Hotuba ya JK ya Mwaka Mpya 2010

...kweli eeeh? charity starts at home, hebu jifikirie kwenye bajeti ya mwaka mzima nyumbani kwako, ilhali wewe ndiye unashikilia funguo za Fedha na Uchumi. Ukabana kila kitu ili ufanikishe kilimo kwenye ekari zako kadhaa. Fikiria, ukajiwekea fungu la kutosha tu kwenye bima ya afya au sijui AAR, na fungu jingine ukawekeza kwenye Elimu!...

Vipi gharama masuala ya Miundombinu ya kukupeleka huko kwenye hizo Investments na kwenye mihangaiko yako ya kila siku?, hii yawezekana ikawa ni daladala, teksi, lori au hata motokaa.

Vipi gharama za Ulinzi kulinda nyumba ukiwa huko maungani? na je, ushirikiano na majirani zako achilia mbali ndugu jamaa na marafiki wa Kimataifa maana vikadi vya mchango haviishi...wakati huo huo, gharama za Luku, Mkaa, Kuni au gesi za kupikia na Mishumaa inakusubiri kwenye Nishati!

Naendelea kutoa mifano ya kufinya bajeti; Mawasiliano na technolojia, hata kama kuna longa longa na cheka time, bado vocha inakula pochi, achilia mbali airtime angalau kudodosa mawili matatu JF?.

Tukija kwenye Mambo ya ndani ndio usiseme, familia ina mahitaji yao muhimu tena ya kila siku, na inakubidi uyadhibiti ili kuweza kudhibiti sheria na katiba ili maliasili watu na wasilia visihujumiwe... pamoja na yote bado kuna mahitaji ya Chakula, Mifugo, na hata watoto kwenye Ustawi wa Jamii...

...hapo bado hujajikatia allowance kidogo, au kaji day-out katika kuburudisha mawazo kwenye 'michezo,' mila na utamaduni! All in all, juhudi yako yote kwenye ile Doubling up bajeti ya Afya, Elimu na hasa Kilimo, haitakuwa na maana iwapo hujawekeza kwenye kutangaza soko la bidhaa zako, hapa namaanisha Biashara!
...kwenye hii dunia ya tatu, mtumishi wa serikali au mashirika ya umma itabidi tu upokee 'mlungula'.

Serikali wao hawana 'mlungula', ila huomba misaada nje kufidia pale penye mapungufu kwenye pato la taifa.
Great Job Muungwana na team yako, lakini juhudi zaidi zinahitajika ili kuikwamua nchi na wananchi wake.

Kumradhi kwa mfano niliotoa, lakini nimejaribu kuangalia picha kwa ukubwa wake.

Mkuu, kwa heshima nadhani umeangalia picha bila umeme, yaani umeshindwa kabisa kufikiria kwa ukubwa.

Kumbuka investment nilizozitaja yaani kwenye elimu, kilimo na afya ni basis ya kufumua uchumi wote na kukuza kipato kwa asilimia kubwa ya asilimia 80% ya wananchi wetu wanaotegemea kilimo na kuishi vijijini.

Sasa kwa kukusaidia tu ni kwamba, kama investment ya kweli itafanyika kwenye kilimo kwa asilimia kubwa basi wananchi vijijini watakuza vipato vyao na kuweza kuinvest hizo hela kwenye mahitaji yao muhimu mfano ujenzi wa nyumba, kupeleka watoto shule, kuanzisha biashara blah blah.

wafanyabiashara watafaidika kwa kusupply vitu, serikali itafaidika kwa kupata kodi, makampuni makubwa ya simu, bia, sigara, cement nk yote yatafaidika na kuongeza investment blah blah in SHORT UCHUMI MZIMA WA NCHI UTAKUWA.

Nchi zote zilizoendelea zinajali sasa kipato cha watu wa chini sababu wao ndio wanaobeba uchumi mzima, yaani watu wa chini wakiwa hawana pesa, basi PYRAMID YOTE INADONDOKA.
 
Hali ya Uchumi wa Taifa

Ndugu Wananchi;
Mwaka uliopita ulikuwa mgumu sana kwa ustawi wa uchumi wa nchi yetu. Matarajio na malengo yetu makuu kuhusu ujenzi na maendeleo ya uchumi wetu hatukuweza kuyafikia. Mauzo yetu ya nje ya bidhaa na mazao ya kilimo, mifugo, viwanda na madini yalipungua kwa kukosa masoko katika nchi za Ulaya, Marekani na Asia. Bei za mazao na bidhaa zetu hizo iliporomoka sana. Watalii walipungua na mapato ya utalii kushuka pia. Wawekezaji wameahirisha uamuzi wa kuwekeza nchini. Biashara ya uchukuzi wa mizigo iendayo na itokayo nchi jirani ilipungua sana. Mapato ya Serikali yakapungua kwa asilimia 9. Jumla ya yote kasi ya kukua kwa uchumi inatarajiwa kushuka kutoka lengo la asilimia 7.8 na kuwa asilimia 5. Hii ni athari kubwa sana kwa taifa letu.

Pamoja na kuwepo kwa sababu nyingine, hali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na matatizo makubwa na ya aina yake yanayoukabili uchumi wa dunia kuanzia mwaka 2007 na kuwa mbaya zaidi tangu mwaka 2008 hadi sasa.

Kama mtakavyokumbuka Juni 10, 2009, mjini Dodoma, nilitangaza Mpango Maalum wa Dharura wa Taifa wa kuhami na kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Kama nilivyoeleza mpango huo umekadiriwa kugharimu takriban shilingi bilioni 1,600 (au shilingi trilioni moja na bilioni mia sita).

Ndugu Wananchi;
Kwa hakika hii ni gharama kubwa mno kwa nchi maskini kama yetu kubeba lakini ilikuwa hapana budi kufanya hivyo. Kufanya kinyume chake kungeifanya hali ya uchumi wa nchi yetu kuwa mbaya zaidi. Utulivu tulionao katika uchumi mkuu ungetoweka na mambo mengi yangeparaganyika. Kama tungeiacha hali ifikie hapo huenda hata utulivu wa kisiasa tunaojivunia nao ungetetereka pia. Kutofanya chochote isingekuwa uamuzi wa busara kuchukua pamoja na ukweli kwamba kwa kupeleka kiasi kikubwa cha fedha kama hiki kwa ajili ya kunusuru uchumi kumepunguza fedha ambazo zingetumika kwa ajili ya shughuli nyingine za maendeleo na Serikali.

Ndugu zangu, Watanzania Wenzangu;
Katika Mpango wetu wa Dharura, miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni ile ya Serikali kubeba mzigo wa madeni ya Benki ya makampuni, na watu waliopata hasara kutokana na kupungua kwa mauzo nje na kuanguka kwa bei za mazao na bidhaa wanazouza katika soko la dunia. Nia yetu ilikuwa kuzuia wasifilisike na mabenki yaliyowakopesha yasiathirike. Pia tulichukua uamuzi wa kufidia bei ya pamba kwa shilingi 80 kwa kilo ili kumpunguzia mkulima mzigo wa hasara na kuwapa moyo waendelee na kilimo cha pamba msimu unaofuata. Tulifidia zao la pamba kwa kuwa ndilo zao lililoathirika zaidi kuliko mazao mengine yote.

Ndugu Wananchi;
Katika mpango wetu huo pia tulianzisha mfuko maalum wa uwekezaji ili kuyapa imani mabenki ambayo yalipata hofu ya kukopesha yaendelee kutoa mikopo kwa wafanyabiashara na wawekezaji. Kwa upande wa Serikali yenyewe mpango huo ulilenga kukabiliana na tatizo la kupungua kwa mapato ya Serikali.

Nafurahi kusema kuwa utekelezaji wa Mpango wetu wa Dharura wa Kuhami na Kuimarisha Uchumi unakwenda vizuri na takriban malengo yote tuliyojiwekea yametekelezwa kama tulivyokusudia. Ni matumaini yangu kuwa utekelezaji wa Mpango huu utafanikiwa ili kuzuia kudidimia zaidi kwa uchumi wa nchi yetu na kusaidia kuuimarisha.

Ndugu zangu, Watanzania Wenzangu;
Mwaka 2010 tunaouanza kesho hautakuwa mwepesi ingawaje tunatarajia kuwe na nafuu kiasi kuliko mwaka huu. Yapo mambo mawili yananifanya niwe na matumaini hayo. Kwanza, kasi ya kuporomoka kwa uchumi katika mataifa makubwa tajiri kulikochimbuka matatizo haya inaelekea kudhibitiwa. Pili, hatua za dharura tulizozichukua zinaelekea kufanikiwa kwa kiasi fulani kuzuia uchumi usididimie na baadhi ya sekta zimeonyesha dalili za kuimarika ikiwemo sekta yetu kuu ya utalii.

Pamoja na hayo, sina budi kukumbusha kuwa safari yetu bado ni ndefu na kuna vikwazo vingi vya kuvuka. Hatuna budi kutambua wajibu wetu wa kufanya kazi kwa makini zaidi, bidii zaidi na maarifa ili tuweze kukabiliana sawasawa na athari za msukosuko wa uchumi wa dunia na kushinda.

Mtanzania ataendelea kuwa masikini ikiwa mtazamo wa Rais wa Tanzania ni kama huu na uchambuzi wake wa mfumo wetu wa uchumi na vipaumbele vitatumia mantiki ya namna hii.

Lakini naona kasahau na kujisuta kwa hilo la mwisho ka wajibu wa kufanya kazi kwa makini, bidii na maarifa zaidi.

Mpaka sasa Mheshimiwa Rais, hujaweza kumuonyesha mtu yeyote duniani kuwa unafanya kazi kwa bidii, umakini na maarifa. Uongozi wako ni wa kivivu, kizembe, kulalamika, kukosa umadhubuti, hauna ufanisi, hauna mwelekeo , hauna maadili na ni kinyume kabisa na kauli zako na hotuba unazowahadaa Wananchi kujifanya u msikivu na mwelewa wa yanayoendelea Tanzania.

Umeongelea kwa kiduchu suala la uawjibikaji na kero zinazolisumbua Taifa za uhujumu na ufisadi na athari zake kwa jamii na uchumi wetu. Sidhani kama ulidhamiria hata kulizungumzia kwa maana linakusuta kwa kuwa umekumbatia na kushikamana na wahujumu wa Uchumi na Mafisadi!

Nikirudi kwenye hili la Uchumi, unaonyesha wazi ulivyo na udwanzi wa kuelewa mambo au ni dharau yako na Serikali yako na zaidi kuwakejeli Watanzania.

Kama Mapato ya Serikali yamepungua kwa asilimia 9, Serikali imechukua hatua gani kukaza mkanda na kupunguza matumizi ili hicho kidogo kende kwenye shughuli za maendeleo ambazo ndio muhimu katika kututumua na kuinua uchumi?

Iweje leo na halii hii mbaya ya Uchumi, chini ya Uongozi wako Tanzania inaendelea kukosa umeme wa kutosha, lakini Viongzi wanaendelea kujiongezea mishahara na marupurupu, matumizi yasiyo ya lazima na bila busara kama ujenzi wa nyumba ya Gavana na mkuu wa Shirika la Tanesco yameendelea na kwa gharama kubwa, Chama chako bila aibu kimeamua kuagiza magari 200 ya kifahari ili kukisaidia kiendehse kampeni ya uchaguzi ifikapo Oktoba, na matumizi mengine mengi yasiyoleta maana wala kueleweka lakin bado unatalii dunia nzima na bakuli kuitangaza Tanzania nakuomba omba kama Mzee Matonya?

Ni heri ungekaa kimya, na umalizie hotuba yako kwa kumshukuru Mungu kama ulivyofanya katika mwanzo wa hotuba yako.

Shame on you Mr. President!
 
wadanganyika ni majitu ya ajabu, kabisa kazi yao kulaumu tu hamuoni hapo kwenye hotuba ya (ni rahisi au rais mimi sajui kiswahili bana) kila jambo litafanyika mwaka 2010? ("Matengenezo ya mtambo wa Songas ulikamilika na Kihansi bado mpaka Januari 2010". "Wakati wowote mwezi Januari mwaka 2010 umeme utawaka Kilindi', "Kwa upande wa usafiri wa anga mwaka huu Serikali imeendelea na jitihada za kuimarisha utendaji na uendeshaji wa Shirika la Ndege la Tanzania. Pamoja na hayo, pia Serikali imeendelea na mchakato wa kupata mbia wa kushirikiana nae kuendesha shirika hilo. Ni matumanini yangu kuwa mchakato huo utakamilika mapema mwaka 2010 ili shirika letu tulipe matumaini mapya ya uhai na maendeleo".
Katika mwaka ujao tunategemea mambo kuwa mazuri zaidi. Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa zile barabara za Tanga – Horohoro, Tunduma – Sumbawanga na Namtumbo – Songea – Mbinga zitaanza kujengwa. Mchakato wa ujenzi wa barabara hizo zinafadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia mfuko wa Millennium Challenge Account, hivi sasa imefikia hatua ya uteuzi wa makandarasi wa barabara hizo. Kazi hiyo ya uteuzi inatarajiwa kukamilika robo ya kwanza ya 2010 na ujenzi kuanza katikati ya mwaka. Ratiba ni hiyo hiyo kwa miradi mingine inayofadhiliwa na MCC.
) yaani miaka yote alikuwa najipanga na kuandaa mambo hivyo utekeleza wa mambo yote ni kuanzia mwanzoni mwa 2010 mpaka kufikia october 2010 yote yatakuwa yamefanyika na kukamilka, yaani ni kama kulipua boma ya pwaaaa kila kitu kimefanyika na kukamilia. jinsi raisi alivyoutaja mwaka 2010. kwanza kaanza kwa kuukaribisha mwaka 2010. pili UHALIFU KUZIBITIWA nanukuu "nawapongeza sana wenzetu wa jeshi la polisi kwani kwa mwaka 2009 walitajwa kwa kuongoza kwa ruswa nchini nawaomba mwaka 2010 waongeze juhudi mara dufu mimi naendela kuwahaidi msaada na ushirikiano wangu".

"Napenda kumalizia salamu zangu za mwaka mpya kwa kumshukuru tena Mwenyezi Mungu kwa rehema zake alizotujalia mwaka 2009. Tumuombe atuzidishie maradufu yale yaliyo mema na kutunyooshea yasiyokuwa na maslahi mema kwetu katika mwaka ujao 2010". (yahaani unamshukuru mungu kuwa ufisadi mliofanya mwaka 2009 kuwa ni rehema na kuwa azidi kuwanyooshea yale yasio na mslahi kwa taifa mzidi kuyafanya kwa mwaka 2010 au unamaanini nini hapo ?)


WALAU HII ITAPUNGUZA SAFARI MOJA YA NJE
Pengine katika heshima kubwa na muhimu tuliyoipata mwaka huu ni ile ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa masuala ya kiuchumi Barani Afrika uitwao World Economic Forum on Afrika. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mikutano hyo kufanyika nje ya Cape Town, Afrika Kusini. Ni heshima kubwa kwa Tanzania, hivyo nawaomba Watanzania wenzangu na hasa wananchi wa Dar es Salaam kuwapokea vizuri wageni wetu wazito kwa utajiri na maarifa. Tuoneshe ukarimu wetu wa kawaida kwa wageni wetu ili wapende kurudi tena Dar es Salaam na Tanzania kwa mikutano mingine au matembezi na shughuli nyingine.



huwenda niko kwenye wale asilimia 70 aliowataja maana hapa sijaona alichoongea.

Kitalolo,

Rahisi (sic) anaashiria kuwa kazi iliyomshinda kwa miaka minne na ahadi zote tangu mwaka 2005, atazifanya kwa ukamilifu kwa miezi 10 ili ikifik Oktoba, achaguliwe tena.

Kama itamchukua miezi 10 kufanya kazi ya miezi 48, alikuwa anachelewa nini na wapi kufanya hilo pale alipochaguliwa? Yaani turidhike naye kwa kukosa kuwajibika na mwamko wa kupima vipaumbele na kuleta maendeleo kwa kutudumaza kwa miezi 48?

Gademu shiti!
 
Kwani chanzo cha mgao wa umeme ni nini na rais wa nchi anawezaje kumaliza shida hiyo? MImi nilidhani TZ tulishaondoka katika zile zama za kufikiri rais tu ndiye anayeweza kuleta mabadiliko nchini peke yake. Matatizo ya Tanzania ni ya jamii nzima na yanahitaji kubadilika kwa mawazo ya jamii nzima. Imetuchukua muda mrefu kufikia kwenye hiyo hali mbaya tuliyonayo sasa hivi, na sote tunaelewa kwamba sababu si JK.Tutakuwa tunajidanganya kama tunategemea rais JK aimalize kwa muda mfupi. Kama tunataka kuwa waganga wakutibu maradhi yanayoisibu Tanzania inabidi tujue chanzo na namna bora na mpya za matibabu na kuyatumia kwa vitendo. Kulaumu tu wale wanaojaribu kutoa matibabu bila kusaidia kwa vitendo, hata kama uwezo wao ni duni hakutusaidii.
 
Usafiri wa Anga



Ndugu Wananchi;


"Kwa upande wa usafiri wa anga mwaka huu Serikali imeendelea na jitihada za kuimarisha utendaji na uendeshaji wa Shirika la Ndege la Tanzania. Pamoja na hayo, pia Serikali imeendelea na mchakato wa kupata mbia wa kushirikiana nae kuendesha shirika hilo. Ni matumanini yangu kuwa mchakato huo utakamilika mapema mwaka 2010 ili shirika letu tulipe matumaini mapya ya uhai na maendeleo"



Ni dhahili kwamba wasaidizi wa Jakaya hawamuambii ukweli kuhusu muwekezaji wa kichina ambaye hata bunge liliambiwa kuwa mchakato ulikuwa umefikia hatua za mwisho wa mbia huyo kuja kuwekeza; inaelekea mchina hana nia tena ya kuja kuwekeza ATCL na ndio maana watendaji wa wizara imewawia vigumu kuwasiliana nae na mara nyingi ahadi zake huwa hazitekelezi. hili linajidhihilika pale waziri Kawambwa na katibu mkuu wake walipopitia Uarabuni wakitokea China na kuwasiliana na waarabu ili waje kuwekeza ATCL!! Bahati mbaya kwa shirika ni kwamba wizara ndio iko mstari wa mbele katika kutafuta muwekezaji na hili lina athari zake kwani watendaji wengi wa serikali wakiwamo mawaziri kama tulivyoona sio waadilifu; wizara ya miundombinu haina capacity ya kuweza kuhandle ubinafsishaji wa shirika kwahiyo kuepuka yaliyotokea enzi za SAA ni vyema exercise hii ikafanywa na wataalam wakishirikiana na bodi ya wakurugenzi. Wengi tunahisi kitendo cha wizara kutaka kuendesha mambo ya ATCL ni njia ya watendaji kutafuta upenyo wa kufanya ufisadi!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom