HOTUBA ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani - Wizara ya Nishati na Madini 2012

Mkuu bomba kubwa la kusafirishia gesi kutoka mikoa ya kusini kuja DAR kuzalisha zaidi ya MW 3000 lilikuwa linahujumiwa na hawa wenye biashara ya mafuta mazito. Maswi na Muhongo wameshaidhinisha kazi hiyo na sasa makampuni matatu ya China yako kazini na kazi itakamilika ndani ya miezi 18 na tatizo la umeme kwisha habari yake. Hongera Maswi na Muhongo, chapeni kazi kwa manufaa ya waTz wote.

hata tenda ya kusambaza mabomba dar walipewa wachina miaka kadhaa iliyopita hembu tujuzeni mabomba yale yanatoa maji,tusubiri huenda yakatimia.
 
Hivi kamaragi ndo tumemsamehe au maana kimya sana,yule msabaha ndiyo hatuelewi ni nini kinaendelea hawa nao si walishiriki wizi pale nishati na madini.
 
Natamani sana kusikia wamenyongwa mafisadi wote,na si uchunguzi huku wanaendelea kula jasho letu kupitia mishahara.kama walivyotuchezesha kwa david jairo.
 
Unajenga bomba, hizo generators za kuzalisha hata 1000mw zimeshawekewa order au?.. Sii ndio kuvuta bomba la maji ktk nyumba ulopanga ukisema utajenga yako baadaye.. Mkuu wangu hilo bomba mnawavutia IPTL , Symbion na mashrika mengine mengi yalojipanga nyuma kusubiri.. Tanesco wanapewa fedha kulipa madeni yao walolimbikiza sio kununua mitambo ya kutosheleza umeme nchini.. Sana sana watakuwa na 200mw hivi za gas na bado watawahitaji IPTL na madeni kuongezeka..

Visima vya Mnazi bay havina uwezo wa ku supply gesi tunayo ihitaji, pekee kinachoweza ni kile cha baharini cha BG ambacho wao wanasema gei yao ni ya ku export.Sasa kitakachotokea ni kuwa tutamaliza kujenga bomba then muda mfupi gas inakwisha na hatujachimba visima vingine, tungechimba visima vya ziada au kuamua kutumia hiyo ya BG. Na pia lazima tununue hizo gas generator haraka. naona kama tumekimbia haraka haraka kwa sababu za kisiasa.
 
Unajenga bomba, hizo generators za kuzalisha hata 1000mw zimeshawekewa order au?.. Sii ndio kuvuta bomba la maji ktk nyumba ulopanga ukisema utajenga yako baadaye.. Mkuu wangu hilo bomba mnawavutia IPTL , Symbion na mashrika mengine mengi yalojipanga nyuma kusubiri.. Tanesco wanapewa fedha kulipa madeni yao walolimbikiza sio kununua mitambo ya kutosheleza umeme nchini.. Sana sana watakuwa na 200mw hivi za gas na bado watawahitaji IPTL na madeni kuongezeka..

Mkandara sijafahamu kwa undani zaidi kuhusu huu mradi. Kuna mkopo kutoka benki ya Exim ya China, sasa sijajuwa kama unaishia kujenga bomba tu halafu kusiwe na mitambo ya kuzalishia huo umeme. Kwa taarifa zaidi soma hapa Waziri anusuru visima vya gesi kuwekwa rehani
 
Mkandara sijafahamu kwa undani zaidi kuhusu huu mradi. Kuna mkopo kutoka benki ya Exim ya China, sasa sijajuwa kama unaishia kujenga bomba tu halafu kusiwe na mitambo ya kuzalishia huo umeme. Kwa taarifa zaidi soma hapa Waziri anusuru visima vya gesi kuwekwa rehani
Majuzi tu nilikuwa nabishana na kiongozi wangu Twiter kwa sababu niliyajua madudu mengi yanayofanyika ktk mpango wa kujenga bomba la gas..Yaani kuna watu hawalali na mpango wa kuimaliza nchi hii na hasa kuwa na ubia ktk mradhi mzima wa gas na nguvu za umeme. Pamoja na kuokoa visima ujue ilikuwa share yetu ndio iwekwe rehani halafu kwa njia za panya wangekuja wao na kuzinunua tena.. Ni uchafu juu ya uchafu. Je, unakumbuka ule mkopo ulivyopatikana?.. Na wala sii ajabu visima visingewekwa rehani ila kuuzwa moja kwa moja waswahili wanasema Palipo na rehani kuna Pawnshop au sio?. Na Pawnshop usiporudisha on time kinafanyika nini?...

Na ndio maana nasema huwezi kuvuta maji wakati huna kiwanja, huna haki ya kujenga nyumba na kadhalika mipango inaanza ktk ujenzi wa nyumba..Sisi tunavuta gas kupeleka Dar ili kuzalisha Umeme, Je mitambo yenyewe tayari mmeisha nunua maana hivi sasa hatuna kwa madai gharama ni kubwa kuagiza mitambo ya 100mw, serikali haina uwezo - hatuna fedha sasa tutaweza kweli inapotakiwa megawatts 500?...

Jamani, na haya kweli majibu kwa watu tuloishi Ulaya?.. Serikali inahitaji iwe na fedha cash ili kununua mitambo ya umeme kweli? au serikali zetu hukopeshwa na mabenki ya dunia au hata Makampuni yenyewe yanayotengeneza mitambo hilyo kwa kuwekeana mkataba! eeeh! lakini wanakazania nchi yetu haina uwezo wakati tunaendelea kukodisha umeme kwa mashirika ambayo kwa mwaka mmoja tu tunalipa gharama sawa na kununua mtambo wa megawatts 1000, Leo tuna miaka 7 tunaliwa na kama kawaida yao Tanesco ndio wenye matatizo tunawapa fedha kibao.. Fedha gani? ukichunguza kumbe wanapewa fedha za kulipia madeni.. madeni ambayo kampuni zao zinalipwa..umeona mchezo huo?.... damn!...

Sasa je tukishaingia gharama za kuweka hilo bomba tutapata wapi fedha za kununua mitambo?.. hakuna jibu isipokuwa utaambia sijui kuna 45mw za temeke na 100mw Segelea na Tabata.. Well in total zinajengwa ngapi?... ooooh kama 200 hivi lakini tutaweze kuongeza baadaye!. Jamani, mahitaji ya jiji la Dar leo na vitongoji vyake inafika 500 to 800 mw kirahisi kabisa maadam half ya population hawana umeme. Sasa kwa nini hatuna mpango tayari wa kuzalisha hizo 800 au 1000mw kabisaaa tuwatoe hao kina IPTL kabla ya kujenga bomba? Hutapata jibu..
 
Na ndio maana nasema huwezi kuvuta maji wakati huna kiwanja, unavuta maji kupelekja Dar ili kuzalsisha Umeme Je mitambo yenyewe tayari mmeisha nunua maana hivi hatuna gharama kubwa wanasema serikali haina uwezo sijui hatuna fesha... jamani haya kweli majibu kwa watu tuloishi Ulaya?.. Serikali inahitaji iwe na fedha kununua miatmbo ya umemem kweli au hukopeshwa na mabenki ya dunia au hata Makampuni yenyewe yanayotengeneza mitambo hilyo kwa kuwekeana mkataba! Heee lakini wanakazania nchi yetu haina uwezo wakati tunaendelea kukodisha umeme kwa mashirika ambayo kwa mwaka mmoja tu tunalipa gharama sawa na kuinunua mtambo wa megawatts 1000, Leo tuna miaka 7 tunaliwa na kama kawaida ytao Tanesco ndio wenye matatizo tunawapa fedha kibao.. Fedhab gani ukichukuza kumbe za kulipa madeni...

Tuko pamoja Mkandara, nchi yetu watu wako bize kuangalia namna gani wanaitafuna na si namna gani ya kuikwamua kutoka katika hali duni na kuipandisha juu. Hiyo kwenye bluu ni sawa kabisa na kama utakumbuka ATCL walikodi ndege huko Dubai ambayo imekaa juu ya mawe kwa kipindi kirefu sana bila kuzalisha na bill yake ilifikia zaidi ya bilioni 322 ambazo zinatosha kununua ndege kubwa mbili mpya, unaona huo ujinga? Yaani mpaka inatia hasira, unajiuliza hivi kweli hawa wafanya maamuzi wanakuwa wanafikiria nini wanapoingia maamuzi ya kuiletea hasara nchi yetu? Pengine ni kutokana na wahusika kutochukuliwa hatua kali ndo maana madudu ya kila namna yanaibuka kila siku. MUNGU atusaidie kwa kweli waTZ.
 
Mnyika leo kadhihirisha nini anakifanya bungeni yeye pamoja na kambi rasmi ya upinzani hongera sana mnyika hongera sana kambi ya upinzani,achana na hao wanaouota urais mchana na usiku
 
HOTUBA YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA NISHATI NA MADINI JOHN JOHN MNYIKA (MB) KUHUSU MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2011/2012 NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, awali ya yote niungane na wote wenye mapenzi mapema katika kuomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu wakati tukitimiza wajibu wa kibunge kwa mujibu wa ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Kanuni Kudumu za Bunge (Toleo la mwaka 2007) kifungu cha 99 (7) wa kuishauri na kuisimamia serikali; kwa kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2011/2012 na makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Mheshimiwa Spika, nitumie pia nafasi hii kuwashukuru Watanzania wenzangu wa kada, hadhi na ngazi mbalimbali katika taasisi na maeneo mengi ndani na nje ya nchi waliouniunga mkono kwa hali na mali katika kipindi chote cha misukosuko ya kusimamia ukweli na uwajibikaji: katika kuifuatilia serikali na kuunganisha wadau wengine kuwezesha maendeleo katika jimbo la Ubungo; wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya ushindi wetu; wakati wa operesheni za
2
kuhamasisha mabadiliko katika maeneo mengine nchini na katika uwakilishi wa wananchi bungeni. Utaratibu wa kupokea maoni na kutoa taarifa za mara kwa mara za maendeleo kupitia mikutano na wananchi pamoja na katika mtandao wa JOHN MNYIKA tutaendelea nao. Kaulimbiu yetu ni ile ile: AMUA; Maslahi ya Umma Kwanza.
Mheshimiwa Spika; Sekta za Nishati na Madini zina umuhimu maalum katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi katika kipindi cha sasa na muda mrefu ujao. Wakati nishati ikiwa nyenzo ya kuendesha maisha ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ya wananchi na nchi kwa ujumla; madini ni mtaji na ni kati ya mitaji mikubwa ya kuwezesha maendeleo ya haraka ya taifa. Hata hivyo, pamoja na Tanzania kujaliwa rasilimali hizi nyingi ikiwemo watu, ardhi yenye rutuba, maji (bahari, mito na maziwa), kuwa katika eneo la kimkakati la kijiografia kwa biashara na maliasili, bado takwimu za hali ya uchumi kwa mwaka 2011 zinaonyesha sehemu kubwa ya Watanzania wako kwenye lindi la umaskini.
Mheshimiwa Spika, tunajadili sekta za nishati na madini wakati taifa likiwa kwa mara nyingine tena kwenye tishio la mgawo wa umeme pamoja na serikali kukanusha kwamba hakutakuwa na mgawo wa umeme. Tunajadili mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2011/2012 wakati kwa mara nyingine tena kukiwa na mvutano
3
baina ya watendaji waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakiwa katika mvutano ambao umeambatana na kutuhumiana hadharani kupitia vyombo vya habari juu ya tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

Tunajadili makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2012/2013 wakati kukiwa na tuhuma za vigogo wa serikali kuingiziwa fedha kifisadi katika akaunti zao za nchini Uswisi na makampuni ya nje ya utafutaji na uchimbaji wa madini, mafuta na gesi asili huku viongozi wa dini wakiwa wamezindua ripoti juu ya ukwepaji kodi na upotevu wa mapato kwa serikali unaogusa pia makampuni kwenye sekta za nishati na madini (The One Billion Dollar Question).
Mheshimiwa Spika, namuomba kila mmoja wetu atafakari kwa ukweli wa nafsi na nafasi yake tumefikaje hapa kama taifa na kwa pamoja tukubaliane kuwa wabunge tuwajibike kuisimamia serikali kuhakikisha maazimio yote ya bunge kuhusu sekta za nishati na madini ya miaka mbalimbali yanatekelezwa kwa haraka na kwa ukamilifu.

Naamini iwapo maazimio ya Bunge juu ya Mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Richmond Development Company LLC yangetekelezwa yote na kwa wakati toka mwaka 2008, maazimio ya bunge juu ya uendeshaji wa sekta ndogo ya gesi asili ya mwaka 2011 yangezingatiwa yote na kwa haraka, maazimio kuhusu uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni ya mwaka 2011 yangechukuliwa
4
kwa uzito unaostahili; taifa lingeepushwa kurudia mijadala ile ile kuhusu Wizara hii hii mara kwa mara. Aidha, kambi rasmi ya upinzani inatoa mwito kwa bunge kupitisha maazimio ya kutaka uwajibikaji wa serikali kwa kushindwa kutekeleza maazimio ya bunge kwa ukamilifu na kwa wakati.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Katiba ya Nchi Ibara ya 52 (1) Waziri Mkuu ndiye mwenye madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni. Ni muhimu basi, badala ya kupokea majibu ya Wizara ya Nishati na Madini pekee ambayo imeendelea kugubikwa na lundo la tuhuma mbalimbali, Waziri Mkuu atoe kauli bungeni kuhusu kujirudia rudia kwa madai ya ufisadi na uzembe katika sekta za nishati na madini.
Aidha, pamoja na mabadiliko ya Mawaziri, Manaibu waziri, Makatibu wakuu na Wakurugenzi wa Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake ya mara kwa mara, Rais ashauriwe kutumia nguvu zake za kikatiba za ibara ya 33, 34, 35 na 36 kuwezesha hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wote waliotuhumiwa kwa ufisadi, uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya madaraka kwa mujibu wa maazimio ya bunge na taarifa mbalimbali za serikali ili kurejesha misingi ya uadilifu na uwajibikaji katika sekta za nishati na madini.
5
Mheshimiwa Spika, hivyo kwa ujumla mjadala wa mapitio ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ulenge katika kuliepusha taifa letu kuendelea kutumbukia katika ‘laana ya rasilimali' kama ilivyojitokeza katika mataifa mengine. Tuhakikishe tunalinda uhuru wa taifa letu dhidi ya uporaji wa ardhi na rasilimali zake yakiwemo madini, mafuta na gesi asili ulio katika tishio la ubeberu mamboleo, ufisadi na udhaifu wa kimifumo. Aidha, kupitia mchakato wa katiba mpya wananchi watoe maoni ya kuhakikisha kuwa rasilimali za muhimu ikiwa ni pamoja na madini, mafuta na gesi zinawekewa mfumo wa kunufaisha watanzania wote na pia mikataba kuhusu rasilimali hizo inaridhiwa na Bunge.
Tuchangie mjadala wa sekta hizi nyeti tukikumbuka maneno ya hayati Mwalimu Nyerere katika kitabu chake cha TUJISAHIHISHE cha mwaka 1962, nanukuu: "Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi wote tunayo tamaa hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza ukamfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni ubinafsi mbaya sana"
6
MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2011/2012
Mheshimiwa Spika, tarehe 15 Julai 2011 niliwasilisha bungeni maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2010/2011 na makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2011/2012. Kufuatia maoni hayo, yapo masuala machache ambayo Serikali imeyazingatia kwenye utekelezaji na mengine mengi serikali haikuyazingatia pamoja na umuhimu wake kwa maslahi ya nchi na maisha ya wananchi. Hivyo kupitia mapitio haya ya utekelezaji, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka serikali ieleze hatua ilizochukua juu ya maoni hayo ambayo baadhi yalijitokeza pia kwenye maoni ya Kamati za Kudumu za Bunge na michango ya wabunge kwa nyakati mbalimbali. Hakuna sababu ya kutumia muda mrefu kutoa na kujadili maoni mapya ikiwa hakuna mfumo thabiti wa kuhakikisha maoni na maazimio yanatekelezwa kwa wakati na kwa ukamilifu.

BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI GUMZO LA JIJI
 
Mi niliadhani wameifisadi hii nchi mpaka mifupa, kumbe bado kuna minofu ya kufisadi!

Asante sana Mh: Mnyika, boy you are as brilliant and composed as I like. Please keep your feet on the ground then we'll have good rewards.

Ok Zitto anadai anasimamia sheria na kanuni, hata kama zinadhulumu na kuua Taifa hili yeye anazo! Tumemjua rangi yake, na CHADEMA wawe makini na waanze kuchukua hatua zinazoonekana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom