1. Tangu lini Anno Domini imekuwa KABLA ya kuzaliwa Kristu?
2. Hauwezi ukazungumzia historia ya Zanziba bila kuzungumzia utumwa. Hao mnaosema kuwa wenyeji walishiriki watuambie ni kabila gani walikuwa na soko la watumwa ambako binadamu walikuwa wakipigwa mnada kama mbuzi? Watuambie ni kabila gani lilikuwa likiwahasi wale waliowateka vitani? Watuambie ni kabila gani ambalo lili m-dehumanise binadamu mwenzao kama walivyofanya hawa waarabu na wazungu? Msitake kuandika historia upya kwa kutaka kujikomba kwa hao mnaoona wamewazidi. Angalau wazungu wameosha utu wa kujutia biashara hii haramu na dhalimu. Kwa mtu anayejiita mmoja wa viongozi wakuu wa kisiasa Zanziba kuinyamazia ni incomprehensible.
Amandla.........
huna la kusema Amandla katafute gazeti la UHURU usome huelimishiki na hutoelimishika.Nimeitoa hapa;http://en.wikipedia.org/wiki/Street_light
kutoka hapa:http://genealogytrails.com/ill/adams/history/aqesl.htm
Kutoka hapa:http://www.zanzibar-holiday.com/brief_history.html
Hizo taa za stimu anazozingumzia Maalim ziliwekwa lini? Kama ni baada ya 1883, New York tayari walikuwa nazo tangu 1880.
Wawindaji wakubwa wa nyangumi kihistoria walikuwa watu wa Norway, Iceland n.k. Wamerekani wawaache wote hao waje kununua mafuta ya nyangumi Zanziba kuwashia taa za mitaani kwao? Zanziba ambao hawakuwa na historia ya kuwinda nyangumi!
Nchi gani hizo ambazo Zanziba ilikuwa ikizidai na ni kiasi gani ilikuwa ikidai? Zanziba ingedaiwaje wakati uwezo wa kukopa kama nchi kutoka nchi nyingine hakikuwa nao? Kwani leo wanadaiwa kiasi gani na NCHI ipi ya kigeni?
Amandla........
Hizo takwimu nilizoquote kwa rangi nyekundu ndio vichekesho japo hazina nambari lakini zinabaki kuwa ni takwimu kwa vile umetumia neno wengi(majority). hivi nikuulize ni nchi gani ambayo kunatokea mauwaji watu wasikimbilie nchi jirani? hii ni sheria ya kimaumbile na huwezi kuchukulia hiki kama ni kigezo cha ukarimu wa wabara kwa wazanzibari.(Mungu awalinde)lakini hata nyinyi mkianza kuuwana basi mtakimbilia zanzibar na kenya hivyo hii haiwezi kuwa ni hoja.
Chukua mfano huu hapa unaweza kufanana na hoja yako hii.Ireland walitawaliwa,kuonewa na kukandamizwa sana na waingereza lakini raia wa kawaida walikimbilia kwa hao hao madhalimu wao wa kiingereza kutafuta usalama wao na huku wakijua kwamba muingereza ndio adui yao.Hivyo wazanzibari kukimbilia bara kwenye matatizo haiondoi uhalisi wa kwamba bara hawezi kuwa adui yetu.
Hoja ya wahindi: hapa naona unajichanganya tena,kwenye mabandiko yako mengine,wahindi na waarabu unawatoa kwenye uzanzibari lakini hapa unawatamka kama wazanzibari kwakuwa tu wamekimbilia bara,tukamate lipi?
Kuhusu kesi ya Okello, ndugu ifatilie tena kesi ya okello kukimbizwa na nyerere usiuzuge umati wa JF. Soma tena mapinduzi ya Zanzibar.
Nakubaliana na wewe kwamba Karume aliungana na bara kwa kupata ulinzi, lakini baada ya kifo chake nini kiliendelea?
Kama Nyerere hakuupenda muungano je kulikuwa na haja gani ya kuunganisha vyama? Au utatwambia kwamba na vyama alitaka jumbe viunganishwe? acheni siasa za shule ,tuongeleeni uhalisi wa mambo jamani!
huna la kusema Amandla katafute gazeti la UHURU usome huelimishiki na hutoelimishika.
si mlimpa cheo kisicho rasmi cha ubaba wa taifa au? labda nikuulize alikuja kufanya nini kwenye kamati ya dharura ya pale kiswandui kabla kutangazwa matokeo ya urais?,mkitaka msitake mguu wa tanganyika unaiathiri sana zanzibar!
Mbona unaongelea matatizo ya umeme zanj. kama vile bara umeme upo? aagh! bara wameshindwa kuleta umeme vijijini na mjini wanaweza kuwasaidia wazenj acheni unafiki hapaNyerere hakuwa na jeshi wala polisi. Alikuja kama raia. Jeshi na polisi wote walikuwa chini ya Mzanzibari mwenzenu. Sasa kama hao wazanzibari waliokuwa kwenye hicho kikao hawakuafikiana nae walishindwa nini basi kukataa mchango wake?
Nimewauliza, bara wanawazuia nini kuendeleza bandari zenu na viwanja vyenu vya ndege? Bara inawazuia nini kuendeleza zao lenu la karafuu? Mlilia bandari mmeachiwa na hadi sasa hamja fanya kitu. Mlianzisha benki yenu imewashinda. Wote mkawa mnafungua akaunti kwenye benki za bara. Mnadhani benki yenu ingeendelea vipi bila nyinyi wenyewe kuweka hela zenu mle? Mkaanzisha viwanda vya soda n.k. vimewashinda! Mnakosa umeme si kwa sababu bara hawaletei umeme bali kwa sababu mmeshindwa kuwekeza kwenye distribution network yenu! Lakini bado hamuoni kuwa nyinyi ndiyo wenye matatizo mnabaki kuilamu bara. Huo mguu wa bara uko wapi? Mbona Hong Kong walitawaliwa na uingereza lakini walipata maendeleo. Nyie mnadhani siasa ndiyo zitawakomboa badala ya kubadilika tabia na kuweka juhudi katika maendeleo yenu! Matumaini ya wengine wenu ni kuwa mkijitoa kwenye Muungano basi ma-ankal kutoka Oman watawamwagia mapesa! Acheni kulalama. Ukombozi wenu uko mikononi mwenu na hakuna anayewazuia isipokuwa nyinyi wenyewe!
Amandla.....
Wengi haina maana ya kuwa majority. Ningesema wengi "wa" hapo ungeweza kusema ninazungumzia majority. Wengi ni "many" na sio "most". Kuna wahindi (katika hawa nawajumuisha wale tunaowaita magoa) ambao walikimbia kuepuka mabinti zao kuolewa. Kuna wengine walikimbia kwa sababu nyingine.
Wapi nilipowatoa wahindi na wengine katika uzanzibari? Ninapozungumzia uarabu, ushihiri, uhindi, ungazija hizi ni identities ambazo zinatumika na zimekuwa zikitumika Zanzibar. Kwa watu wa nje, watu wote waliokuwa wakiishi Zanzibar walionekana kama wazanzibari. Lakini miongoni mwenu hadi leo mnajuana nani ni mngazija na nani ni muarabu. Hivi karibuni tumeona juhudi zikifanywa kuwanyang'anya haki wangazija za kuwa wazanzibari. Sio mimi, bali ni nyinyi ambao mnakataana.
Unazungumzia Ireland bila kuelewa historia yake. Waliokuwa wakigandamizwa ni wakatoliki na wengi walikimbilia Marekani, Canada, Australia n.k. hasa baada ya Great famine (an Gorta Mór) ya 1845-1852. Usisahau vilevile kuwa waingereza wahamiaji walikuwepo kibao Ireland na hasa Ireland Magharibi wao walikuwa ndiyo majority. Wengine wao baada ya njaa kali bila shaka walirudi kwao. Hivi karibuni wa-irish wamekuwa wakihamia uingereza kuganga njaa. Wa-Irish waliohamia uingereza hata hivyo waliendelea kubaguliwa. Hii ni tofauti na wazanzibari waliohamia bara wakati wa utawala wa Karume I. Hawa hawakubaguliwa bara bali walikubaliwa kama watanzania wengine. Ingawa wengine walihamia bara kuganga njaa bado wapo wengi waliokimbia utawala wa kidhalimu wa mzanzibari mwenzao tofauti na wa-Irish waliokimbia utawala dhalimu wa wageni. Labda utuambie kuwa hao ndugu zako walikimbilia bara kukimbia utawala dhalimu wa watu wa bara! Utufahamishe vile vile ni lini watu wa bara wametawala Unguja!
Mimi nimesoma historia ya Zanzibar (pamoja na mchango wa Okello) na nimeweka tafsiri yangu. Wewe kama unaelewa tofauti basi weka tafsiri yako badala ya kutoa maagizo ya kipuuzi ya ati niisome upya. Unashindwa nini kuiweka hapa unavyoielewa?
Nani amesema Nyerere hakupenda Muungano? Nyerere alikuwa na ndoto ya kuunganisha Afrika nzima acha hako ka-Zanzibar. Nyerere ali-ofa kusogeza mbele uhuru wa Tanganyika ili tuweze kuungana na Kenya na Uganda. Nyerere aliupenda sana Muungano kinadharia lakini hakuuhitaji kama alivyouhitaji Karume. Baada ya kuungana na kuona mambo yaliyokuwa yakiendelea Zanzibar ndiyo akapendekeza vyama viungane.Waulize waliokuwa Zanzibar wakati wa utawala wa Karume I watakueleza hali ilivyokuwa. Haikuwa tu televisheni ya rangi (na viwanja vya michezo) alivyozungumzia Maalim.
Unataka kujua nini kiliendelea baada ya kifo cha Karume I? Waulizie wakina Ussi, Hanga na wengine! Hawa nao walinyongwa na Nyerere?
Amandla.......
Nyerere hakuwa na jeshi wala polisi. Alikuja kama raia. Jeshi na polisi wote walikuwa chini ya Mzanzibari mwenzenu. Sasa kama hao wazanzibari waliokuwa kwenye hicho kikao hawakuafikiana nae walishindwa nini basi kukataa mchango wake?
Nimewauliza, bara wanawazuia nini kuendeleza bandari zenu na viwanja vyenu vya ndege? Bara inawazuia nini kuendeleza zao lenu la karafuu? Mlilia bandari mmeachiwa na hadi sasa hamja fanya kitu. Mlianzisha benki yenu imewashinda. Wote mkawa mnafungua akaunti kwenye benki za bara. Mnadhani benki yenu ingeendelea vipi bila nyinyi wenyewe kuweka hela zenu mle? Mkaanzisha viwanda vya soda n.k. vimewashinda! Mnakosa umeme si kwa sababu bara hawaletei umeme bali kwa sababu mmeshindwa kuwekeza kwenye distribution network yenu! Lakini bado hamuoni kuwa nyinyi ndiyo wenye matatizo mnabaki kuilamu bara. Huo mguu wa bara uko wapi? Mbona Hong Kong walitawaliwa na uingereza lakini walipata maendeleo. Nyie mnadhani siasa ndiyo zitawakomboa badala ya kubadilika tabia na kuweka juhudi katika maendeleo yenu! Matumaini ya wengine wenu ni kuwa mkijitoa kwenye Muungano basi ma-ankal kutoka Oman watawamwagia mapesa! Acheni kulalama. Ukombozi wenu uko mikononi mwenu na hakuna anayewazuia isipokuwa nyinyi wenyewe!
Amandla.....
Mutake musitake, haiwezekani kwenye dunia ya leo ati ukapindue jeshi kwa upanga kama alivyo fanya Okello.
Huyo Okello na watanganyika wenzake walikuwa ni watu wa Nyerere walikwenda Zanzibar kupindua.Hii ndio theory ambayo inaingia akilini mwangu, lakini najua itapingwa sana, na badala yake itakuwa Okello na gurupu la watanganyika wenzake wote walikuwa ni wazanzibari walipinduana.
Hizi theory za kuwa ati Nyerere hakutaka kabisa Zanzibar, alikuwa anatamani aisogeze huko mbali ndani ya visiwa vya Hindi...hizi theory ni bora mukaendelea kudanganyana huko huko Mbagala.
Huku kwetu haziingii akilini, na mtu yoyote mwenye akili timamu hawezi kubali ati nchi yenye jeshi na silaha ilipinduliwa kwa upanga wa Okello!...Hata huyo Rambo pia hupewa angalau bastola ndio akashinda!!
Sasa vyovyote iwanvyo, Tanganyika iko bizzi sana na Zanzibar.Kila uchaguzi ni lazima jeshi sijuwi kama si nusu hupelekwa visiwani.Mara ya mwisho nafikiria 2005 Unguja yote ilibidi itekwe....au pia Mkapa ni mzanzibari kama alivyokuwa Mwinyi?
Na huyo Mkapa ajitahidi sana asije akafa kabla Zanzibar haijapata kiongozi mwenye uchungu...lakini akiwacha mwanya basi ajue ana kesi The Hague ya kuuwa wazanzibari huko Pemba.
for the sake of argument acha nikubaliane na wewe yote hayo uliosema. naomba nikuulize masuali madogo sana ambayo hayahitaji uchambuzi.
1)kabla ya muungano na baada ya muungano ni wapi zanzibar ilikuwa na nguvu za kiuchumi na wapi ilikufa kiuchumi?
2)naomba unijibu yes or no, je nyerere hakuwa na athari yoyote katika uendeshaji wa nchi baada ya kung'atuka kwake?
3)nini kinachowapelekea watanganyika kuung'ang'ania muungano wakati zanzibar ni mzigo kwao?
4)ccm kiswandui wanapompendekeza dr.bilal kuwa rais wa zanzibar na ccm dodoma wanapompitisha amani karume.Je hapa huoni kama wazanzibari tumetawaliwa? au hili unalichukuliaje?
yapo masuali mengi yanayonitatiza lakini tuanze na hayo.Guu la tanganyika lipo zanzibar,huu ndio ukweli wenyewe.
Sasa unataka nikupeleke shule? Sasa kama haya ni maswali madogo unaniulizia nini? Majibu si unayo tayari? Hata hivyo:
1.Kabla ya Muungano uchumi wa Zanzibar ulitegemea sana karafuu na kabla ya hapo utumwa. Baada ya Muungano, wenye mashamba ya karafuu wengi walikimbia nchi. Waliorithi hawakuwa na uwezo wa kuyaendeleza. Vile vile kazi ya uvunaji na utunzaji wa mashamba hayo ni ngumu na awali ilikuwa ikifanywa na watumwa na watu kutoka bara waliokuwa wako tayari kuifanya kwa ujira mdogo. Kama vile ilivyokuwa kwa zao la katani, baada ya uhuru watu waliokuwa tayari kufanya kazi hiyo walipungua sana. Ubora wa zao uliathirika na kule kwenye soko kubwa (Indonesia n.k.) nao wakaanza kulima karafuu na badala ya kuwa wanunuzi wakawa washindani. Baada ya Muungano, vile vile badala ya kuwekeza kwenye vitega uchumi, SMZ ikawekeza kwenye maeneo yasiyo na tija kama televisheni ya rangi n.k. Uzembe huu unaendelea hadi leo.
2. Hatuko mahakamani kuniambia nikujibu yes or no. Hata hivyo sioni athari yeyote ambayo Nyerere angeweza kuileta baada ya kung'atuka kwake.
3. Watanganyika hawang'ang'anii Zanzibar. Usichanganye viongozi wachache na watanganyika kama jamii. Wanaotaka Muungano uendelee wengi wanafanya hivyo kutokana na sentimental reasons kutotaka kuwaangusha waliouanzisha hata kama hawapo. Kama vile ilivyo na kuhamia Dodoma.
4. Hayo ya kisiwandui ni ya CCM. Hata kama palikuwa pendekezo kutoka upande mmoj, walipokutana Dodoma ni lazima masuala ya CCM kitaifa yaliangaliwa na ndio yaliopelekea uamuzi wa kuona Karume anafaa kuliko Bilal. Ukweli unabaki kuwa Zanzibar ni sehemu ya Muungano na uamuzi wowote ni lazima uangalie hatma ya Muungano kabla ya yote. CCM sera yao ni Muungano kwa hiyo wasingeweza kuweka mtu ambae wanaona angeweza kuhatarisha sera yao. Ubaya ingekuwa kama wangewawekea mtu kutoka bara. Hawakufanya hivyo. Ule ulikuwa uamuzi wa CCM. Wazanzibari wasingeafikiana nao basi wasingempigia kura waliyebambikiwa. Au huyo aliyeona amedhulumiwa angesema wazi. Hawakufanya hivyo. Kosa lao.Ndiyo demokrasi.
Bahati mbaya siko hapa kutoa shule kwa hiyo sitaweza kujibu maswali yako mengine. Nakushauri tumia mtandao na waulize waliokutangulia, watakufahamisha.
Amandla.......
unaonekana sana ulivyo mgeni na masuali ya zanzibar na hata mimi sikukusudia kukuuliza zaidi kwani haya niliyokuuliza na ulivyoyajibu tayari yananionesha kwamba tuna uelewa tafauti wa mambo!
Mtu mwenye upeo wa mambo hata siku moja huwezi ukasema eti watanganyika hawautaki muungano lakini wachache wa serikali ndio wanautaka!
au ukasema nyerere hakuwa na athari katika serikali baada ya kung'atuka kwake na ukazungumzia kuporomoka soko la karafuu bila kuhusisha uchumi mbadala wa utalii zanzibar n.k hapa nadoubt u great thinker wako!
tuvumilianeni mpaka pale mtakapoamua kuutuwa huu mzigo wa zanzibar!
elewa tu kwamba nje ya muungano zanzibar itakuwa na:
sarafu yake
benki kuu yake
balozi kuu za nchi za nje
uhuru wa kujiunga na jumuia za kimataifa
itapokea misaada 100% na itapokea direct.
na kadhalika na kadhalika!
mimi nafikia hapa kwa leo.kila la heri ndugu
elewa tu kwamba nje ya muungano zanzibar itakuwa na:
sarafu yake
benki kuu yake
balozi kuu za nchi za nje
uhuru wa kujiunga na jumuia za kimataifa
itapokea misaada 100% na itapokea direct.
na kadhalika na kadhalika!
mimi nafikia hapa kwa leo.kila la heri ndugu.
Sasa hapa unajizonga zonga, u dont care less but you dont wanna let it go.Kumbe Zenji tamu, kila mtanganyika hataki kuvunja muungano kwa alivyokolea marashi ya karafuuNa unajua lakini hatma ya serikali tatu? Ulikuwa ndiyo mwanzo wa kuuvunja Muungano
Sasa ndugu under age ukiwa na vitu ulivyovitaja ndio maendeleo au ni kitu gani maana umevitaja tu hukuvitolea melezo. Ninavyojua mimi unaweza kuwa na vitu vyoote hivyo na bado ndio matatizo yanazidi zaidi ya wakati ulipokuwa hunavyo.
Shida hapa ni kwamba kwanini wanaanzisha mambo haya this late?
Kwa miaka yote walikuwa wapi?..matokeo yake inaleta hisia kwamba kuna uroho wa madaraka unataka kujiinua, ambapo hawa jamaa wanataka kutumia mgongo wa vitu kama serikali ya mseto, ili kuendelea kutawala.
Kimsingi wazo ulilosema la serikali ya mseto ni la msingi sana, na ni wakati muafaka lije, Lakini Karume a'step aside, amwachie mwingine asongeshe jambo hilo, maana si la kufanya overnight!
Thats my take!