Hotuba ya Mwisho ya mtume mohammad

Abuu- Amin

Member
Aug 5, 2012
88
21
After praising, and thanking God, he said:
"O People, listen well to my words, for I do not know whether, after this year, I shall ever be amongst you again. Therefore listen to what I am saying to you very carefully and TAKE THESE WORDS TO THOSE WHO COULD NOT BE PRESENT HERE TODAY.

O People, just as you regard this month, this day, this city as Sacred, so regard the life and property of every Muslim as a sacred trust. Return the goods entrusted to you to their rightful owners. Treat others justly so that no one would be unjust to you. Remember that you will indeed meet your LORD, and that HE will indeed reckon your deeds. God has forbidden you to take usury (riba), therefore all riba obligation shall henceforth be waived. Your capital , however, is yours to keep. You will neither inflict nor suffer inequity. God has judged that there shall be no riba and that all the riba due to `Abbas ibn `Abd al Muttalib shall henceforth be waived.

Every right arising out of homicide in pre-Islamic days is henceforth waived and the first such right that I waive is that arising from the murder of Rabi`ah ibn al Harith ibn `Abd al Muttalib.

O Men, the Unbelievers indulge in tampering with the calendar in order to make permissible that which God forbade, and to forbid that which God has made permissible. With God the months are twelve in number. Four of them are sacred, three of these are successive and one occurs singly between the months of Jumada and Sha`ban. Beware of the devil, for the safety of your religion. He has lost all hope that he will ever be able to lead you astray in big things, so beware of following him in small things.

O People, it is true that you have certain rights over your women, but they also have rights over you. Remember that you have taken them as your wives only under God's trust and with His permission. If they abide by your right then to them belongs the right to be fed and clothed in kindness. Treat your women well and be kind to them, for they are your partners and committed helpers. It is your right and they do not make friends with anyone of whom you do not approve, as well as never to be unchaste...

O People, listen to me in earnest, worship God (The One Creator of the Universe), perform your five daily prayers (Salah), fast during the month of Ramadan, and give your financial obligation (zakah) of your wealth. Perform Hajj if you can afford to.

All mankind is from Adam and Eve, an Arab has no superiority over a non-Arab nor a non-Arab has any superiority over an Arab; also a white has no superiority over a black nor a black has any superiority over white except by piety and good action. Learn that every Muslim is a brother to every Muslim and that the Muslims constitute one brotherhood. Nothing shall be legitimate to a Muslim which belongs to a fellow Muslim unless it was given freely and willingly. Do not, therefore, do injustice to yourselves.

Remember, one day you will appear before God (The Creator) and you will answer for your deeds. So beware, do not stray from the path of righteousness after I am gone.

O People, NO PROPHET OR MESSENGER WILL COME AFTER ME AND NO NEW FAITH WILL BE BORN. Reason well, therefore, O People, and understand words which I convey to you. I am leaving you with the Book of God (the QUR'AN*) and my SUNNAH (the life style and the behavioral mode of the Prophet), if you follow them you will never go astray.

All those who listen to me shall pass on my words to others and those to others again; and may the last ones understand my words better than those who listen to me directly. Be my witness O God, that I have conveyed your message to your people.
 
NGOJA TUUFUFUE
HOTUBA YA MWISHO YA MTUME MUHAMMAD (s.a.w)

Siku ya 9 ya Mwezi wa Dhulhijja, mwaka wa 10 Hijriya, baada ya kuonesha kwa vitendo jinsi hijja itakavyotekelezwa na umma wake na baada ya kukamilisha wajibu zote zinazohusu hija, Mtukufu Mtume (s.a.w) alitoa Hotuba yake ya Kuaga, katika mlima Arafat, mahali ambapo leo kuna Masjid Namirah:

“Enyi watu!

Yasikilizeni maneno yangu kwa umakini! Hakuna ajuaye…huwenda mwaka huu ukawa wa mwisho kwangu kuwa hapa pamoja nanyi!

Enyi watu!

Kama ambavyo siku hizi, miezi hii na mji huu ni vitukufu, vivyo hivyo, uhai wenu, mali zenu na staha zenu ni vitukufu. Ni haramu kuvikiuka.

Enyi Waislamu!

Kesho, mtakutana na Mola wenu na kuhesabiwa kwa yale mnayoyatenda leo! Msirejee kinyumenyume kwenye mila zenu za zamani na kuchinjana nyinyi kwa nyinyi baada yangu! Jueni kwamba nitawatangulieni na kuwasubiri kwenye Birika (la Kawthar)! Nitajifakhiri kwa idadi yenu juu ya umma nyingine! Angalieni msinishushe chini (kwa kuangukia katika dhambi)!

Enyi Waislamu!
Kila mwenye amana ya mtu airejeshe kwa mwenye nayo! Kila aina ya riba imefutwa; iko chini ya migu yangu. Bali mtu anatakiwa kurejesha mkopo. Usidhulumu wala usidhulumiwe! Sasa kujihusisha na riba kumeharamishwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Mambo yote yenye kuchukiza, yaliyokuwa yakifanywa katika zama za Ujahiliya, sasa yako chini ya miguu yangu. Riba ya kwanza ninayoifuta ni ile ya (ami yangu) Abbas ibn Abdulmuttalib.

Enyi Maswahaba!

Uhasama wa enzi za Ujahiliya, nao umefutwa moja kwa moja. Taasubi ya kwanza ninayoifuta ni ile ya Rabia, mjukuu wa AbdulMuttalib.

Enyi watu!

Leo shetani amepoteza nguvu yake ya kurejesha ushawishi na mamlaka yake katika hii ardhi yenu. Lakini, bado ataendelea kufurahi iwapo mtamfuata katika mambo ya upuuzi, mbali na yale ambayo nimeyafuta. Jiepusheni nayo pia ili kuilinda dini yenu!

Enyi watu!

Chungeni haki za wanawake! Amilianeni nao kwa upendo na huruma! Ninawausieni kumcha Mwenyezi Mungu kuwahusu wanawake! Mmewachukuwa wanawake kama amana ya Mwenyezi Mungu; staha na heshima yao kwa jina la Mwenyezi Mungu! Mna haki juu ya wanawake, nao wana haki juu yenu! Haki mliyonayo juu ya wanawake ni kwamba wasiruhusu yeyote kuikanyaga heshima ya familia yenu! Haki ya wanawake juu yenu ni kuwa mnatakiwa kuwapa, kihalali, matumizi na mavazi. Hairuhusiwi kwa mwanamke kutoa kitu katika mali ya mumewe na kumpa mtu bila ruhusa yake.

Ama kuhusu watumishi wenu, walisheni katika vile mnavyokula nyinyi wenyewe na muwavike katika vile mnavyofaa nyinyi wenyewe. Wakifanya kitu ambacho hamuwezi kuwasamehe, basi waacheni waondoke! Lakini msiwaadhibu; kwa maana, nao ni waja wa Mwenyezi Mungu.

Enyi waumini!

Sikilizeni maneno yangu na myazingatie vizuri! Muislamu ni ndugu wa Muislamu; hivyo Waislamu wote ni ndugu. Hairuhusiwi kudhulumu haki ya ndugu yako katika dini, labda kama ataitoa kwa ridhaa yake mwenyewe.

Enyi Maswahaba!

Msizidhulumu nafsi zenu! Nafsi zenu zina haki juu yenu pia!

Enyi watu!

Mhalifu ni mwenye kuwajibika kwa kosa lake yeye mwenyewe. Mtoto hatabeba adhabu ya kosa la baba! Wala baba hatawajibika kwa uhalifu wa mwanaye!

Enyi watu!

Mwenyezi Mungu amempa kila mwenye kustahiki, haki yake (katika Qur’an)! Mwenye kurithi hahitaji wosia! Kitanda atakachozaliwa mtoto, hapo ndipo kwake. Mzinifu atanyimwa. Ghadhabu na laana ya Mwenyezi Mungu, Malaika na Waislamu wote itamkuta yule mwenye kudai kuwa katika nasaba tofauti na ile ya baba yake au mtumishi asiye na fadhila anayedai kuwa anatoka kwa mtu mwingine tofauti na bwana wake! Mwenyezi Mungu haikubali toba na ushuhuda wa watu hao.

Enyi watu!

Mola wenu ni Mmoja! Vivyo hivyo baba yenu ni mmoja; nyote ni watoto wa Adam, na Adam anatokana na udongo. Mwenye thamani zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule mwenye taqwa zaidi. Mwarabu hana ubora juu ya asiyekuwa mwarabu, isipokuwa kama atakuwa na taqwa.

Enyi watu!

Hakika zama ambazo zimeendelea kuzunguka, zimerejea katika awamu ambapo Mwenyezi Mungu aliumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili. Kati yake kuna minne mitukufu (haram). Mitatu kati yake ni yenye kufuatana, ambayo ni Dhil-qadah, Dhil-hijjah na Muharram, na wa nne ni Rajab ((baina ya Jamadi’al-Akhir na Shaban). Mwaka huu, miezi mitukufu imerejea katika zama zake za kale. Msimu wa hijja umesadifiana na siku ya kumi ya Dhil-hijjah.

Enyi Waumini!

Ninakuachieni amana, ambayo mkishikamana nayo hamtapotea kamwe. Amana hiyo ni Qur’an, Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Enyi watu!

Muabuduni Mwenyezi Mungu! Tekelezeni swala tano za kila siku! Fungeni swaumu wakati wa mwezi wa Ramadhan na mtii maamrisho yangu! Hivyo mtaingia Peponi.

Enyi watu!

Tahadharini na kupindukia hali ya kiasi! Kupindukia katika dini ndiyo sababu iliyowafanya waliokuwa kabla yenu kuangamia! Jifunzeni taratibu za hijja kutoka kwangu! Huwenda nisiweze kukutana nanyi tena hapa, baada ya mwaka huu! Wale waliopo wafikishe maneno yangu kwa wale ambao hawapo! Huwenda yule aliyefikishiwa akayaelewa vizuri zaidi na kuyalinda maneno yangu kuliko mfikishaji.”

Baada ya kusema maneno hayo, aliwauliza maswahaba zaidi ya laki moja na elfu ishirini waliokuwepo hapo: “Enyi watu…kesho mtaulizwa kuhusu mimi; mtasema nini?”
“Tunashuhudia kuwa ulitekeleza wajibu wako kama Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ukatuonya na kutuusia”, umati wa waumini ulisema kwa pamoja.

Kufuatia ushuhuda huo wa Waumini, Mtukufu Mtume (s.a.w) akauliza mara tatu: “Je nimefikisha?” Maswahaba wote wakatoa kauli za ushuhuda, ndipo alipoinua mikono yake juu na kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awe shahidi:

“Shuhudia ewe Mola wangu! Shuhudia ewe Mola Wangu! Shuhudia ewe Mola wangu!”

(REJEA: Muslim, Hajj, 147; Abu Dawud, Manasiq, 56; Ibn Majah, Manasiq, 76, 84; Ahmad, V, 30; Ibn Hisham, IV, 275; Hamidullah, al-Wasaiq, uk. 360)

***************************

MAZINGATIO

Hotuba hii ya Kuaga ni sheria zinazoratibu mahusiano ya kijamii, mukhtasari wa mafunzo ya Uislamu na, wakati huo huo, ni mizani ya mwenendo na haki za binaadamu. Kabla ya uundwaji wa Azimio maarufu la Haki za Binaadamu, La Fayette, mwanafalsafa maarufu wa Kifaransa anayetambulika kuwa miongoni mwa waasisi na nguzo muhimu ya Mapinduzi ya Ufaransa ya mwaka 1789, baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu mifumo mbalimbali ya kisheria duniani, hatimaye alikutana na Hotuba ya Mwisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w); na alipoiona kuwa inawakilisha misingi ya haki na uadilifu kwa wanadamu wote, akalazimika kukiria: “Ewe Muhammad Mwenye ukuu…! Umefikia kilele cha juu kabisa cha uadilifu kiasi kwamba hakuna mtu aliyekifikia na hakuna atakayekifikia!”

Katika Hotuba hiyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) anaainisha kanuni ambazo wanadamu wanatakiwa kuzijua ili pasiwepo na udhuru kwa kutozijua. Umati mkubwa uliokuwepo uliwezesha yaliyomo katika Hotuba hiyo kuwafikia wanadamu wote.
 
Jazak Allahu Khayran. Shukran sana kwa ukumbusho.
OMBI MUHIMU:
Enyi ndugu zetu, wana forum wenzetu, wapendwa wetu, kumekuwa na tabia ya kusikitisha ya baadhi yetu kuvamia nyuzi za dini na kutoa matusi na lugha chafu. Tuwe waungwana, kama jambo halijakupendeza au sio imani yako waachie wanao amini. Haimpendezi muislam/mkristo kutukana.
 
Yesu atabaki kuwa mwokozi na atasimama kuhukumu ulimwengu.
SIYO ULIMWENGU USIPINDISHE MAANDIKO ANASIMAMA NA WANAFUNZI WAKE KUZIHUKU KABILA 12 ZA ISRAEL
"27 Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?
28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.(MATHAYO 19:27-28)
AU WEWE UTUAMBIE KTK ZILE KABILA 12 WEWE LAKO LIKO NI LIPI ILI UPATE KUHUKUMIWA KWALO
 
SIYO ULIMWENGU USIPINDISHE MAANDIKO ANASIMAMA NA WANAFUNZI WAKE KUZIHUKU KABILA 12 ZA ISRAEL
"27 Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?
28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.(MATHAYO 19:27-28)
AU WEWE UTUAMBIE KTK ZILE KABILA 12 WEWE LAKO LIKO NI LIPI ILI UPATE KUHUKUMIWA KWALO
mkuu mngeendelea na hotuba ya mohammad.
wakija hapa wenye Yesu wao, sioni kama utaweza kuuzima moto na kuulinda uzi.
mmeanza vizuri mmalize vizuri inshallah Mwenyezi Mungu akujalie hikma, ilim na neema ndogondogo na kubwakubwa.
 
Hebu tujiulize waumini wote wa dini.Enzi hizo za AC na BC kulikua hakuna technology yeyote.Hata karatasi hakuna.Je hizo hutuba za dini zote zilihifadhiwa kwenye nini hadi leo tunaletewa na kuboreshwa.Nipeni jibu ili na mi niwe mmoja wenu waumini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu tujiulize waumini wote wa dini.Enzi hizo za AC na BC kulikua hakuna technology yeyote.Hata karatasi hakuna.Je hizo hutuba za dini zote zilihifadhiwa kwenye nini hadi leo tunaletewa na kuboreshwa.Nipeni jibu ili na mi niwe mmoja wenu waumini.

Sent using Jamii Forums mobile app
WATU WAMEHIFADHI MSAHAFU MZIMA SEMBUSE IYO HADITHI.....IYO IKO MEMORIZED KICHWANI NOW ZIPO VITABUNI PIA
 
Ndugu mleta mada, inasemekana moja ya maneno ya mwisho kabla ya kifo chake mtume ( S.A.W) ...alisema hivi " Ewe Issa Bin Mariam mikononi mwako naiweka roho yangu". Upi ukweli wa maneno haya? Ningependa kufahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kipofu flan, in kipofu anayeuadaa ulimwengu kwa mafundisho yake aliyojitungia, anao wafuasi vipofu weng sana..Siku inakuja vipofu walioomfuata watakuta mambo ni tofaut..watalia na kusaga meno na kumlaumu but watakua too late..ushaur wa bure njia ni moja tu mwamini Yesu ndie mwokoz wako achana na hadith za kufikirika...
 
Jazak Allahu Khayran. Shukran sana kwa ukumbusho.
OMBI MUHIMU:
Enyi ndugu zetu, wana forum wenzetu, wapendwa wetu, kumekuwa na tabia ya kusikitisha ya baadhi yetu kuvamia nyuzi za dini na kutoa matusi na lugha chafu. Tuwe waungwana, kama jambo halijakupendeza au sio imani yako waachie wanao amini. Haimpendezi muislam/mkristo kutukana.
hatuwezi kukaa kimya wakati kweli ya Mungu inapindishwa, lazima tuseme tu..
 
Hebu tujiulize waumini wote wa dini.Enzi hizo za AC na BC kulikua hakuna technology yeyote.Hata karatasi hakuna.Je hizo hutuba za dini zote zilihifadhiwa kwenye nini hadi leo tunaletewa na kuboreshwa.Nipeni jibu ili na mi niwe mmoja wenu waumini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Quran ilikua inahifadhiwa kwenye ngozi zilikauka na mapande ya majabali,magome ya miti kuusu bible sijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom