Hotuba Mbalimbali za Mzee Rashid Mfaume Kawawa

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Wana JF;

Yeyote aliye na hotuba za Mzee Wetu Mzee Rashid Mfaume Kawawa aziweke hapa.

Kwa kuanzia nina kipande hiki kidogo:

akiwa kaimu mwenyekiti wa bodi hiyo, ilisema kwamba viongozi wa serikali, mashirika yasiyo ya serikali, jumuia zake na viongozi wa vyama vya siasa wanahitaji elimu ya chuo cha Kivukoni kwa lengo la kuimarisha umoja, upendo, mshikamano na utaifa.

Alisema chuo bado kina nafasi nzuri ya kuimarisha utafiti katika masuala ya Tanzania na kwamba utafiti unakuwa na maana zaidi matokeo yake yanapowafikia wananchi wengi na kuwawezesha kubadili maisha yao.

Mzee Kawawa alisema utafiti usiwe wa kitaaluma tu bali usaidie kubadili maisha ya Watanzania.

Gazeti-Uhuru
ISSN 0876-3896
Tarehe: Jumatatu Novemba 28, 2005
 
WAZIRI mkuu mstaafu na mwanasiasa mkongwe nchini, Rashid Mfaume Kawawa, maarufu kama "Simba wa Vita" amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema kuwa ubinafsi wa baadhi ya viongozi na wanachama wake ni hatari kwa masilahi ya nchi.

Kawawa, ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za juu serikalini ikiwemo makamu wa pili wa rais, uwaziri na uongozi wa chama hicho, alitoa tahadhari hiyo jana wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu kiitwacho "Simba wa Vita, Rashid Mfaume Kawawa katika Historia ya Tanzania".

Ameungana na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho - Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Joseph Butiku, waziri mkuu wa zamani, Joseph Warioba na Hassy Kitine- kukosoa wazi wazi mwenendo wa chama hicho kwa kutoa tahadhari kwa baadhi ya viongozi wanaotanguliza mbele masilahi yao binafsi badala ya wananchi.

Kitabu hicho, ambacho kinaelezea historia ya maisha ya Kawawa pamoja na harakati zake kisiasa katika ukombozi wa nchi, kilizinduliwa jana na Rais Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam na hafla hiyo ilienda sambamba na sherehe ya mkongwe huyo wa siasa nchini ya kuadhimisha kutimiza miaka 83 ya kuzaliwa.

"Katika umri wangu huu wa miaka 83, nina wajibu wa kuwaasa viongozi wenzangu na wananchi kwa ujumla," alisema Kawawa wakati akitoa salamu zake za shukrani kwa ajili ya kitabu hicho kabla ya kuzinduliwa.

"Tusitangulize masilahi yetu mbele, bali tuweke utaifa mbele. CCM isikubali kuyumba kwa sababu ya ubinafsi wa viongozi wachache."

Kawawa, akinukuu wosia wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alionya kuwa ikiwa chama hicho hakitakuwa imara kitasababisha hata nchi kuyumba.

"Tukumbuke wosia wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuwa, bila CCM kuwa madhubuti nchi itayumba," alisema Kawawa katika hotuba yake.

Kauli ya Kawawa inajazia katika tahadhari nyingi zinazotolewa na viongozi wa CCM, akiwemo Rais Kikwete ambaye aliwahi kuwaambia wabunge kuwa wajiepushe na watu wanaotoa kauli zenye mwelekeo wa kuleta mgawanyiko ndani ya chama.

Kama ambavyo Kawawa alizungumza jana, Rais Kikwete hakuweka bayana watu hao wala kutoa mifano inayoonekana kuwalenga watu hao, lakini kauli ya Kawawa inazidi kutoa ishara kuwa hali si shwari ndani ya chama hicho tawala.

Tuhuma za ufisadi zimekuwa zikirushwa dhidi ya viongozi na wanachama wake, huku kampeni za chini chini kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa wabunge wa mwaka 2010 zikitawaliwa na kauli kama, "mafisadi wanataka kuniangusha."

Kuhusu maisha yake ya harakati za ukombozi, Kawawa alisema elimu aliyoipata ameitumia kikamilifu katika mapambano hayo, alianzia kwenye vyama vya wafanyakazi kama mtetezi wa masilahi ya wafanyakazi tangu enzi za ukoloni.

Alisema aliamua kuingia katika uwanja wa kisiasa na kujiunga na mapambano ya ukombozi wa nchi kwa kuwa alitambua kuwa ukombozi wao utapatikana kutokana na uhuru wa kisiasa.

Alisema ni kupitia kwenye vyama hivyo- ambako alikuwa kiongozi katika nafasi mbalimbali, ikiwemo ya ukatibu mkuu na urais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi- alipokutana na Mwalimu Nyerere na kwamba tangu kipindi hicho alifanya kazi na muasisi huyo wa taifa na kujifunza mengi katika nyanja ya siasa.

"Kutoka kwa Mwalimu nilijifunza uchapakazi, uadilifu, uaminifu na kuongoza nchi kwa misingi ya kidemokrasia na kuwapenda Watanzania," alisema Kawawa.

Akizungumza mara baada ya kuzindua kitabu hicho, Rais Kikwete alimwelezea Kawawa kuwa ni kiongozi aliyetekeleza majukumu yake katika nafasi zote alizowahi kushika serikalini na ndani ya chama hicho kwa uadilifu na unyenyekevu.

Alisema licha ya kupanda na kushuka katika nafasi za uongozi, lakini hakuna siku ambayo Kawawa aliwahi kunung'unika, bali kila nafasi aliyoishika alitekeleza majukumu yake bila kujali kama ni ya chini ama ya juu.

Kufuatia historia hiyo ya utendaji wake, Rais Kikwete alitoa wito kwa viongozi wote kujifunza siasa kwake na kutambua kuwa kila kitu kina nafasi yake huku akiwaasa viongozi kuwa wajibu wao ni kusaidia wanaowaongoza na si kuwa kikwazo kwao.

Pia alimshukru Kawawa kwa kukubali kwake kuandikwa kwa kitabu hicho ambacho kinaelezea historia ya maisha yake binafsi na mapambano yake kisiasa katika kulikomboa taifa.

Rais Kikwete alisema kuandikwa kwa kitabu hicho si tu kwamba kinazungumzia historia ya Simba huyo wa Vita, bali pia kinatoa historia halisi ya Tanzania.

"Kukubali kwake kuandikwa kwa historia ya maisha yake ni kulisaidia taifa kujua mambo yalivyo, kwani ukiwepo mwenyewe unaeleza kwa uhakika mambo yaliyotukia tofauti na mwandishi anavyoweza kuandika kwa hisia tu na tafsiri yake," alisema Kikwete na kuongeza.

"Tukifanya hivyo hatutaweza kupata tabu ya wanaopotosha historia. Hivyo kila mmoja kwa nafasi yake aandike historia yake anayoijua mwenyewe," alisisitiza Rais Kikwete.

Pia Kikwete alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa viongozi wengine wenye historia ya nchi hii kuandika historia yao wangali bado hai ili kulinda ukweli wa historia ya taifa.

Hata hivyo, Rais Kikwete alisema licha ya kitabu hicho kuwa na mambo mengi ya kujifunza ambayo yanatoa elimu kubwa, lakini kuna tatizo kuwa Watanzania si watu wanaopenda kujisomea.

Akisisitiza umuhimu wa kujisomea Kikwete alisema katika vitabu kuna elimu kubwa na kutoa wito kwa Watanzania kujipangia ratiba ya kusoma japo kitabu kimoja kwa mwezi ambapo alisema kwa kufanya hivyo kwa mwaka watakuwa wamesoma vitabu 12 na kupata elimu na mambo mapya 12.

Kitabu hicho cha Simba wa Vita cha Rashid Mfaume Kawawa chenye kurasa 127 na sura sita kimeandikwa na Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kivukoni, Dk. John Magoti na dibaji yake imeandikwa na Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Pius Msekwa na kuchapishwa na Kampuni Matai & Company Ltd.

Awali, Mwandishi wa Kitabu hicho, Dk. John Magoti alisema kitabu hicho ingawa kinaelezea historia ya Kawawa tangu akiwa shule ya msingi hadi harakati na mapambano ya ukombozi wa taifa, kina mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa mkongwe huyo wa siasa nchini na kutokana na nafasi yake katika historia ya Tanzania

Washiriki katika uzinduzi wa kitabu hicho waliweza kujipatia nakala kwa bei ya Sh.15,000 na kutiwa saini na Kawawa mwenyewe.

Miongoni mwa watu walioshiriki katika uzinduzi wa kitabu hicho ni pamoja na marais wastaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi maarufu kama Mzee ruksa, na wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wastaafu Joseph Warioba, Samwel Malecela, Spika Mstaafu, Pius Msekwa na mawaziri na wabunge mbalimbali wa sasa wastaafu.

Source: Gazeti la Mwananchi
 
MMOJA wa waasisi wa Taifa la Tanzania, Mzee Rashid Mfaume Kawawa, amemmwagia sifa Rais Jakaya Kikwete, kuwa ni kiongozi anayekubalika na kuwa ameanza vizuri kuiongoza nchi.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini hapa, alipohojiwa na mwandishi wa habari hii juu ya mabadiliko ya uongozi Tanzania na uchaguzi mkuu uliopita wa rais, wabunge na madiwani, ambapo Rais Kikwete aliibuka na ushindi mkubwa.

Mzee Kawawa alisema mataifa yaje kujifunza mabadiliko ya uongozi hapa Tanzania ambapo kila chama kinapewa nafasi kujinadi na wananchi watoe uamuzi wa chama gani kinafaa kuwaongoza kama ilivyotokea katika uchaguzi mbalimbali nchini.

Alimtaja Kikwete kuwa ni kiongozi mwenye uchungu na wananchi na hivyo hotuba zake na usimamizi wa yale anayoyasema umeegemea katika utekelezaji na kuwafanya Watanzania waondokane na matatizo yasiyokuwa ya lazima na ambayo serikali yao inaweza kuwaondolea kero.

Aliwataka Watanzania kuipa ushirikiano serikali yake ili aweze kutekeleza majukumu ya taifa kwa kuwapa hali bora ya maisha kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.

Mzee Kawawa ambaye anafikisha miaka 80 leo, Februari 27, 2006, anamshukuru Mungu kwa kumweka hai baada ya misukosuko mikubwa aliyoipata katika maisha yake na kuivuka salama.

Aliitaja misukosuko hiyo ni pamoja na kunusurika kutunguliwa akiwa kwenye ndege kule Nachingwea miaka ya sabini, ambako alikwenda kumzika Askofu wa jimbo la Masasi na wakati akirudi Dar es Salaam, askari wa JWTZ kambi ya Nachingwea, ambao wakati huo walikuwa katika tahadhari ya mashambulizi na Wareno waliivurumishia mizinga ndege yake.

Alifafanua kuwa Mungu bariki rubani wa ndege hiyo aliigeuza ghafla na kurudi tena Masasi, ambako walilala na kamanda wa kambi ya Nachingwea alifika Masasi kuomba radhi baada ya kuarifiwa kuwa ndege iliyorushiwa mizinga ilikuwa ya Mzee Kawawa.

Tukio jingine ambalo amelieleza kuwa ni la kukumbukwa katika maisha yake, ni vita vya Kagera ambavyo mara kadhaa alikwenda mstari wa mbele kushuhudia mapigano na wakati mwingine kuvurumishiwa risasi, lakini Mungu alimuokoa.

Akizungumzia uongozi wa Tanzania, Mzee Kawawa alisema kama kulikuwa na wakati mgumu kwake kiuongozi ni pale alipotakiwa na Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere asimamie ujenzi wa vijiji vya ujamaa, zoezi ambalo lilikuwa gumu lakini chini ya uongozi wake akiwa waziri mkuu lilifanikiwa vyema.

Kuhusu ujenzi wa taifa huru, Mzee Kawawa alieleza kuwa wafanyakazi wa Tanganyika ndiyo waliojenga umoja wa kulikomboa taifa hili kuwa huru pale walipoanzisha migomo ya mara kwa mara na kuifanya serikali ya kikoloni kuona nchi hii haitawaliki tena.

Akiwa Rais wa Chama cha Wafanyakazi wa Kiafrika (Tanganyika African Servants Association) alishirikiana na vyama vingine vya wafanyakazi nchini kuandaa migomo hiyo hadi kufanikiwa kwa serikali ya mkoloni kukubali kukaa pamoja kuzungumza.

Chini ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TFL) ambalo alikuwa Katibu Mkuu waliandaa mkakati wa kuwataka kila mfanyakazi anayetaka kujiunga na vyama vya wafanyakazi kwanza sharti ajiunge na TANU, jambo lililoifanya TANU kuwa imara na kuwa na watu ambao walifanya vitimbi kumwondoa mkoloni.

Kufuatia kufanikiwa kuwaingiza wafanyakazi katika TANU Mzee Kawawa alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU mwaka 1958 mkutano uliofanyika Tabora ambapo wakati huo hakuwepo Tabora kwa kuwa alikuwa akisimamia migomo.

Alisema, lakini wana TANU walithamini kazi aliyokuwa anaifanya nje ya TANU na kumchagua kuwa mjumbe.

Amewataka viongozi wote wanaomsaidia Rais Kikwete kuwa watii na waaminifu wa hali ya juu kwani bila ya utii utekelezaji wa majukumu anayokusudia Rais hayatafanikiwa na kutolea mfano kila ilipotokea suala gumu kwa utekelezaji Mwalimu Nyrere alimtuma yeye kwenda kutekeleza na hivyo wakati mwingine kuwa katika mazingira magumu lakini hatimaye walifanikiwa kufikia malengo.

Kuhusu familia yake alisema amewapa uhuru kila mmoja afanye atakalo na kuwa hakumlazimisha hata mtoto mmoja miongoni mwa watoto wake awe mwanasiasa, hata hivyo amefurahi kuona mtoto wake Vita amekuwa mbunge wa jimbo la Namtumbo na hivyo kufuata nyayo zake.

Alimwelezea Vita kuwa ni msikivu, mtii na mvumilivu ambapo aliwahakikishia wananchi wa Namtumbo atawatumikia kwa nguvu zake zote katika kililetea maendeleo jimbo hilo na kuwataka wananchi wampe ushirikiano katika kufikia mafanikio hayo.

Mzee kawawa amewataka Watanzania waelewe kuwa hivi sasa dunia ni eneo lenye fursa kwa kila mtu, hivyo Watanzania wakazane kujinasua kielimu ili kuzitumia fursa zilizopo ambapo elimu ndiyo inayotumika kugombea fursa hizo.

Aliongeza kuwa teknolojia ndiyo inayoendesha dunia na hivyo alitoa wito kwa viongozi wa Tanzania kwa kila kata kuwe na shule ya sekondari ambalo ndiyo njia pekee ya kujikomboa katika kugombea fulsa kimataifa.

Kuhusu kizazi chake, Mzee Kawawa anao watoto 20, 16 kati yao ni wanawake, wajukuu 39 na vitukuu vitatu na kueleza kuwa kila mtoto anajituma kimaisha , hakuna mtoto anayemtegemea mwenzake katika kuendesha maisha.

Sherehe za kutimiza miaka 80 tangu kuzaliwa zinatarajia kufanyika leo mjini Songea sambamba na kumbukumbu ya Vita vya Majimaji ambavyo kitaifa maazimisho yake yanafanyika mjini hapa ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Kikwete.


Kutoka gazeti la Uhuru
ISSN 0876-3896 NA.19244
Na Mussa Homera, Songea

 
Anastahili heshima. Mzee alijitahidi. Pamoja na "shule" yake kuwa ya chini kidogo alikuwa na macho ya kuihurumia nchi.

Ngoja tuanze kusikia sauti za wanasiasa watakavyoendelea kujifanya kuiga nyayo za Mfaume Kawawa!!!!. Unafiki mtupu!
 
Source: Majira

Chimbuko na mafanikio ya JKT kwa Taifa

*Ni nguzo muhimu ya malezi, uzalendo, kiuchumi na ulinzi wa nchi

09 July 2009
Na Juma Kiyenze

JESHI la Kujenga Taifa (JKT), Leo linatimiza miaka 46, tangu kuanzishwa kwake Jijini Dar es Salaam, kwenye Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Ndani na aliyekuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Hayati Joseph Nyerere.

Sherehe za uzinduzi wa jeshi hilo, zilifanyika Julai 10,1963 ambapo Hayati Nyerere, alifafanua malengo ya kuanzishwa kwa chombo hicho muhimu na masharti ya kujiunga na JKT.

Wazo la kuanzishwa kwa JKT, lilitolewa mwaka 1958, kwenye Mkutano wa Umoja wa Vijana wa (TANU), mkoani Tabora. Wazo hilo lilitolewa na Mzee Rashid Mfaume Kawawa, baada ya kurejea kutoka nchini Ghana alikokwenda kuhudhuria sherehe za Uhuru wa nchi hiyo.

Akiwa nchini humo, Mzee Kawawa alikutana na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Israel, Bw. Golda Meir, ambapo walifanya mazungumzo yaliyohusu maendeleo ya nchi zao.

Bw. Meir ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Israel, alimweleza Mzee Kawawa jinsi nchi yake ilivyokuwa ikiwaandaa vijana kijeshi na kushiriki katika shughuli za ujenzi wa Taifa kwa njia ya kujitolea.

Alimfahamisha jinsi vijana hao, walivyokuwa wakitayarishwa kuitumikia nchi yao kwa moyo wa uzalendo, upendo, kujituma, ujasiri, uvumilivu, kuinua uchumi, ulinzi na usalama wa nchi yao.

Mara baada ya Mzee Kawawa kurejea hotelini kwake, alikwenda kuonana na Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa pamoja naye nchini humo. Alimweleza kiini cha mazungumzo kati yake na Bw. Meir ambapo Mwalimu Nyerere, alifurahishwa na maelezo hayo na kumtaka ayafanyie kazi baada ya kurudi nyumbani Tanganyika.

Baada ya Mzee Kawawa kurejea nyumbani, aliwasilisha wazo hilo kwa viongozi wa Umoja wa Vijana wa TANU. Wazo hilo lilifanyiwa upembuzi yakinifu na kufikishwa kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja huo uliofanyika mkoani Tabora mwaka 1958.

Mkutano huo kwa kauli moja, uliafiki wazo la kuanzishwa kwa JKT, ili kuwatayarisha vijana kujikomboa kutoka kwenye makucha ya Wakoloni. Wakati maandalizi hayo yakishika kasi, nchi ilikuwa chini ya utawala wa Waingereza.

Malengo mengine ya JKT, yalikuwa ni kufuta makosa na makovu yaliyotokana na Wakoloni kuwagawa wananchi katika matabaka mbalimbali ili kurahisisha utawala wao, kudharau kazi za mikono, tofauti za makabila, dini, kipato, jinsia na rangi.

Tanganyika ilipopata madaraka mwaka 1960 na uhuru wake mwaka 1961, vuguvugu la utekelezaji wa maamuzi yaliyofikiwa kwenye mkutano wa Tabora, yalipamba moto.

Mwaka mmoja kabla ya Tanganyika kupata uhuru, Mzee Kawawa, alialikwa nchini Israel 1960. Akiwa nchini humo, alitembezwa sehemu mbalimbali kujionea shughuli zilizokuwa zikifanywa na vijana.

Baada ya uhuru mwaka 1961, Serikali iliomba msaada wa mafunzo nchini Israel yaliyosaidia kuanzishwa kwa JKT. Israel iliridhia ombi hilo na kutoa nafasi mbalimbali za mafunzo ya uongozi kwa vijana nchini.

Miongoni mwa vijana wa kwanza kupelekwa katika ya uongozi nchini humo ni Meja Jenerali (mstaafu) Makame Rashid Nalihinga, ambaye alikuwa Mkuu wa JKT wa tano.

Wengine ni Brigedia Jenerali Dismas Msilu na Marehemu Brigedia Jenerali Irungi Athumani Msonge. Israel iliendelea kutoa nafasi zaidi za masomo kwa vijana wa Tanganyika na ilileta wataalam wake nchini kusimamia uanzishwaji wa JKT.

Serikali iliwapeleka vijana wengine nchini Bulgaria na Yugoslavia kujifunza mbinu mbalimbali za malezi ya vijana. Baada ya kukamilika kwa maandalizi muhimu na kuwapata viongozi waliohitajika, Julai 10, 1963, JKT ilianzishwa kwa kuanza kuwachuka vijana wa kujitolea kutoka mijini na vijijini.

Baada ya kuimarishwa kwa JKT, Serikali ilitangaza utaratibu mwingine wa kuwachukua vijana wasomi kutoka sekondari, vyuo na chuo kikiuu kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kuwajenga uwezo kisaikolojia.

Kuanzishwa kwa JKT:

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lilipitisha sheria nambari 16 ya 1964, ambayo ilianzisha chombo hicho na kutoa uwezo wa kuandikisha vijana kujiunga na JKT. Hata hivyo, sheria nambari 64 ya mwaka 1966, ilifanyiwa marekebisho, ili iweze kukidhi matakwa ya kuwachukua vijana wasomi .

Vijana mbalimbali wasomi wa Kitanzania waliomaliza elimu ya sekondari kidato cha nne na kupata kozi zaidi ya miezi sita vyuoni pamoja na wahitimu wa kidato cha sita na kuendelea, walitakiwa kujiunga na JKT kwa mafunzo ya kijeshi na stadi za kazi.

JKT iliunganishwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwaka 1975, kutokana na marekebisho ya sheria namba 22 ya mwaka 1975 (The National Service ammendment act No. 22 of 1975, amalgamation with TPDF).

Lengo la kuanzishwa kwa JKT ni kutoa malezi kwa vijana wa taifa huru kwa kuwafundisha moyo wa upendo, kuondoa dhana ya ubaguzi, kupenda kazi za mikono, kuwa raia wema wenye kujituma, kujiamini, uzalendo, uchungu kwa nchi yao na kuthamini mila, desturi na kudumisha utamaduni wa taifa.

Dhima ya JKT ni kuwapatia vijana mbinu za kijeshi ili kuwa na Jeshi la akiba, kuwaandaa vijana kujiunga kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na kuwatayarisha kushiriki katika maafa yanayoweza kujitokeza katika kuokoa mali na maisha ya jamii.

Vijana hutayarishwa kisaikolojia kwa kupatiwa mafunzo ya nadharia na vitendo yenye kukidhi haja ya kulitumikia taifa katika nyanja mbalimbali za kijamii, kiuchumi na ulinzi wa taifa kikamilifu.

Jukumu kubwa la JKT ni kuwafunza vijana mafunzo ya kijeshi na ufundi, ili kuwajengea uwezo wa kujiamini, nidhamu, uzalendo, ushirikiano, maadili, ubunifu, uwajibikaji na kujituma katika utekelezaji wa majukumu yao mbalimbali yatakayotolewa kitaifa na kimatifa.

Mafunzo ya kwanza ya JKT yalifanyika katika ya mafunzo ya JKT Mgulani, Dar es Salaam yaliyofahamika kama Operesheni 1JLC. Mafunzo hayo yalianza Julai 10 hadi Septemba 28,1963 na kushirikisha vijana mbalimbali wa Watanzania.

Mgomo wa wasomi kujiunga JKT:

Kutokana na uelewa mdogo, baadhi ya vijana wasomi wa vyuo vya elimu ya juu na chuo kikuu walisusia kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria, baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo mwaka 1967.

Vijana hao, walifanya maandamano kupinga mpango huo wa Serikali. Hata hivyo, Hayati Mwalimu Nyerere kwa kushirikiana na viongozi wengine wa kitaifa, walisimama imara kutetea uamuzi wao.

Serikali iliwarejesha majumbani vijana waliokaidi kujiunga na JKT, ili waungane na wazazi wao waweze kutafakari kwa kina kitendo hicho. Baada ya kuona ukweli huo, waliomba radhi.

Yapo mafanikio mengi yaliyofikiwa na JKT ikiwa ni pamoja na kuimarisha umoja wa kitaifa, maadili kwa vijana, kupanua ajira katika sekta binafsi, kujituma katika majukumu, kupenda kazi za mikono na kuboreka kwa nidhamu sehemu mbalimbaliza kazi.

Vijana wengi waliopitia mafunzo hayo, waliajiriwa Serikalini, sekta binafsi na wengine walijiajiri wenyewe kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali kulingana na ubunifu walioupata.

JKT ilisaidia kupika viongozi wazuri wa kitaifa na kimataifa, ambao wanafanya kazi kwa uadilifu, ubunifu, uhodari, kujituma, wavumilivu na wenye nidhamu ya hali juu.

Vijana wa JKT walikuwa chachu ya kuthamini na kuhifadhi utamaduni wa taifa kwa kuibua vipaji vingi vya wasanii na wachezaji wa fani mbalimbali katika medani ya michezo kitaifa na kimatifa kwa kuiletea sifa Taifa.

Walishiriki kikamilifu kuitetea nchi yao wakati wa Vita vya Kagera dhidi ya uvamizi wa Majeshi ya Uganda mwaka 1978/79, kuhamisha waathirika wa majanga yaliyotokea nchini kwa nyakati tofauti, hasa ilipotokea ajali ya treni mkoani Dodoma, kuporomoka kwa jengo la ghorofa kumi jijini Dar es Salaam, na maeneo mengine.

Mkuu wa Majeshi (mstaafu), Jenerali David Msuguli alisema, wakati wa Vita vya Kagera, vijana wa JKT walionesha moyo wa uzalendo, kujituma na nidhamu ya hali ya juu kuihami nchi yao dhidi ya uvamizi wa majeshi ya Uganda, yaliyoongozwa na Marehemu Nduli Idd Amin.

Alitoa mwito kwa Serikali, kutilia mkazo mafunzo ya JKT kwa vijana na wale wanaohitimu watafutiwe ajira katika sekta za umma na binafsi kutokana na uadilifu na nidhamu yao. Jenerali Msuguli aliitaka Serikali, kuisaidia JKT ili iweze kufungua shule zaidi za ufundi, kuwawezesha vijana wengi kujifunza mbinu mbadala ili kupata wataalamu wengi wa nyanja mbalimbali za ufundi.

JKT ilisitisha mafunzo kwa vijana wa kujitolea kwa mujibu wa sheria mwaka 1994 kwa sababu za kiuchumi mpaka 2001, yalipoanza kutolewa kwa vijana wa kujitolea. Pamoja hayo, katika kipindi hicho cha mpito, taifa liliathirika kimaadili kutokana na vijana wengi kujihusisha katika vitendo vyenye kuhatarisha uvunjifu wa amani na usalama katika jamii.

Urejeshwaji mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria, ulitokana na Serikali kutafakari kwa kina na kufanya uamuzi wa busara kurejesha mafunzo hayo kwa vijana wasomi ili kuwajengea dhana ya uzalendo, kujitegemea na kuitumikia nchi yao kwa uadilifu.

Mbunge wa Kuteuliwa, Bw. Kingunge Ngambare Mwiru, aliitaka Serikali ijiandae kwa hilo, kwani idadi ya vijana wanaomaliza shule na vyuo kila mwaka ni kubwa.

Akichangia hotuba ya makadirio ya matumizi bajeti ya Wizara ya Ulinzi na JKT iliyowasilishwa bungeni na Waziri wake, Dkt. Hussein Mwinyi, Juni 6 mwaka huu, anasema takribani vijana 80,000 wanahitimu elimu ya juu katika vyuo mbalimbali nchini.

Alifafanua kuwa, maandalizi hayo ni pamoja na upatikanaji wa wakufunzi bora wenye uwezo wa kuwapatia mafunzo yenye maadili mazuri yanayolingana na utamaduni wa nchi.

Akiwasilisha hotuba ya makario ya matumizi ya bajeti ya Wizara yake, Dkt. Mwinyi anasema, vijana waliopo kwenye makambi ni 7,110, ambapo kati ya hao 2,819 ni wa Operesheni Maisha Bora na 4,219 Operesheni Uadilifu.

Anaeleza kuwa, hatua mbalimbali za kuboresha malezi na mafunzo ya vijana zimechukuliwa ili kuimarisha kada ya ukufunzi kwa kuwapeleka kozi za ukufunzi zinazoendeshwa na Mamlaka ya Ufundi Stadi nchini (VETA).

Malengo mengine ni kuendesha semina za kilimo, ufugaji na ufundi kwa wakufunzi na kuwahimiza kujiendeleza kitaaluma ili waweze kumudu malezi ya vijana na kushiriki kozi za ujasiriamali ambazo zitawajengea uwezo wa kuwafundisha vijana kubuni na kuendesha miradi mbalimbali baada ya kumaliza mkataba wao.

Aliyataja makambi saba ambayo yatatumika kwa ajili ya mafunzo ya stadi za kazi kwa vijana wa kujitolea kuwa ni Rwamkoma-Mara, Mgulani-Dar es Salaam, Chita-Morogoro, Maramba-Tanga, Itende-Mbeya, Nachingwea-Lindi na Mbweni-Dar es Salaam.

Akitoa salamu za JKT, Mkuu wa Jeshi hilo, Meja Jenerali Samuel Kitundu, anasema JKT inatarajia kuanza kupokea vijana wasomi wa kidato cha nne na sita ifikapo 2010, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali.

''Vijana hawa ni wengi na hatuwezi kumudu kuwachukua wote, tumependekeza kuchukua vijana wa kidato cha sita wanaotegemea kujiunga na vyuo kikuu, tunaendelea na maandalizi ya wakufunzi, miundombinu, upanuzi wa makambi na kufungua mengine, ili kuwapokea hapo mwakani'', anafafanua Meja Jenerali Kitundu.

Anafafanua kuwa, changamoto nyingine ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuitaka JKT kuzalisha mbegu bora. Jukumu hilo ni kubwa na muhimu sana, inabidi tujipange vizuri sana kwa kuwa JKT haina nyenzo za kutosha. Msimu wa mvua JKT huanzisha kilimo cha umwagiliaji ili kukabiliana na changamoto ya ukame.

JKT imefungua kambi mpya ya Kanembwa mkoani Kigoma na kufufua kambi ya zamani ya Msange iliyoko kilomita 15 kutoka Tabora mjini. Hivi sasa, wanaendelea na mikakati endelevu na utaratibu wa kufuatiliaji maeneo katika mikoa ambayo haina kambi za JKT.

Mapinduzi ya Kilimo:

Alifafanua kuwa, JKT inaendelea kufufua shughuli za kilimo ambazo mara baada ya kusitisha shughuli za JKT mwaka 1994, uzalishaji ulishuka kwa kiwango kikubwa. Nyenzo nyingi kama matrekta ya kulimia na yale ya kuvuna, yaliachwa na kuchakaa vikosini baada ya idadi ya watendaji kupungua.

Anasema kwa mujibu wa sheria, mwaaka 2010 watasaidia kuinua hali hiyo. Juhudi za ununuzi wa matrekta kwa mfumo wa vikosi wa kujinunulia kupitia faida ya miradi yao zimeanza kutekelezwa,

Changamoto:

Dkt. Mwinyi anasema, changamoto iliyopo ni ufufuaji wa mafunzo ya JKT na kujenga uwezo wa makambi yake kuweza kuwachukua vijana 10,000 kwa wakati mmoja.

Changamoto nyingine ni jinsi ya kuwatumia vijana watakaohitimu mafunzo hayo kuleta mageuzi ya kilimo, kuimarisha ulinzi na uzalendo wa taifa dhidi ya athari hasi zinazotokana na utandawazi, maendeleo ya teknolojia na mwingiliano wa watu duniani.

Sekta ya ujenzi:

JKT inamiliki Shirika la Uzalishaji Mali (SUMAJKT), linalojishughulisha na ujenzi wa majengo marefu (maghorofa), nyumba za kawaida, barabara, kilimo, uvuvi, ufugaji, kufanya biashara, viwanda na kufanya shughuli zingine ili kufikia lengo.

SUMAJKT inaendelea na ujenzi wa barabara ya Bagamoyo-Msata kwa ushirikiano na Kampuni ya Korea, ujenzi wa nyumba za Chama cha Walimu Tanzania (CWT) unaotekelezwa katika mikoa 21 ya Tanzania Bara, nyumba za watumishi wa umma na machinjio ya kisasa mkoani Pwani.

Katika salamu zake kwa JKT kutimiza miaka 46, Meja Jenerali Kitundu anasema, umuhimu umeelekezwa katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi na viwanda, ili viweze kuongeza tija na mapato.

Tangu kuanzishwa kwake, JKT limeongozwa na wakuu mbalimbali kwa nyakati tofauti. Viongozi hao ni Assistant Supaeritendant of Police (ASP), David Nkulila kuanzia Julai 1963-Desemba 1967.

Wengine ni Robert Kaswende Januari 1968-Mei 1970, Laurence Gama Mei 1970-Januari 1973, Meja Jenerali (mstaafu) Nelson Mkisi Januari 1973-Januari 1989, Meja Jenerali (mstaafu) Makame Rashid Nalihinga Januari 1989-Oktoba 2001.

Wengeni ni Meja Jenerali (Jenerali) Davis Mwamunyange, Novemba 2001-Juni 2006, Meja Jenerali (Luteni Jenerali) Abdulrahman Shimbo Januari 2006- Septemba 2007, Meja Jenerali (mstaafu) Martine Madata, Septemba 2007-Septemba 6, 2008 na Meja Jenerali Samuel Kitundu Februari 9, 2009 ambaye ni Mkuu wa JKT kwa sasa.
 
Sifa kubwa alizokuwa nazo Mzee Kawawa ni Utii, uaminifu, uvumilivu na upendo kwa nchi yake. Kawawa Rashid Mfaume hana mfano katika haya labda Mwalimu Nyerere ndiyo anaweza kumzidi kwa haya. Viongozi wengine waige mfano.
 
Kwa jinsi nijuavyo mimi, huyo ndiye mzalendo wa mwisho taifa linaloitwa Tanzania! RIP
 
Source: http://www.dacb.org/stories/tanzania/nyerere.html

He traveled throughout the country campaigning for independence (Uhuru in Swahili), continuing on even in the face of numerous threats and obstacles from the colonial government. In 1958 he went in front of the United Nations Organization (UNO) to plea for the independence of Tanganyika which was then under the ordinance of the British Trusteeship Territory.

On December 9, 1961, Tanzania received its independence and Nyerere became the first prime minister of Tanganyika. After a few months, he resigned from his position in order to strengthen the party and Rashid Mfaume Kawawa became prime minister. On December 9, 1962, Nyerere was elected the first president of the Republic of Tanganyika. When Tanganyika and Zanzibar united to form the United Republic of Tanzania on April 26, 1964, Nyerere became the first president of Tanzania.
 
Kawawa ashangaa viongozi kumiliki mabilioni ya fedha


WAZIRI Mkuu Mstaafu, Rashidi Mfaume Kawawa, ameitaka serikali kuwasaka viongozi wanaojihusisha na vitendo vya ufisadi nchini na kuwabana waeleze fedha wanazozimiliki namna walivyozipata.

Kawawa ambaye ni mmoja wa waasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kiongozi anayeheshimika kutokana na kushika nyadhifa mbalimbali za kitaifa, alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari, muda mfupi baada ya kuzindua kitabu kiitwacho: 'CCM na Mustakbali wa Nchi Yetu', katika hoteli ya Courtyard, jijini Dar es Salaam jana.


Alisema yeye pamoja na watu wengine waadilifu, hawapendi tabia ya kujilimbikizia mali isivyo halali inayoendekezwa na baadhi ya viongozi nchini, ambayo haikuwahi kufanywa na waasisi wa taifa hili, wakiongozwa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

"Hatupendi ulimbikizaji mali wa haramu, hivyo wote wanaojilimbikizia mali kwa njia hiyo, wafuatiliwe, waulizwe, waseme walizipataje," alisema Kawawa ambaye alipata pia kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema Mwalimu Nyerere ambaye ni kielelezo cha uadilifu na uaminifu kati ya viongozi wachache duniani, hakuwahi hata siku moja kujipatia mali kwa njia zisizo za halali.


"JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) walimjengea nyumba, alikubali kwa sababu alihitaji nyumba. Sijui kama alikuwa na uwezo au alikuwa hana wa kujenga hiyo nyumba, ila hakuwahi kujipatia mali kwa njia za haramu," alisema Kawawa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu.


Alisema mbali na Mwalimu Nyerere, hata yeye (Kawawa) hadi anastaafu kazi serikalini na katika chama, hajawahi kujipatia mali kwa njia za haramu.

"Ningeyapata wapi hayo mabilioni ya shilingi?," alihoji Kawawa ambaye ni Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM.

Kuhusu Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge ya kuyaita mabilioni ya shilingi anayotuhumiwa kuyahifadhi katika akaunti ndani na nje ya nchi kuwa ni "vijisenti", Kawawa alisema: "Hayo ni maoni ya mtu, kila mtu ana maoni yake".


Alipoulizwa, ni hatari gani inayoweza kukikumba chama baadaye kutokana na ufisadi, alisema kwa ufupi: "si jambo zuri".

Kauli hiyo ya Kawawa inatokana na kuibuliwa tuhuma za ufisadi na ulimbikizaji wa mabilioni ya shilingi kwa njia za haramu, kunakodaiwa kufanywa na baadhi ya vigogo, wakiwamo viongozi wa serikali na kulisababishia taifa hasara kubwa.


Zaidi ya Sh133 bilioni zilithibitishwa na serikali kupotea katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika mazingira yanayosadikiwa kuwa ni ya kifisadi.

Mbali na hilo, Waziri Chenge, ambaye juzi alikiri kuchunguzwa na vyombo mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, anatuhumiwa kumiliki dola 1 milioni (Sh1.2 bilioni) katika akaunti iliyoko katika kisiwa cha Jersey, nchini Uingereza katika mazingira ya kutantanisha, yanayohusishwa rushwa ya ununuzi wa rada ya kijeshi miaka iliyopita.


Awali, akitoa nasaha katika uzinduzi wa kitabu hicho, Makwaia wa Kuhenga, Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Issa Shivji alionyesha kushangazwa kwake na mabadiliko ya uongozi nchini, kutoka kwenye utumishi wa umma kuwa mradi kwa baadhi ya watu.


"Kila siku hivi sasa, kwenye magazeti utasikia ufisadi. Lazima tuhoji, kwa nini uongozi umekuwa mradi badala ya utumishi wa umma?," alihoji Profesa Shivji.


Kawawa ambaye amewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), pia alitoa ushauri kwa wana CCM kudumisha utamaduni wa kujikosoa na kukosoana ili kuleta mabadiliko katika chama na taifa kwa jumla.

Kawawa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa kwanza wa chama hicho, alisema tangu enzi za TANU na ASP hadi sasa, CCM imekuwa na utamaduni wa kuwa na mijadala katika mambo mazito yanayohusu chama na taifa na kwamba, hakiogopi kukosolewa kwa kuwa Mwongozo wa chama hicho wa mwaka 1981 umetamka bayana kwamba kujikosoa na kukosoana ni silaha ya mapinduzi.

Source:http://www.bongo5.com/content/view/4244/232/lang,en/
 
Kawawa: Tuna imani na Makamba

KATIBU Mkuu wa CCM mstaafu, Rashidi Kawawa amesema yeye binafsi na wana-CCM wana matumaini na Katibu Mkuu mpya wa chama, Yussuf Makamba, kuwa atakiongoza Chama Cha Mapinduzi kwa umahiri mkubwa.

Mzee Kawawa, ambaye ni muasisi wa chama, alisema hayo alipoungana na viongozi wa chama na serikali mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kumpokea Makamba, eneo la Kiluvya jana.

Makamba aliwasili Kiluvya saa 9. 58 alasiri akitokea Tanga ambako alikuwa na ziara ya kikazi ya siku sita, ya kwanza tangu ateuliwe kuwa Katibu Mkuu wa CCM mwishoni mwa mwezi uliopita.

Mzee Kawawa alisema, yeye na wanachama wana imani naye kwa sababu Makamba ni kiongozi ambaye amekuwa akifanya kazi za chama vizuri na kwa uadilifu kwa muda mrefu, hivyo anakifahamu vizuri chama na malengo yake.

"Wewe ni mwenzetu siku nyingi, tunaujua uchapakazi na uadilifu wako katika chama, tuna matumaini makubwa na wewe," alisema na kuongeza: "Sasa chama ni kikubwa na kinafaa sasa kuongozwa na wewe."

Akizungumza kwenye mapokezi hayo, Makamba alisema hatua aliyofikia ni matunda ya Mzee Kawawa kwa kuwa alimpa malezi mazuri kichama, hasa miaka ya 1970 akiwa katibu Mkuu wa CCM.

Makamba alisema, ameshukuru kupata mapokezi makubwa kiasi kile, lakini akaeleza kwamba kimsingi aliyepolewa si yeye, bali kimepokewa chama.

Alisema, ili kudhihirisha kuwa wanachama wanathibitisha kwa dhati kuwa yeye ndiye njia katika chama, wamuunge mkono kwa kuhakikisha wanakuwa hai kwa kulipia ada za uanachama.

Makamba aliwataka wanachama kote nchini kuwa kama waliozaliwa upya na kuimarisha zaidi chama kwa kufuata falsafa ya Mwenyekiti wa Chama, Rais Jakaya Kikwete ya Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya.

Alisema CCM ni chama cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi, hivyo lazima kujishughulisha na utatuzi wa kero na umasikini wa watu.

Katibu Mkuu aliwaasa wananchi ambao hawajajiunga na CCM kujiunga haraka iwezekanavyo kwa kuwa ndicho chama pekee chenye uhakika wa kushughulikia kero.

"Wananchi sasa jiungeni na chama hiki kwa sababu ndicho chama tawala chenye uwezo wa kushughulikia kero zenu... msikimbilie upinzani mtapoteza muda wenu bure," alieleza.

Aliwataka wananchi wasidanganyike kwenda upinzani akiwatanabahisha kwamba kuchagua kujiunga na CCM ni kuchagua amani, maendeleo na mahala maalum pa utatuzi wa kero zao.

Makamba aliwashukuru wananchi na viongozi aliokuwa akifanya nao kazi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

"... Enyi wa Dar es Salaam, sitawasahau... nitakuwa nanyi katika ufalme wangu... wale niliowakosea kwa namna moja au nyingine naomba mnisamehe," alisema Makamba.

Aliwataka viongozi na wananchi mkoani kumpa ushirikiano wa dhati Mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro ambaye amechukua nafasi yake.

Pamoja na Kawawa, viongozi waliofika kumlaki Makamba, kwa Dar es Salaam ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa, Hemedi Mkali, Katibu wa CCM mkoa huo, Mattson Chizi, wenyeviti na makatibu wa chama wilaya zote wakati viongozi wa mkoa wa Pwani waliongozwa na Katibu wa CCM, Amina Makilage.

Baadaye msafara mkubwa ulitoka Kiluvya na kumsindikiza Makamba hadi nyumbani kwake mtaa wa Luthuri.

Wakati huohuo, ziara ya Katibu wa uenezi wa Chama Cha Mapinduzim Aggrey Mwanri, iliyokuwa ianze leo mkoani Kilimanjaro imeahirishwa kutokana na majukumu mengine ya kikazi anayotakiwa kuyafanya

Source: http://www.habaritanzania.com/articles/511/1/Kawawa:-Tuna-imani-na-Makamba.
 
Mzee Kawawa Alonga

WAKATI joto la uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) likizidi kupanda, mwanasiasa mkongwe na kiongozi mstaafu wa chama hicho, mzee Rashid Mfaume Kawawa, ametoa nasaha zake kwa wanachama wote wanaowania uongozi pamoja na wapiga kura.

Nasaha hizo ni aina ya mwongozo, kutokana na maono ya mkongwe huyo wa siasa nchini, ambaye alidumu katika uongozi wa nchi kwa muda mrefu, wakati Tanzania ikipitia misukosuko mbalimbali.

Nasaha hizo za mzee Kawawa, ambaye ni miongoni mwa watu waliosaidia kukifikisha chama hicho kilipo leo, zinakuja wakati kukiwa na taarifa za migongano inayowahusisha hata viongozi wa ngazi, hasa wale wanaowania nafasi za juu za uongozi ndani ya chama.

Aidha, mzee Kawawa amezungumza wakati kuna migawanyiko ndani ya chama hicho kutokana na kuzaliwa kwa makundi mbalimbali, yakiiga kuzuka kwa kundi lijulikanalo kama mtandao, wakati wa kinyang'anyiro cha kumpata mgombea urais kupitia chama hicho mwaka 2005.

Katika nasaha zake, Kawawa amewata wanaCCM wote wanaowania kuchaguliwa kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), kuwa na dhamira ya dhati ya kukitumikia chama.

Akizungumza na gazeti hili katika Ikulu ndogo mjini hapa, ambako pamoja na mambo mengine, alikuja kuangalia miradi yake ya kilimo, Kawawa alisema kuwa itakuwa ni kukisaliti chama iwapo ubinafsi ndio utakaowasukuma watu kusaka uongozi ndani ya chama.

Alisema wagombea watakaoingia katika kinyang'anyiro hicho kwa lengo la kutimiza matakwa binafsi, watakuwa wanajiharibia wao wenyewe na chama hicho.

Kwa hiyo, aliwataka wapiga kura kuwa makini kwa kuwachagua wana-CCM halisi wenye nia thabiti ya kugombea na si kujiingiza katika mchakato huo wakiwa na malengo yao binafsi bali kwa ajili ya manufaa ya chama na wananchi kwa ujumla.

Katika mazungumzo hayo, Kawawa alisema kuwa, inafurahisha kuona kuwa wanachama wengi wamejitokeza kugombea nafasi hiyo, lakini akawaonya kuwa wale wote waliojitokeza kuwania nafasi hiyo wakipende chama kwanza na kukubali kukilinda kwa gharama yoyote.

Mzee Kawawa alisema kuwa, hali iliyopo sasa inajidhihirisha miongoni mwa wananchi na kuonyesha ni jinsi gani chama hicho kinathaminiwa, hivyo kuwataka wale wote watakaochaguliwa kupitia uchaguzi, kujali maslahi ya chama.

"Uongozi ni dhamana, walielewe hilo kwanza, wasijitokeze kugombea wakati hawako tayari kuongoza, sisi kama chama, tumepokea majina na tutawachunguza na kuwajadili mmoja mmoja, kama wapo safi hakutakuwa na matatizo, lakini tukiona huyu hafai, tunamuondoa. Kuna wale wachache ambao huharibu sifa za chama, lakini safari hii hatutaki mchezo… tutawakomesha," alisema.

Aidha, mzee Kawawa alisema kuwa, CCM imeweka milango wazi kwa kila mwanachama aliyekuwa na uwezo wa kuongoza kugombea nafasi hiyo ya ujumbe wa NEC, lakini alisisitiza kuwa, ni lazima mgombea agombee kwa maslahi ya chama na si kwa maslahi binafsi.

Wakati mzee Kawawa akitoa onyo hilo, baadhi ya viongozi wa matawi na wanachama wa kawaida wa CCM mjini Musoma, mkoani Mara, nao wametishia kufanya uasi ndani ya chama hicho, iwapo wanachama kutoka vyama vya upinzani waliojiunga na chama hicho hivi karibuni, watapewa upendeleo na kupitishwa kuwania uongozi katika uchaguzi huo.

Wakizungumza na Tanzania Daima, nje ya ofisi za CCM mkoani Mara, hivi karibuni, wanachama hao, ambao hawakutaja majina yao, walidai kuwa, wametishwa na wimbi la waliokuwa wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) kuwalioingia CCM hivi karibuni, kuchukua fomu za kuomba uongozi.

Aidha, walionya kuhusu wanachama wa CCM ambao wanatambulika kuwa walikuwa kikwazo katika kampeni za uchaguzi mkuu uliopita kwa kuishabikia CUF na wagombea wake.
Walidai kuwa, mashabiki na wafuasi hao wa CUF, ambao pia wana kadi za CCM, walikuwa wapiga debe wakubwa wa mgombea wa ubunge wa CUF, Mustapha Wandwi, pamoja na baadhi ya wagombea udiwani wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
"Iwapo watu hao watapitishwa kuwania uongozi katika CCM, sisi viongozi wa matawi pamoja na wanachama tutafanya uasi mkubwa ambao utakiangusha chama chetu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, kama walivyofanya hao, ambao sasa wanawania uongozi katika chama chetu," alisema kiongozi mmoja wa Tawi la CCM Kaminyonge.

Mwenyekiti mmoja wa tawi katika Kata ya Mwisenge, alidai kuwa chama kinawajua watu hao kwa kuwa walikuwa wakifanya kampeni za wazi wazi kumpinga mgombea ubunge wa CCM, Vedastus Mathayo na baadhi yao walisimamishwa uongozi wa chama hicho hadi uchaguzi ulipomalizika.

"Kuna baadhi ya watu hao, walikuwa na nyadhifa kubwa na mmoja wao alikiri ndani ya kikao cha kamati ya siasa ya wilaya kuwa anampinga mgombea wa CCM, akasimamishwa uongozi, sasa leo anaomba uongozi mkubwa katika wilaya na mkoa, kama watapitishwa, CCM Musoma mjini itasambaratika kabisa," alionya mwenyekiti huyo.

Ilidaiwa kuwa, wafuasi hao wa CUF wamejipanga katika nafasi zote za uongozi wilayani na mkoani, pamoja na ujumbe wa NEC.
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Musoma Mjini, Luteni mstaafu Maganga Sengerema, alipohojiwa kuhusu madai hayo, alisema kuwa wanaotakiwa kuulizwa juu ya hilo ni viongozi wa mkoa, kwa kuwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, alikuwa katibu wa CCM wa wilaya ya Serengeti.

Wakati huo huo, habari kutoka wilayani Tarime zinasema kuwa, wanachama wa CCM katika Jimbo la Tarime, wanakusudia kuandika barua makao makuu ya chama hicho, wakitaka baadhi ya wanachama wasipitishwe na vikao vya uteuzi kwa madai kuwa walimsaidia mgombea ubunge wa Chadema, Chacha Wangwe, kushinda kiti hicho.

Wanachama wawili wa CCM kutoka Jimbo la Tarime, walidai kuwa chama katika wilaya hiyo kiliwahi kupendekeza wanachama hao wafukuzwe uanachama kwa kuwa ndumilakuwili kwa kumpinga mgombea wa CCM, Kisyeri Chambiri na kusababisha ashindwe vibaya katika uchaguzi huo wa mwaka 2005.

"Wanachama hao walikuwa wakitumia fedha kumsaidia Chacha Wangwe na wengine wakimnadi mgombea huyo wa Chadema katika mikutano ya kampeni ya CCM, halafu leo wanataka uongozi CCM, wakipitishwa basi Jimbo la Tarime litaendelea kuwa ngome ya Chadema," alisema mmoja wao.

Wakati huo huo, Mwandishi Wetu anaripoti kutokea Musoma kuwa, kada wa CCM wilayani Musoma mjini, Kapteni mstaafu, Benjamin Musai (54), amelalamikia vitendo vya rushwa na mizengwe katika uchaguzi wa chama hicho ngazi ya kata, ambao ulifanyika jana.
Akizungumza na Tanzania Daima, kada huyo alisema akiwa mwanachama aliye na sifa zote, aliomba nafasi ya Katibu wa Kata ya Mwisenge ambapo alidai alifuata taratibu zote zinazotakiwa, ikiwa ni pamoja na kulipia fomu.

Musai alisema kuwa siku ya mahojiano walijitokeza wanachama wengine wawili waliokuwa wakiomba nafasi hiyo, na mmoja ambaye ilikuja kufahamika baadaye kuwa hakulipia fomu kwa ajili ya kuomba nafasi hiyo, hakujitokeza na kukawa na taarifa kwamba alishaandika barua ya kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.

Aliendelea kusema kuwa, alishangazwa na kitendo cha vikao husika ngazi ya wilaya kukata jina lake na kurudisha jina la mwanachama anayedaiwa kutolipia fomu, na ambaye alishaandika barua ya kujitoa.

Alisema kutokana na kitendo hicho, aliona wazi kuwa hakutendewa haki, hivyo Juni 7, mwaka huu, aliandika barua ya malalamiko kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, akilalamikia ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi.

Tanzania Daima inayo nakala ya barua ya malalamiko hayo, ambayo pia imetolewa kwa Katibu wa CCM Wilaya na kwa Katibu Mkuu wa chama hicho ngazi ya taifa. Hata hivyo, hadi uchaguzi huo unafanyika jana, alikuwa hajajibiwa barua hiyo.
Alipoulizwa juu ya malalamiko hayo, Katibu wa Itikadi na Uenezi Wilaya ya Musoma Mjini, ambaye kimsingi ndiye msemaji wa chama ngazi ya wilaya, Phares Godfrey, alikataa kusema lolote na kudai kuwa yeye si msemaji wa chama wilaya.
 
Kawawa apewa tuzo

Ubalozi wa Marekani nchini, umemtunukia tuzo ya Martin Luther King, Waziri Mkuu (Mstaafu), Mzee Rashid Mfaume Kawawa. Alikabidhiwa tuzo hiyo jana na Balozi wa Marekani nchini, Bw. Michael Retzer.

Akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo hiyo, Bw. Retzer alisema tuzo hiyo ni kumbukumbu ya mwanaharakati aliyekuwa mstari wa mbele kutetea haki za binadamu.

Alisema kila mwaka wamekuwa wakisherehekea maisha ya Dk. Luther Kingkwa ajili ya kujikumbusha harakati zake katika kudai usawa baina ya watu weupe na weusi.

Mji ninakotokea wa Mississippi uko kusini ambako harakati nyingi za kudai usawa zilifanyika na kutokana na harakati za Dk. King mambo yalibadilika na sheria za ubaguzi zilifutwa, `` alisema.

Alisema Dk. King ni shujaa kwa Wamarekani wengi na kwamba maisha yake yanaonyesha namna mtu mmoja anavyoweza kuleta mabadiliko katika taifa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mzee Kawawa alisema anaufahamu mchango mkubwa na msimamo thabiti wa marehemu Dk. Luther King juu ya ukombozi na kutetea haki za binadamu alioutoa.

Kamwe Dk. King hatasahaulika na ndiyo sababu mpaka leo jina lake bado linatajwa na kukumbukwa hata kama hayuko nasi, yeye ni mfano wa kuigwa, ``alisema mzee Kawawa.

Mzee Kawawa alisema heshima aliyopewa mbali na kumletea faraja ni kichocheo cha kuwatumikia Watanzania bila kujali itikadi zao za kidini au za kisiasa.

Alisema kuna umuhimu wa kuendeleza mshikamano uliopo baina ya Tanzania na Marekani ambao aliuelezea kuwa unachangia maendeleo ya nchi hizo mbili.

Aliishukuru serikali ya Marekani kwa misaada ya hali na mali ambayo imekuwa ikiipa Tanzania na aliiomba kuendelea kufanya hivyo.

Naomba msituchoke, muendelee kutusaidia mkizingatia kuwa nchi yetu bado ni changa na inahitaji misaada ili iweze kuendelea kijamii na kiuchumi, `` alisema.

Aliomba ubalozi huo kutupia macho makundi madogo madogo ya wajasiriamali ambayo hayajawezeshwa, ili yaweze kujikwamua kiuchumi na hivyo kuondokana na umaskini.


Source: http://216.69.164.44/ipp/nipashe/2007/01/24/82974.html
 
Waziri Mkuu mstaafu Mzee Kawawa amesikitishwa na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni

Waziri Mkuu mstaafu Mzee Rashid Mfaume Kawawa ameelezea kusikitishwa kwake na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kwa kile alichodai kuchelewesha uamuzi ya kuthibitisha eneo la mafundi gereji lililopo Asbestos Wazo Tegeta.

Mzee Kawawa amesema kuchelewa kutolewa kwa uamuzi huo kukwamisha juhudi za vijana kufanyakazi na kujiletea maisha bora.

Mzee Kawawa ambaye ametangaza mapema mwaka huu kuwa mlezi wa mafundi hao wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 3,000 waliojikusanya kutoka gereji bubu za Manispaa ya Kinondoni na kuhamia eneo hilo.

Hiyo ni kutokana na taarifa kutoka kwa kamati ya Mipango Miji na uongozi wa manispaa kuwa eneo hilo limetengwa kwa ajili ya shuguli za gereji.

Mzee Kawawa amesema hayo alipotembelea eneo hilo na kuzungumza na mafundi kuwa pamoja na taarifa za uongozi wa manispaa kumuahidi mara kwa mara kulitatua, lakini umekuwa ukisita hali aliyoitafsiri kuwa ni mbadiliko ya utendaji usiozingatia tija kwa jamii ya watu wanaowaongoza.


Source: http://216.69.164.44/ipp/radio1/2008/07/02/117658.html
 
Kawawa ajengewa makumbusho


WAZIRI Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu, Rashid Mfaume Kawawa, amesema viongozi walioko madarakani wanapaswa kuwa na moyo wa kujitolea zaidi na si kutanguliza maslahi yao binafsi.

Mzee Kawawa alitoa kauli hiyo jana nyumbani kwake Madale nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam wakati akitoa shukurani za kujengewa makumbusho ambayo itahifadhi mambo mbalimbali aliyopita katika nyanja za kisiasa.

"Nimefurahishwa sana na hatua hii ya watu kukaa chini na kufikiria hatua ya kunijengea makumbusho ambayo itakuwa na historia yangu, nasema hili ni jambo la kujivunia, na viongozi wanapaswa kuwa na moyo wa kujitolea kwa wengine badala ya wao tu," alisema Mzee Kawawa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa jengo hilo, John Morro alisema ili kukamilika jengo hilo kunahitajia sh bilioni moja, hivyo kutaka kila mtu mwenye mapenzi mema na Mzee Kawawa kujitolea kumchangia.
Alisema kamati yake imepanga mipango mbalimbali ya kuhakikisha inapata fedha hizo, mojawapo ukiwa ni kuandaa chakula cha hisani kwa lengo la kuchangisha fedha ambapo mgeni rasmi atakuwa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na lengo litakuwa kupata sh milioni 500.

"Tunashukuru kuona mzee wetu mwenyewe ametoa eneo kwa ajili ya kujenga jengo hili, lakini uwezo wetu ni mdogo sana ili kufanikisha hili, tumeandaa chakula cha hisani ambacho mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wetu Mizengo Pinda," alisema Morro.

Alisema baada ya hatua hiyo, wataandaa tena matembezi ya hisani ambayo yataongozwa na Rais Jakaya Kikwete yakiwa tena na lengo la kukusanya sh milioni 500 ambazo wanaamini kama zikipatikana zinaweza kumaliza ujenzi wa jengo hilo.

Morro alisema matembezi hayo yataanzia ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Rashid Kawawa- Madale na kumalizikia nyumbani kwa Mzee Kawawa ambako jengo hilo litajengwa.

Alisema katika awamu hiyo, kamati ya ujenzi itahusisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Mzee Kawawa kwa vile alikuwa kiongozi wa pande zote mbili.

Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Kanali (mstaafu) Fabian Masawe alisema kitendo cha kujenga makumbusho kitakuwa cha kujivunia na kwamba nguvu za haraka zinahitajika.
Jengo hilo litakuwa la ghorofa nne na litakuwa na ofisi ya Mzee Kawawa, ofisi za CCM tawi la Kawawa, ofisi za kituo ambacho kitatunza kumbukumbu zote za uelimishaji jamii kuhusu magonjwa ya ukimwi, afya ya mama na mtoto na kumbi za mikutano.


Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/7/habari5.php
 
Excessive hunting and poaching for 30 years in...

August 05, 1987

DAR ES SALAAM, TANZANIA - CAT FOOD. Excessive hunting and poaching for 30 years in the Selous Game Reserve caused a food shortage. Hungry lions began feasting on humans. ''We cannot allow beasts to play with people,'' political leader Rashidi Kawawa said Monday as he boarded a plane for southern Tanzania. He is going to lead a hunt for lions that killed 36 people in the last 18 months. Kawawa said efforts by local peasants, who have killed 15 lions since January 1986, had been hindered by a shortage of bullets.

http://articles.orlandosentinel.com...60026_1_southern-tanzania-lions-food-shortage
 
TFF honours Karume, Kawawa

Former Prime Minister Rashid Kawawa and Zanzibar's first President, the late Abeid Aman Karume, were among dignitaries who were awarded at a special function to honour ex- Taifa Stars and other personalities, at the National Museum in Dar es Salaam yesterday.

Both former premier and the late Karume were presented with the special recognition awards by Prime Minister, Mizengo Pinda, who was the guest of honour at the function which also saw the former Taifa Stars players and other dignitaries awarded certificates of excellence, for their contribution in football.

Players who benefited are those who featured for the nation between 1940 and March 1980. According to the Tanzania Football Federation (TFF) President, Leodegar Tenga, there were178 players who featured for the national team in that particular period of time and from them 118 are still alive.

The ex-Stars players - Kitwana Manara, Peter Tino, Mbwana Abushiri and Abdul Rajabu, picked the awards on behalf of other players who were selected for the award. Kawawa is well known to be fond of football, notably as both player and referee. He also at different occasions consulted to solve the conflicts mostly for the mainland clubs.

During his hey days, the former premier is said to have at different times, played for the Members of the Parliament team as their captain and also as the match official. The late Karume was recognised as a player. He was also the founder of African Sports team of Zanzibar, but also he contributed funds to finish Young Africans building at the Jangwani Street in Dar es Salaam.

He also supported giants Simba to buy its building at Msimbazi Street. Karume is also known to use sports to unite people during liberation struggle in Zanzibar. Speaking at the occasion, Kawawa urged the government to speed revival of school games, saying it was the only way the country could spot talented footballers, as it was in the past.

He added that the country will not succeed in sports, unless the concerned authorities make sure that they create as much playing ground for the youth as possible. He was not happy with the current situation where youth just play randomly in the street, saying it was not healthy for the country sport development.

He thanked the TFF and National Museum for recognising his contribution in football development. "This goes deep down my heart as something memorable. I will always cherish this memory," said the former premier. Pinda told the gathering that it was delightful to see the ex-national team players honoured.

He said the former players had left a strong foundation that the youngsters need to follow and build on. "They really deserve to be valued because apart from earning the nation respect, they also laid strong foundation that is still followed todate, "he said. He also reiterated the government intention to revive school games at all levels, saying everything was in the pipeline. He said that the fourth phase government will continue supporting sports in the country, because it was the best way to unite people.

Source: http://www.dailynews.co.tz/sports/?n=2228
 
Back
Top Bottom