Hotuba ya Rais Kikwete kwa watanzania mwezi Septemba 2011

Huna cha kusema? soma hapa kuhusu jitihada za umeme wa uhakika, ambapo hakuna Rais yoyote tangu tupate Uhuru anaejitahidi kwa dhati kutatua tatizo la umeme zaidi ya Kikwete: Home

JK katatua tatizo zaidi kivipi wakati mgao umeshamiri kuliko kipindi chochote kile?

Mahaba uliyonayo juu ya JK yamekupofua.
 
Huna cha kusema? soma hapa kuhusu jitihada za umeme wa uhakika, ambapo hakuna Rais yoyote tangu tupate Uhuru anaejitahidi kwa dhati kutatua tatizo la umeme zaidi ya Kikwete: Home

Sidhani kama kuna mtu anamlalamikia Kikwete as individuals kinachozungumzwa hapa ni yeye na wote waliomtangulia... miaka 50 tunayosema hatumaanishi Kikwete pekee ni wote waliopita yaani MKAPA, MWINYI na MCHONGA. na ndo maana tunasema hana lolote kwani hata yeye aliahidi maisha bora na akatoa pesa za KIKWETE lakini zikaishia mikononi mwa Ridhwan na familia ya rafiki zake, huku watanzania tulio wengi tukizisikia tu kwenye vyembo vya habari...
 
TBC1 imetangaza kwenye taarifa ya saa 2 usiku kwamba rais Kikwete atahutubia taifa: Hii hapa Taarifa Hotuba yake. Pekua chini kwa hotuba yake kimaandishi.

amesahu mengine ngoja niyaongeze " Basi nimekwea pipa nikatua kwa Obama , nimekutana na washikaji kibao, si mnamjua yule actor .... ,nilipiga nae picha, aha kuna mademu wakali huko, vimini vimini Bwana, misosi ya uhakika ,nimepiga picha na...., nikawaonyesha na mimi najua piga porojo,
 
Last edited by a moderator:
ndugu yangu hajapata mkopo wa chuo halafu huyu boya analeta porojo. Hotuba mavi matupu aaaarrrgggghhh bora 2015 ifike aondoke TUMECHOKAAAAAA
 
jipya hakuna, tunashukuru kwa hotuba
Sasa kama Mkuu wa nchi anatoa Taarifa ya safari yake na mambo yaliyotokea, ambayo wananchi wameshayasikia kupitia vyombo vya Habari, kuna maana gari yeye kuwa na wasaidizi?

Nilitegemea akiwa mkuu wa nchi angetoa chachu au michanganuo ya mipango ya maendeleo, at least on a monthly basis....yani malengo yetu kuanzia hii Octoba yawe nini?

Nilitegemea Rais angegusia nchi yetu inajiandaa vipi na possible economic meltdown, kufuatia matatizo katika sector ya fedha huko Ulaya.....mana madhara yake yatafika Tanzania sooner than later....

Mambo kama haya na jinsi gani uchumi wetu unaendelea, huyu jamaa haongelei kabisa.... nadhani ni kupoteza muda kusikiliza reporti zake kama vile yeye ni msaidizi wa raisi.
 
Safari ya marekani imembadilisha kidogo namna ya kufikiri, maana hotuba hii angeitoa kabla hajaenda marekani ingekuwa tofauti na ilivyo leo.

Zite heshima alizopewa na wazungu kule zinamfikirisha asije haribu jina tena.
 
Sasa kama Mkuu wa nchi anatoa Taarifa ya safari yake na mambo yaliyotokea, ambayo wananchi wameshayasikia kupitia vyombo vya Habari, kuna maana gari yeye kuwa na wasaidizi?
Nilitegemea akiwa mkuu wa nchi angetoa chachu au michanganuo ya mipango ya maendeleo, at least on a monthly basis....yani malengo yetu kuanzia hii Octoba yawe nini?
Nilitegemea Rais angegusia nchi yetu inajiandaa vipi na possible economic meltdown, kufuatia matatizo katika sector ya fedha huko Ulaya.....mana madhara yake yatafika Tanzania sooner than later....
mambo kama haya na jinsi gani uchumi wetu unaendelea, huyu jamaa haongelei kabisa.... nadhani ni kupoteza muda kusikiliza reporti zake kama vile yeye ni msaidizi wa raisi.

Kwangu sijaona kitu kibaya alichoongea, maana vyombo vya habari havikawii kuchakachua ukweli wa kilichojilia na kwa mfululizo wa mantiki aliyosema. Kwa mtazamo alionao kama atafikiria kuiweka nchi mahali pazuri mfano wa Zambia anatakiwa aendelee kuiangalia Tanzania kama taifa na si kama tanzania ni CCM.

Hapa leo hajaongelea ya vyama ila ya taifa, ndilo tunalotazamia. Kwenye ukweli tuwe wakomavu kuelewa na tutamtia moyo kuliko kubeza hata chema cha manufaa kwa taifa letu.
 
Wewe kwenu ni wapi? kuna watanzania wangapi wanahitaji uraia wa nchi mbili? yaani umefurahishwa na nini wewe hapo? acheni kuwa wabinafsi. Kama aliwajibu akiwa huko ilitosha maana huko ndiyo kwenye hadhira iliyopaswa kusikia kuhusu mambo ya uraia wa nchi mbili sisi tulioko Bagamoyo,Mgeta,Chalinze na Mlandizi hii haikuwa habari ya kutuambia!
Mkuu huyo ni Mwita25 usihangaike
 
Kwangu sijaona kitu kibaya alichoongea, maana vyombo vya habari havikawii kuchakachua ukweli wa kilichojilia na kwa mfululizo wa mantiki aliyosema. Kwa mtazamo alionao kama atafikiria kuiweka nchi mahali pazuri mfano wa Zambia anatakiwa aendelee kuiangalia Tanzania kama taifa na si kama tanzania ni CCM. Hapa leo hajaongelea ya vyama ila ya taifa, ndilo tunalotazamia. Kwenye ukweli tuwe wakomavu kuelewa na tutamtia moyo kuliko kubeza hata chema cha manufaa kwa taifa letu.

Sawa lakini ni suala gani alilolitoa lenye tija kwa taifa? Kutoa taarifa ya yaliyotokea, most of which ni personal...vitu kama tuzo etc vinasaidia vipi kurudisha umoja wa kitaifa?

Anapoongelea mambo ya watanzania waishio Marekani, je yanawagusa vipi wananchi wa kawaida walio Tanzania ambao ndio wanaoteseka?
Yeye kama raisi natarajia awe mtu anayetoa au kuchgagisha discussion ya mambo yenye tija kwa maendeleo ya watanzania wengi ambao wanateseka kwa kukosa huduma muhimu.

Sijakataa yeye kutoa taarifa alichofanya, lakini unapo adress umma wa watanzania wana wanatarajia kuona mtazamo wake kama rais katika kutatua mambo mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Kwa kifupi hotuba ilikosa msisimko wa kuwafanya watanazania waongeze nguvu kufikia malengo ya kitaifa mana imegusa vitu ambavyo wananchi wengi haviwagusi...huu ni mtazamo wangu anyway!
 
Huna cha kusema? soma hapa kuhusu jitihada za umeme wa uhakika, ambapo hakuna Rais yoyote tangu tupate Uhuru anaejitahidi kwa dhati kutatua tatizo la umeme zaidi ya Kikwete: Home
Faiza nakuunga mkono! JK ndiye rais anayejitahidi kuliko waliopita wote(mimi ni mfuasi mkubwa wa Nyerere) kuhusu suala la nishati, unless mtu uwe na ushabiki.
Miradi mingi ya nguvu za umeme imesainiwa chini ya JK, tuacheni ushabik.
 
JK katatua tatizo zaidi kivipi wakati mgao umeshamiri kuliko kipindi chochote kile? Mahaba uliyonayo juu ya JK yamekupofua.

Mgao wa umeme uiopo leo Tanzania unatokana uongozi na viongozi waliokuwepo hapa miaka iliyopita, walikuwa hawana muono wa kuona kesho. Soma link niliyokuwekea uone JMK anafanya nini cha kusaidia njia za umeme za miaka ijayo.
 
meli ya MV Spice Islander iliyokuwa na watu wengi na shehena kubwa ya mizigo.



Tupe tarakimu bwana wewe. Rais mzima mpaka leo haujapata hata wa kukutonya idadi kamili. Can you be serious?


Kwa kweli hatujui kwa uhakika kama wapo watu waliozama pamoja na meli hiyo au hapana. Bahati mbaya idadi kamili ya watu waliokuwamo katika meli hiyo haijulikani kwa uhakika.


Kama haujui kwa nini Tanzania ni masikini utajua nini wewe kuhusu meli iliyozama baharini, kina kirefu?



Orodha rasmi ya wenye meli inaonesha idadi ya watu waliokuwemo kwenye meli wakati inaondoka bandari ya Malindi, Zanzibar kuwa pungufu kuliko idadi ya watu waliookolewa na maiti waliopatikana. Kwa sababu hiyo, huenda wapo watu waliozama na meli na kushindwa kutoka.



kweli kama ulivyosema Watanzania ni majuha. Au wewe siyo Mtanzania?

kwani meli ni dala dala kwamba kuna watu walidandia huko mbele ya safari hata idadi ya waliotoka Bandari ya Malindi ikawa ndogo kuliko idadi ya waliokufa na kuokolewa.

Wana hasara waliokupigia kura, na kwa kweli wasaidizi wako na waandaaji wako wa hotuba ni vilaza.


Safari ya Marekani

Sijaona ukitaja ulivyopiga picha na yule mlanguzi wa dawa za kulevya mstaafu a.k.a 50 Cent.






Na wanaodhani kuwa tunatania wathubutu, watadhibitiwa ipasavyo.
kiongozi dhaifu kama wewe siku zote hutumia vitisho. Waambie wajaribu kuchakachua. Hapo ndiyo utajua kwa namna watu walivyokuchoka wewe na chama cha mafisadi.



Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa Kunisikiliza.




acha unafiki bwana wewe. rushwa na umasikini kila kona tutabarikiwa vipi?
 
Mi naona hii hotuba hainihusu maana cjui haya mambo ya marekani yatanisaidia nini wakati cn umeme,sukari bei juu, dowans wanachukua bilioni zao ye anajisifia na tuzo. Je anaweza kutupa mchanganuo wa gharama alizotumia yeye na syndicate yake kwa siku zote alizokaa marekani? Ati uraia wa nchi mbili utatusaidia nini sie kapuku ambao ndo tuko wengi hata kutoka nje ya mkoa hatuwezi?

Hotuba haina hata the way foward. Baba bora ukae kimya tu maana naona huna hata plan ya kesho unaongoza kwa kufuata matukio tu. Amezungumzia ajali na tume but hajazungumzia serikali ina mkakati gani kuepusha ajali kama hizi tena. Na kuhusu Igunga inashangaza hv hakuna uandikishaji mpya wa wapiga kura?

Wangapi wamehamia,wamekufa, wametimiza miaka 18, wamepoteza vitambulisho na wana haki ya kumchagua mbunge wamtakae? Serikali nzima imehamia igunga kuna nini hasa behind hilo jimbo? Mawaziri wanatoa ahadi hewa kule Igunga wakati bajeti tumeisikia. Jamani sasa umefika wakati tuseme basi inatosha 2015 is very far tukiamua tunaweza na hata sasa.
 
Pananitatiza pale kwenye red: Hajui au anajifanya hajui hali halisi. Orodha ya wapiga kura ni ileile ya mwaka jana hivyo kuna maelfu ya watu (vijana) waliotimiza miaka 18 katika kipindi cha takriban mwaka mmoja uliopita hawamo katika orodha, kwa sababu NEC haiikufanya utaratibu wa kuwaandikisha.

Pili kuna maelfu pia ambao wamepoteza kadi zao za uandikishaji ambao hawataweza kupiga kura kwa sababu NEC haikufanya utaratibu wa kuwapatia kadi nyingine.

Sasa hiyo haki ya Kikatiba iko wapi?

Baba kwani wewe ni mpiga kura wa Igunga?
 
Nasikitika kwa hotuba iliyojaa chai na mambo yasiyo kipaumbele kwa wananchi wa TZ. Namshauri atafiti nn wananchi wanataka kusikia kutoka kwa raisi ndio aandae hotuba
 
jipya hakuna, tunashukuru kwa hotuba
Shantel jipya lipo bwana. Jamaa kwa mara ya kwanza bila ya kigugumizi amemuita Julius Kambarage Nyerere kuwa ni Baba wa Taifa.
Kweli shinikizo la JF ni kiboko kwani ni humu ndani ndimo watu walikuwa wanajiuliza ni kwa nini jamaa hamuiti Kambarage baba wa Taifa.
 
Back
Top Bottom