Hotuba ya rais Kikwete ya kufunga mwaka 2010

Samahani kama nimekukwaza ndugu. Hebu tuendelee na mada bila kuchoka,kwani ndio kwanza ngoma iko kilingeni. Je Mnyika na hoja yake Bungeni ina haja ya kusikilizwa?

mimi naona aina haja tena kwa sababu mzee mkwere kamaliza kila kitu au mnaonaje alafu nimehis kitu kikwete anaweza tufanyia mambo hasa kwenye katiba
 
Kikwete: Ataunda tume itayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea kuratibu maoni juu ya kuandikwa kwa katiba mpya. Wanajamvi naomba mnijuze Wanasheria wetu hapa waliobobea ktk KATIBA

Mkuu.
Mimi najua at least huyu.
Prof Shivji ni gwiji wa mambo ya katiba.

jee atakuwemo katika hiyo tume?
 
walipata maelekezo "KANISANI ILI WAMGOMBANISHE JK NA WANANCHI. NDIO MAANA KAWASHTUKIA SANA HAWA JAMAA'".

Kanisa lipi na lini walipewa maelekezo? Baadaye mtakuja kulialia majukwaani kwamba kuna udini kumbe mind-set zenu zimekaa tenge!
 
hivi Kenya iliwachukua muda gani kupata katiba mpya?

Kama anamaanisha anachosema kuhusu katiba mpya, ina maana amekuwa upande mmoja na Pinda wakatijaji Werema na Kombani wapo upande wa pili. Kwa dhana ya uwajibikaji ina maana JK na Pinda vs Werema na Kombani ni kambi mbili tofauti. Na ilitakiwa Jk achukue jukumu kuwawajibisha hao wawili haraka sana kulinda maamuzi yake na ya MP maana hawatakuwa na mawazo mamoja ktk utendaji na muundo wa tume anayosema Jk. Wao ni kikwazo kwa sasa maana kitaifa ndio wanashikilia mfumo wa katiba na sheria.
 
  1. Sasa Jaji Werema wakati anatoa maoni yake kuhusu katiba alikuwa ame base wapi? au alikuwa hajui ofisi yake imemshauri nini Rais? au Ikulu imeamua nini kuhusu ushauri alioutoa? Sielewi vizuri haya mambo yanavyokwenda
    1. Celina Kombani -- Serikali haina pesa wala bajeti ya kuandaa katiba mpya
    2. PM Pinda: Serikali inalipokea swala la katiba mpya, italifanyia kazi kwa kumshauri Rais
    3. AG Werema: Katiba mpya hapana, tuweke viraka kwenye hii iliyopo kama ni lazima
    4. President: Anakubali katiba mpya ni muhimu, na ataunda tume kushughulikia hilo
    Haya yote ni ndani ya siku 60 baada ya uchaguzi.
Mtumiabusara: Hivi hujui kama kuna serikali mbili. Hii tulioichagua na serikali Kivuli? Serikali kivuli ni ile inayoendesha mambo yake kupitia mgongo wa nyuma. Lengo la Serikali hiyo ni Kuvuruga utawala uliopo madarakani hasa Rais au Waziri aliyepo madarakani anapokuwa ni wa DINI wasioitaka wao. HUKO NDIKO WANAKOPATA UJASIRI ILI KUMCHONGANISHA RAIS NA WANANCHI WAKE.Tumia busara kidogo tu utagundua hayo.
Kwani hukusikia kwenye mikesha ya KRISTIMASI Paroko akiagiza Jeshi lake lililoko Jeshini kuhakikisha linawang'oa madarakani wale waliothubutu kuzungumza hadharani kuwa UDINI ulikuwa kigezo katika uchaguzi uliopita? Mlengwa ni nani??? Kwa ushujaa gani??
Kwani umesahau yale magari 67 yaliyopo pale bandarini yaliyoletwa na kanisa kwa ajili ya kumpa tafu Dr.????? Na jamaa kayazuia??
Huoni jeuri hiyo???
Kikwete amechomoa na amejichomoa katika mtego huo!!!! Big up JK wa ukweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Think twice and laugh once for ur country.


 
Kanisa lipi na lini walipewa maelekezo? Baadaye mtakuja kulialia majukwaani kwamba kuna udini kumbe mind-set zenu zimekaa tenge!

mkuu nikumbushe .... tenge tafsiri yake ni bevel in english au...?
 
Jambo lolote linalosimamiwa na Jk siliamini kabisa. mwaka 2005 aliaahidi maisha bora kwa kila Mtanzania leo kuna nini? Wakati anapokea mitambo Richmond uwanja wa ndege aliahidi kwamba mgawo wa Umeme Tz utakuwa historia lakini hadi leo ahadi yake haijatimia. Badala yake Richmond ikawa kampuni hewa na leo Dowans inatudai bil.185. Leo hata kuzungumzia Dowans hajazungumzia. tuendelee kusubiri usanii wa Jk hadi hapo atakapotuacha 2015

Xaygan alkomare gan!
Hapo nyekundu inaonyesha ya kuwa ile dhana kwamba JK ni mtu wa watu sasa mkubali kuwa ilikuwa ninkuwahadaa wananchi. Kusingizia gharama za TANESCO bila kuwataja RichMonduli and Ndoana, ni hadaa nyingine iliyowazi!!:embarrassed:
 
Kivumah .... mimi concern yangu ni.... the type of Constitution review commission... would it be presidential or independent constitution review commision...?


Mkuu hiyo ni concern ya muhimu na umeiweka wakati mwafaka kabisa...umenikumbusha kilichojiri katika Tume ya Rais ya Jaji Nyalali na ile ya Jaji Dr R. Kisanga...ooooh Kisanga aliadhiriwa mbele ya watu na Mkapa eti kafanya kazi ambayo hakutumwa...kile ambacho Mkapa, any way tuachane nayo sasa hayo...kama itaundwa tume ya rais kutaibua shaka maana watatoa ushauri kwa rais naye, kwa mujibu wa katiba mbovu ya sasa, halazimiki kuchukua au kufanyia kazi ushauri wa mtu yeyote katika utendaji kazi wake....inapaswa kuwa independent committee katika uhalisia wa neno lenyewe kamati/tume huru
 
hizi ni geresha na sarakasi tu za CCM. Kama hawako organized kutoa tamko unison, tutawaaminije kwa hili. Anyway hapa wanajaribu kupoza mambo tu na mpaka nitakaapoona hatua za msingi zinachukuliwa ndipo nitaamini. Huyu si ndiye aliahidi mambo lukuki yasiyotekelezeka?

Mtakao kuamini aminini, but I'm still very skeptical. I will move with no president as a person till 2015.
That is!

Mkuu,

Mimi pia leo nimehitimisha kuwa CCM wameiteka nyara rasmi hoja ya Katiba Mpya.
Sasa wale wapiga kelele inawabidi watafute issue nyengine .

Kwani hata maandamano ya kudai katiba yameshakosa nafasi baada ya kauli ya Mkulu.
Maandamano yataitwa uchochezi, kutaka kuvunja amani na utulivu.


Amesema ataunda tume, lakini hakusema ataiunda lini.
That means time frame haipo....Lakini pia tume itawasilisha mapendekezo sehemu inayohusika na maamuzi yatafanya, pia kuamua lini ianze kutumika.

Ufahamu wangu ni kuwa kinachokuja ni utiaji viraka wa hii iliyopo,
Lini tume itateuliwa, hakuna anayejua...
Muda gani tume itatumia kufanya kazi zake..hakuna anayejua..
Lini hiyo katiba itakayopendekezwa na kupitishwa hakuna anayejua lini itakuwa tayari na lini itaanza kutumika.
Mwishowe hiyo tume itapeleka,itakabidhi mapendekezo yake kwa nani? kwa chombo gani? Jee kuna anayejua?

Tunaweza kufurahia kauli yake kama tulitaka tu kusikia anasema nini, lakini ameacha masuali mengi kuliko kutolea majibu.
 
Mkuu hiyo ni concern ya muhimu na umeiweka wakati mwafaka kabisa...umenikumbusha kilichojiri katika Tume ya Rais ya Jaji Nyalali na ile ya Jaji Dr R. Kisanga...ooooh Kisanga aliadhiriwa mbele ya watu na Mkapa eti kafanya kazi ambayo hakutumwa...kile ambacho Mkapa, any way tuachane nayo sasa hayo...kama itaundwa tume ya rais kutaibua shaka maana watatoa ushauri kwa rais naye, kwa mujibu wa katiba mbovu ya sasa, halazimiki kuchukua au kufanyia kazi ushauri wa mtu yeyote katika utendaji kazi wake....inapaswa kuwa independent committee katika uhalisia wa neno lenyewe kamati/tume huru

mkuu....nashukuru kwa kunisoma.... likely the past would reverse na mwisho ikawa ni michezo ya kuigiza kama watu hawatashtuka mapema kama wewe na mimi
 
Rais ameshauri tuwaepuke wanasiasa wanaoleta chokochoko ili wakifuatiliwa na vyombo vya dola, wakimbilie katika Jumuiya ya kimataifa. Pia ametuasa tuchape kazi na tusikalie POLITIKI. Kazi kwanza, politiki baadae. Zaidi ya yote ameahidi kufungua rasmi mjadala wa katiba. Inaonesha huyu jamaa amekomaa na kuiva kisiasa. Anaijua jamii yake inataka nini na kwa muda gani. LONG LIVE JAKAYA
Kwa maneno mengine amesema hali si shwali nje manake anaulizwa kwa nini FFU wanapiga watu mabomu, kwa nini Uchaguzi wa Mameya Una kelele nyingi, kwa nini watu hawaridhiki na uongozi wako.
With this note hali yake nje ya Bongo si nzuri na pozi lake la kusafiri nje limeharibika kwa hiyo anataka kuwalaumu wanasiasa wasio wa ccm bila kujali kwamba ccm ndiyo chanzo cha hayo yote. Let kikwete know that we can read between the line and understand the real thing man, nanyi wapambe wake kamwambieni tumeelewa kuwa yuko kwenye hot soup na ndiyo maana ameogopa kwenda Brazil kamtuma Membe na bado mpaka kieleweke
 
what a shame to a 'learned brother' AG Werema! Mama Kombani naweza kumuonea huruma kwani alistukizwa na waandishi wa habari na kwa bahati mbaya hajawahi kuiona hata katiba yenyewe! Si mnajua teuzi za Jk hazifuati merits! Ningekuwa Judge Werema ningejiuzuru kwa kulinda heshima yangu pamoja na taaluma yangu! Ni jambo la kushangaza, inakuaje ofisi ya Mwanasheria Mkuu isijue imemshauri nini Rais? Je kikwete kashauriana na nani kufikia uamuzi huu? Jambo hili linazua utata zaidi juu ya namna serikali inavyoendeshwa!
 
Niridhani labda nitasikia hili la dowans mbona hasimi hayo mabilion nani anayelipwa? Hili la katiba kweli kalipatia.
 
Ifuatayo ni dondoo kutoka hotuba ya Kikwete kwa Taifa ya kufunga mwaka:

Ndiyo maana tukaamua kuanzisha mchakato huu na kwa ajili hiyo, nimeamua kuunda Tume maalum ya Katiba, yaani [/SIZE][/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]Constitutional Review Commission. [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]Tume hiyo [/FONT][FONT=Palatino Linotype, serif]itakayoongozwa na Mwanasheria aliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali katika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano. Jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato utakaowashirikisha wananchi wote bila kubagua, vyama vya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetu kote nchini, katika kutoa maoni yao juu ya wayatakayo kuhusu Katiba ya nchi yao.[/FONT]

hapa penye red napata wasiwasi ..., did he have to tell us who is credible to do this piece of job ...., au ameshamchagua wa kuchakachua constitution review process ...., i think credibility ya head of constitution review commission will be commended after the job is well done
 
Mi nimepoteza Imani kwa asilimia mia moja kwa Kombani na Werema. Hawa tayari wametia doa timu ya JK na wameonyesha kushindwa na kajaribio cha awali cha uongozi wao. Wameonyesha hawajatulia na hawako makini na hakika hiki ni kipimo tosha kwamba uwezo wao wa kufikiri na kuamua kwa maslahi ya Taifa una mushkeli. Kombani arudi SUA na werema akaendelee na kazi zake za mtaa kwa mtaa hafai kuwepo katika nafasi nyeti namna hiyo.
 
Mkuu,

Mimi pia leo nimehitimisha kuwa CCM wameiteka nyara rasmi hoja ya Katiba Mpya.
Sasa wale wapiga kelele inawabidi watafute issue nyengine .

Kwani hata maandamano ya kudai katiba yameshakosa nafasi baada ya kauli ya Mkulu.
Maandamano yataitwa uchochezi, kutaka kuvunja amani na utulivu.


Amesema ataunda tume, lakini hakusema ataiunda lini.
That means time frame haipo....Lakini pia tume itawasilisha mapendekezo sehemu inayohusika na maamuzi yatafanya, pia kuamua lini ianze kutumika.

Ufahamu wangu ni kuwa kinachokuja ni utiaji viraka wa hii iliyopo,
Lini tume itateuliwa, hakuna anayejua...
Muda gani tume itatumia kufanya kazi zake..hakuna anayejua..
Lini hiyo katiba itakayopendekezwa na kupitishwa hakuna anayejua lini itakuwa tayari na lini itaanza kutumika.
Mwishowe hiyo tume itapeleka,itakabidhi mapendekezo yake kwa nani? kwa chombo gani? Jee kuna anayejua?

Tunaweza kufurahia kauli yake kama tulitaka tu kusikia anasema nini, lakini ameacha masuali mengi kuliko kutolea majibu.

NONDA, kwa kweli umeuliza maswali ya msingii kabisa.. mimi tatizo langu kubwa ni timeframe na process.. nani ataidhinisha nini na lini na asipotekeleza nini kitafanywa dhidi yake.. cha kushangaza watanzania walio wengi tutashindwa kujiuliza maswali ya msingi kama aliyouliza NONDA. natamani wachambuzi wa habari ... narudia wachambuzi wa habari na si waandishi wa habari watumie issues alizo-raise Nonda kuzindua jamii ya watanzania!!

Happy new year!!
 
Kwa hakika thinking aloud sijaona kiongozi aliyekosea.

Kombani - Amejibu issue ya katiba kwa information zilizokuwepo wakati huo.
Pinda--tutamshauri Rais...na amefanya.
Werema--> he think reviewing the current constitution and see either create new or make ammendment.
Rais---> note amesema anaunda "Constitution Review Commision" --- What does this mean, kwamba tume ndio itasema kipi kitendeke vilaka au mpya kabisa baada ya kusikiliza what wananchi see missing or to be added.

In short hakuna aliyesema kunahitajika katiba mpya only that tume itatuambia... which will be best fit.
 
Back
Top Bottom