Hotuba ya JK kwa Taifa mwisho wa mwezi Februari 2010

mimi nadhani JK haishi katika muda tunaoishi maana miezi mingine ina mwisho mingine haina!

Hahahaa! Ngoja tuone. Mwezi ujao unaweza kuwa na 93 days.
Mm sijaona alichoongea wala sijui hii sheria itasaidia nn mtz wa namtumbo ambaye kituo cha afya kipo 15km kutoka alipo.
Hivi kwani isue ni rushwa kwnye uchaguzi au kutumia fedha nyingi? Kama ni matumizi, basi nyani haoni kundule.
Tutaona kama kaptni komba hatapewa brand new scania semi la kufany tours kwenye kampeni.
 
Pamoja na mapungufu yake. Kwa hili Rais ameliezea vizuri na kwa kweli maudhui ya sheria yakifuatwa vizuri yatatatua mambo mengi sana...

Kwangu mimi ninayeamini mifumo zaidi ya kubwatuka maneno nadhani ... hili ni miongoni mwa yale ambayo atatakiwa kujivunia kwenye utawala wake.

hii sheria inashughulikia vipi kampeni chafu za kuchafua wagombea? inalazimisha vipi vyama kuweka wazi vyanzo vyote vya fedha zake; inaweka mipaka kiasi gani cha fedha mwananchi wa kawaida anaweza kuchangia au taasisi?
 
Jamani eeh, tumpeni sifa na hongera rais. Labda tutaacha kusakamwa hapa JF na wageni wanaoingia na kupost post moja tu na kuondoka kwamba hatuna lolote zuri la kumsifia rais.
 
hii sheria inashughulikia vipi kampeni chafu za kuchafua wagombea?

Mzee mzima sheria ni ya matumizi ya fedha kwenye uchaguzi... this is so far the scope.

inalazimisha vipi vyama kuweka wazi vyanzo vyote vya fedha zake;
inaweka mipaka kiasi gani cha fedha mwananchi wa kawaida anaweza kuchangia au taasisi?

Sheria itaweka wazi hivi kwenye kanununi... lakini framework is ready... in reality sheria inajibu kiu yako yote!!! Yaani sheria imwachia waziri mwenye dhamana kuweka kanununi... na kwa kweli kila kitu kitakuwa wazi.

Shughuli ni kuisoma kuelewa ili iweze kutekelezeka badala ya kulalama.....
 
Naona mkuu ana imani kubwa na sheria hii ya uchaguzi kama ndio mwokozi wa yale yatakayojiri baada ya 2010.
Ngumu kujua fikra zake ila kama ni sheria tu, tunazo ngapi na hazitusaidii lolote?
 
Mzee mzima sheria ni ya matumizi ya fedha kwenye uchaguzi... this is so far the scope.



Sheria itaweka wazi hivi kwenye kanununi... lakini framework is ready... in reality sheria inajibu kiu yako yote!!! Yaani sheria imwachia waziri mwenye dhamana kuweka kanununi... na kwa kweli kila kitu kitakuwa wazi.

Shughuli ni kuisoma kuelewa ili iweze kutekelezeka badala ya kulalama.....


nilidhaani hiyo sheria tayari imeshapitishwa; bado?
 
nilidhaani hiyo sheria tayari imeshapitishwa; bado?

kilichobaki ni logistics za Rais ku-isaini tu! And he will... kwa kuwa yeye ndio chanzo... rejea hotuba yake ya 2005. and ya leo 28th Feb, 2010.

Kanuni a.k.a regulations zinafanywa baada ya sheria kusainiwa na ku-be-gazette kama iko now active!!!
 
Is it worthy listening?

Nadhani hizi ni hotuba za kukamilisha ratiba tu. Nilibahatika kuona hotuba yake ya mwisho wa mwaka. Nilimuona kama vile hakujiandaa (anasoma kwa kusukumiza na anakosea kosea), kachoka & uninterested.
 
Kama hamkuwa mkijua ni kuwa, rais keshaona alivyoharibu. Kila alipotaka kupagusa pana mtu wa karibu sana. Sasa anakuja upya, na believe me, hatatumia hela ya fisadi yeyote. Keshapata somo. The guy is cool but his crew is cruel
 
Rais Kikwete ameanza kuhutubia Taifa katika utaratibu wa mwisho wa mwezi. Ameanza kuzungumzia suala la rushwa katika uchaguzi kama alivyozungumzia kule kwenye Mkutano wa TAKUKURU Mwanza.. more to come..


Wakuu lazima muelewe kuwa, CCM wamesha anza kampeni. Viongozi wote wa Serikali wapo mikoani na mitaani, wakigawa fweza na vizawadi njaa, kuteka watu kifikra na kimawazo.

Jamaa wapo round ya kwanza ya Uchagu, kuweni macho, wakulu. Hivi Pinda yupo wapi? Makamu wa Rais na yeye yupo wapi? Mama wa Kwanza na yeye pia, lolz
 
Inamaana hakuna mtu aliyepelekwa mahakamani kwa sababu ya EPA ? BOT ? hakuna watu waliojiuzuru kwa ajili ya Richmond/Dowans ?

Katika mambo yote hujawahi kuona mafanikio ya serikali ya sasa ? Tanzania ni nchi inayokuwa kwa kasi sana kiuchumi afrika ya mashariki ukiacha rwanda

Can you say again! loudly
 
mie wala sioni baya alilolisema Muungwana
GT,
Wewe huwezi kuona ubaya. It is the timing. These things were supposed to have been
said/done long time ago, siyo kusubiri muda wa majeruhi wa uchaguzi mkuu. Watanzania si mabwege.
 
Tusisahau kwamba wanasiasa ni kama wanajimu mbao wanaahidi jambo halafu wakishindwa kulitekeleza wanakuja na sababu lukuki ili tuwaamini,wanaweza kuahidi kujenga daraja kwenye jangwa ukiwauliza mbona hakuna mito watakwambia tutaleta mitomsipate shida...kwa hiyo mimi ahadi za Kikwete nazichukulia kwa mtazamo huo.
 
Tatizo la Tanzania (na nchi nyingi za Africa) siyo kukosa sheria, bali ni kukosa uongozi unaoweza kuzifanyia kazi hizo sheria. Hata tukipata sheria zote zilizowasaidia wengine kuendelea, kama hatukujifunza kuheshimu utawala wa sheria hakuna chochote kitakachobadilika.
 
Msingi wa hotuba yake kasema ni sheria ijayo ya gharama za uchaguzi


Kwa hiyo ni hotuba anayoforecast sheria zitakazotungwa na bunge.Mi nadhani kama mambo mengine ni muhimu kuyaongea basi ayaseme PM sababu ndio kiongozi mkuu wa serikali bungeni.

Hii inaleta swali madarakana na wajibu wa PM yanaanzia na kuishia wapi na ya Rais yanaanzia wapi?
 
Hiyo sheria mpya ya uchaguzi ni msingi imara wa utawala bora,
Kwa hili Mh. Rais nampa pongezi zangu
Kwa wale waliosikiliza mpaka mwisho ile hotuba kama mimi, Rais alisema ametoa vidokezo tu vya nini hiyo sheria inataka, ila kuna mambo mengine mengi ambayo yamo ndani ya hiyo sheria ambayo hakuweza kuyaongelea.

Hii sheria imekuja wakati muafaka na itasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha misingi ya kweli ya utawala bora, kwani viongozi watachaguliwa kutokana na uwezo wao na sio fedha!

Ila tatizo linaweza kuwa kwenye implementation! Ila katika hilo nadhani hata sisi tunaweza kuplay our part if we are true activists wa utawala bora!
 
Back
Top Bottom