzani kuhusu hali ya uchumi ya nchi yetu na bajeti kwa mwaka 2011/2012 kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kanuni ya 96(6).

Mheshimiwa Spika, Naomba kwa niaba ya waheshimwa wabunge wote wa Kambi ya Upinzani ambao hawakupata nafasi ya kushiriki au kutoa rambirambi zao kwako kwa msiba mkubwa uliokupata wa kuondokewa na Mama yako mpenzi, nifanye hivyo kwa niaba yao.

Mheshimiwa Spika, Kabla ya kuanza kutoa mtazamo wetu naomba nikishukuru chama changu cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, viongozi wangu wakuu wote, kwa juhudi kubwa tunazozifanya ili kuhakikisha Watanzania wanaelewa maana halisi ya “wananchi kuwa na mamlaka kwa Serikali waliyoiweka madarakani kwa njia ya kura”. Vile vile na kwa umuhimu wa kipekee namshukuru Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Aikael Mbowe (Mb) kwa kuniteua kuwa Waziri Kivuli wa Wizara hii nyeti katika uchumi na maendeleo ya nchi. Kama ilivyo ada yangu, nitaifanya kazi hii kwa uaminifu, uadilifu na umakini mkubwa sana.

Endelea kusoma katika attachment hii chini
 
Tupe dondoo za maeneo muhimu alizosema.

UDHAIFU KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA.
Ripoti ta CAG katika Mwaka wa Fedha 2009/10
Mheshimiwa Spika,
Matumizi mabaya ya fedha za umma yameendelea kuwa kikwazo
kikubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.
Uchambuzi wetu juu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2009/2010 pekee, umebaini
takribani jumla ya Tsh trilioni 2.4 za fedha za umma zilitumika vibaya,
ambazo ni sawa na asilimia 25% ya bajeti yote ya mwaka huo
ambayo ilikuwa na jumla ya Sh 9.5 trilioni. Hii inaonyesha kuwa
katika kila Shilingi 100 tunayopitisha hapa Bungeni katika Bajeti
Shilingi 25 zinaingia kwenye mifuko ya wezi na wabadhirifu wa fedha
za Umma. Hali hii lazima ikomeshwe mara moja.
Mheshimiwa Spika,
Mifano ya fedha zilizopotea au kutumiwa vibaya katika mwaka wa
fedha wa 2009/10 ni manunuzi yaliyofanywa nje ya mpango wa
mwaka ya jumla ya Tsh bilioni 50.6, malipo yenye shaka ya jumla ya
14
Tsh bilioni 15.5, upotevu wa fedha na mali za serikali wa jumla ya Tsh
bilioni 11.1 na malipo ya mishahara kwa watumishi waliostaafu,
waliokufa na watoro kazini ya jumla ya Tsh bilioni 1.8.
Aidha, Mkaguzi hakukabidhiwa nyaraka na orodha ya walionufaika
na kiasi cha jumla ya Sh. bilioni 48 (Stimulus package) kilichotolewa
kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi toka Benki Kuu ya Tanzania
katika juhudi za kukabiliana na msukosuko wa uchumi ulioikumba
dunia.
Katika mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi nilimwuliza Mheshimiwa
Waziri Mkuu kuhusu suala la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali kunyimwa nyaraka ili kukagua jumla ya Tshs 48 bilioni
zilizotajwa hapo juu. Natumai sasa Serikali itakuwa na majibu juu ya
suala hili. Kambi inaendelea kusisitiza ombi lililotolewa na aliyekuwa
Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Hamad Rashid
Mohammed kwamba Fedha zote zilizotolewa kwa ajili ya Stimulus
Package zikaguliwe na CAG na kuwasilisha Taarifa hiyo maalumu
Bungeni. Serikali ilikubaliana na ombi hili hivyo tunaomba taarifa hiyo
mara moja.
Mheshimiwa Spika,
Tunalisema hili la Stimulus Package kwa kuwa kuna ushahidi wa
barua kutoka kwa Katibu Mkuu Hazina akiwaandikia Mameneja wa
vyama vya ushirika vya mikoa ya Kilimanjaro na Kagera akiwaeleza
kuwa Serikali pamoja na kuidhinisha kulipwa kwa vyama hivyo, kwa
sasa hakuna fedha kwa ajili ya kufanya malipo hayo.
Barua iliyoandikwa kwa Meneja Kagera Cooperative Union (1990)
ltd ya tarehe 16 Septemba 2010 yenye kumb. Na TYC/B/40/143
ilikuwa ikimweleza Meneja kuhusiana na serikali kulipa kiasi cha
shilingi 734,369,379.49 . Ila ilipofika tarehe 27 Aprili 2011 Katibu Mkuu
wa Hazina aliandika barua nyingine kwa Meneja husika yenye
kumb.Na.TYC/B/40/143/45 kwa ajili ya kusitisha Malipo ya fidia
15
kutokana na mdororo wa uchumi kwa kuwa Serikali haina fedha na
pia muda wa kulipa fidia hizo ulikwisha tangu mwaka 2010.
Kuhusiana na chama cha ushirika cha Mkoa wa Kilimanjaro
(Kilimanjaro Native Cooperation Union (1984), Katibu Mkuu Hazina,
Ndugu Ramadhan Kijjah mnamo tarehe 16 Septemba aliandika
barua yenye kumb.Na TYC/B/40/143 iliyowajulisha kuwa Serikali
imeridhika kuwa wanastahili kupewa fidia ya shilingi 255,107,570.17
waliyopata kutokana na mdororo wa uchumi duniani. Ila ilipofika
tarehe 27 Aprili 2011 Katibu Mkuu huyo huyo aliandika barua
nyingine yenye kumb.Na.TYC/B/40/143/43 akiwajulisha kuwa Serikali
haina fedha kwa ajili ya kulipa fidia hiyo na kuwa muda wa kulipa
fidia ulikuwa umekwisha tangu mwaka 2010.
Mheshimiwa Spika,
Kupatikana kwa barua hizi ni uthibitisho wa wazi kuwa kuna tatizo
kubwa kuhusiana na fedha zilizotolewa na Serikali kwani wakati
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Omar Yusuph Mzee akiwa anajibu swali
la msingi la Mhe. Mhonga Saidi Ruhanywa wakati wa Bunge la Bajeti
la mwaka 2010/11 alisema kuwa mpango ulikuwa unaenda vizuri.
Pia wakati Waziri wa Fedha Mhe. Mkullo akiwa anahitimisha hotuba
ya bajeti ya mwaka 2010/11 alilieleza bunge hili kuwa mpango
ulikuwa unaenda vizuri.
 
Kwa kweli ni nzuri na rahisi sana kutekelezeka na imejali maslahi ya kila mtu kuanzia wale wa chini mpaka juu.

Suala linabaki pale pale kwa waTanzania je mtaweza kuisimamia na kuitekeleza kwa 100% au ndio inabaki kwenye makaratasi tu.

Hongera sana Zitto
 
Nimesoma ila naona itabidi nirudie tena, hivyo vyanzo mbadala vya mapato naona kama havijaainishwa zaidi, yaani kuweka specifics.
 
Mheshimiwa Spika​
, Asilimia 33.4 ya Watanzania wanaishi chini yamstari wa umasikini na kwa waishio vijijini ni asilimia 37.4 wakatiasilimia 16.2 tu ya Watanzania waishio Dar es Salaam wanaishi chiniya mstari wa Umasikini. Wakati tofauti ya kipato kwa Watanzania niasilimia 35, matajiri wa juu asilimia 20 wanamiliki asilimia 42 ya Patola Taifa (consumption expenditure) na masikini wa chini kabisa
asilimia 20 wanamiliki asilimi 7 tu ya Pato la Taifa.
 
Mheshimiwa Spika,​
taarifa ya Hali ya uchumi inaonyesha kuwapamoja na sekta kadhaa kukua lakini bado hazijaongeza mchangowake katika ukuaji wa pato la taifa ukilinganisha na ukuaji wa sektahusika. Kwa mfano, sekta ya mawasiliano imekuwa kwa asilimia 22.1ila mchango wake katika pato la Taifa ni asilimia 2.1 tu, shughulindogo za hoteli na migahawa ukuaji wake ulikuwa 6.1 lakinimchango wake katika ukuaji wa pato la taifa ni 2.3% tu. Hii inamaana kuwa sekta hizi hazina uhusiano wa moja kwa moja (stronglinkages) katika ukuaji wa uchumi na katika kukuza pato la taifa na
hivyo kushindwa kupunguza hali ngumu ya maisha kwa wananchi
 
Kambi ya Upinzani​
inaunga mkono ushauriuliotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Ummakwamba sasa Benki Kuu ya Tanzania ianze kutunza sehemu yaHifadhi ya nchi katika Dhahabu. Benki Kuu inunue dhahabu kutokakwa wachimbaji wadogo na pia tuangalie uwezekano wa kutozasehemu ya mrahaba katika madini kama ‘dhahabu safi' (‘pure
gold').
 
UDHAIFU KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA.
Ripoti ta CAG katika Mwaka wa Fedha 2009/10
Mheshimiwa Spika,
Matumizi mabaya ya fedha za umma yameendelea kuwa kikwazo
kikubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.
Uchambuzi wetu juu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2009/2010 pekee, umebaini
takribani jumla ya Tsh trilioni 2.4 za fedha za umma zilitumika vibaya,
ambazo ni sawa na asilimia 25% ya bajeti yote ya mwaka huo
ambayo ilikuwa na jumla ya Sh 9.5 trilioni. Hii inaonyesha kuwa
katika kila Shilingi 100 tunayopitisha hapa Bungeni katika Bajeti
Shilingi 25 zinaingia kwenye mifuko ya wezi na wabadhirifu wa fedha
za Umma. Hali hii lazima ikomeshwe mara moja.
Mheshimiwa Spika,
Mifano ya fedha zilizopotea au kutumiwa vibaya katika mwaka wa
fedha wa 2009/10 ni manunuzi yaliyofanywa nje ya mpango wa
mwaka ya jumla ya Tsh bilioni 50.6, malipo yenye shaka ya jumla ya
14
Tsh bilioni 15.5, upotevu wa fedha na mali za serikali wa jumla ya Tsh
bilioni 11.1 na malipo ya mishahara kwa watumishi waliostaafu,
waliokufa na watoro kazini ya jumla ya Tsh bilioni 1.8.
Aidha, Mkaguzi hakukabidhiwa nyaraka na orodha ya walionufaika
na kiasi cha jumla ya Sh. bilioni 48 (Stimulus package) kilichotolewa
kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi toka Benki Kuu ya Tanzania
katika juhudi za kukabiliana na msukosuko wa uchumi ulioikumba
dunia.
Katika mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi nilimwuliza Mheshimiwa
Waziri Mkuu kuhusu suala la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali kunyimwa nyaraka ili kukagua jumla ya Tshs 48 bilioni
zilizotajwa hapo juu. Natumai sasa Serikali itakuwa na majibu juu ya
suala hili. Kambi inaendelea kusisitiza ombi lililotolewa na aliyekuwa
Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Hamad Rashid
Mohammed kwamba Fedha zote zilizotolewa kwa ajili ya Stimulus
Package zikaguliwe na CAG na kuwasilisha Taarifa hiyo maalumu
Bungeni. Serikali ilikubaliana na ombi hili hivyo tunaomba taarifa hiyo
mara moja.
Mheshimiwa Spika,
Tunalisema hili la Stimulus Package kwa kuwa kuna ushahidi wa
barua kutoka kwa Katibu Mkuu Hazina akiwaandikia Mameneja wa
vyama vya ushirika vya mikoa ya Kilimanjaro na Kagera akiwaeleza
kuwa Serikali pamoja na kuidhinisha kulipwa kwa vyama hivyo, kwa
sasa hakuna fedha kwa ajili ya kufanya malipo hayo.
Barua iliyoandikwa kwa Meneja Kagera Cooperative Union (1990)
ltd ya tarehe 16 Septemba 2010 yenye kumb. Na TYC/B/40/143
ilikuwa ikimweleza Meneja kuhusiana na serikali kulipa kiasi cha
shilingi 734,369,379.49 . Ila ilipofika tarehe 27 Aprili 2011 Katibu Mkuu
wa Hazina aliandika barua nyingine kwa Meneja husika yenye
kumb.Na.TYC/B/40/143/45 kwa ajili ya kusitisha Malipo ya fidia
15
kutokana na mdororo wa uchumi kwa kuwa Serikali haina fedha na
pia muda wa kulipa fidia hizo ulikwisha tangu mwaka 2010.
Kuhusiana na chama cha ushirika cha Mkoa wa Kilimanjaro
(Kilimanjaro Native Cooperation Union (1984), Katibu Mkuu Hazina,
Ndugu Ramadhan Kijjah mnamo tarehe 16 Septemba aliandika
barua yenye kumb.Na TYC/B/40/143 iliyowajulisha kuwa Serikali
imeridhika kuwa wanastahili kupewa fidia ya shilingi 255,107,570.17
waliyopata kutokana na mdororo wa uchumi duniani. Ila ilipofika
tarehe 27 Aprili 2011 Katibu Mkuu huyo huyo aliandika barua
nyingine yenye kumb.Na.TYC/B/40/143/43 akiwajulisha kuwa Serikali
haina fedha kwa ajili ya kulipa fidia hiyo na kuwa muda wa kulipa
fidia ulikuwa umekwisha tangu mwaka 2010.
Mheshimiwa Spika,
Kupatikana kwa barua hizi ni uthibitisho wa wazi kuwa kuna tatizo
kubwa kuhusiana na fedha zilizotolewa na Serikali kwani wakati
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Omar Yusuph Mzee akiwa anajibu swali
la msingi la Mhe. Mhonga Saidi Ruhanywa wakati wa Bunge la Bajeti
la mwaka 2010/11 alisema kuwa mpango ulikuwa unaenda vizuri.
Pia wakati Waziri wa Fedha Mhe. Mkullo akiwa anahitimisha hotuba
ya bajeti ya mwaka 2010/11 alilieleza bunge hili kuwa mpango
ulikuwa unaenda vizuri.

aiseee hii ishu ya stimulus package lazima tuzae nao hawa.. watueleze kinagaubaga hizi fedha zimekwenda wapi na zimefanya nini kumsaidia mtanzania wa kawaida
 
stimulus package nadhani itakuwa inatumika ktk mambo tofauti na ilivyokusudia,na hakutakuwa na majibu sahihi juu ya hilo,unaweza kuta ndio inayotumika kujinunulia ktk kusomesha watoto wa vigogo hapa tz
 
Back
Top Bottom