HOTUBA ya Seif Sharrif na Majibu yake kuhusu Maridhiano Zanzibar!

Well nilikuwa sijamaliza bado, kuna suala jengine ambalo watanganyika wengi wamekuwa wakijiuliza ni kwanini mzanzibari hapendelei kupoteza utaifa wake na kujivunia utanzania.

Nafikiria Maalim Seif amejaribu sana kujibu suala hili, kwa kuonesha records muhimu ambazo Zanzibar iliweza kuziweka katika dunia kiasi ambacho unaweza kumwambia mtu mimi ni mzanzibari na akafahamu kama unatoka kwenye nchi iliyopata ustaarabu kwa miaka mingi sana.

Tanzania ambayo ni 90% Tanganyika, haina record yoyote ambayo mimi kama mzanzibari naweza kukaa mbele ya dunia na kujivunia.Labda ufisadi na umasikini au ufukara!Ni vipi nitaweza kujivunia utaifa huu, wakati taifa langu la Zanzibar lina pretty good records za kuheshimika kabisa.

Shukurani za dhati kwa Maalim Seif kwa kuweka mbele records hizo za Zanzibar, ambazo tunatarajia zitaweza kurudishwa.

Natanguliza samahani kwa wale nitakao rusha sparks humo :D

Ni kweli kuwa Zanzibar ina historia lakini si kweli kwamba Tanganyika haina historia. Huwezi kuwa na cradle of mankind halafu ukawa huna historia. Wakina Zinjatrophous wana historia kweli kweli. Unajua historia ya Tanganyika toka enzi za ugunduzi wa chuma? Ngoja waje hapa wanahistoria wanaozijua dola za kale watakuhadithia

serayamajimbo
 
Endeleni kubweka na matazidi kubweka Damu nzito kuliko maji ,Zanzibar wamesha libaini udugu wenu Tanganyika ni wakitu na sio utu na ndio leo hii Tanganyika limegeuzwa shamba la bibi huku mnapiga mayowe . (Zanzibar walikupeni shubiri mkachukuwa pima )
 
Tumain, you have talked. We can't be slave of our own minds. in today's world we make history....
 
2. Hauwezi ukazungumzia historia ya Zanziba bila kuzungumzia utumwa.

Amandla.........
Ni kweli uwezi kuzungumzia Zanzibar bila utumwa, kwa hili Maalimu atakuwa amechemka. Hata hivyo bado ana nafasi nzuri ya kurekebisha historia yake. Ikumbukwe kuwa zaidi ya watumwa milioni 1 walifika pwani na Zanzibar kipindi hicho cha utumwa.
 
Mie Wazenji nawashangaa sana.

Hamfahamu nini wamekubaliana na nyie mnakurupuka kusema "tuwaachie mambo yao wenyewe". Hapa napata wasiwasi kuwa au ni kambi ya Karume au ya Maalim na wanafanya hivi kwa mipango ya siri ambayo wao wamekubaliana.

Kama kweli mna akili na mmesoma na kuelimika, kwa nini bado mnataka kununua paka akiwa kwenye gunia? Si huwa mnalalamika kuwa Nyerere aliwaingiza Mkenge kwa kukubalkiana na Karume (sr) na mambo yao kuyaficha? Tena sintashangaa kusikia baba/babu zenu hadi walishangilia Muungano wa Tanzania.

Mie umuhimu wa Zanzibar wala siuoni. Kama tumeishi bila mafuta miaka yote hiyo, kwani yakipatikana ndiyo kutakuwa nini? Kama kuna kitu ninaombea kila siku ya Mungu ni Afya, amani na kiongozi IMARA wa Tanzania/Tanganyika ambaye atabadili hadi akili za Watu na ikibidi atumie mbinde ni sawa tu. Watu wakibadilika akili, ni sawa na kupata sijui malita mangapi ya mafuta ardhini. Mjapan hana kitu chochote ardhini ila anatesa dunia hii kwa sababu tu kichwa kinafanya kazi.

Wasiwasi wangu ni mmoja. Nikikumbushia maneno ya Fundi Mchundo ni kuwa nyie Wazenji mkiachiwa hiyo ardhi, mtaivunjavunja na mwisho mje mkilialia kuwa tuwasaidie Superglue kuviunga vipande vipande vilivyomeguka.
 
kwa vile hakuna wa kulaumiwa hivyo historia haitajwi tena? fikra za namna hii ni fikra za denial; sasa wale walionunuliwa watumwa (acha waliouza au walionunua) wao hawana wa kumlaumu bali kushukuru?

ukienda visiwa vya carribean kama Haiti, Jamaica au USA, Brazil, Paraguay, Basra,Iraq au Kusini ya Iran(Shat-al Arab) ukisema mimi natoka Afrika, wakikuzoea watakuambia 'brother' nyie ndio mliotuuza utumwani kwa wafanyabiashara ya utumwa toka ulaya na arabuni.

Ukiangalia itawezekana vipi hawa wafanyabiashara ya utumwa wakafika Uvira, DRC au Lilongwe, Malawi au Timbukti,Mali bila kushambuliwa na watemi mbalimbali bila kutaja tawala zilizokuwa na nguvu za kiafrika kama Dola za Songai, Matembele, Luganda, n.k

Hivyo sote tulishiriki ktk biashara ya utumwa iwe ni mbara, mzanzibari, mwarabu, mreno, mwingereza, mhispaniola, Ottoman empire(Uturuki na kofia zao za tunga). Kwa taarifa Ottoman empire pia walikuwa wanapeleka watumwa wa kizungu sokoni Zanzibar kama wabara tulivyowauza mateka wetu kwa wafanyabiashara halafu baadaye tukageukwa vilevile. Jiulize kwanini Somali kuna maelfu ya watu wazigua(Somali bantu wanaongea kizigua)

Hivyo hii dhana ya kumsukumia mzigo wa lawama watu fulani umepitwa na wakati, ka-historia haka sio denial syndrome ila ni kubainisha ukweli kwa facts.
 
Bagamoyo,

Acha uwongo. Siyo wote walifanya hii biashara. Mirambo aliwapa sana shida Waarabu na Wazungu na hata watu wengine wote waliokuwa wakikatiza eneo lake la Nyamwezi Empire. Sasa unafikiri angeliruhusu mtu aje achukue Mnyamwezi wake kuwa Mtumwa?

Halafu hao wanaosema kuwa eti "sisi tuliwauza", jibu ni moja tu tu kuwa "njia nyeupe kabisaa, wanaweza wakarudi Africa" na mwisho kama wamekosa wa kumlaumu juu ya umasikini wao, basi waendelee na kilio chao na uvivu wao na lawama watutupie sisi Waafrica.
 
Inashangaza katika historia nzima "fupi" ya Zanzibar.. neno utumwa hata halikuingia mawazoni kwa maalim; anaamini kabisa watu weusi wote walioko Zanzibar walikuja kwa ajili ya kutafuta maisha ya kheri visiwani humo na kuwa watu wote walioishi Zanzibar waliishi kama watu sawa na huru! This in history is known as revisionism!

In the compacted political history of hon Seif, slavery never happened and there is no evidence of its existence in the beautiful islands of Zanzibar!
Tatizo lako mwanakijiji ni tatizo ambalo watanganyika wengi mnalo hamuijui historia ya zanzibar na napata wasiwasi hata yenu ya tanganyika hamuijui nyinyi mnamjua nyerere tu.na ikitajwa historia ya zanzibar ni utumwa tu.Historia ya zanzibar haihusiani kabisa na utumwa mtu mweusi hakuingia zanzibar kwa njia ya utumwa kama walivoingia marekani na baadhi ya nchi nyengine za ulaya weusi wa zanzibar waliingia kuja kutafuta maisha na ushahidi wa hayo ni kina karume ambao waliingia wakitokea malawi na baadae wakawa wanashiriki katika siasa na kuwa viongozi wazanzibar.Tunaushahidi wa kutosha kwamba biashara ya utumwa ilikuwa inafanywa na mapadri na mapaster walioingia africa kama wamishionary na ushahidi wa haya tunaona masoko ya utumwa yako makanisani i.e.zanzibar na bagamoyo.wala hayako misikitini na athari za utumwa duniani tunaziona ulaya na marekani sio arabuni.Nilikuwa nakuamini sana mwanakijiji kama ni mtu muelewa lakini sasa napata wasiwasi na wewe na inaonekana mgumu kuelewa na kukubaliana na ukweli soma historia ya ukweli kuhusu zanzibar kama ilivoelezwa kwa ufupi na maalim seif.au unataka tuseme zanzibar inatokana na tanganyika kama alivotaka mapuri wazanzibari tukaungana tukamzima.zanzibar is a unique na ni mchanganyiko na iko kabla ya tanganyika.Kubali tu japo hupendi lakini si ukweli kubaliana nao.
 
Ni kweli uwezi kuzungumzia Zanzibar bila utumwa, kwa hili Maalimu atakuwa amechemka. Hata hivyo bado ana nafasi nzuri ya kurekebisha historia yake. Ikumbukwe kuwa zaidi ya watumwa milioni 1 walifika pwani na Zanzibar kipindi hicho cha utumwa.
Unakosea kibunango hiyo ndio historia mliolishwa na kina nyerere na ninaamini huwezi kubadilika kwa sababu umepindwa na kufinyangwa uwe hivo licha ya maovu yote aliyoyafanya nyerere katika nchi hii mpaka leo unaamini nyerere ni hero of this country maskini roho yako unapotea kaka.Enzi za utumwa njia kuu ya usafiri kutoka nchi moja au bara moja kwenda nyengine au jengine ilikuwa maji na zanibar imeshiriki katika utumwa kutokana na jiografia yake tuu.na waliokuwa wakishiriki biashara hii ni wamishionary kupitia njia kuu walizokuwa wakipitishwa watumwa ambazo ni maknisa ya kianglingana ambayo yanasifika sasa kwa ushoga.Na walikuwa wakiifanya kwa siri kwa sababu mamlaka ya zanzibar ilikuw haikubaliani nayo na some time hata ikijua ilikuwa haina uwezo wa kupigana na waingereza.ungereza waliianzisha na baadae wao wakawa wa mwanzo kuipiga marufuku baada ya kutosheka.utumwa katika historia ya zanzibar simuhimu kwa sababu haukuleta athari yoyote iwe mbaya au njema.Hakuna hata mzanzibari mmoja anaeweza kuthibitisha kuwa kizazi chake kimeingia zanzibar kwa njia za utumwa.
 
Bagamoyo,

Acha uwongo. Siyo wote walifanya hii biashara. Mirambo aliwapa sana shida Waarabu na Wazungu na hata watu wengine wote waliokuwa wakikatiza eneo lake la Nyamwezi Empire. Sasa unafikiri angeliruhusu mtu aje achukue Mnyamwezi wake kuwa Mtumwa?

Halafu hao wanaosema kuwa eti "sisi tuliwauza", jibu ni moja tu tu kuwa "njia nyeupe kabisaa, wanaweza wakarudi Africa" na mwisho kama wamekosa wa kumlaumu juu ya umasikini wao, basi waendelee na kilio chao na uvivu wao na lawama watutupie sisi Waafrica.

Kama Mtemi Mirambo alikuwa anawapenda majirani zake, kwa nini aliruhusu biashara ya watumwa na pembe za ndovu zipite ktk himaya yake au kwa vile alikuwa anakusanya kodi?

Nini tumejifunza kutokana na historia hii fupi, ni kuwa na vijihimaya vidogo kuna karibisha unyonge, maana wakati mwenzio ananyolewa ulikuwa unachekelea na kweli tukanyolewa bila maji baadaye kwa kukubali kodi ya njia kwa biashara ya utumwa.

Mimi nikiangalia Tanganyika yetu, historia inasema msomi sana alikuwa Mwl Nyerere, lakini kulikuwapo wasomi wengine wengi miaka hiyo ya 1950 kabla Mwalimu Nyerere hajaenda Scotland. Je kwa nini tusiichimbe historia ya Tanganyika kuhusu washairi wa huko Ukerewe waliowakuna wanazuoni wa Ulaya miaka ya mwisho ya 1800? Dr. Kyaruzi alikuwa nani? Sheikh Amri Abeid alikuwa nani mpaka uwanja wa michezo Arusha ukapewa jina Kumbukumbu Ya Sheikh Amri Abeid, Mwaisela alikuwa nani? Sewa Haji alikuwa nani? kwa nini Tanganyika tutumie jina la bandia Tanzania Bara?
 
Japo nakubaliana na wewe kwenye vipengele vingi lakini uongeze kuwa wazanzibar wenye kutaka madaraka kwa kutumia system iliyopo i.e. Dodoma kuamua rais wa Zenj ni kikwazo kwa maelewano ya wazanzibar

1. Wazenj wenye kutaka madaraka wanashikiana na wabara kwa kutumia system mbovu kujustify thier politic desire and ends..hilo mliangalie kwa uzuri zaidi
2. Wa Tanganyika wanaopenda mgawanyike hawafaidi na chochote isipokuwa tu kuwafaidisha marafiki zao wazenj wanaopenda madaraka kwa kutoa habari za uwongo kujustify their desire and political ends
3. Mimi naenda zanzibar mara kwa mara ila ikifika karibu na uchaguzi sitii mguu kwa hofu ya kuonekana mamluki...napendekeza wazanzibar waamue watakayo bila tone la influence kutoka Bara...peace.
Kwanini woga, I thought people are free to move kama hawavunji sheria?
 
maalim seif vipi tena?

Hizi sanamu si zipo zenji?

sanamu za wa binadamu wakati wa biashara ya utumwa sanamu hizi zinapatikana kisiwani zanzibar.
sanamu hizi ziko ndani ya kanisa anglikana zanzibar ,makanisa ya anglikana duniani yanasifika kwa kufungisha ndoa za jinsia moja
 
Macho yangu yana makengeza(macho mkasi) nikijitahidi sana kuaangalia hiki kinachoitwa maridhiano hapa ya ccm na caf siyaoni kabisa. Ninachoona ni maridhiano ya Seif na Amani. Hatari inayokikabili chama cha caf ni kuondoka kwa Amani, kama jitihada haitafanyika kuweza kuweka hiki kinachoitwa maridhiano katika maandishi kupitia vikao au wawakilishi wa hivi vyama, kuna kila dalili za caf kuwa imeingizwa kingi. Hii itadhihirika mara tu baada ya uchaguzi mkuu ujao. ---YANGU MACHO!!---
na kusema kweli Macho yako ni Mazuripengine labda ungeliona hilo la wakati. Ili kuyaweka hayo majambo katika maandishi na kuyahalalisha kupitia hao wawakilishi si unahitaji muda wa kutosha (siyo miezi hii tisa ambayo inakabiliwa na joto kubwa la uchaguzi) Hivyo kuahirisha uchaguzi wa Zanzibar na kuufanya hapo mbele nafikiri ni wazo la busara. Na zaidi utaondoa ule mtafaruku wa kuwalundikia wapiga kura wa zanzibar chaguzi nyingi kwa wakati mmoja (Ukiunganisha na uchaguzi wa Rais wa JMT na Wabunge)
 
Unakosea kibunango hiyo ndio historia mliolishwa na kina nyerere na ninaamini huwezi kubadilika kwa sababu umepindwa na kufinyangwa uwe hivo licha ya maovu yote aliyoyafanya nyerere katika nchi hii mpaka leo unaamini nyerere ni hero of this country maskini roho yako unapotea kaka.Enzi za utumwa njia kuu ya usafiri kutoka nchi moja au bara moja kwenda nyengine au jengine ilikuwa maji na zanibar imeshiriki katika utumwa kutokana na jiografia yake tuu.na waliokuwa wakishiriki biashara hii ni wamishionary kupitia njia kuu walizokuwa wakipitishwa watumwa ambazo ni maknisa ya kianglingana ambayo yanasifika sasa kwa ushoga.Na walikuwa wakiifanya kwa siri kwa sababu mamlaka ya zanzibar ilikuw haikubaliani nayo na some time hata ikijua ilikuwa haina uwezo wa kupigana na waingereza.ungereza waliianzisha na baadae wao wakawa wa mwanzo kuipiga marufuku baada ya kutosheka.utumwa katika historia ya zanzibar simuhimu kwa sababu haukuleta athari yoyote iwe mbaya au njema.Hakuna hata mzanzibari mmoja anaeweza kuthibitisha kuwa kizazi chake kimeingia zanzibar kwa njia za utumwa.

Pamoja na maelezo yako mazuri ni vema ukajua hata Maalim Seif anajua nafasi ya utumwa katika historia ya Zanzibar. Ndio maana hata kwenye kuelezea historia ya Zanzibar aliweza kunukuu kauli ambayo iliashiria umaarufu wa Zanzibar katika utumwa... soma hapa chini

“Ipigwapo zumari Zanzibar , hucheza walioko katika Maziwa Makuu.” Huu ni usemi wa kihistoria unaoeleza nafasi kubwa viliyokuwa nayo visiwa vyetu katika kusarifu na kushawishi mwenendo wa mambo katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.

Kauli hii ilitokana na biashara ya utumwa na umaarufu na Zanzibar kipindi hicho. Na unaweza kuipata katika kitabu kilichoandikwa na Amin, Mohamed; Willetts, Duncan and Marshall, Peter. Kiitwacho Journey Through Tanzania, ukurasa wa 13.

Aidha sioni nafasi ya ushoga katika historia hiyo na kanisa la Anglikani, labda kama una maelezo yakinifu kuhusu hilo. Itakuwa ni jambo la maana iwapo utaweza kutuwekea hapa ili kupata ufahamu wake.

Kumbuka watumwa aliokuwa wakipelekwa Uarabuni walifanywa nini kabla ya kuondoka Zanzibar.
 
..naona Maalim Seif is in denial kuhusu biashara ya Watumwa iliyokuwa ikifanywa na watawala wa Kiarabu wa Zanzibar.

Ni nyie wale vidudu mtu! kwani hapa tunazungumzia watawala au utawala wetu na chaguzi?
Pengine uelewa wa wengine mdogo tusiseme mengi/
 
Inashangaza katika historia nzima "fupi" ya Zanzibar.. neno utumwa hata halikuingia mawazoni kwa maalim; anaamini kabisa watu weusi wote walioko Zanzibar walikuja kwa ajili ya kutafuta maisha ya kheri visiwani humo na kuwa watu wote walioishi Zanzibar waliishi kama watu sawa na huru! This in history is known as revisionism!

In the compacted political history of hon Seif, slavery never happened and there is no evidence of its existence in the beautiful islands of Zanzibar!

Tatizo ni kwamba nyinyi wengine mko katika somo la Historia wakati lengo la makala hili ni mustakabali wa Zanzibar.
Hivyo hata wewe Mzee unajifanya hujui lengo la kilichoandikwa?
Mbona yaliyofanyiwa Zanzibar na Tanganyika hayamo hunu kama mnataka kuona Dark sides za uvamizi wa wageni Zanzibar?
 
haya makubaliano ni baina ya karume na viongozi wa juu cuf znz, lakini viongzozi wa juu ccm znz hawapo kabisa na wala hawataki kusikia.
hii inaonekana karume anataka kuendelea kuongoza znz at any cost, swali je ccm znz watakubali karume apate huo nusu muhula (miaka miwili)?
je akipewa nusu muhula kuna uwakika gani kama hata taka muhula mzima ukamilike...
 
Tatizo ni kwamba nyinyi wengine mko katika somo la Historia wakati lengo la makala hili ni mustakabali wa Zanzibar.
Hivyo hata wewe Mzee unajifanya hujui lengo la kilichoandikwa?
Mbona yaliyofanyiwa Zanzibar na Tanganyika hayamo hunu kama mnataka kuona Dark sides za uvamizi wa wageni Zanzibar?

Ndugu huyo mwkjj,

Ndiyo kuni za wanafiki, yeye yuko kwenye special task force nakupa angalizo

Anajifanya kichaa hapo kumbe nia kuchochea kuni..wazenj amkeni chukueni haki zenu kutoka kwa wadhalimu wasiochoka kushabikia mkiuana..
 
KATIBU mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amependekeza uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwaka huu usogezwe mbele au Rais Amani Abeid Karume aongezewe muda ili kuweka misingi imara ya kuondoa siasa za chuki visiwani humu.

Hamad alitoa pendekezo hilo jana alipokuwa akiwasilisha mada kwenye kongamano la siku moja la kujadili maridhiano na mustakabali wa Zanzibar lililofanyika kwenye Hoteli ya Bwawani mjini Unguja.

Pendekezo hilo limekuja siku mbili baada ya Rais Amani Abeid Karume kueleza kwenye sherehe za Mapinduzi kuwa hakuna muhula wa tatu kwa urais wa Zanzibar katika hotuba iliyoonekana kama ya kuaga Wazanzibari.

http://tzlivenews.com/blogs/blog/3428-maalim-seif-ataka-uchaguzi-zanzibar-usogezwe-mbele.html
 
ccm walishalamba dume!!!!!!!!!!!! kadi yake imeishaandaliwa, tunamsubiri JK tu atuambie lini ana muda akamkabidhi mbele ya presss.

eti upinzani, pila mchuzi utaweza kupinga kweli?????????? haya bana ngoja nikimbie wasije kusema naleta uchochezi!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom