Hotuba ya Rais Kikwete Sept 30, 2012

Leo rais kalihutubia taifa na kwa Mara ya kwanza kazungumzia japo bila kusema neno 'pole' kwa Familia ya Mwangosi, ila yeye kazungumzia kuhusu polisi na matumizi ya nguvu na pia polisi watendewe haki.

Kutokana na Kauli Yake kuwa polisi watendewe haki, ukitazama kwa kina hayo maneno utaona kuwa kwake hakuna hatua za kuchukuliwa zaidi na hakuna wa kuwajibishwa tena, kwani tayari mmoja yuko mahakamani, na kuwa hatari amefikishwa mtuhumiwa bila kujali alikuwa anatekeleza amri kutoka kwa nani.

Sasa swali la kujiuliza, hivi Kamati ya Nchimbi inaendelea kufanya kazi gani wakati mwenye jukumu Anaona Kama kazi imekamilika? Will Nchimbi's committee be able to present its findings regardless the statement of the boss?

Nawashauri Wenye kulinda heshima zao kwenye kamati hiyo Wajitoe Mapema kwani naona aibu kubwa mbeleni itawakumba...
 
Hashawishi kutokufanya maandamano anashawishi kutokufanya fujo kufikia uvunjifu wa amani. Anashawishi kutowabughudhi wa vyama vingine wanapohudhuria mikutano ya kisiasa. Anashawishi amani na utulivu na kutofautiana kwetu kuwe ni chachu ya kutupelekea kwenye amani zaidi.
zomba, Rais ame-site mfano wowote wa kutokuelewana kwetu huko anakokusisitiza? Ama anaongea kama kipofu, au ni mjenga halafu anadhani hatuujui ujenga wake? Yaani watu wamekufa, hakerwi na watu wake kufa, anahukumu kuwa mwananchi wake kafa kwa uzembe wake wakati akivunja amani?
Amani inalindwa kwa sheria ipi? Kuua ni kosa kisheria. Kuvunja amani ni kosa gani? Zomba ukiiba mihogo kwa sababu ya njaa, utashitakiwa kwa kuiba mihogo, njaa haitakuwa kisingizio wala utetezi wako zomba!!!!!!

kwa staili hii, ccm inathibitisha kuwa haina tena uwezo wa kutuletea kandideti afaaye kukaa magogoni. TUNAHITAJI MUAJIRIWA WETU AFANYE KAZI TULIYOMTUMA NA MAMLAKA TUKAMPA.
 
Last edited by a moderator:
Keshawasafisha polisi,na yeye ni amiri jeshi mkuu.Kamati ya Nchimbi haina maana na ni upotevu wa pesa za wananchi.

Pili, since hajaonyesha kuwa neutral, ni wazi ni kama ameingilia kazi ya kamati hiyo.

Mwisho, kuna pahala nimesoma akisema kwamba askari aliyuwa tayari keshafikishwa mahakamani, na akasema tu wasiwe wanatumia nguvu za ziada,sasa tutegemee kamati iseme tofauti na yeye?

Kweli rais huyu ni janga la Taifa, na hii miaka iliyobaki hadi 2015 ni mingi sana kwa mwendo huu! Kiukweli ni kama ameilaumu chadema. Kumbe yale yanayozungumzwa humu na kina zomba ndo vile na yeye anaamini? Ukimya wake ulikuwa una walakini.

Ama kweli mh rais ana roho kutu!
 
Last edited by a moderator:
BIHECHITII najua mwaka huu hatuumalizi lazima wakuchukue jumla jumla,
sasa usiponichangia...........!hahahaha.UNATENGANISHA UKOO

Kama Samson alivyochoma mashamba ya ngano kwa kuiwasha mikia ya mbweha nao wakausambaza.
 
Nilishasahau hata kama huwa anahutubia taifa!!!

kiongozi wa nchi anawasifia wazungu kupitiliza, speach yake karibu yote ni kutulainisha tuone ardhi yetu sii mali kama hatutawapa wawekezaji wakubwa wa kilimo na uzalishaji wa mbegu, anayalenga makampuni ya kizungu!!! Huyu mtu ni hatari kwa taifa letu. Hana nafasi ya kuyaongelea ya taifa letu, anasuka dili tukishtuka hatuna ardhi.
 
Kamati ya Nchimbi haina kazi yoyote zaidi ya kufuja pesa bila sababu.Rais alifurahia vile vifo na ameshindwa kujizuia.Amezunguka wee,lakini wapi.Vile vifo labda ndo kwanza alisheherekea.

Ndiyo maana Kamuhanda alikuwa na kiburi akasema hajiuzulu.Kwasababu mauwaji hayo yana baraka kutoka "juu"
 
Sasa kama kachukua hii inchi kilo ya mchele ikiwa 500 hivi sasa ni 2500, sukari kilo 1 ilikuwa inauzwa 300 hivi sasa ni 2600, kilo ya maharage ilikuwa inauzwa 250 hivi sasa ni 2500. Mapinduzi ya kilimo anayo yaongelea ni yapi kama sio siasa zisizo na mashiko? The end is near CCM will be going to hell.

dah hizo bei za mkoa gani mkuu maana ie kanda ya ziwa naona tofauti au my fair plaza?
 
Mie nilipokuta anaongea tu nilizima TV yangu niliona umeme unatumika bila sababu, au shoti ya umeme inawezatokea na TV yangu ikaungua bila sababu yoyote
 
dah hizo bei za mkoa gani mkuu maana ie kanda ya ziwa naona tofauti au my fair plaza?
..Hizo bei za bidhaa (Sasa kama kachukua hii inchi kilo ya mchele ikiwa 500 hivi sasa ni 2500, sukari kilo 1 ilikuwa inauzwa 300 hivi sasa ni 2600, kilo ya maharage ilikuwa inauzwa 250 hivi sasa ni 2500. Mapinduzi ya kilimo anayo yaongelea ni yapi kama sio siasa zisizo na mashiko? The end is near CCM will be going to hell)ni kubwa sana ama kidogo? upo nchi/mkoa gani? funguka
 
Kamati ya Nchimbi haina kazo yoyote zaidi ya kufuja pesa bila sababu.Rais alifurahia vile vifo na ameshindwa kujizuia.Amezunguka wee,lakini wapi.Vile vifo labda ndo kwanza alisheherekea.

Ndiyo maana Kamuhanda alikuwa na kiburi akasema hajiuzulu.Kwasababu mauwaji hayo yana baraka kutoka "juu"

Kwa ujumla jamaa ni kama kasema yaliyopita si ndwele ila bado tunawaandama kupitia polisi.
 
Kwa ujumla jamaa ni kama kasema yaliyopita si ndwele ila bado tunawaandama kupitia polisi.
Mkulu hakutakiwa awe rais,hilo siyo siri.Rais gani anafanya na kuongea ujinga kama hivi.

Kwanza mwanzoni alitakiwa ayalaani yale mauwaji,awape pole wafiwa.Atoe onyo kuwa matumizi ya nguvu hayatakiwi especially kwa wananchi wasiokuwa na silaha.

Halafu labda aseme wataangalia kuhusu training ya maofisa wa polisi kuhakikisha kuwa wako well equiped kulinda amani na si kufanya mauwaji.

Yeye amesema eti polis hao hawana tofauti na polisi wengine duaniani.Binafsi sijawahi kuona hayo ya polisi kulipuwa wananchi.Na hata ya kuwapiga risasi,huwa hayatokei kwenye shughuli za kisiasa.NI mambo ya crimes etc.

Pia yeye kama rais,ameshindwa kumwajibisha yule kamanda?Mkuu wa polisi wa mkoa?Huyu mtu ni janga kubwa kabisa kwa taifa.
 
..Hizo bei za bidhaa (Sasa kama kachukua hii inchi kilo ya mchele ikiwa 500 hivi sasa ni 2500, sukari kilo 1 ilikuwa inauzwa 300 hivi sasa ni 2600, kilo ya maharage ilikuwa inauzwa 250 hivi sasa ni 2500. Mapinduzi ya kilimo anayo yaongelea ni yapi kama sio siasa zisizo na mashiko? The end is near CCM will be going to hell)ni kubwa sana ama kidogo? upo nchi/mkoa gani? funguka

Kama hali ndo hiyo huku mwanza sukari 2000 mchele 1500 nk yani bei izo kubwa sana aisee mtu anaweza hama mji na nahisi ni Dasilama hiyo kazi mnayo
 
Nasinzia mwenye attachment atutumie tusome asubuhi, JF ni ugonjwa flani maana mtu unajipinda utasema unaandika Proposal kumbe busy na JF mpaka usingiuzi na kama familia imesafiri ndio kabisa. TUNAOMBA ATTACHMENT
 
Keshawasafisha polisi,na yeye ni amiri jeshi mkuu.Kamati ya Nchimbi haina maana na ni upotevu wa pesa za wananchi.

Pili, since hajaonyesha kuwa neutral, ni wazi ni kama ameingilia kazi ya kamati hiyo.

Mwisho, kuna pahala nimesoma akisema kwamba askari aliyuwa tayari keshafikishwa mahakamani, na akasema tu wasiwe wanatumia nguvu za ziada,sasa tutegemee kamati iseme tofauti na yeye?

Kweli rais huyu ni janga la Taifa, na hii miaka iliyobaki hadi 2015 ni mingi sana kwa mwendo huu! Kiukweli ni kama ameilaumu chadema. Kumbe yale yanayozungumzwa humu na kina zomba ndo vile na yeye anaamini? Ukimya wake ulikuwa una walakini.

*Ama kweli mh rais ana roho kutu!
DHAIFU ni DHAIFU tu hakuna siku atakuja na suluhu yakueleweka ndo busara za KILAZA hizo mara zote ni upumbavu,maana husema jambo kinyume na ukweli hali ya kuwa anajua ukweli na kuuficha,kadanganya MABWEPANDE na KINA IGONDWE+RAIA wa kenya,Vitu vizito vinavyorushwa toka mbali,leo anadanganya na hili,kweli haya MAJANGA mpaka 2015!
 
Keshawasafisha polisi,na yeye ni amiri jeshi mkuu.Kamati ya Nchimbi haina maana na ni upotevu wa pesa za wananchi.

Pili, since hajaonyesha kuwa neutral, ni wazi ni kama ameingilia kazi ya kamati hiyo.

Mwisho, kuna pahala nimesoma akisema kwamba askari aliyuwa tayari keshafikishwa mahakamani, na akasema tu wasiwe wanatumia nguvu za ziada,sasa tutegemee kamati iseme tofauti na yeye?

Kweli rais huyu ni janga la Taifa, na hii miaka iliyobaki hadi 2015 ni mingi sana kwa mwendo huu! Kiukweli ni kama ameilaumu chadema. Kumbe yale yanayozungumzwa humu na kina zomba ndo vile na yeye anaamini? Ukimya wake ulikuwa una walakini.

Ama kweli mh rais ana roho kutu!

Rais katika hotuba yake ameegemea kutetea mauaji ya raia yanayofanywa na polisi, na mbaya kwa kusema "polisi watendewe vizuri," hii ina maana gani wakati polisi wana kinga ya kujilinda wakati raia hawana kinga ya kujilinda wanapouawa na polisi? Rais hana uchungu na wapiga kura wake wanaouawa na jeshi lake?

Je, ni makosa kumtafisiri Rais katika hotuba yake ya leo kwamba polisi katika mauaji yake walikuwa wanatekeleza amri yake?
 
Sehemu ambazo nilitegemea JK angerudisha angalau imani ndogo kutoka kwa wananchi, lakini yeye ndiyo kwanza anazidi kujididimiza.
Basi bana huyu jamaa hawezi kubadilika.
 
Back
Top Bottom