Hotuba ya kutisha!!!!!!!!

nikiwa ndani ya daladala asubuhi hii, karibu nusu ya abiria walikuwa wanajadiri kitendo cha serikali kuingilia kati matibabu ya babu loliondo wengine walikuwa wakipinga na wengine wakiunga mkono, wakiwa wanaendelea kubishana, ghafla nikasikia redioni mtu anahutubia taifa sauti kama jk hivi.

Serikali yenu mliyo ichagua itahakikisha haiingilii imani za watu maana serikali yenu haina dini, ila kutokana na ukweli kwamba serikali inawajibika kumlinda mwananchi na mambo yanayoweza kumuathiri kwa namna yeyote ile, serikali yenu inaangalia uwezekano wa


  1. kusitisha kwa mda matibabu ya babu loliondo mpaka ijiridhishe na ubora wake.
  2. kusitisha kwa mda ubatizaji makanisani kwa kutumia maji mpaka ijiridhishe kama maji yanayotumika kubatizia ni maji safi na salama kwa matumizi ya binaadam.
  3. kuzuia kwa mda matumizi ya ubani wakati wa kuendesha sala na ibada mbalimbali mpaka ijirishishe kwamba ule moshi hauathiri afya za binaadamu.
  4. kusitisha matumizi ya biblia na quran kwa mda tunataka kuunda kamati maalum itakayochunguza kisayansi kama yaliyomo ni ya kweli au la. Hii tunaifanya kwa makusudi ya kumlinda mlaji wa hivi vitabu.

ghafla nikasikia kelele za "coins" nikashtuka usingizini na kumuona konda anataka nimlipe nauli yake kumbe nilikuwa ndotoni!!!!!!!!.





we unaleta ya kibwetele, tuache yatokee ya kibwetele, ndoto yako inakaukweli kiasi fulani.................................
 
ahahahaha nimeipenda kweli,
wewe ni g.thinker ndo mana ndoto zako zipo great.
 
Afadhali ulishituliwa na konda ole wako ungeendelea kuota halafu ukapata hasira na kuanza kuvunja vunja radio kumbe una mnyuka jirani yako makonde hapo ingekuwa balaaa
 
mkuu kwenye daladala unalala mpaka unaota bila shaka ni gmboto - tegeta
 
Pole kwa uchovu mkuu...mpaka kupata usingizi mnono kiasi cha kuota!! uliupiga haswa hata Ngele..utakuwa ulimzidi kwa kuuchapa kwenye "kadamnasi" tena mbele ya umati wa watu

Nikiwa ndani ya daladala asubuhi hii, karibu nusu ya abiria walikuwa wanajadiri kitendo cha Serikali kuingilia kati matibabu ya Babu Loliondo wengine walikuwa wakipinga na wengine wakiunga mkono, wakiwa wanaendelea kubishana, ghafla nikasikia redioni mtu anahutubia Taifa sauti kama JK hivi.

"Serikali yenu mliyo ichagua itahakikisha haiingilii imani za watu maana serikali yenu haina dini, ila kutokana na ukweli kwamba serikali inawajibika kumlinda mwananchi na mambo yanayoweza kumuathiri kwa namna yeyote ile, Serikali yenu inaangalia uwezekano wa



  1. Kusitisha kwa mda matibabu ya Babu Loliondo mpaka ijiridhishe na ubora wake.
  2. Kusitisha kwa mda ubatizaji makanisani kwa kutumia maji mpaka ijiridhishe kama maji yanayotumika kubatizia ni maji safi na salama kwa matumizi ya binaadam.
  3. Kuzuia kwa mda matumizi ya ubani wakati wa kuendesha Sala na ibada mbalimbali mpaka ijirishishe kwamba ule moshi hauathiri afya za binaadamu.
  4. Kusitisha matumizi ya Biblia na Quran kwa mda tunataka kuunda kamati maalum itakayochunguza kisayansi kama yaliyomo ni ya kweli au la. Hii tunaifanya kwa makusudi ya kumlinda mlaji wa hivi vitabu."


Ghafla nikasikia kelele za “Coins” nikashtuka usingizini na kumuona konda anataka nimlipe nauli yake kumbe nilikuwa NDOTONI!!!!!!!!.




 
we! Siku hizi watu wakisinzia hadharani ni mwiko kukiri ulisinzia. Sema ulikuwa unasali au unakemea mapepo.
 
Unajua sijawahi kuchangia sehemu hii ya udaku na mara nyingi huwa sivijari humu kabisa. Niliingia hapa kutokana na curiosity ya hii headline sasa wakati naanza kusoma maneno haya...
Nikiwa ndani ya daladala asubuhi hii, karibu nusu ya abiria walikuwa wanajadiri kitendo cha Serikali kuingilia kati matibabu ya Babu Loliondo
... sikuwa makini sana (yaani sikuwa attentive na ninacho kisoma), nikaendelea kusoma mpaka nikafika hapa...

ghafla nikasikia redioni mtu anahutubia Taifa sauti kama JK hivi.

... hapo pia sikuwa na shaka (nikasema inawezeka ni kweli) kwasababu nipo mbali na nyumbani kwahiyo yanayozungumzwa redioni siyafahamu, mambo ya bongo nayapatia hapa JF.

Nilipofika hapo...

"Serikali yenu mliyo ichagua itahakikisha haiingilii imani za watu maana serikali yenu haina dini

... pia sikuona tatizo kwasababu nilishasoma hapa jamvini kuwa wamesitisha huduma ya babu, nikaendela mpaka hapa...

  1. Kusitisha kwa mda matibabu ya Babu Loliondo mpaka ijiridhishe na ubora wake.
kufika namba mbili...

2. Kusitisha kwa mda ubatizaji makanisani kwa kutumia maji

Nikasituka! (kumbuka sikujua nipo jukwaa gani), ghafla nikaanza kutia shaka na ninacho kisoma kwasababu mara nyingi wakati na soma kitu hupenda kusoma huku nikiangalia lengo la mwandishi. Kwahiyo nikaacha kusoma kabisa na kuangalia juu kwenye browser bar kutaka kujua kama ninacho kisoma ni kweli au ni mauzauza tu.

Ndipo niakaona https://www.jamiiforums.com/jokes-utani-udaku-gossips/116935-hotuba-ya-kutisha-2.html. Nilicheka sana huku nikamalizia kusoma.

Mkuu ubarikiwe kwa kutupatia kisheko hiki kweli kuna watu mmejaaliwa ku-hit home katika ujumbe.
 
Back
Top Bottom