Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

mhe Jk usitupotoshe umma,vijana wako ndio wamemdhulu Dr ulimboka,na wewe unafahamu kwan ndio umewatuma!kama unabisha we bishi,sis tunaanza maombi maalumu na majibu utayapata
 
"separation of powerz na sakata la madaktari, kumbe upande mmoja unaweza kufanya maamuzi wakat suala lipo mahakamani (serikali) lakini upande wa pili unaambiwa uheshimu amri ya mahakama(bunge, madaktari), the exit point of the government !!!!!!! The best way of dispute resolution iz "negotiation and dialogue" na kutoa option kwenye "diedlock". Serikali imeshindwa kwenye "diedlock option" na kukimbilia mabavu"

moj ya comments za wadau
 
imetulia.....imeeleza bayana madai na uwezo wa serikali...! asieweza kufanya kazi aondoke ili serikali itafute replacement
 
huu uwezo wa serikali unakuwa mdogo kwa madaktari tu na sio wabunge au tume ya katiba?

Milioni 10 bila makato kwa mbunge mwenye elimu ya drs la saba au form four inawezekana lakini milioni 7+PAYE kwa mtu mwenye degree ya udaktari haiwezekani.

Imekuwaje hatua za kiutumishi zimeanza kutumika huku suala hili likiwa mahakamani?

Naona katutajia bajeti za afya za miaka yote kasoro projection ya 2012/13

Hapa naona ile kauli ya LIWALO NA LIWE imekuja kwa style ya asiyetaka aache kazi!

YANGU MACHO!
 
Ameisoma saa ngapi? Kama imetoka kabla ya yeye kuisoma basi huu ni udhaifu mwengine. Ila hotuma imetulia lakini kwa nini hakusomwa jana?
 
Kama mbunge alisema kuna watu wanaofadhili mgomo wa madaktari na mtotn wamkulima akasema serikal imeshalisikia hlo nauchunguzi unafanyika kubain hilo, kisha usiku Dr ulimboka akatekwa! nakwamaneno yake dr ulimboka anasema walipokuwa wanamsulubu walimuuliza tuambie ninani aliye nyuma yamgomo huu! Je mh rais anashangaa nin' tena dr anasema ni mtumish wa ikulu Tanzania hatujafika hko ila viongoz we2 hamtakwepa lawama hii yakuli2mbukiza taifa kwenye machafuko. Kama walivyosema wanaharakati HATUTAKI VYOMBO VYADOLA VICHUNGUZE TUKIO HLO KWAN WAO NIWATUHUMIWA NAMB 1. MUNGU WA AMANI ATUPE WATANZANIA AMAN LAKIN 2NAMUOMB AWAWEKE WAZI HAWAVIONGOZ WASERIKAL WANAWAUWA WATANZANIA WAKAT WANADAI HAKI ZAO!
 
Aache kuwadanganya watanzania, jk hana jipya! Kawaita wakina Michuzi na kuwapa hiyo hotuba waiweke kwenye blogs. Kwa nini hakuwa na uso wa kusimama mbele ya camera tuuone uso wake akiisoma hotuba hiyo? Tumeacha shughuli zetu muhimu na kusubiri mpaka usiku sana hakuhutubia! Siku zenu zinahesabika!
 
Suala la madaktari naona Mkuu ameendeleza propanganda zilezile za kwamba kulikuwa na makubaliano. Makubaliano gani wakati mazungumzo yalikuwa hayajakamilika, hebu tuwekeeni haya makubaliano yakiwa na sahihi za pande zote mbili tuone.

Na JK ameendelea kuudanganya umma na kuufitinisha na madaktari kwa kuonyesha kuwa madaktari tatizo kubwa waling'ang'ania mshahari wa mil 3.5 wakati walikuwa wanajadiliana na kabla ya makubaliano serikali ikatangaza hizo 15% na labda sasa wanafikiri kuongeza mpaka 20% maana hii haikuwepo mwanzo. JK bila aibu anautangazia umma nyongeza ya posho ya kuchunguza maiti, dai ambalo halikuwepo kati ya yale waliyokuwa wanajadili.

JK acha kutishia nyau, hamuwezi kufukuza madaktari wote walioko kwenye mgomo, mnajidanganya, wasikilizeni madaktari na mfikie muafaka warudi kazini, kuendeleza vitisho na kuwakamata na kutesa viongozi wao haitawasidia.

Huduma gani zimeboreshwa kwenye hospitali za mikoa eti na sasa wanageukia wilayani, hii sio era ya kusema uongo na ukafikiri utapata watu. Ukifika mahospitalini sasa hivi hakuna dawa, hakuna vifaa tiba, hakuna watumishi. Hospitali eti zimepandishwa hadhi ya kuwa za rufaa zikiwa hazina madaktari bingwa, sasa nashangaa kama rufaa inatoka kwa MD inakwenda Kwa MD sijui itakuwa rufaa ya namna gani hiyo. Hospitali kuzitaja kwa uchache ni mfano hospitali ya mkoa wa rukwa ambayo ina bingwa mmoja tu ambaye ni surgeon nae yuko kwenye administration. JK usitupige changa la macho hakuna maboresho yoyote yalofanywe. Nchi imekushinda step down.

mkuu sio kwamba utashindwa kwenda Jamaica kubembea.Mnafiki Mkubwa dhaifu, TISS na mwanao ndio ulowatuma kumfanyia unyama Ulimboka, utalipa hapahapa duniani.

Huna hoja.

Waliyokubaliana kayasema na ambayo serikali imekataa na hayo kayasema waziwazi na ambayo hawajakubaliana kayasema waziwazi na kasema asiyeyataka hayo ambayo serikali imeyakataa aache mwenyewe kazi. Nini zaidi usichokielewa?

Kama huna hoja kaa kimya kama wenzako.
 
vipi kuhusu kuboresha sekta ya afya hajazungumzia?
Nadhani atasema, 'wagonjwa wanaoona hospitali za serikali hazlna vifaa au huduma nzuri, waende kwenye hospitali wanazoona zina vifaa vya kutosha na huduma nzuri'. Huyo ndiyo Jakaya.
 
SEHEMU YA HOTUBA YA JK YA 30/06/2012
Suala la Dkt. Steven Ulimboka
Ndugu Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Steven Ulimboka usiku wa tarehe 26 Juni, 2012. Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.
Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa kiungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na Madkatari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.

Ndugu Wananchi;
Kama nilivyoeleza, mazungumzo yalienda vizuri na mafanikio makubwa yamepatikana. Yapo maeneo machache na hasa eneo la mshahara ambalo hatukuweza kukubaliana. Hapo tulipofikia si pabaya na tulikubaliana sote kurudi kwenye mkondo wa Sheria kusaidiwa. Kwa nini Serikali imdhuru Dkt. Ulimboka? Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha mgomo. Anayekaidi amri ya Mahakama ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo. Hivi baada ya kufika hapo Serikali iwe na ugomvi na Dkt. Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo lipi hata iamue kumdhuru? Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali.

Ndugu Wananchi;
Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali natoa mkono wa pole kwa Dkt. Steven Ulimboka na kumuombea apone haraka ili aungane na familia yake na Watanzania wenzake katika ujenzi wa taifa. Kwa namna ya pekee namshukuru na kumpongeza Bwana Juma Mgaza, kwa moyo wake wa huruma na upendo na kwa hatua alizochukua za kumsaidia Dkt. Ulimboka.
Naomba kumaliza kwa kuwasihi madaktari kuacha mgomo na kurejea kazini. Watanzania wenzenu wanateseka na kupoteza maisha. Muwe na moyo wa huruma na upendo na msaada kwa wagonjwa kama kiapo chenu kinavyowataka.


Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa Kunisikiliza.


WAKUU, HEBU TUJADILI HII

SOURCE: HOTUBA YA JK YA 30.06.2012 KWA MUJIBU WA MICHUZI BLOG
 
Aache kuwadanganya watanzania, jk hana jipya! Kawaita wakina Michuzi na kuwapa hiyo hotuba waiweke kwenye blogs. Kwa nini hakuwa na uso wa kusimama mbele ya camera tuuone uso wake akiisoma hotuba hiyo? Tumeacha shughuli zetu muhimu na kusubiri mpaka usiku sana hakuhutubia! Siku zenu zinahesabika!

Nyinyi ndio umewashuka kwa uongo wenu. Kikwete kaweka wazi asiyetaka aache kazi kwanini ahangaike kugoma? si aende atakapoyapata hayo?

Kumbe Kikwete ndiye aliyewazidishia mishahara ya kuanzia kutoka chini ya laki mbili mpaka zaidi ya millioni, leo yeye ndiye mbaya? amma kweli hamna zaidi ya ufataani tu.
 
Hivi katika uboreshaji wa huduma za afya, kuna sehemu yeyote waliyokubaliana kutengeneza CT scan mashine? Kuna sehemu wakiyozungumzia mchakato wa kuounguza idadi ya wagonjwa wanaolala wawili wawili?
 
Serikali imeweka wazi madai na makubaliano ya pande mbili (serikali na kamati ya Madaktari) na kwa kiwango kikubwa inaonekana madai mengi ni ya maslahi binafsi ya Madaktari kwa maana ya posho na mishahara, suala la kuboresha mazingira ya sekta ya afya halijawekwa wazi sana na ndiyo maana serikali inasema limetekelezwa kwa kuhesabu majengo ya hospitali au majina ya hospitali zilizopo bila kujali kama kuna vitendea kazi stahiki kwa level ya kila hospitali.

Kwa uungwana wa kawaida tunaomba wajumbe wa kamati ya madaktari watujulishe kama hayo yaliyosema na Serikali siyo madai yao au la ili jamii iweze kuona ukweli halisi. Aidha, watueleze wazi kama kipengele kilichopelekea kushindikana kwa muafaka ni hicho cha posho na mishahara kama ilivyoelezwa na serikali?

Hapa hakuna ushabiki, kinachohitajika ni kuweka ukweli wa kilichoendelea, kuepusha kupotosha jamii. Ieleweke kuwa hadi taarifa ya serikali inatolewa nilikuwa naamini kuwa madai makubwa yalikuwa siyo maslahi bali mazimgira ya kazi.
 
huu uwezo wa serikali unakuwa mdogo kwa madaktari tu na sio wabunge au tume ya katiba?

Milioni 10 bila makato kwa mbunge mwenye elimu ya drs la saba au form four inawezekana lakini milioni 7+PAYE kwa mtu mwenye degree ya udaktari haiwezekani.

Imekuwaje hatua za kiutumishi zimeanza kutumika huku suala hili likiwa mahakamani?

Naona katutajia bajeti za afya za miaka yote kasoro projection ya 2012/13

Hapa naona ile kauli ya LIWALO NA LIWE imekuja kwa style ya asiyetaka aache kazi!

YANGU MACHO!

Usichanganye mada. Kama unaweza fanya kazi kama huwezi acha, nenda utakapopata zaidi waachie wengine watakaoona zinawafaa wachukuwe hizo kazi.

Kama wanaona Ubunge unalipa zaidi si waende wakagombee Ubunge? mbona wapo pale wengi walioacha kutibu, nani aliwazuia? au huwajui kina Kigwangallah?
 
Back
Top Bottom