Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

  1. Uongo haukusaidii kitu wala kupindisha maneno hakukufanyi uwe huru. saba yamekubaliwa moja limekataliwa yaliobaki nusu nusu.
  2. Hakuna kinyongo hapo, kasema wazi wazi, mishahara wanayotaka hakuna, kilichoongezwa ndio hivyo kimeongezwa, ukitaka fanya hutaki acha, uamuzi ni wako si wa Kikwete. Mshahara wa kuanzia million 3.5 hakuna.
  3. Swala la Ulimboka haliachi mpaka ukweli ujulikane. Unaogopa nini?
  4. Hotuba imepitia mambo yote 12 ya madai ya madaktari.

wapi umeona amefafanu swala la uboreshwaji wa huduma za afya kama alivyozingumzia stahili za madaktari?
swala la ulimboka akae kimya kabisa na hotuba yake inaonyesha jinsi alivyoshiriki kumdhuru ....hata umtetee vip ihotuba yake ni ya hovyo sana
 
Naona maendeleo Tanzania,siku hizi MHESHIMIWA RAISI anahutubia kupitia Mjengwa blog!

amerekodi leo asubuhi saa mbili na robo..kisha akaoga na kupanda ndege kuelekea rwanda..kwenye runinga itaonyeshwa usiku.
 
Ukiiangalia kauli yake kwa undani utagundua kuwa ni kauli ya kibaguzi. Confirmed JK ni mbaguzi kwa kwenda mbele, naona silaha yake ya ubaguzi wa kidini na kumtumia Sheikh Ponda haifanikiwi sasa analeta ubaguzi wa huyu mtumishi wa serikali na yule sio ili wabaguane, bahati nzuri madaktari wanaunganishwa na taaluma tofauti na mawazo yake kudhani wanaunganishwa na ajira au fedha au itikadi za kisiasa. Natamani US wamlime barua nyingine
Hata wewe ukiwa na kijana wako wa ng'ombe halafu siku ya kudai nyongeza ya posho akaja na mpambe ambaye hahusiki, it takes mtu mvumilivu kukaa kitako na kumsikiza huyu kihelehele.
 
kwa mujibu ya hotuba hii kiwete anahusika sana na kilichomtokea Dr. ulimboka...anajifnya kuongea kwa machungu na kuguswa lakinih hovyo ...''Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.''

Hapa naona lugha yake iko cynical zaidi.
 
Huna hoja.

Waliyokubaliana kayasema na ambayo serikali imekataa na hayo kayasema waziwazi na ambayo hawajakubaliana kayasema waziwazi na kasema asiyeyataka hayo ambayo serikali imeyakataa aache mwenyewe kazi. Nini zaidi usichokielewa?

Kama huna hoja kaa kimya kama wenzako.
Kacheze mdundiko, mnanda, bao na kunywa kahawa..huko ndio utakutana na wenzako wenye akili kama zako ndio utatetee hii hotoba, sio hapa JF
 
hii hotuba yake imejaa kuonewa huruma na wananchi walio wajinga lakini werevu na wapembuzi tushajua kuwa hotuba ya mwisho wa mwezi wa 6 ni changa la macho...
 
SEHEMU YA HOTUBA YA JK YA 30/06/2012
Suala la Dkt. Steven Ulimboka
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Steven Ulimboka usiku wa tarehe 26 Juni, 2012. Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.
Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa kiungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na Madkatari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.

Ndugu Wananchi;
Kama nilivyoeleza, mazungumzo yalienda vizuri na mafanikio makubwa yamepatikana. Yapo maeneo machache na hasa eneo la mshahara ambalo hatukuweza kukubaliana. Hapo tulipofikia si pabaya na tulikubaliana sote kurudi kwenye mkondo wa Sheria kusaidiwa. Kwa nini Serikali imdhuru Dkt. Ulimboka? Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha mgomo. Anayekaidi amri ya Mahakama ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo. Hivi baada ya kufika hapo Serikali iwe na ugomvi na Dkt. Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo lipi hata iamue kumdhuru? Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali.

Ndugu Wananchi;
Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali natoa mkono wa pole kwa Dkt. Steven Ulimboka na kumuombea apone haraka ili aungane na familia yake na Watanzania wenzake katika ujenzi wa taifa. Kwa namna ya pekee namshukuru na kumpongeza Bwana Juma Mgaza, kwa moyo wake wa huruma na upendo na kwa hatua alizochukua za kumsaidia Dkt. Ulimboka.
Naomba kumaliza kwa kuwasihi madaktari kuacha mgomo na kurejea kazini. Watanzania wenzenu wanateseka na kupoteza maisha. Muwe na moyo wa huruma na upendo na msaada kwa wagonjwa kama kiapo chenu kinavyowataka.


Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa Kunisikiliza.


WAKUU, HEBU TUJADILI HII

SOURCE: HOTUBA YA JK YA 30.06.2012 KWA MUJIBU WA MICHUZI BLOG




Mbona wale majambazi walomuua mgeni( Mtalii) Serengeti serikali ilipeleka mpaka wanajeshi na wakakamatwa ndani ya siku tano. Why not this issue ? So disappointed with this so called Government Of united republic of Tanzania
 
Hapa naona lugha yake iko cynical zaidi.

kwanza anawanga madaktari waajiriwa wa serikali kuwa hawajui kuongea na kulinda na kudai maslahi yao hivyo akaona huyu wa nje(dr ulimboka) kwa kuwa yeye ndio mtetezi na hakubali kuhongwa wala kununuliwa ..basi mkuu wa kaya akaagiza njia pekee ya kumnyamazisha ni costra nostra...sentesi hiyo inaonyesha mkuu wanchi anahusika na swala hili la utekwaji nyara dr ulimboka...
 
Kwa nini swala la kuundwa kwa tume huru kalikwepa wakati amekili serikali kutuhumiwa kwenywe hili swala?

Kweli mtuhumiwa anapewa nafasi ya kujichunguza tutegemee nini kama si upotoshaji wa ukweli?

Kwa tume hiyo ya serikali tutegemee kusikia bado uchunguzi unaendelea
 
Wahamiaji haramu wamekuwa wanaingia nchini kwa kupitia njia zisizo rasmi.
*

Wacha uongo, nyie mliingia kichwa kichwa kwenye swala la EAC mlikuwa mnafikiri nini? Hayo ndiyo matunda ambayo mnayapata. Kama huwezi kumudu swala la mipaka ya Tanzania ambalo umekubali makahaba kuingia kama wanakwenda sokoni unalalamika nini? Kazi ya urais ni ngumu kuliko kuiba kura. Uwezo huna * ..... * *...... *


Watanzania wenzenu wanateseka na kupoteza maisha. Muwe na moyo wa huruma na upendo na msaada kwa wagonjwa kama kiapo chenu kinavyowataka.


Sasa huruma wawe nayo wengine, Je yeye huruma yake ipo wapi wakati mfano Benki kuu wanapotumia fedha za walala hoi kujenga mahekalu wakati kina mama Temeke wanalala chini wakati wa kujifungua?

Huruma yake ipo wapi wakati bei ya umeme anapandisha kama vile wote wana hisa kwenye kampuni ya kuchimba dhahabu?

Huruma yake ipo wapi wakati anawatajirisha Mafisadi kwa kuwawezesha kumiliki njia kuu za uchumi mojawapo ikiwa ni simu za mkononi?

Huruma yake ipo wapi wakati wawekezaji hawalipi kodi muafaka kwa wanachochuma Tanzania?

The list goes on and on *and on *..... .... what a shame!
 
SEHEMU YA HOTUBA YA JK YA 30/06/2012
Suala la Dkt. Steven Ulimboka
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Steven Ulimboka usiku wa tarehe 26 Juni, 2012. Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi ........... ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa......Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. .

Huyu Rais haoni jinsi anavyojikanganya na kusababisha hali mbaya zaidi? Ni heri engenyamaza kimya kama kawaidayake.

1) Ni nini tofauti kati ya serikali na vyombo vya ulinzi na usalama? Kama hakuna tofauti, basi haoni kuwa matokeo yoyote ya mshtakiwa kujichunguza hayakubaliwa wala kuondoa "wingu baya" ambalo hasa ndio msingi wa hoja yake kubwa hapa.

2) Kwa vile Rais anasukumwa zaidi kuitetea serikali (anayoingoza) haoni amekwisha ingilia na kwa namna fulani kushawishi matokeo ya uchunguzi huo (batili)? Haoni kuwa haki na ukweli havina msukumo na nafasi stahaki katka uchunguzi huu? badala yake kusafishwa kwa serikali ndio mada kuu ya kamisheni yake.

3) Kama alivyokiri mwenyewe (kwenye para ya mwisho), ni wazi serikali haikuwa na nia ya dhati wala utashi katika majadiliano na madaktari.

a) Kwa nini? Kwa sababu katika hitimisho lake hilo anawataka madaktari warejee kazini eti wananchi wanakufa......so he's (as expected) interested in the blame game more than critical solution finding.

b) Je mh. Kikwete daktari (hata bingwa) bila madawa, bila vifaa vya tiba mfano majengo na x-rays, bila wataalam (hasa wa maabara), bila motisha anaweza kupunguza vipi vifo? Na je vifo vinavyotokana na uzembe wa serikali yake (ambavyo ni vingi sana na ushahidi upo lukuki mfano ukienda hapo Mwananyamala Hospital tu ) tuitendeje serikali yake?

4) Kwa ukiri wake wa "uwezekano wa mtu wa serikali yake kumdhuru Dr. Ulimboka bila kutumwa na serikali" (pengine kwa vile Uli si mwajiriwa) haoni kuwa yeye ni rais dhaifu, asiyewajibika vema kwa usalama na mustakabali wa wananchi wa Tz ? Je Mh. Kikwete huoni kuwa unathibitisha tetesi za kuwa YOU ARE NOT IN CONTROL? Je ni kwa nini usijiuzulu W.E.F.?

5) Je Mtu wa serikali anaweza kufanya jambo la "faida" kwa serikali bila hiyo serikali kumtuma au hiyo serikali kutokuwa na maslahi au taarifa za awali? (rejea namba 4)


 
Lakini ndiye "mbora" kati yetu, ndo mana tumimchagua. Mtihani ulikuwa mkali kati yake na yule muasi wa kanisa katoliki.

Aliyekusanya vingi hakuzidi wala yeye aliyekusanya vichache hakupungukiwa.Sie twamwomba Rab atujalie paji la imani thabiti, tusadiki kwamba Rab anaweza yote na kwake hakuna lisilowezeka.Aliyezoea umbeya na unafiki utamfahamu tu endelea na udini wako .
 
images

Ndugu Wananchi;

  • Mwaka 2004/2005, mshahara wa kuanzia wa daktari ulikuwa shilingi 178,700/=,
  • mwaka 2005/ 2006 tuliupandisha na kuwa shilingi 403,120/=. Tuliendelea kuupandisha
  • mwaka hadi mwaka mpaka kufikia shilingi 957,700/= wanazolipwa sasa.
  • Kiasi hicho ni mara mbili ya mishahara ya watumishi wa taaluma nyingine wenye shahada ya kwanza wanaoanza kazi ambao kwa wastani hupata shilingi 446,100/=.
Tunafanya hivyo kwa kutambua na kuthamini nafasi maalum ya madaktari katika jamii na ukweli kwamba bado tunayo safari ndefu ya kuziba pengo la madaktari nchini. Lakini inaonekana juhudi zetu zote hizo hazithaminiwi.

Ndugu Wananchi;
Sina budi kusisitiza kwamba tunapofanya hivyo tunaongozwa na uwezo tulio nao wa kulipa.

  • Kwa sasa hatuwezi kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi 3,500,000/= na posho zote zile.
  • Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa shilingi 7,700,000/=. Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari.

Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri.
  • Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo.
  • Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka.
  • Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24.

Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na sheria za kazi na maadili ya kazi ya udaktari.

Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma. Najua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi. Vinginevyo atakuwa anajidanganya kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.

Huu ndio uamuzi Mgumu tunaotazamia ambao Kikwete ametamka leo.
Kauli ya Rais Kikwete imetulia na ameeleza ukweli ambao serikali ilivyochukua hatua na tahadhari dhidi ya madai na migomo ya madaktari. Pia imesaidia kutoa picha upande wa pili ambao wengi hutukuweza kuelewa kwa uwazi. Aliyoongea Rais kwa wenye kujua hali halisi ya uchumi wa nchi yetu na matatizo mengine ameeleweka. Kwa waajiriwa wa serikali wanajua mishahara wanayolipwa.
Dao kubwa hilo la Madaktari la Shilling 7,000,000 lisilozingatia uwezo wa serikali na uboreshwaji wa huduma nyingine za afya na hali kadhalika kutojali uboreshwaji wenye uwiano na idara nyingine za serikali usipishane kwa kiwango kikubwa mno. Ni mambo yale yale yaliyokuwa yanalalamikiwa na wananchi dhidi ya wabunge, kwani wengine wanavyohangaika na njaa wengine wanataka wawe wanaichi kama wako peponi.

Mishahara ya serikali kupandishwa kila mwaka nimeona tu Tanzania, kwani nchi nyingine huchukua miaka mingi hadi kima kipandishwe, kwani upandishwaji wa mishahara ni sababu nyigine inayodhoofisha uchumi na mfumuko wa bei kupanda holela. Ukishapandisha mishahara lazima kila kitu kitapanda, kodi nayo itapanda hakuna unafuu ila ni kuendelea kupiga mark-time. Mfano Marekani kwa wastani wa zaidi ya miaka 15 mishahara imepandishwa mara moja tu kipindi cha utawala wa Rais wa zamani George Bush kutoka $5.15/75 na kufikia $7.25/75 per hour kwa kima cha chini.

Nchi nyingi zina utaratibu kama aliofafanua Rais Kikwete kwamba asiyekubaliana na mshahara basi aache kazi aende kwa mwajiri mwingine ambaye atampa mshahara anaoutaka. Hii ndiyo sababu nchi kama za Ulaya na Marekani utaona watu hawalalamikii mishahara, ila huacha kazi na kwenda kwenye makampuni mengine ambayo hulipa zaidi kidogo. Kutokana na tatizo hilo utaona idara za elimu hasa walimu vyuo vya serikali wamejaa wahadhiri wa kumwaga toka mataifa mengine na kabisa toka Afrika kama nchini Marekani kwa sababu wamarekani hupenda kufundisha vyuo binafsi ambako hulipwa vizuri zaidi na hakuna kodi nyingi kama serikalini.

Madaktari nchi nyingi hawategemei malipo mahospitalini tu, bali wana ziada ya mitandao katika mashirika mengine na zahanati ampako hufanya part time, na huko ndiko wanakopata ziada ya kuendeshea maisha yao. Hata secta nyingine nchi tajiri duniani wafanyakazi hawategemea pato moja tu vinginevyo kuna ziada ya muda wa kazi ambao huwaongezea pato, vinginevyo wanakuwa na pato la ziada kwa kufanya kazi nyingine part time au kujiajiri baada ya kazi.

Kwa ufafanuzi wa Rais Kikwete nakubaliana naye Madaktari ambao hawako tayari wajiondoe na kwenda kwa mwajiri ambaye wanaona atawalipa kiwango wanachokitaka cha kufikia millioni 7 kama wanazolipwa wabunge. Kuendelea kuidai serikali kiwango ambacho serikali haina uwezo ni sawa na kunyonga mzazi wako kumdai zaidi ya uwezo unaomruhusu.
 
Nilikwishawaambia!

Kikwete ni Mdini and is part of Jihad mkakataa. Baada ya kuwaleta hao jihad from Iran mambo yatakuwa Kama ilivyotokea Huko Kenya lea,

Grenade Attacks on Kenya Churches Kill 10


By REUTERS
NAIROBI (Reuters) - Masked attackers killed at least 17 people on Sunday in gun and grenade attacks on churches in a Kenyan town used as a base for operations against al Qaeda-linked insurgents in Somalia.
At least 45 people were wounded in the simultaneous attacks on Garissa, in the north of the East African country which has suffered a series of blasts since sending troops into Somalia last October to crush Somalia's al Shabaab militants.
"We have 17 bodies at the mortuary so far," regional medical officer Abdikadir Sheikh told Reuters.
There was no immediate claim of responsibility.
Police said they suspected the attacks could have been the work of al Shabaab sympathizers or bandits, but it was too early to say. Inside Somalia, al Shabaab declined comment.
"The goons were clad in balaclavas," regional deputy police chief Philip Ndolo told Reuters from Garissa.
He said a total of seven attackers hurled grenades inside the Catholic Church and the African Inland Church and then opened fire with guns. They struck the churches, which are 3 km (two miles) apart, at around 10.15 a.m. (0715 GMT)
Two policemen were among the dead.
They were the latest attacks on Christian worshippers in Kenya after two people were killed in grenade blasts in March and April.
But Sunday's coordinated attacks on churches resembled the tactics of Nigeria's Islamist militant group Boko Haram, which has killed hundreds of people on the other side of the continent.
Other blasts in Kenya have hit nightclubs and bus stations in the capital Nairobi, the coastal city of Mombasa and areas near the Somalia border.
Although a majority of Kenyans are Christian, Garissa is more heavily Muslim.
The town of around 150,000, a market centre for the trade in camels, donkeys, goats and cattle, is largely populated by ethnic Somalis.
"You can imagine for such a small town how the police and medical services have been stretched trying to deal with this," the police's Ndolo said.
Garissa is about 100 km (60 miles) from Kenya's Dadaab refugee camp, where gunmen kidnapped four aid workers and killed a driver on Friday before fleeing towards the border with Somalia.
Last Sunday, three people were killed in a grenade attack at a night club in the port city of Mombasa, a day after the U.S. embassy in Kenya warned of an imminent attack on the city.
(Additional reporting by Noor Ali and Feisal Omar)
■


PUBLISHED 1 JULAI 2012
 
Kumbe nilivyokuwa naelewa kuhusu madai ya madaktari nilikuwa sahihi. Bila ushabiki, nimependa alivyoelezea mgomo wa madaktari
 
Ukiiangalia kauli yake kwa undani utagundua kuwa ni kauli ya kibaguzi. Confirmed JK ni mbaguzi kwa kwenda mbele, naona silaha yake ya ubaguzi wa kidini na kumtumia Sheikh Ponda haifanikiwi sasa analeta ubaguzi wa huyu mtumishi wa serikali na yule sio ili wabaguane, bahati nzuri madaktari wanaunganishwa na taaluma tofauti na mawazo yake kudhani wanaunganishwa na ajira au fedha au itikadi za kisiasa. Natamani US wamlime barua nyingine[/QUOTE]

Mungu wangu! Hivi wakifanya hivyo na weye uliyemchagua si umidhalilishwa pia! kweli njaa mbaya!:redface:
 
Huyu rais wetu sasa anachemka kwa kiwango kilichopitiliza. Sasa amejimaliza mwenyewe! Hivi anadhania akifukuza madaktari option nyingine ya madaktari atapata wapi? Serikali imetumia fedha nyingi sana kusomesha hawa madaktari CREAM OF THE NATION halafu kirahisi tu anasema atawafukuza! Embu afukuze madaktari wote halafu tuone wengine atawatoa wapi na kwa fedha zipi? Labda kama atawakodi kwa pesa zake za mfukoni!

Haiingii akilini gharama kubwa serikali itakayoingia na gharama ya kuwahudumia hao wageni na matatizo ya lugha/communication watakayoyapata hao madaktari wageni! Sidhani kama wabunge wa nchi hii wataridhia upuuzi huo wa kuzidi kuitia serikali katika gharama kubwa namna hiyo wakati ilikwisha invest kwa hawa wazawa! Sijui kama wanaomshauri wamefanya cost-benefit analysis na kujua faida na hasara ya hatua wanayotaka kuichukua.

Mimi namshauri rais atumie hekima na busara kutatua hili suala! Kwanza akae na hao madaktari atekeleze matakwa yao yote angalau kwa awamu. Madaktari ni watu waelewa sana, angalau angeanza na kununua vifaa tiba na madawa kwa awamu kwa kuongeza budget ya vitu hivyo. Pili angeongeza mishahara yao kwa kiasi fulani na si lazima iwe milioni 3.5. Kama kima cha chini kilikuwa ni shilingi laki 9 why asiongeze kufika angalau milioni 1.5 kwa kufanya comparison na nchi jirani viwango vya chini vya mishahara vinavyolipwa madaktari angalau kuwe na uniformity na nchi jirani? Unadhania madaktari wangekataa? Hizo gharama za kununua vifaa, madawa na kuwaongeza mishahara pamoja na matakwa yao mengine kama na nyumba na risk allowances, green cards n.k unadhania zitakuwa kubwa kaliko kuwakodi madaktari wa nje wenye masharti magumu kuliko hawa wazalendo wa hapa ndani?

Angalia hapo Mh. Rais sio unataka kujimaliza wewe mwenyewe na serikali ya chama chako! Hivi unadhania ukijishusha na serikali yako ukawatimizia matakwa yao (tena watumishi wote wa afya) kwa awamu/portions unadhania hili tatizo litaendelea? Hivi ukijishusha ukaonyesha kutimiza matakwa ya madaktari ambayo yako genuine utaonekana wewe ni dhaifu? Amini nakwambia utaonekana dhaifu sana Mh. Rais kama utatunisha misuli na hali kuendelea kuwa mbaya! Amin nakwambiwa utaonekana una hekima na busara kama utatekeleza matakwa yao yote kumi kila moja kidogo kidogo na madaktari wakaendelea na kazi na kutoa huduma kuliko hilo unalolifanya la kutunisha misuli.

Nadhani pia hao washauri wako wasipokushauri kama ninavyokushauri naomba wachukulie hatua mapema especially huyo waziri mpya wa afya na washauri wengine wote wakushaurio kuhusu hilo. Haiwezekani ku-substitute madaktari wote kwa madaktari wageni? Ni gharama kubwa sana na jambo hili halitekelezeki na competency ya hao watu sijui kama inajulikana vizuri na pia compatibility kwa mazingira ya hapa bongo na vitendea kazi feki vya hapa pamoja na mawasiliano.

Hivi unataka uniambie kada ya madaktari na watumishi wengine wa afya sio cream of the Nation? Hivi kada hiyo kweli serikali haijainvest pesa nyingi kusomesha hao madaktari hao n.k. Hivi hao wanaosema kuwa sijui wamdaktari wasiringe na wasideke je wao waseme kiukweki wanaweza waka compare uwezo wao kitaaluma na wa madaktari? IQ za madaktari ziko juu sana na hivyo thamani yao haiwezi kulinganishwa na watu wengine. Ni watu wachacheambao sio madaktari wamepita huo uwezo na ndio maana kwa kuelewa hilo nchi nyingi sana Duniani zinawathamini na kuwalipa fedha nyingi kutokana na ugumu wa elimu waipatayo, ugumu wa kazi zao na pia kwa ajili ya kiwango cha akili kitumikacho katika kazi hiyo na ugumu wa kazi yenye na risk kubwa iambatanayo na kazi hiyo. Nasema ugumu wa elimu hiyo kwa kuanza kumchambua daktari toka alipoanza shule mpaka anapofikia kufuzu. Muda wote ana kazi ya kuongoza darasani kuanzia elimu ya msingi, sekondari mpaka chuo kikuu anapokutana na wakali wenzake ambao ukiwa lele mama shule ya chuo hauimalizi. Sasa itakuwaje madaktari walipwe mishahara sawa na hao waliokuwa wakiwaongoza? Mimi kwa kweli nawaheshimu sana madaktari na wanasayansi wengine kwa uwezo walionao na bidii juhudi na maarifa waliyojaaliwa na mwenyezi Mungu na ugumu wanaoupitia katika shule zao. Mimi binafsi sistahili kupata kiwango sawa na wao. Naunga sana mkono haki wanayoidai, na wale wanaopinga nadhani ni suala la wivu wa kipuuzi baadhi ya Watanzania tulionao. Kama unauwezo na akili ya kama daktari aliyonayo na unaweza kufanya afanyayo daktari kajaribu leo kidogo kukaa darasa moja na daktari halafu mpewe pepa uone utakachopata na daktari atakachopata halafu ndo uthamini kama unastahili kuwa sawa na daktari kimaslahi.

Nchi zilizopiga hatua kimaendeleo zili invest sana kwenye saynsi na wanasayansi wake. Lakini sisi watanzania tuna invest kwa wanasiasa. Sijui kama tutaendelea. Jamani serikali iwathamini madaktari wake badala ya hao wa nje. Iwape value fo money madaktari wake waliogharamia kuwasomesha. Kama kila solution ya kila kitu ktk nchi nchi hii ni ku-import basi serkali yetu haina uhalali wa kuitwa serikali kwani itakuwa imekosa ubunifu na kutegemea akili za nje.

Embu fikiria hao madaktari wa nje wakija watakavyosikilizwa kwa kuwapa magari, nyumba nzuri, anasa nyingine, mishahara mikubwa na bado ufanisi wao unaweza usiwe kama wa hawa wa kwetu! Kwanini serikali ni rahisi kuwasikiliza wataalamu wa nje kuliko wa hapa kwetu?

Serikali itumie busara katika hili ama sivyo itakosa uhalali wa kuitwa serikali na pia kukosa kura 2015 au vurugu kutokea. Serikali iwaadhibu watu wachahce ndani ya serikali waliohusika na kutaka kumuua dr. ulimboka na wale wanaoishauri vibaya! Ichezee ovyo fedha za wananchi wa Tanzania wakati solution zipo hapa ndani na ni rahisi kutekelezeka.

Imagine mikoa yooote na wilaya zote zipate madaktari toka nje! Je jambo hili linawezekana? Liyumba na akina mramba wameshtakiwa kwa maamuzi/matumizi mabaya yaliyoiingizia seriakli hasara je, ni kwanini na huyo asemaye ataleta madaktari nje na huyo asemaye atafukuza madaktari nje asishtakiwe kwa kuiingiza serikali hasara?

Pia nashauri jumuiya ya madaktari wamfiche ulimboka na aende kwenye ubalozi wa marekani au nchi nyingine makini akahifadhiwe kwani popote alipo atafuatwa aangamizwe. Na wale wenye nyeti na ushahidi wa kuteswa kwake wajifiche wapiganie vita hii mafichoni na wauweke ushahidi wao kwa maandishi na kurekodi na wawape mawakili na wawakilishi wa vyama vya upinzani na jumuiya za kimataifa ushahidi wao kabla hawajawindwa na kuangamizwa.

Mungu ibariki Tanzanian madaktari na Dr. Ulimboka.
 
images


Huu ndio uamuzi Mgumu tunaotazamia ambao Kikwete ametamka leo.
Kauli ya Rais Kikwete imetulia na ameeleza ukweli ambao serikali ilivyochukua hatua na tahadhari dhidi ya madai na migomo ya madaktari. Pia imesaidia kutoa picha upande wa pili ambao wengi hutukuweza kuelewa kwa uwazi. Aliyoongea Rais kwa wenye kujua hali halisi ya uchumi wa nchi yetu na matatizo mengine ameeleweka. Kwa waajiriwa wa serikali wanajua mishahara wanayolipwa.
Dao kubwa hilo la Madaktari la Shilling 7,000,000 lisilozingatia uwezo wa serikali na uboreshwaji wa huduma nyingine za afya na hali kadhalika kutojali uboreshwaji wenye uwiano na idara nyingine za serikali usipishane kwa kiwango kikubwa mno. Ni mambo yale yale yaliyokuwa yanalalamikiwa na wananchi dhidi ya wabunge, kwani wengine wanavyohangaika na njaa wengine wanataka wawe wanaichi kama wako peponi.

Mishahara ya serikali kupandishwa kila mwaka nimeona tu Tanzania, kwani nchi nyingine huchukua miaka mingi hadi kima kipandishwe, kwani upandishwaji wa mishahara ni sababu nyigine inayodhoofisha uchumi na mfumuko wa bei kupanda holela. Ukishapandisha mishahara lazima kila kitu kitapanda, kodi nayo itapanda hakuna unafuu ila ni kuendelea kupiga mark-time. Mfano Marekani kwa wastani wa zaidi ya miaka 15 mishahara imepandishwa mara moja tu kipindi cha utawala wa Rais wa zamani George Bush kutoka $5.15/75 na kufikia $7.25/75 per hour kwa kima cha chini.

Nchi nyingi zina utaratibu kama aliofafanua Rais Kikwete kwamba asiyekubaliana na mshahara basi aache kazi aende kwa mwajiri mwingine ambaye atampa mshahara anaoutaka. Hii ndiyo sababu nchi kama za Ulaya na Marekani utaona watu hawalalamikii mishahara, ila huacha kazi na kwenda kwenye makampuni mengine ambayo hulipa zaidi kidogo. Kutokana na tatizo hilo utaona idara za elimu hasa walimu vyuo vya serikali wamejaa wahadhiri wa kumwaga toka mataifa mengine na kabisa toka Afrika kama nchini Marekani kwa sababu wamarekani hupenda kufundisha vyuo binafsi ambako hulipwa vizuri zaidi na hakuna kodi nyingi kama serikalini.

Madaktari nchi nyingi hawategemei malipo mahospitalini tu, bali wana ziada ya mitandao katika mashirika mengine na zahanati ampako hufanya part time, na huko ndiko wanakopata ziada ya kuendeshea maisha yao. Hata secta nyingine nchi tajiri duniani wafanyakazi hawategemea pato moja tu vinginevyo kuna ziada ya muda wa kazi ambao huwaongezea pato, vinginevyo wanakuwa na pato la ziada kwa kufanya kazi nyingine part time au kujiajiri baada ya kazi.

Kwa ufafanuzi wa Rais Kikwete nakubaliana naye Madaktari ambao hawako tayari wajiondoe na kwenda kwa mwajiri ambaye wanaona atawalipa kiwango wanachokitaka cha kufikia millioni 7 kama wanazolipwa wabunge. Kuendelea kuidai serikali kiwango ambacho serikali haina uwezo ni sawa na kunyonga mzazi wako kumdai zaidi ya uwezo unaomruhusu.

Mjumbe mmoja kwenye tume ya katiba analipwa laki nne na nusu kwa siku halafu anapewa nyumba,gari na mafuta.Tafakari!
 
Mjumbe mmoja kwenye tume ya katiba analipwa laki nne na nusu kwa siku halafu anapewa nyumba,gari na mafuta.Tafakari!

Kazi ya muda mfupi ni tofauti na kazi ya masiaha inayochukua maelefu ya watumishi, jaribu kutofautisha kdigo utaona.
 
Back
Top Bottom