Hayo mambo wakiyasema wapinzani utasikia wazushi wakati yalitakiwa kuwa addressed na rais mwenyewe ili kuondoa hisia potofu..............Wakuu tuwe wazi kabisa,mbona inatia hasira? wapi mambo yafuatayo?
Yani hotuba nzima imejaa safari ya marekani wakuu,full kujisifia sifa zisizo na tija wala manufaa kwa watanzania? Ndio maana watu wengi wameacha kusoma au kusikiliza hotuba za huyu jamaa...Kuna nini hapo cha kuleta matumaini? Jamani huyu jamaa tumfanyaje?
- Kupanda gharama za maisha...
- Kupanda kwa bei ya mafuta kila siku....
- Malipo ya Dowans na mikataba mengine feki...
- Ajali za kila siku(hili sio kificho,kila siku watu wanakufa hii nchi kwa ajali)
- Matatizo ya umeme yasiyokwisha....tulidanganywa kuwa mwezi wa 9 mgao utapungua,badala yake makali ndio yanaongezeka..
Najutia muda wangu niliokaa kumsikiliza na kusoma hotuba hii....
Hotuba nzuri sana, amejitahidi kuelezea juu ya uraia wa nchi mbili kitu ambacho kimekuwa kikisumbua sana wananchi. Nadhani baada ya hii hotuba watu watakuwa wameshapata majibu ya matatizo yao mbalimbali.
Pili, niliwataka wasisahau nyumbani kwao. Wametoka huku nyumbani kwenda nje kuchuma ili wajiletee maendeleo. Wakumbuke kujenga nyumba nzuri kwao ili wawe na mahali pazuri pa kufikia. Wakati mwingine kukosa mahali pazuri pa kufikia kunawafanya wasije nyumbani au wakija waishie mjini kwa sababu nyumbani kwao hakuwafai kwa viwango vyao. Aidha, niliwataka wasaidie kuwaendeleza wazazi na ndugu zao kwa elimu au hata kwa misaada mingine ya kuwaendeleza kiuchumi na kuwapatia kipato.
Nawachukia wale wote wanaosema eti tunasherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania/Tanzania Bara. Ni wa kuogopwa kama UKOMA.
TBC-Televisheni ya Taifa inapotoa tangazo, halifanyiki na hawatoi ufafanuzi tuwaeleweje?Sisi kama watanzania tunaihitaji sana hiyo hotuba, tena hotuba inayotoa ufafanuzi wa matatizo ya wananchi na sio kuwatuhumu watu au vyama juu ya vitu fulani.
Jaman mi nadhani tunakuwa wepesi mno kusahau, Rais alisha sema yeye mwenyewe hajui kwanini Tanzania ni maskin, sasa kama Rais hajui tatizo la nchi yake, mnadhani atatatua tatizo gani hapo wakati haelewi tatizo ni nini?Hii siyo hotuba ya rais, nashindwa kuamini kabisa. DACOTA na uraia wa nchi mbili unawhusu watu asilimia ngapi ya wa Tanzania. Watanzania wengi sasa wanakabiliwa na matatizo mengi sana ambayo halitakiwa hayatolee maelezo.
Mkuu Unamaanisha NEC? Maana yake Watu niliofanikiwa kuwauliza walisema hawakumchagua!Watu waliomchagua JK 2010 kweli wametuingiza mkenge.......!
Umeme wa uhakika utapatikana DICOTA sijui? kwenye eneo linalohusu kuchakachua na kulazimisha sifa kwa CCM wasizostahili wanakuwa wa kwanza kutolea maelezo na mikwara lakini mambo ya maana yanayomgusa kila mtanzania ya kila siku kama kutokuwa na huduma za uhakika za maji safi,umeme,kupanda kwa bei za bidhaa mbali mbali,kushuka kwa thamani ya shilingi na mambo mengine ya maana huwasikii wakiyatolea maelezo.
Nahisi dhumuni la hii hotuba ya leo ilikuwa kupiga mkwara wa Igunga basi lakini hayo mengine hayamhusu moja kwa moja Mtanzania anayeishi Kasulu,Mwembetogwa,Marangu au Loliondo.Nchi hii ina safari ndefu sana kufikia matumaini ya kweli,miaka 4 natamani iishe haraka! Hakika Mungu atatupigania na kama taifa tutatoka katika mambo haya ya sifa za kijinga jinga za tuzo na vitu visivyo na maana kabisa!
Hivi mtu wa kasulu ana matatizo kibao unamwambia uraia wa nchi mbili ili iwe nini? angeyafanya hayo kimya kimya tu basi.aaaaaaaaaaaaaaaaaah
wewe ndio wa kuogopwa kama ukoma. wewe hujui kwamba tulipata uhuru toka kwa mwingereza tokea tisa desemba 1961
jipya hakuna, tunashukuru kwa hotuba