Hotuba Rasmi Kambi ya Upinzani - Makadirio ya Mapato na Matumizi Wizara ya Fedha na Uchumi 2012/2013

TeamZitto

Member
May 5, 2012
18
197
Full version inapatikana hapa HOTUBA YA WAZIRI KIVULI NA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI NDUGU KABWE ZUBERI ZITTO KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2012-2013 « Zitto na Demokrasia

Highlights:
Sakata La Rada bado bichi
2.5 MKOPO WAKUNUNUA RADA ILIYOGUBIKWA NA UFISADI
Mheshimiwa Spika, sehemuya Malipo ya Deni la Taifa ni Mkopo ambao Serikali ilichukua ili kununua Radakutoka kampuni ya BAE ya Uingereza. Suala hili la rada limejadiliwa sana nchinikwa upande mmoja tu wa ufisadi wa kupandisha bei ya Rada na hatimaye kurejeshwakwa iliyoitwa chenji ya Rada. Hiyo ilikuwa ni nusu tu ya ukweli kuhusu suala laRada kwani Serikali ilikopa kiasi cha dola za kimarekani 40 milioni kutokaBenki ya Barclays ya Uingereza kwa ajili ya kununulia Rada. Mkopo huo ulikuwana Riba ya asilimia 4.9 juu ya kiwango cha riba zinazotolewa na Benki ya Duniaau IMF.KambiRasmi ya Upinzani inataka kujua kama mkopo huu umeshalipwa wote na jumlatulilipa kiasi gani cha fedha. Ukilinganisha fedha iliyorejeshwa kama chenji yaRada na Fedha ambayo Tanzania iliilipa Benki ya Barclays (Principal amount naInterest), je chenji ya Rada ilikuwa na thamani yoyote kifedha? Mjadala wa ununuzi wa Rada hauwezi kuisha kwakufurahia kurejeshewa chenji tu. Mjadala huu bado mbichi kabisa kwani tunatakaukweli na ukweli mtupu uelezwe kwa umma na kuona Taifa lilipata hasara kiasigani kwa ufisadi huu wa kimataifa na hatua stahiki za kisheria kuchukuliwadhidi ya wote walioingiza hasara kwa Taifa letu.

TZS 70 bilioni zalipwa kama mishahara hewa ilihali Walimu na Madaktari na Madaktari wanalia

3.0 Mishahara hewanchini
Mheshimiwa Spika, katikahotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu makadirio ya mapato namatumizi katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa mwaka wafedha 2012/2013, tulitaja kiasi cha shilingi bilioni 9[1]ambazo zililipwa kama mishahara kwa watumishi hewa kama ilivyoripotiwa namagazeti ya 'The Daily News' na 'The Guardian' ya Machi 23, 2011. Mheshimiwa Spika,ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya tarehe 31 Machi,2012 inaonesha kwamba kwa mwaka wa fedha 2010/2011 jumla ya shilingi142,715,827.99[2]zililipwa kama mishahara kwa wastaafu, watumishi walioacha au kufukuzwa kazi nawatumishi wengine ambao hawakustahili. Aidha, ripoti hiyo imeonesha kiasi chashilingi 1,842,607,565.29 zilizolipwa kama mishahara hewa kwa mwaka wa fedha2009/2010.Mheshimiwa Spika,kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Fedha kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya fedhana uchumi ya tarehe 7 Agosti, 2012 ni kwamba uhakiki wa watumishi uliofanyika mwezi Januari, 2012 kwenyeHalimashauri 133 na kwenye taasisi na wakala za Serikali 154 ulibaini majina 9,949 ya watumishi wasiostahili kuwemokwenye orodha ya mishahara. Idadi hii ya watumishi hewa ni sawasawa natakribani idadi ya watumishi walioajiriwa katika sekta nzima ya madini kwenyemigodi ya dhahabu hapa nchini. Watumishi hewa wanaokaribia 10,000 ni wengi mnona inaonyesha dhahiri namna Serikali isivyo makini katika suala hili ambalolinasababisha upotevu mkubwa wa Fedha za Umma.Mheshimiwa Spika,Waziri wa Fedha alikiri mbele ya Kamati ya Fedha na Uchumi kwamba mweziFebruari Serikali ililipa shilingi bilioni 5.1 kama mishahara hewa. Hii maanayake ni kwamba Serikali hutumia zaidi ya shilingi bilioni 70 kila mwaka kwawatumishi hewa wa Serikali.Mheshimiwa Spika,tunataka fedha hizi wanazolipwa watumishi hewa zitumike kuwalipa walimu namadaktari madai yao kwani ni nyingi na zinatosha sana. Siku zote sababu zaSerikali kutotimiza matakwa ya wafanyakazi kwenye sekta ya Afya na Elimu nikwamba Serikali haina Fedha. Lakini hapa tunashuhudia Shilingi bilioni 70 kilamwaka zikiteketea kulipa watumishi hewa ambao hawapo, hawafanyi kazi na hivyokufaidisha mtandao wa kifisadi ambao kwa vyovyote vile unaanzia Wizara ya Fedhana Wizara ya Utumishi. Serikali inakosa vipi fedha za kulipa madai ya Walimu nainapata za kulipa watumishi hewa? Serikali inakosa vipi fedha za kulipaMadaktari na Manesi lakini inapata shilingi bilioni 70 kila mwaka kulipawatumishi hewa?Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inataka mradi huu wa watumishi hewa wenye mauzo(turnover) ya shilingi 70 bilioni kwa mwaka uvunjwevunjwe ili kupata fedha zakulipa Walimu na Madaktari. Waziri wa Fedha asambaratishe mtandao huu mwovuambao sasa umeota mizizi kwenye Taasisi za Serikali. Vile vile Waziri agawe kwaWabunge taarifa ya uhakiki wa wafanyakazi wa Serikali na pia hatua ambazoSerikali imechukua dhidi ya vinara wa mtandao wa watumishi hewa Serikalini.

Mafuta yala dhahabu yote, Korosho na viwanda

2.1 Mauzo ya Nje
Mheshimiwa Spika, Wizaraya Fedha kupitia Benki Kuu ya Tanzania inapaswa kuhakikisha kuwa Akiba ya Fedhaza Kigeni nchini inakuwa imara muda wote. Biashara ya nje ndio inaingiza Fedhaza kigeni nchini kwa hiyo ni eneo la kutazama kwa makini na kuchukua hatuamwafaka. Taarifa ya mwenendo wa uchumi kwa mwezi Julai iliyotolewa na Benki kuuinaonyesha kuwa jumla ya mauzo ya Tanzania nje yalikuwa dola za kimarekani 7,990.0 milioni ukilinganisha na kiasicha dola 7,050.7 milioni kwa kipindikama hicho kwa mwaka 2011 na hali hii ilisababishwa kwa kiasi kikubwa kutokanana kuongezeka kwa bei ya mauzo ya dhahabu.Hata hivyo Manunuzi yetu kutoka nje yamefikia dola za Kimarekani 12,959milioni.Mheshimiwa Spika,taarifa hiyo inaonyesha kuwa mauzo ya dhahabu Nje kwa mwaka 2011 yalikuwa kiasicha dola 2,330.7 milioni sawa naaslimia 56.7% ya mauzo yote nje,wakati mauzo ya nje kutokana na bidhaa zilizozalishwa viwandani yalikuwa najumla ya dola 922.0 milioni sawa naasilimia 22.4% ya mauzo yote ya nje.Aidha mauzo ya mazao mbalimbali kama Pamba, Katani, Korosho, Chai, Kahawa namengineyo yalikuwa na thamani ya dola 761.1milioni kwa kipindi hicho cha mwaka 2012. Mheshimiwa Spika,taarifa hiyo imeendelea kuonyesha kuwa tuliagiza bidhaa kutoka nje zenye thamaniya dola za Kimarekani milioni 12,958.7. Katika manunuzi hayo tuliyofanya mafuta pekeyake yalikuwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni 3,586.1 ambalo ni ongezekola asilimia 60.08% ukilinganisha nakipindi kama hicho kwa mwaka 2011. Mheshimiwa Spika,takwimu hizi zinaonyesha kwamba fedha zote za kigeni zilizotokana na mauzo yadhahabu, bidhaa za viwandani na Korosho zilitumika kuagiza mafuta pekee yake!Hali hii ni mbaya sana kwa uchumi wa Taifa letu na juhudi zote za kuongezamauzo nje zinaliwa na uagizaji wa Mafuta ambao umepanda sana katika siku zahivi karibuni.Kambi Rasmi yaUpinzani inatambua kuwa kuanzia mwaka janaSerikali imekuwa ikitekeleza mpango wa Umeme wa dharura ambao umepelekeamatumizi makubwa ya Mafuta. Hata hivyo ieleweke kuwa Mpango mzima wa Manunuziya Mafuta ya kuendesha mitambo ya Umeme inaligharimu Taifa Fedha nyingi sana.Takwimu zinaonyesha kuwa Serikali inapaswa kutumia zaidi ya shilingi42 bilionikila Mwezi kuendesha mitambo ya dharura ya Umeme. Manunuzi yenyewe ya Mafutayamejaa mazonge ya ufisadi uliokithiri. Licha ya kutaka Spika aunde timu yakuchunguza ufisadi katika manunuzi ya Mafuta na licha ya Kamati ya Bunge kutakaUchunguzi wa kibunge kufanyika katika manunuzi haya bado hakuna hatuainayochukuliwa. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Mamlaka ya Manunuzi ya UmmaPPRA kufanya uchunguzi wa kina kuhusu manunuzi ya mafuta kuzalisha Umeme ambayoyanachoma bilioni 42 za Serikalikila Mwezi. PPRA hapaswi kufumbia macho manunuzi yanayotafuna shilingi 1.4bilioni kila siku na yanayoongeza manunuzi ya nchi kutoka nje (imports) nahivyo kupoteza fedha za kigeni hovyo. Mheshimiwa Spika,Wizara ya Fedha ambayo ndio wizara mama ya PPRA kupitia Fungu 50, na ndioWizara yenye kusimamia uchumi wa nchi kwa ujumla ituletee Bungeni Taarifa yaUchunguzi utakaofanywa na PPRA kuhusu manunuzi shilingi 1.4 bilioni kila sikuya mafuta kuendesha mitambo ya kuzalisha Umeme.



 
Hii ndiyo maana ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kuonesha njia mbadala. Hotuba hii imesheni mambo mengi mazuri ambayo yakizingatiwa umasikini Tanzania bye bye!!!! The speech is surely inspirational and it realy shows that The Opposition is now ready and capable to assume state power.
 
Back
Top Bottom