Hotuba ya Rais Karume kwenye Sherehe za Mapinduzi Zanzibar:The Best Ever!

Lini nchi ya Zanzibar imekufa?Nyie acheni mchezo wenu wa kitoto huo, Zanzibar ni moja ya nchi kongwe barani Afrika.Zanzibar ni nchi ipo tokea hata hicho kijinchi chenu cha Tanganyika, musianze dharau zenu.

Nchi ya Zanzibar ipo, na bendera yake itaendelea kupepea milelele.Nchi iliyofutwa na kupotea ni Tanganyika tuu, lakini Zanzibar bado ipo.
.
MrFroasty, Ni kweli Zanzibar ni nchi in a sense of teritorial, yaani eneo linaloitwa Zanzibar lipo, hili halina ubishi, hivyo nchi ya Zanzibar ipo.

Ila ile iliokuwa nchi ya Zanzibar, ambayo ilipata uhuru wake Desemba 1963, uliodumu kwa mwezi mmoja tuu, na kufuatiwa na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 12, 1964. Nchi hiyo ilidumu mpaka April 26, 1964 kwa ridhaa yake yenyewe, ilikubali kuungana na iliyokuwa Tanganyika, tangu siku hiyo, nchi ya Zanzibar ilikufa, ikapoteza mamlaka ya kuitwa nchi, ila ikabakia na mamlaka ya kujitawala kwa mambo yake ya ndani.

Ili nchi iitwe nchi/taifa/state inatakiwa iwe na sifa kuu nne, yoyote kati ya sifa hizo ikikosekana, hiyo si nchi. Sifa hizo za nchi ni
  1. Eneo/land/teritorial-Zanzibar inayo
  2. MipakaDefined bondaries-Zanzibar inayo
  3. Utawala/Government- huu utawala uwe ni halali de-jure au mabavu de-facto haijalishi-Zanzibar wanao
  4. Dola/State Organs, vyombo vya dola, hivi ni vyombo vya ulinzi na usalama kama Jeshi, Polisi, TISS etc-Zanzibar haina.
Hivyo ndugu zetu Wanzanzibari, Zanzibar yenu inasifa zote za kuwa ichi/taifa lakini haina dola, hivyo Zanzibar sio dola.

Najua ukiwaona KMKM na JKU, mnajifariji kuwa eti nanyi mna polisi wenu hao wa KMKM na Jeshi lenu la JKU, vyombo vyote hivyo ni kama wagambo tuu, kama tunavyowavisha watoto wetu nguo za jeshi na kujiproud watoto wetu wajeshi!.

Sorry to say, vikosi vya SMZ ndani ya katiba ya JMT, ni kama mgambo tuu, ama ultimet security ama makampuni ya ulinzi.

Ili kuzua migogoro na mitafaruku isiyo ya lazima, ukiwa mwanasiasa to survive, lazima uwe mnafiki. Pinda was bold and genuine alipotamka wazi, Zanzibar sio nchi, this is a fact. Moto uliowaka, ilimbidi JK akubali kuwa mnafiki kwa kuwapa peremende mnyamaze na mmenyamaza.

Mtoto akilia sana bila sababu ya msingi, mpe peremende, atanyamaza. Ila kama akilia huku anatatizo genuine, hata umpe peremende, hanyamazi. JK alipowapa peremende pale Dodoma eti Zanzibar ni nchi ndani ya Tanzania, nje ya Tanzania nchi ni Tanzania!. Kwenye hili there is only one way, ni nchi au si nchi, hakuna ni nchi si nchi, hiyo ilikuwa peremende tuu, Zanzibar sio nchi this is a fact no matter how bitter it is. Poleni!.
 
Mr.Froasty,

..tunachotaka ni usawa ktk muungano huu. kama suala hilo haliwezekani baina ya Tanganyika na Zenj ni bora Muungano uvunjwe.

..ninachosema mimi ni kwamba Wazenj wawekewe masharti yaleyale wanayokumbana nayo Watanganyika wanapofika Zenj.

..nakumbuka majuzi hapa kuliibuka suala la vibali vya kazi Zenj. ilielekezwa kwamba Watanganyika watakuwa-treated kama raia wengine wa kigeni ktk masuala masuala ya kazi Zenj. yaani Mtanganyika anakuwa hana tofauti na Msudan,Mnigeria etc.

..kama ni mashirikiano ktk muungano, basi yasielemee kwa wa Tanganyika kama ilivyo sasa hivi.

..kwa mfano: kama mnadai Zenj ni ndogo sana, na uwezo wake ni kupokea wahamiaji 1000 tu kwa mwaka toka Tanganyika, basi Tanganyika nayo isipokee Wazenj zaidi ya 1000 kwa mwaka.

..kwasasa hivi Mzenj akiingia Tanganyika anakuwa na haki zote kana kwamba amezaliwa upande huu. lakini hilo haliwezekani kwa Watanganyika kwanini? kwanini hakuna usawa ktk muungano huu?

..pia si kweli kwamba Wazenj hawafaidiki na madini na rasilimali nyingine zinazopatikana huku Tanganyika. Wazenj wana uwezo wa kumiliki ardhi huku Tanganyika. kuna maeneo ktk miji ya Tanganyika ambako Wazenj wana majumba makubwa makubwa, mashamba makubwa, biashara, na hakuna anayewasumbua.

..pia Wazenj wanayo haki ya kumiliki machimbo ya madini[dhahabu,tanzanite,ruby,... yoyote yale yanayopatikana Tanganyika. sasa hii habari kwamba waZenj hawafaidiki na "dhahabu" za Tanganyika yanatoka wapi?

NB:

..kuhusu suala la bajeti ni kweli huwezi kusikia suala la barabara za Zenj ktk bunge la muungano. hii ni kwasababu suala la barabara siyo la muungano. lakini inaposomwa bajeti ya wizara kama ulinzi, au ile ya mambo ya ndani, basi Zenj iko-included humo. hapa ni suala la kuelewa tu wizara zipi zinashughulika na masuala ya muungano.

..nilitegemea ungekwenda mbali zaidi na kuuliza kwanini wabunge toka Zenj huhudhuria na hupokea posho za vikao vya bunge vinavyozungumzia masuala yasiyo ya muungano?

Unapodai usawa usiwe unabagua sehemu gani kuwe na usawa.Usawa huo na uwe hata kugawana mapato ya Tanzania, yapigwe 50-50.Hata hayo mapato ya bahari nayo 50-50.

Ukiweza kufanya hivyo, basi Zanzibar tutakubali kila kitu kigawiwe 50%.

Hoja zako hazina msimamo, unaposema Zanzibar inafaidika na madini ya bara.Hapa tunaposema kufaidika manaake mapato yakipatakina kutokana na rasili mali hiyo, basi nusu inakwenda SMZ na nusu inakwenda SMT.Sasa unaweza kutaja ni asilimia ngapi hupelekwa SMZ kutoka kwenye madini?

Kumbuka Zanzibar inachangia uendeshaji wa serekali ya Muungano, ambapo ndio hizo gharama za ulinzi zinapokuja na gharama zengine.Usije sema ulinzi ndio Zanzibar tayari imeshafaidika.
 
hata Mwalimu Nyerere kuna wakati alisema angekuwa na uwezo angekisukuma kisiwa hiki kiende mbali baharini maana kimemchosha kila siku kuomba kitu kipya na yeye alichoka nasi kuna siku tutachoka kuwabeba.

Nyerere kweli alikuwa genius na kuweza kukudanganyeni.Hivi kweli Nyerere angelikuwa hana interests na Zanzibar, angelivikumbatia visiwa hivyo na kufanya muungano na kuweka sera madhubuti za kuimeza nchi hiyo?

Zungumza huko huko Mbagala propaganda hiyo, Nyerere alikuwa anavikodolea macho visiwa hivyo tokea asubuhi.Na hayo mapinduzi, muungano haikuwa bahati mbaya ilikuwa ni mipango yake maalum.

Kama angelikuwa Nyerere hataki muungano, usingelitokezea hata siku moja.Ametumia nguvu zake zote akiwa hai kulinda muungano, na hilo unalijua.Sasa unaleta hadithi ati alikuwa hapendi Zanzibar anataka kuisukuma iende mbali.Wakati ukweli anaonekana sera zake ni za kuivuta Zanzibar iwe chini ya himaya yake.
 
.
MrFroasty, Ni kweli Zanzibar ni nchi in a sense of teritorial, yaani eneo linaloitwa Zanzibar lipo, hili halina ubishi, hivyo nchi ya Zanzibar ipo.

Ila ile iliokuwa nchi ya Zanzibar, ambayo ilipata uhuru wake Desemba 1963, uliodumu kwa mwezi mmoja tuu, na kufuatiwa na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 12, 1964. Nchi hiyo ilidumu mpaka April 26, 1964 kwa ridhaa yake yenyewe, ilikubali kuungana na iliyokuwa Tanganyika, tangu siku hiyo, nchi ya Zanzibar ilikufa, ikapoteza mamlaka ya kuitwa nchi, ila ikabakia na mamlaka ya kujitawala kwa mambo yake ya ndani.

Ili nchi iitwe nchi/taifa/state inatakiwa iwe na sifa kuu nne, yoyote kati ya sifa hizo ikikosekana, hiyo si nchi. Sifa hizo za nchi ni
  1. Eneo/land/teritorial-Zanzibar inayo
  2. MipakaDefined bondaries-Zanzibar inayo
  3. Utawala/Government- huu utawala uwe ni halali de-jure au mabavu de-facto haijalishi-Zanzibar wanao
  4. Dola/State Organs, vyombo vya dola, hivi ni vyombo vya ulinzi na usalama kama Jeshi, Polisi, TISS etc-Zanzibar haina.
Hivyo ndugu zetu Wanzanzibari, Zanzibar yenu inasifa zote za kuwa ichi/taifa lakini haina dola, hivyo Zanzibar sio dola.

Najua ukiwaona KMKM na JKU, mnajifariji kuwa eti nanyi mna polisi wenu hao wa KMKM na Jeshi lenu la JKU, vyombo vyote hivyo ni kama wagambo tuu, kama tunavyowavisha watoto wetu nguo za jeshi na kujiproud watoto wetu wajeshi!.

Sorry to say, vikosi vya SMZ ndani ya katiba ya JMT, ni kama mgambo tuu, ama ultimet security ama makampuni ya ulinzi.

Ili kuzua migogoro na mitafaruku isiyo ya lazima, ukiwa mwanasiasa to survive, lazima uwe mnafiki. Pinda was bold and genuine alipotamka wazi, Zanzibar sio nchi, this is a fact. Moto uliowaka, ilimbidi JK akubali kuwa mnafiki kwa kuwapa peremende mnyamaze na mmenyamaza.

Mtoto akilia sana bila sababu ya msingi, mpe peremende, atanyamaza. Ila kama akilia huku anatatizo genuine, hata umpe peremende, hanyamazi. JK alipowapa peremende pale Dodoma eti Zanzibar ni nchi ndani ya Tanzania, nje ya Tanzania nchi ni Tanzania!. Kwenye hili there is only one way, ni nchi au si nchi, hakuna ni nchi si nchi, hiyo ilikuwa peremende tuu, Zanzibar sio nchi this is a fact no matter how bitter it is. Poleni!.

Nyie endelezeni dharau zenu dhidi ya Zenji.Lakini mukumbuke tuu wahenga walisema MDHARAU MWIBA HUMCHOMA.

Na itakuwa hivyo hivyo hawajakosea hao wazee, Zenji itasimama miguu miwili.Mimi naamini kabisa katika moyo wangu iko siku huu muungano wa kiini macho utakufa au utarekebishwa na mamlaka ya Zenji yatarudi kwa wazanzibari wenyewe.

Mungu ibariki Zanzibar... :D
 
Nyerere kweli alikuwa genius na kuweza kukudanganyeni.Hivi kweli Nyerere angelikuwa hana interests na Zanzibar, angelivikumbatia visiwa hivyo na kufanya muungano na kuweka sera madhubuti za kuimeza nchi hiyo?

Nakubaliana na wewe kuwa Nyerere alikuwa genious ndiyo maana hamkumwelewa wakati ule.
Kweli Nyerere alikuwa na interest na Zanzibar kwa wakati ule wa nchi zisizofungamana na upande wowote enzi za cold war USSR na Marekani sisi tulikuwa upande wa Russia zaidi,wakati huo kulikuwa na tention za nchi za magharibi kuichukua Zanzibar ndio maana aliwakumbatia sana hata hiyo kauli ya kuvisukuma visiwa alikuja kuitoa juzijuzi tu baada ya kumkinai.
 
Hadi alifariki bado alikuwa na msimamo huo huo wa kutetea muungano na kupoteza taifa la Zanzibar.

Angelibadili msimamo, basi 1995 asingetia mkono.Angeliwacha demokrasia ikachukua mkondo wake.
 
Mr.Froasty said:
Unapodai usawa usiwe unabagua sehemu gani kuwe na usawa.Usawa huo na uwe hata kugawana mapato ya Tanzania, yapigwe 50-50.Hata hayo mapato ya bahari nayo 50-50.

Mr.Froasty,

..katika posting yangu ambayo uli-quote nilieleza ktk sentensi ya kwanza kabisa na najinukuuu hapa chini:

..tunachotaka ni usawa ktk muungano huu. kama suala hilo haliwezekani baina ya Tanganyika na Zenj ni bora Muungano uvunjwe.

..kwa mtizamo wangu, Zenj is too small kuwa na muungano unaoeleweka baina yake ya Tanganyika.

..probably Tanganyika and Zenj needed each other in the 60s, but I dont think that is the case today.
 
.
Zile Sherehe za Mapinduzi, sio sherehe za muungano, ni sherehe za ile nchi ilikuwa Zanzibar kabla ya muungano, kwa hiyo kihalali Tanzania is nothing, na Kikwete there is nobody, ila wamempa tuu heshima.

Vivyo hivyo Karume akija huku bara, he is nobody, ila tuu amepewa heshima ya recognition kiprotocali na ni waziri asiye na wizara maalum ili aingie cabnet ya huku, nasikia alisusaga hata kuja kwenye vikao hivi.

Kwa hili WildCard, you are damm right, how can The President of URT be second to rais wa kijisehemu cha nchi hiyo, ama nchi jina tuu iso dola?.

Tunaposema Zanzibar tunakusudia Zanzibar na hivyo kiongozi anaetambuliwa ni yule wa Zanzibar. Bahati mbaya kuwa mseto wetu wa Muungano unamfanya Kiongozi wa Tanganyika aitwe wa Muungano.
Wewe huwezi kufahamu lakini viongozi wenu wa Tanganyika wanalielewa hilo na ndio maana wanasubiri waalikwe ndio wahudhurie na wanapohudhuria ugeni unawakumba. Huo ndio uamuzi ulifanywa na hao mnawawaita waanzilishi wa Muungano na kwa vile Muungano huu hauwahusu wananchi basi tubaki tulie tu.
 
tukizungumzia kugombea nadhani ni dhana pana kidogo,inawezekana asigombee phyisically,lakini akawa ameshamteua mtu wa kuenforce kile anachoamini,na anachokitaka,hivyo uwepo wa Karume iwe nje au ndani katika kutekeleza muafaka wa Zanzibar na mambo mengineyo yahusuyo Zanzibar ni wa lazima,mpende msipende.

Itategemea nani atatatawala badala yake. Umesahau ya Komandoo?
 
Nchi hiyo haipo! si ndio ule mjadala ulivyoishia. Au kuna mwingine uliisha tofauti?

Aliumaliza nani? Kwani anaesema haipo ni nani na huyo unaesema kamaliza ni nani? Mbona bado hiyo taarifa ya Wanasheria wa pande mbili haijatoka au unayo mwenzetu?
 
Wapi wazanzibari wametamka kuwa mafuta yakipatikana bara yawe ya bara peke yao na sio ya Muungano?

Amandla......

Kwa mie nisiesoma mtu akisema mafuta si suala la Muungano ninafahamu kuwa mafuta ya Bara si ya Tanzania na mafuta ya Zanzibar si ya Tanzania. Nieleweshe iwapo ufahamu wangu una kasoro.
 
Na wewe nawe unasema nini tena? Wote tunajua kuwa waziri wa SMZ hana nafasi katika bunge la JMT. Wote tunajua bajeti ya wizara za ulinzi, mambo ya nje zinapitishwa na bunge la JMT na si Baraza la mapinduzi. Hizi wizara zinasimamia masuala ya Muungano na si bara peke yake. Lini tumeambiwa na waziri wa fedha zanzibar kuwa mchango wa SMZ kwenye wizara hizi ni kiasi fulani?

Serikali ya JMT haitoi fedha moja kwa moja kwenye bajeti ya SMZ bali kwa njia mbadala. Kwa mfano kwa miaka mingi serikali ya JMT iliibeba serikali ya SMZ kwa kuruhusu watu waingize bidhaa kupitia Zanziba bila kulipia ushuru unaotakiwa. Serikali ya JMT kwa kupitia shirika lake la Tanesco imekuwa iki-subsidize bei ya umeme kwa wazanzibari. Kwa kuwaruhusu wazanzibari kutumia hospitali, shule n.k. ambazo si za Muungano, serikali ya JMT nawa-subsidize wazanzibari. Serikali ya JMT kwa kutoa mikopo kwa serikali ya SMZ inapokwama inawasaidia wazanzibari maana tunajua kuwa hata siku moja hamtakuja lipa.

Mnabebwa sana na serikali ya JMT na bahati mbaya mnajisahau na kuona sasa ni haki yenu!

Amandla.....

Nikuulize na wewe unazungumziai kitu gani?
Kwanza unafikiri Zanzibar inaendeshwa na wizara ya ulinzi na mambo ya nje peke yake? Hebu jiulize Zanzibar inahitaji kulindwa dhidi ya nasni? Jiulize percentage wise nani ananufaika na misaada na uhusiano wa Kimataifa iwapo Zanzibar haina nafasi ya kuingia mikataba kwa kupitia Serikali ya Tanzania? Jiulize safari za viongozi wa Zanzibar wanalipa nani?
Suwala la Serikali ya Tanzania kulipia mambo yanayoitwa ya Muungano ni kujikomba kwa Tanganyika ionekane kiuwa eti Zanzibar inashirikishwa. Tanganyika inajitowa muhanga bila sababu kuwapatia hongo viongozi wa kisiasa ili waendelee kuikalia Zanzibar. Hebu jiulize kuna haja gani ya fedha nyingi inayotoka kwa Wabunge wa Zanzibar ambao pengine wangehitajika kuwepo Bungeni siku nne tu kwa kipindi cha Bajeti. Wangekuwepo kupitisha bajeti ya mambo ya ndani na nje peke yake lakini kinyume chake wamo hata kwenye kamati zisizowahusu. huu ni udanganyifu wa kisiasa na kwa vile kuna umuhimu wa kuikamata Zanzibar hakuna hata mmoja anaesemea hili.
Kuhusu Hospitali ndugu yangu hakuna rufaa ya Hospitali ya Muhimbili kutoka Hospitali kuu ya Mnazi mmoja. Hakuna uhusiano wowote wa huduma za afya na Muungano na kinachofanyika pale Muhimbili mtu haulizwi paspoti na kwa hivyo hata Wakenya ,Wacongo na wenineo wanapata huduma mradi ukiwa na fedha yako aidha official au unofficial.

Unajuwa haya mambo yakukaa mkajisifu k7wa mnaifanyia Zanzibar hiki au hiki ni majilabu matupu eti umeme hivy nani anaekosa usingizi Tanganyika kwa vile Wazanzibari wamekuwa hawana umeme kwa kipindi cha miezi miwili sasa?
Kawadanganye wengine lakini hakuna la maana kwa Zanzibar kwa Muungano huu isipokuwa kutansfer ufisadi kule na mko tayari hata kuuwa ili mfanikiwe kwa yenu.
 
Zanzibar si nchi piga ua PM alishamaliza mtapiga kelele sana hata rais wa Zanzibar ndani ya muungano is a ceremonial president tu akija ndani ya muungano ni sawa kama RC. Tatizo la waZenji ni wabishi huwa hawataki kuelewa mambo waliomba wimbo wao wakapewa wakaomba bendera yao wakapewa rais wao apigiwe mizinga haya nasikia hata timu ya taifa eti wanataka kama bara itatoa wacheza 10 na wao watoe 10 hata kama hawana uwezo ajabu kweli kweli.

Ubishi wenu utawamaliza kwanza wenyewe kwa wenyewe hampendani mnajiita kuna waunguja na wapemba sasa tukiwaacha si mtamalizana hata Mwalimu Nyerere kuna wakati alisema angekuwa na uwezo angekisukuma kisiwa hiki kiende mbali baharini maana kimemchosha kila siku kuomba kitu kipya na yeye alichoka nasi kuna siku tutachoka kuwabeba.

Mbona unajikanganya Bro au maarifa hayapo na badala yake choyo na chuki?
Ukishasema Zanzibar haipo halafu unaanza kusema nyie nyie nyie na baadae sijui hampendani wabishi mtauwana, sasa sisi ni nani na nyie ni nani ?
Utake usitake Zanzibar ipo na ndio maana unazungumzia Zanzibar kama entity huku unashindwa kutaja Mkowa fulani na kuujadili.
Nasema maarifa hayapo kwani waswahili husema Nyani haoni kund ul e.
Sisi hatupendani sawa lakini kutopendana kwetu hakuleti vita vya Tarime, kwa wamasai na dhidi ya wanaadamu wenzetu wenye ulemavu. Hongera kwa mapenzi kati yenu lakini si umeshakubali kuwa sisi na nyi ni tofauti?
 
Mr.Froasty,

..tunachotaka ni usawa ktk muungano huu. kama suala hilo haliwezekani baina ya Tanganyika na Zenj ni bora Muungano uvunjwe.

..ninachosema mimi ni kwamba Wazenj wawekewe masharti yaleyale wanayokumbana nayo Watanganyika wanapofika Zenj.

..nakumbuka majuzi hapa kuliibuka suala la vibali vya kazi Zenj. ilielekezwa kwamba Watanganyika watakuwa-treated kama raia wengine wa kigeni ktk masuala masuala ya kazi Zenj. yaani Mtanganyika anakuwa hana tofauti na Msudan,Mnigeria etc.

..kama ni mashirikiano ktk muungano, basi yasielemee kwa wa Tanganyika kama ilivyo sasa hivi.

..kwa mfano: kama mnadai Zenj ni ndogo sana, na uwezo wake ni kupokea wahamiaji 1000 tu kwa mwaka toka Tanganyika, basi Tanganyika nayo isipokee Wazenj zaidi ya 1000 kwa mwaka.

..kwasasa hivi Mzenj akiingia Tanganyika anakuwa na haki zote kana kwamba amezaliwa upande huu. lakini hilo haliwezekani kwa Watanganyika kwanini? kwanini hakuna usawa ktk muungano huu?

..pia si kweli kwamba Wazenj hawafaidiki na madini na rasilimali nyingine zinazopatikana huku Tanganyika. Wazenj wana uwezo wa kumiliki ardhi huku Tanganyika. kuna maeneo ktk miji ya Tanganyika ambako Wazenj wana majumba makubwa makubwa, mashamba makubwa, biashara, na hakuna anayewasumbua.

..pia Wazenj wanayo haki ya kumiliki machimbo ya madini[dhahabu,tanzanite,ruby,... yoyote yale yanayopatikana Tanganyika. sasa hii habari kwamba waZenj hawafaidiki na "dhahabu" za Tanganyika yanatoka wapi?

NB:

..kuhusu suala la bajeti ni kweli huwezi kusikia suala la barabara za Zenj ktk bunge la muungano. hii ni kwasababu suala la barabara siyo la muungano. lakini inaposomwa bajeti ya wizara kama ulinzi, au ile ya mambo ya ndani, basi Zenj iko-included humo. hapa ni suala la kuelewa tu wizara zipi zinashughulika na masuala ya muungano.

..nilitegemea ungekwenda mbali zaidi na kuuliza kwanini wabunge toka Zenj huhudhuria na hupokea posho za vikao vya bunge vinavyozungumzia masuala yasiyo ya muungano?

Maswala unayouliza ni maswali ya msingi ambayo jawabu lake ni moja tu. Tunahitaji kulinda nchi yetu zanzibar kutofanywa kuwa ya kuhamia. Sioni ajabu kwa hili kwani sisi bado tunatambuwa kuwa sisi ni nchi na tunapozungumzia haki sawa basi usawa uanzie hapo. Kuwe na Zanzibar na kuwe na Tanganyika lakini hii hali ya mmoja kujificha kwenye serikali ya Muungano unahisi ni haki?
Kunakosekana mipaka ya Tanganyika na ile ya Muungano na ndio maana mnalazimika kupokea Wazanzibari na kuwapa kila kitu kwani si mmeamuwa kuvaa koti la Muungano? Zanzibar ilikataa hilo na kuamuwa kubaki na uwezo wake kwa mambo yake ya ndani na kusalimisha ya kimataifa.
Maamuzi ya pande zote mbili sasa yanazitafuna nchi husika kwa vile Zanzibar imepoteza uwezo wake wa Kimataifa (hasara kubwa sana) na Tanganyika imepoteza uwezo wa kuwawekea vikwazo Wazanzibari (hakuna hasara nionavyo kwani Zanzibar ni sawa na tone la chumvi baharini)

Ama hili la kupoteza fedha zenu ( kwa vile mnachanga nyingi zaidi) kwa mambo yasiyo na faida yoyote (suwala la uwakilishi bungeni) ni hili ni gharama ya kutawala kwani si mnataka Muungano wa kutawala kama huu?
 
.
MrFroasty, Ni kweli Zanzibar ni nchi in a sense of teritorial, yaani eneo linaloitwa Zanzibar lipo, hili halina ubishi, hivyo nchi ya Zanzibar ipo.

Ila ile iliokuwa nchi ya Zanzibar, ambayo ilipata uhuru wake Desemba 1963, uliodumu kwa mwezi mmoja tuu, na kufuatiwa na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 12, 1964. Nchi hiyo ilidumu mpaka April 26, 1964 kwa ridhaa yake yenyewe, ilikubali kuungana na iliyokuwa Tanganyika, tangu siku hiyo, nchi ya Zanzibar ilikufa, ikapoteza mamlaka ya kuitwa nchi, ila ikabakia na mamlaka ya kujitawala kwa mambo yake ya ndani.

Ili nchi iitwe nchi/taifa/state inatakiwa iwe na sifa kuu nne, yoyote kati ya sifa hizo ikikosekana, hiyo si nchi. Sifa hizo za nchi ni
  1. Eneo/land/teritorial-Zanzibar inayo
  2. MipakaDefined bondaries-Zanzibar inayo
  3. Utawala/Government- huu utawala uwe ni halali de-jure au mabavu de-facto haijalishi-Zanzibar wanao
  4. Dola/State Organs, vyombo vya dola, hivi ni vyombo vya ulinzi na usalama kama Jeshi, Polisi, TISS etc-Zanzibar haina.
Hivyo ndugu zetu Wanzanzibari, Zanzibar yenu inasifa zote za kuwa ichi/taifa lakini haina dola, hivyo Zanzibar sio dola.

Najua ukiwaona KMKM na JKU, mnajifariji kuwa eti nanyi mna polisi wenu hao wa KMKM na Jeshi lenu la JKU, vyombo vyote hivyo ni kama wagambo tuu, kama tunavyowavisha watoto wetu nguo za jeshi na kujiproud watoto wetu wajeshi!.

Sorry to say, vikosi vya SMZ ndani ya katiba ya JMT, ni kama mgambo tuu, ama ultimet security ama makampuni ya ulinzi.

Ili kuzua migogoro na mitafaruku isiyo ya lazima, ukiwa mwanasiasa to survive, lazima uwe mnafiki. Pinda was bold and genuine alipotamka wazi, Zanzibar sio nchi, this is a fact. Moto uliowaka, ilimbidi JK akubali kuwa mnafiki kwa kuwapa peremende mnyamaze na mmenyamaza.

Mtoto akilia sana bila sababu ya msingi, mpe peremende, atanyamaza. Ila kama akilia huku anatatizo genuine, hata umpe peremende, hanyamazi. JK alipowapa peremende pale Dodoma eti Zanzibar ni nchi ndani ya Tanzania, nje ya Tanzania nchi ni Tanzania!. Kwenye hili there is only one way, ni nchi au si nchi, hakuna ni nchi si nchi, hiyo ilikuwa peremende tuu, Zanzibar sio nchi this is a fact no matter how bitter it is. Poleni!.

PASCO,
Tunachozungumza Zanzibar ni kuwa sisi ni nchi na mnachozungumza nyie kuwa sisi si nchi, iite dola au upendavyo.
Kwa bahati mbaya Katiba ya Tanzania haizungumzii dola bali inazungumzia suwala la nchi na kusema kuwa Tanzania ni Muungano wa nchi mbili zilizokuwa huru zilizoamuwa kwa hiyari yao kuungana.

Nafikiri kejeli na fidhuli zako zingetowa ufafanuzi wa hapo halafu uwanja uko wazi kwa wastaarabu na wenye nyoyo za ......
 
Mbona unajikanganya Bro au maarifa hayapo na badala yake choyo na chuki?
Ukishasema Zanzibar haipo halafu unaanza kusema nyie nyie nyie na baadae sijui hampendani wabishi mtauwana, sasa sisi ni nani na nyie ni nani ?
Utake usitake Zanzibar ipo na ndio maana unazungumzia Zanzibar kama entity huku unashindwa kutaja Mkowa fulani na kuujadili.
Nasema maarifa hayapo kwani waswahili husema Nyani haoni kund ul e.
Sisi hatupendani sawa lakini kutopendana kwetu hakuleti vita vya Tarime, kwa wamasai na dhidi ya wanaadamu wenzetu wenye ulemavu. Hongera kwa mapenzi kati yenu lakini si umeshakubali kuwa sisi na nyi ni tofauti?

Uwe unasoma vizuri posts kuna mtu kasema Zanzibar haipo Zanzibar ipo kama ninavyoweza kusema Mbeya ipo, mimi nimesema hakuna kitu kinachoitwa NCHI YA ZANZIBAR mna jeshi nyie mtaitwaje nchi hata UN hamtambuliki hamna kiti kule JK anakiti chake lakini Karume hana labda akasimame, ukweli ndo huo.
 
Rais Karume ndio kwanza amemaza kuhutubu sherehe za Mapinduzi Zanzibar kutokea kisiwani Pemba.

Kwa maoni yangu, its the best ever tangu nimekuwa nikimsikiliza Mheshimiwa huyu huko nyuma.

Dondoo Muhimu:
  1. Amesema hatogombea tena kwa mujibu wa katiba.
  2. Ameupongeza muafaka wake na Maalim Seif na kusifu motokea mema yake ya awali.
  3. Ametumia lugha ya kistaaranu iliyojaa hekima na busara, huko nyuma zilikuwa ni mafumbo na vijembe.
  4. Amezungumzia issue zote muhimu kwa mustakabali wa Zanzibar
  5. Amezungumzia Muungano ni Dhima.
  6. Ametoa hakikisho la Uchaguri huru na wa haki.
  7. Wenye sifa wote, wataandikishwa. ZEK itapitisha tena uandikishaji upya.
  8. Wote wenye sifa za kupata ZID, watapatiwa na wote wenye ZID walionywima kwenda kuzichukua, wakazichukue.
  9. Kwa ujasiri mkubwa na lugha ya kistaarabu sana, ameyaomba gesi na mafuta yao, yawe yao, kama ilivyo bara na dhahabu yetu.
  10. Amemsifu sana Rais Kikwete, na kumalizia kwa ile ile kauli Adhimu "Mapinduzi Daima".

- Mkuu vipi hapo kweli pamekaa sawa? Mbona habari za ground zero zinasema tofauti? kwa jinsi anavyohaha!

Respect

FMEs!
 
Mr.Froasty,

..katika posting yangu ambayo uli-quote nilieleza ktk sentensi ya kwanza kabisa na najinukuuu hapa chini:

..tunachotaka ni usawa ktk muungano huu. kama suala hilo haliwezekani baina ya Tanganyika na Zenj ni bora Muungano uvunjwe.

..kwa mtizamo wangu, Zenj is too small kuwa na muungano unaoeleweka baina yake ya Tanganyika.

..probably Tanganyika and Zenj needed each other in the 60s, but I dont think that is the case today.

Unfortunately, I cant speak for those who made the decisions in the 60's.I wasnt there when Zanzibar needed Tanganyika.What I know with what I have on the table is that Zanzibar's economy is being blocked its way forward with this creepy union.

I dont believe that the union will be able to stand the challenges if Zanzibar's democracy will be allowed to take place.We have very tough questions on this subject, but what really makes me wonder is that you guys seemed to be pretty confortable with the situation as if you are not affected by it at all.

I know one thing for sure that Tanganyika have invested a lot on Tanzania, but thats not our problem.If you dont care about our economy, why should we care about yours?

This is probably one of the fundamental issue, why you guys are so worried about every little thing is going on in Zanzibar.

So if I get this right, you guys are doing whatever it takes to protect the union and your interests.But will I be wrong to call you guys selfish? :D

Cheers...
 
Back
Top Bottom