Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

najiuliza ni kwa nini serikali kwa mara kadhaa ndio imekuwa ikitoa ufafanuzi wa madai ya madaktari?alianza mwinyi akaja pinda akaja mwinyi na sasa ni mkulu mwenyewe.
Ombi langu kwa kamati ya madaktari,sasa ni wakati wa kusikia kwa kina juu ya madai na mchakato wa majadiliano ili tuamuwe!!
 
Huna hoja.

Waliyokubaliana kayasema na ambayo serikali imekataa na hayo kayasema waziwazi na ambayo hawajakubaliana kayasema waziwazi na kasema asiyeyataka hayo ambayo serikali imeyakataa aache mwenyewe kazi. Nini zaidi usichokielewa?

Kama huna hoja kaa kimya kama wenzako.
Dhaifu keshadanganya mara ngapi, endelea kumwamini dhaifu wako, kwa wewe yoyote anaeongea kinyume cha dhaifu hana hoja. Lakini dhaifu ni mwongo, muuaji na zake zinahesabika, endelea kumtetea utaenda nae. Nenda hospitali sasa hivi utaona kama nina hoja ama sina. Limbwata la ulafi litawafikisha kubaya
 
Kikwete ahsante sana.

Sasa ondokeni mkafanye kazi zenu za private au mrudi kazini, uamuzi ni wenu, na huko mahospitali tutaanza kuwawekea tathmini ya kujuwa ni nani anaefanya kazi na anastahili kulipwa na nani asiyefanya. Mnalo?
Labda wale wenye Honoris causa ndio watarudi kazini.
 
1. kwamujibu wa hotuba hi hakuna makubaliano yaliyofikiwa yote ni nusu nusu

2. kikwete an kinyongo na anategemea kuwafukuza kazi madaktari

3. swala la ulimboka aliache na huo mkono wa pole huko huko abaki nao

4. hotuba imekazania swala la mishahara na swala la kuboresha huduma za afya hajalifafanua vilivyo..nachelea kusem nae ni miongoni mwa wasiojua madai y madaktari..anajua nusu nusu tu


  1. Uongo haukusaidii kitu wala kupindisha maneno hakukufanyi uwe huru. saba yamekubaliwa moja limekataliwa yaliobaki nusu nusu.
  2. Hakuna kinyongo hapo, kasema wazi wazi, mishahara wanayotaka hakuna, kilichoongezwa ndio hivyo kimeongezwa, ukitaka fanya hutaki acha, uamuzi ni wako si wa Kikwete. Mshahara wa kuanzia million 3.5 hakuna.
  3. Swala la Ulimboka haliachi mpaka ukweli ujulikane. Unaogopa nini?
  4. Hotuba imepitia mambo yote 12 ya madai ya madaktari.

Hiki ni nini:

Jambo la sita ni kuhusu mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na madaktari kuhusu kuboresha huduma ya afya. Mapendekezo hayo yalihusu kutathmini sera na mpango wa afya ya msingi, bajeti ya afya kuwa asilimia 15 ya bajeti ya Serikali, kuwepo na utaratibu mzuri wa kuajiri madaktari na kuboresha viwango vya ubora wa madaktari na kadhalika. Serikali imeyaafiki mapendekezo hayo na yatafanyiwa kazi.
 
hivi lini mara ya mwisho JK kutembelea hospitali za serikali. siku moja akiwa hana safari za nje atembelee hospital za temeke muhimbili aone wagonjwa wanavyolala chini sakafuni ndio aone hali halisi ilivyo sio akae ikulu asubiri report kutoka kwa wasaidizi wake ambao mara nyingi hawampi hali halisi ya nchi ilivyo
 
Laiti kama angeisoma live ingenoga sana, lakini nasikia mkuu anaumwa na ndiyo maana ameshindwa kuisoma hotuba jana.


kwa taarifa yako yuko rwanda kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru....ana masaa mawili linaenda la tatu sasa yuko hapo
 
Hivi amesema atachukua hatua gani kuwaokoa wananchi wanaondelea kufa, naona alichoongea ni kuwashutumu na kuwatisha madaktari, kama rais tulitakiwa tusikie anachukua hatua gani kwanza kumaliza mgogoro lakini pili kuwasaidia wapiga kura wake, ingawa sina uhakika kama alikuwa na wapiga kura
 
Mbona mkuu wa kaya hataji ile agenda muhimu ya kuboresha huduma ya afya kama vile madawa na vitendea kazi? Mbona JK hajaisema hii? Kama kuna mtu mwenye negotiation paper tunaomba uipost hapa ili tujue kama kweli yalikuwepo hayo madai 12.
 
Hakuna lolote hapo! Ameweka kwenye blog! Ana ogopa kuwaangalia watanzania, hana lolote. Eti ana sikitishwa kwa kile kilicho mkuta ulimboka.

Unafiki mtupu
 
angekataa asiingie kwene majadiliano bado mngelaumu
Ukiiangalia kauli yake kwa undani utagundua kuwa ni kauli ya kibaguzi. Confirmed JK ni mbaguzi kwa kwenda mbele, naona silaha yake ya ubaguzi wa kidini na kumtumia Sheikh Ponda haifanikiwi sasa analeta ubaguzi wa huyu mtumishi wa serikali na yule sio ili wabaguane, bahati nzuri madaktari wanaunganishwa na taaluma tofauti na mawazo yake kudhani wanaunganishwa na ajira au fedha au itikadi za kisiasa. Natamani US wamlime barua nyingine
 
Huyu baba kanyimwa busara kweli kweli..khaaa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Lakini ndiye "mbora" kati yetu, ndo mana tumimchagua. Mtihani ulikuwa mkali kati yake na yule muasi wa kanisa katoliki.
 
Ndio maana nimeuliza kuwa alihutubia saa ngapi maana hata mimi skulala mapema nilikuwa nasubiri nisikie atakachozungumza.

Naona maendeleo Tanzania,siku hizi MHESHIMIWA RAISI anahutubia kupitia blog!
 
Back
Top Bottom