Hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi Februari, 2011

mapungufu niliyoyaona katika hoyuba hii

1.Ameongelea kupanda kwa bei ya sukari tu bila kutaja bidhaa nyingine kama vinywaji na vifaa vya ujenzi nk
2.Ameongelea kuhusu mabomu ya g/mboto na kupooza waathirika bila kugusia aina yoyote ya uwajibikaji,achilia mbali habari ya baraza la usalamala taifa na uchunguzi unaoendelea ambao tunajua ni funika kombe....
3.Tafsiri potofu(MAKUSUDI) kuwa maandamano/mikutano ya CDM yana lengo la kuchochea ghasia na fujo
4.Na yeye amekuwa mlalamikaji tu kama raia wa kawaida wasio na mamlaka yoyote
Mimi nasema uwezo wake ndio umeishia hapo
 
mapungufu niliyoyaona katika hoyuba hii

1.ameongelea kupanda kwa bei ya sukari tu bila kutaja bidhaa nyingine kama vinywaji na vifaa vya ujenzi nk
2.ameongelea kuhusu mabomu ya g/mboto na kupooza waathirika bila kugusia aina yoyote ya uwajibikaji,achilia mbali habari ya baraza la usalamala taifa na uchunguzi unaoendelea ambao tunajua ni funika kombe....
3.tafsiri potofu(makusudi) kuwa maandamano/mikutano ya cdm yana lengo la kuchochea ghasia na fujo
4.na yeye amekuwa mlalamikaji tu kama raia wa kawaida wasio na mamlaka yoyote
mimi nasema uwezo wake ndio umeishia hapo
mkuu ni kweli uwezo wake umeishia hapo!
 
jk simwelewi. Alisema chadema chama cha msimu hadi uchaguzi ndio wanaibuka. Leo wanafanya kazi ya siasa unasema wanahatarisha amani. Sasa wafanyeje?
hapo usingizi hapati ndo maana!
 
Hapo tisa,kumi mi nasubiria ahadi 91 alizotoa wakati wa kampeni.Pamoja na kwamba sikumpa kura ila naamini kuna baadhi walimpa kura kwa hadi zake.Kutozitimiza ni kudanganya wapiga kura.Hotuba haina mashiko,miaka 50 ya uhuru bado unasema umeme wa dharura?Huu si utani kwa wananchi?Gadafi amekaa miaka 42,nchi ya jangwa lakini nchi iko juu sana.Tanzania sijui tuna nini.Wakati wa porojo umeisha watu wantaka maendeleo.
 
hakuna jipya ni vichefuchefu vile vile, data za uongo na upupu mtupu, kwa nini rais unaongea kama waziri wa afya, ulinzi nk, and you dont talk kama rais mwenye authority, hutoi solution ni kulalamika tu, mmeamua kuleta richmond nyingine baada ya hii kushtukiwa, shameless president arrrrgggggggggggg!

afadhali mkuu wa wilaya
 
Hapo tisa,kumi mi nasubiria ahadi 91 alizotoa wakati wa kampeni.Pamoja na kwamba sikumpa kura ila naamini kuna baadhi walimpa kura kwa hadi zake.Kutozitimiza ni kudanganya wapiga kura.Hotuba haina mashiko,miaka 50 ya uhuru bado unasema umeme wa dharura?Huu si utani kwa wananchi?Gadafi amekaa miaka 42,nchi ya jangwa lakini nchi iko juu sana.Tanzania sijui tuna nini.Wakati wa porojo umeisha watu wantaka maendeleo.
afadhali na wewe mkuu unamatumaini unasubiri!
MIMI NIMEKATA TAMAA HAKUNA KITU KAMA HICHO KWA JK!
 
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, 28 FEBRUARI, 2011





Hali ya Usalama Nchini

Ndugu Wananchi;
​Hivi karibuni wananchi wengi wameingiwa na hofu kubwa kuhusu usalama wa nchi yetu. *Ni mara ya kwanza Watanzania wamekuwa hivyo. *Hofu hiyo inatokana na kauli na vitendo vya wenzetu wa CHADEMA vyenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini.
Mheshimiwa rais;
Kama mkuu wa nchi unapaswa kuwa kiongozi wa watanzania bila kujali vyama ni dhahili kuwa umekosa washauri madhubuti. Na nina doubt uwezo wa washauri wako katika hili. Hukutakiwa kuonesha woga, kutisha wananchi kwa machafuko ama kutumia lugha ya kukishambulia chama cha siasa kinachotimiza wajibu wake. Ulichotakiwa kuonesha kwa sasa ni kuwa tayari kufanya kazi na CHADEMA katika kutatua hali ngumu za maisha ya wananchi. Ule wakati wa kuonesha kuwa CCM is everything umeisha watu sasa wanataka results na siyo maneno ya kulialia Mheshimiwa. Kinachoendelea kufanywa na CDM ni dhahiri kinawaumiza sana na kuwapa hard time maana CDM wanawaamsha wananchi kujua haki zao na kwa viongozi wavivu wasiotaka kufiri na kufanya kazi basi wanaona kufanya hivyo ni kuchochea vurugu. Haya ni mawazo mgando ambayo kiongozi wa nchi hapaswi kuyatoa ama kuyakubali toka kwa washauri wake.





HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, 28 FEBRUARI, 2011





Hali ya Usalama Nchini

​Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila miaka mitano tunafanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wetu. *Uchaguzi wa mwisho tumefanya tarehe 31 Oktoba, 2010. *Kabla ya hapo tulikuwa na kampeni zilizochukua karibu miezi mwili na nusu. *Kila chama kilielezea jinsi kitakavyokabiliana na matatizo yanayowakabili wananchi wa nchi yetu ikiwa ni pamoja na haya wanayoyazungumza sasa. *Hatimaye siku ya uchaguzi wananchi walifanya uamuzi wa kuchagua chama walichokiamini, nacho ni Chama cha Mapinduzi. *Iweje leo, miezi mitatu baadae kwa mtu au chama cha siasa kufanya maandamano kwa masuala yale yale waliyoyasema kwenye kampeni. *Siyo sawa hata kidogo. *Kuchochea ghasia ati kwa nia ya kuiondoa Serikali madarakani ni kinyume cha Katiba na ni kuiingiza nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima. *Tutasababisha umwagaji wa damu, watu kupoteza maisha na mali zao kuharibiwa bila sababu yoyote ya msingi.
Mheshimiwa rais;

Uchaguzi wa mwisho kufanyika 2010 haina maana kuwa sasa watanzania wakae watulie tu kwani sasa mabomba yanatoa asali na maziwa na milima imegeuka mikate, unatakiwa kujua kuwa kila siku za mtanzania ni siku za uchaguzi kwa walio wengi hasa vijana wa ama kuendelea kuteseka na maisha magumu ama kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu kwa ukosefu wa ajira.
Kuhusu kampeni na uchaguzi kufanyika, jua kuwa tume yako ya uchaguzi (NEC) imekosa imani na Public trust ya kuwa referee kwa kuwa wananchi wanajua wazi kuwa CCM wanaitumia kama Jumuiya yake ya kujihalalishia utawala wa milele. Hivyo basi uchaguzi kufanyika hauondoi utashi wa watanzania wa kutaka kuongozwa na chama au viongozi wanaodhani kuwa ni chaguo lao. Njia pekee ya kuondoa malalamiko ya uchaguzi na pande zote kuwa wameridhika si kutumia hila kama zilizobuniwa na kutolewa maagizo "La Cairo" au NEC kucheleweshaa matokeo kwa makusudi, au kutangaza wale amabao wewe na CCM chama chako mnataka washinde bali ni kuwa na uchaguzi transparent kuanzia kwenye kuandikisha wapiga kura mpaka kutangaza matokeo. Mheshimiwa rais, ujue kuwa zaidi unavyoongelea uchaguzi wa 2010 ndivyo anavyowakumbusha wapiga kura jinsi NEC yako ilivyowanyanyasa kwa makusudi kwa kuwawekea watu wasiokuwa chaguo lao.

Suala la kuchagua nini cha kusema katika maandamano liwe ni kwa masuala yaleyale au mengine hiyo ni haki ya mwandamanaji mradi tu havunji sheria, kama hoja zile zina nguvu na support toka kwa wananchi mpaka leo ni dhahiri zitaendelea kuzungumziwa, kwa mtawala au kiongozi makini basi huu ulikuwa ni wakati muafaka wa kuzifanyia kazi hoja zile na kuzi deliver kwa wananchi kama ni popular na si kulalama tu kana kwamba umeonewa unahitaji huruma, hakuna aliyekuomba uwe rais bali ni wewe mwenyewe na kundi lako mliona kazi hii unaiweza basi huna budi kuifanya kwa umahiri mkubwa bila kuonesha upendeleo wa uCCM au uCDM. Kwa kiongozi wa nchi kulalama kwenye hotuba kuhusu chama fulani hiyo ni weakness katika uongozi, ulitakiwa kuonesha kuwa wewe ni baba na wote waliomo ndani ya nyumba ni wanao na hivyo chukua mazuri wherever they come from.

Wananchi kuitaka serikali ambayo inaamini imeshinda na kutokana na ridhaa yao kufanya jambo fulani si kusababisha vurugu bali ni wajibu wao kufanya hivyo kama kweli serikali hiyo ipo kwa ajili yao.





HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, 28 FEBRUARI, 2011





Hali ya Usalama Nchini

Ndugu Wananchi;
​Katika nchi ya kidemokrasia na kwa wanademokrasia wa kweli, mnapomaliza uchaguzi mmoja, mnajiandaa kwa uchaguzi mwingine. *Mnajenga upya chama chenu, mnaongeza wanachama, mnaboresha sera na hoja zenu pamoja na namna ya kuziwasilisha ili watu wawakubali nyinyi na kuwakataa wenzenu. *Na, uwanja muhimu wa kufanya sehemu kubwa ya hayo ni katika Bunge na Halmashauri za wilaya kupitia Wabunge na Madiwani wenu.

​
Muheshimiwa Rais;
Hupaswi kuvisemea vyama shindani ambavyo havipo chini yako wafanye nini. Hii tactic CCM mmekuwa mkiitumia tokea 1995, Nyie kwa kuwa mpo madarakani huwa mnafanya kampeni kwa muda wote wa miaka mitano kwa kuhusisha kila suala serikali inayolifanya kwa fedha ama za walipa kodi au za wafadhili kuwa ni hisani inayotolewa na CCM. Siasa ni strategy, wewe kama rais wa nchi na kiongozi wa chama chako, kama unaona strategy wanayotumia CDM inawaweka ninyi kwenye disadvantage basi huwapaswi kutoa amri kwa polisi za kuzuia maandamano kwa sababu za kiintelijensia za uongo, maana kufanya hivyo ni kuzidi kuli-isolate jeshi la polisi na raia wema wanaopenda mabadiliko na kuongeza chuki miongoni mwetu. Mnachopaswa kufanya CCM ni kubadili strategy na ku-focus kwenye kuboresha na kuya implement yale ambayo CDM wanaona yanawavutia wananchi na kukiongezea nguvu chama chao, mkifanya hivi mtakuwa mmeondoa hoja hizo za CDM kwa wananchi, na hiyo ndiyo strategy badala ya kudectate wafanye nini.

Mheshimiwa rais;
Kutumia bunge ambalo limeisha poteza mvuto tokea mwanzo kwa kuwekewa Speaker asiye huru bali kufanya kazi kwa remote control kwa matakwa yako wewe na chama chako hakitoi fursa ya wazi kwa siasa kufanyikia huko kwa haki, tumeisha ona speaker wa chama chako jinsi alivyo na "Pre determined preferences, Prejudices" hasa anaposimama mbunge yeyote wa CHADEMA, Nafikiri utarajie maandamano haya kwa miaka yako yote mitano iliyobaki, kwani siasa za ndani ya vyombo hivi hazipo kwa ajili ya PUBLIC INTERESTS balini CCM INTERESTS. Kitendo cha Speaker wako cha kumlipukia Mbunge aliyetaka mwongozo ni dhahiri kuwa humo hakuna siasa wala uhuru wa kueleza mawazo zaidi ya majukwaani.






HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, 28 FEBRUARI, 2011





Hali ya Usalama Nchini

​Kuacha kufanya hivyo na badala yake kuamua kuzunguka nchi nzima na kuchochea ghasia kwa lengo la kuwaondoa walioshinda ili muingie nyie ni kinyume kabisa na misingi ya demokrasia. *Tutajenga misingi ya hovyo na nchi yetu itakosa amani na utulivu daima. *Hebu fikirieni, kama kila atakayeshindwa uchaguzi anafanya hivyo tutakuwa nchi ya namna gani? *Tanzania yetu hii yenye sifa na heshima ya kuwa nchi ya amani na utulivu itapoteza kabisa sifa hiyo na badala yake umwagaji wa damu na mateso kwa watu wasiokuwa na hatia vitageuka kuwa maisha ya kawaida. *Hatuitendei haki nchi yetu na hatuwatendei hai wananchi tunaodai tunawapenda na kuwatetea.

Mheshimiwa rais;
Wewe ndiyo unayedhani kuwa CDM wana lengo la kukuondoa kwa maandamano, na kama una uthibitisho wa hilo kwa rais wa nchi si busara kuliweka kwenye hotuba ambayo wananchi wanafikiri itakuwa suluhu ya maisha yao badala yake ni defence yako wewe na madaraka. Kama una uthibitisho na hili unalolisema kwa statesman ni aibu sana kulalama badala ya kulikabidhi kwa vyombo ya sheria. Vinginevyo unaweza kuwa unajigeuza "papa kujikaanga kwa mafuta yako", maana kama wananchi wamekuchoka na kutamani usiwe rais wao basi wataona kama vile umewapa suluhisho ambalo halikuwa kwenye mawazo yao.

Suala la kushindwa uchaguzi usiliongelee maana ni imani ya wapiga kura wengi(majority) kuwa hata wewe na chama chako hamkushinda uchaguzi bali mlichakachua, na wao wakiuliza je kila anayeshindwa akitaka kuchakachua hii itakuwa nchi ya namna gani?, suluhisho ni moja tu mheshimiwa rais, nalo ni "KATIBA MPYA ITAKAYOTOKANA NA MATAKWA YA WANANCHI NA MARIDHIANO YA WADAU WOTE" na si mtu mmoja kujitwalia madaraka ya kuunda tume yake ya kufanya hivyo hata kama katiba hiyo inampa fursa hiyo, Public trust haijengwi kwa mtutu au mabomu ya machozi bali ni kwa maridhiano na majadiliano yatakayopelekea kwenye "TRANSPARENCY" of all which we do as a Nation and not closed door meetings of the so called "Halmashauri kuu au kamati kuu ya chama chako", kwani kwa watanzania wengi Chama is nothing mbele ya masilahi ya Taifa. Wakati wa chama kushika hatamu uliisha 1995 tulipokubali kuingia katika uchaguzi wa vyama vingi.






HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, 28 FEBRUARI, 2011





Ndugu Zangu;
Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa. Mzee Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii. *Na wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang'atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. *Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa nae kakaa miaka 10 hakuyamaliza. *Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote. *Lililo muhimu kuliko yote ni kuwa katika kila awamu nchi yetu imekuwa inapiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo. *Hali iliyokuwa wakati ule sivyo ilivyokuwa mwaka 1985, wala 1995 au 2005 na ilivyo sasa. *Katika miaka mitano hii kuna maendeleo yanayoonekana wazi, pamoja na changamoto nyingi tumefanya juhudi kubwa na mafanikio yanaonekana katika nyanja zote za maisha ya Watanzania. Mwenye macho haambiwi tazama.

Muheshimiwa Rais;
kushindwa kwa waliokutangulia hakukupi wewe haki ya kushindwa pia. Maana kama ulijua unagombea ili uje kushindwa kulikuwa hakuna haja ya wewe kujiingiza kwenye kazi ambayo kwako wewe was a "FAILURE AB INITIO". usingetumia mbinu chafu za kuwachafua wenzako ambao huenda walikuwa optimistic kuwa wanaweza kutatua matatizo yote ndani ya siku saba tu. Maana tunajua matatizo yetu mengi ni ya kimfumo, mfumo wa rushwa na kujuana katika kupeana majukumu bila kuangalia sifa ndiyo sababu kubwa ya failures, "UMWENZETU" ndiyo unaokufanya sasa hivi uonekane kuwa a "FAILED PRESIDENT", unashindwa kuwachukulia hatua rafiki zako ambao leo hii hata mtoto wa darasa la kwanza ukimpatia kazi ya kuwahukumu atawatia hatiani, ila wewe umekaa na kutaka kuendelea kuwapotezea watanzania miaka mingine mitano huku ukijua kuwa hutawafanyia chochote kama ambavyo waliokutangulia walivyofanya. Kwa kukumbusha tu Muheshimiwa Rais ni kwamba mmoja kati ya walikutangulia Mwl J K Nyerere mwaka 1985 aliamua kung'atuka kwa hiyari yake baada ya kuona amehemewa na uwezo wake ulikuwa umefikia kikomo, kwa nini wewe usifuate nyayo zake kama ambavyo unavyotaka kufuata nyazo zake za kushindwa?






HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, 28 FEBRUARI, 2011





Hali ya Usalama Nchini

Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
​Ni kweli kuna hali ngumu ya maisha, na kukabiliana nayo ndiyo kazi tunayoendelea nayo kufanya kila siku. *Tumeelekeza nguvu zetu na rasilimali zetu huko na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali. *Kikwazo siyo upungufu wa sera wala dhamira, kikwazo kikubwa ni kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi wetu na hivyo uwezo wetu siyo mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo yote haraka kama ambavyo tunapenda iwe.

Mheshimiwa Rais;
Kama kweli mnayafanyia kazi, matatizo haya ya kupanda kwa maisha kwa nini basi bado yanaendelea kuongezeka badala ya kupungua?, Mheshimiwa unaposema tatizo si sera bali ni uchumi unakuwa taratibu kwa watanzania walio makini unawachanganya, maana hivi vitu viwili vina positive correlation, unapokuwa na sera nzuri na kuzisimamia zipasavyo basi ni lazima zitakuwa na positive effect. Sasa Mheshimiwa wewe na chama chako kila uchaguzi mnatuijia na ilani mpya wakati ile iliyopita hamkuitekeleza au kuifanyia kazi hauoni kuwa huu ni uongo wa baba kwa mtoto kuwa kila siku akitoka kazini anasema kasahau kununua pipi wakati aliahidi, matokeo yake ni mtoto kutomuani tena baba huyo. Muheshimiwa rais ujanja wenu wa kutupiana vijiti ili kulinda masilahi ya wachache wananchi tumeujua na tunaona kuwa hakuna tofauti kati ya No.1 au No.4 kama tu wote wanatoka chama kilekile kilichopewa muda wakuiongoza kwa miaka 50 na kwa hiyo kunakuwa hakuna tofauti kati ya Gaddafi aliyekaa 41 years au CCM. Maana wananchi wakitaka kuikupumzisha kwa amani kwa njia ya kura zinachakachuliwa sasa unawashari wafanye nini?, ni bora waandamane kutoa madukuduku yao kwa amani huenda mkasoma alama za nyakati na kuwasikiliza kabla hayo uliyotabiri hapo juu hayajatokea. Ridhaa ya kuongozi isiwe tu inaoneshwa kuwa imetoka kwa wananchi bali iaminike, ithibitike na pia itoke kwa wananchi kwa kura zao halali. Leo hii mtu akikuuliza swali ni nani alishinda urais wa JMT 2010 utamuona ni kichaa kwani inajulika kuwa ni rais aliye madarakani lakini wengi hatuamini kabisa kuwa wewe unatokana na kura halali za wananchi, ingekuwa hivyo kama tungekuwa na Tume ya uchaguzi iliyo huru na tranparent kwenye kila sehemu. Amani yetu muheshimiwa rais haitadumishwa na chama chochote bali ni haki na usawa ila kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa Itavunjwa na Chama chako cha CCM kwa kutokuwa tayari kukubaliana na matakwa ya wananchi kama yalivyo na matumizi haramu ya vyombo vya dola kwa manufaa yenu binafsi. Ningekuwa mimi ndiyo wewe nisingehofia CHADEMA, maana, hawana dola bali ningehofia chama cha CCM katika kuvuruga amani.
 
Maiti wote 25 wameshazikwa kwa gharama ya serikali kule ambako ndugu waliamua wakazikwe. Kwa ajili hiyo maiti 10 wamezikwa dar es salaam na wengineo mikoani kama ifuatavyo:- mara - wanne, pwani – watatu, tanga - wawili, lindi – mmoja, kagera - mmoja, kilimanjaro – mmoja, mbeya – mmoja na mtwara – mmoja[/i]. Majeruhi wameendelea kupatiwa matibabu na huduma stahili. Mpaka sasa kuna majeruhi 36 ambao bado wamelazwa katika hospitali za amana, temeke na muhimbili. Watoto 857 waliopotezana na wazazi wao wameshaunganishwa na familia zao. Hata hivyo, watoto 15 bado hawajatambuliwa na wazazi au walezi wao. Kwa sasa watoto hao wamepelekwa kwenye kituo cha kulelea watoto cha kurasini. Napenda kuwakumbusha wazazi waliopotelewa na watoto kufika kituoni hapo kuwatambua watoto wao. Ni jambo la kustaajabisha kwamba zaidi ya siku kumi sasa zimepita wazazi au walezi hawajajitokeza kutafuta watoto wao.

wakuu labda hesabu inanipiga chenga mwenzenu, mbona mimi nikihesabu napata hesabu ya waliokufa na kuzikwa ni 24, wakati mwanzo mkuu kasema 25? Mmoja kazikwa wapi?
 
Chadema inampandisha presha sana jamaa na haoni chama kingine cho chote cha siasa cha upinzani isipokuwa Chadema. Juzi anarudi toka West Afrika anapokelewa na maandamano makubwa ya Wanachadema huko Kanda ya ziwa.
Duh anachoongelea hakuna cha kuongelea maendeleo bali kulalamikia Chadema tu.
Rais Kikwete Chama Cha Chadema kinamchanganya kabisa hajui wapi wa kuinusuru CCM.
:msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela::msela:
 
Hali ya Usalama Nchini

Ndugu Wananchi;
​Hivi karibuni wananchi wengi wameingiwa na hofu kubwa kuhusu usalama wa nchi yetu. *Ni mara ya kwanza Watanzania wamekuwa hivyo. *Hofu hiyo inatokana na kauli na vitendo vya wenzetu wa CHADEMA vyenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini. *Kufanya maandamano na mikutano ni haki ya msingi ya vyama vya siasa na raia. *Lakini, kuigeuza fursa hiyo kuwa ni jukwaa la kuchochea ghasia na kwa nia ya kuiondoa Serikali iliyoko madarakani kwa mabavu ni matumizi mabaya ya fursa hiyo.

​Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila miaka mitano tunafanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wetu. *Uchaguzi wa mwisho tumefanya tarehe 31 Oktoba, 2010. *Kabla ya hapo tulikuwa na kampeni zilizochukua karibu miezi mwili na nusu. *Kila chama kilielezea jinsi kitakavyokabiliana na matatizo yanayowakabili wananchi wa nchi yetu ikiwa ni pamoja na haya wanayoyazungumza sasa. *Hatimaye siku ya uchaguzi wananchi walifanya uamuzi wa kuchagua chama walichokiamini, nacho ni Chama cha Mapinduzi. *Iweje leo, miezi mitatu baadae kwa mtu au chama cha siasa kufanya maandamano kwa masuala yale yale waliyoyasema kwenye kampeni. *Siyo sawa hata kidogo. *Kuchochea ghasia ati kwa nia ya kuiondoa Serikali madarakani ni kinyume cha Katiba na ni kuiingiza nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima. *Tutasababisha umwagaji wa damu, watu kupoteza maisha na mali zao kuharibiwa bila sababu yoyote ya msingi.

Ndugu Wananchi;
​Katika nchi ya kidemokrasia na kwa wanademokrasia wa kweli, mnapomaliza uchaguzi mmoja, mnajiandaa kwa uchaguzi mwingine. *Mnajenga upya chama chenu, mnaongeza wanachama, mnaboresha sera na hoja zenu pamoja na namna ya kuziwasilisha ili watu wawakubali nyinyi na kuwakataa wenzenu. *Na, uwanja muhimu wa kufanya sehemu kubwa ya hayo ni katika Bunge na Halmashauri za wilaya kupitia Wabunge na Madiwani wenu.

​Kuacha kufanya hivyo na badala yake kuamua kuzunguka nchi nzima na kuchochea ghasia kwa lengo la kuwaondoa walioshinda ili muingie nyie ni kinyume kabisa na misingi ya demokrasia. *Tutajenga misingi ya hovyo na nchi yetu itakosa amani na utulivu daima. *Hebu fikirieni, kama kila atakayeshindwa uchaguzi anafanya hivyo tutakuwa nchi ya namna gani? *Tanzania yetu hii yenye sifa na heshima ya kuwa nchi ya amani na utulivu itapoteza kabisa sifa hiyo na badala yake umwagaji wa damu na mateso kwa watu wasiokuwa na hatia vitageuka kuwa maisha ya kawaida. *Hatuitendei haki nchi yetu na hatuwatendei hai wananchi tunaodai tunawapenda na kuwatetea.

Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Ndugu zetu wa CHADEMA wanayajua yote haya, lakini wanalo lao jambo. *Wanataka kuipeleka nchi yetu pabaya kwa kukidhi uchu wao wa madaraka. *Kwao sasa demokrasia haina maana, inaweza kusubiri. *Wanataka kutumia mabavu. *Naomba *tuyakatae mambo yao. *Tusiwafuate. *Waambieni mchezo wao ni hatari na ni mauti yetu. *Sisi katika Serikali tutajitahidi kutimiza wajibu wetu wa kulinda usalama wa nchi yetu, watu wake na mali zao.



a threat, a warning, or cdm they are givin those guys the hard time?
 
It is so shameful for a presidents speech to base on what the opposition party did instead of advocating to the issues that disturbing the citizen and telling us what he will do to make us enjoy the better life as he promise. SHAME NO YOU Mr PRESIDENT.
 
Nadhani Kikwete anashindwa kupata picha HAlisi ya kujua ni wakina nani waliomuweka hapo madarakani, Kuwalalumu Chadema ni kuwaonea, hakuna hata kiongozi mmoja wa Chadema aliyeenda ndani ya nyumba ya mtu na kumshurutisha kuja kuandamana, watu wametoka majumbani mwao bila kujali Dini zao, Kabila zao wala ukanda zao (Zones), JK ilimpasa kujibu shutuma hizo za Chadema na hao wanaoandamana kwa hoja zenye mshiko,
Kama anavyoseama wakati wa "Mzee" Nyerere (Maana yeye kamwe hamuiti Nyerere baba wa Taifa) si kama huu wa sasa, basi inampasa kujua kuwa watu wa sasa wako huru na wameelimika, kama anashindwa kushughulikia suala la mafisadi, basi akae akijua kuwa watu wanajua kuwa kashindwa

hali ngumu ya Maisha ya pande zote nchini zinamuhusu yeye, yeye kama kiongozi mkuu yuko responsible na matatizo yote, kama anaona hawezi kuyatatua basi njia bora ni ku step out
 
mapungufu niliyoyaona katika hoyuba hii

1.ameongelea kupanda kwa bei ya sukari tu bila kutaja bidhaa nyingine kama vinywaji na vifaa vya ujenzi nk
2.ameongelea kuhusu mabomu ya g/mboto na kupooza waathirika bila kugusia aina yoyote ya uwajibikaji,achilia mbali habari ya baraza la usalamala taifa na uchunguzi unaoendelea ambao tunajua ni funika kombe....
3.tafsiri potofu(makusudi) kuwa maandamano/mikutano ya cdm yana lengo la kuchochea ghasia na fujo
4.na yeye amekuwa mlalamikaji tu kama raia wa kawaida wasio na mamlaka yoyote
mimi nasema uwezo wake ndio umeishia hapo

hakuwa anatoa hotuba alikuwa anawapasha chadema, hoja zote zaihusu chadema. Uwezo wake mdogo
 
"Tarehe 15 Februari, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme."


Haya dharula nyingine, TANESCO haina mitambo yake yenyewe siku zote inakodi serikali haifikiri kununua maji yakiisha kwenye mabwawa "dharula" huu ndio mwanzo wa deals zaidi

"Kigumu Chama Cha Mapinduzi" "Kigumu"
 
Katika umri wangu huu wa miaka 30, sijawahi kumsikia na kumuona RAIS mwenye hofu kama JK
 
Hili la sukari nafikiri ni ufisadi mwingine ambao unasubiriwa kulipuka siku za karibuni. Kuna haja ya kufikiria upya juu ya hili my President.
 
Back
Top Bottom