Hotuba Maarufu Za Kisiasa

Petu Hapa

JF-Expert Member
Jan 2, 2008
714
55
Wale ambao mmesikiliza hotuba mbalimbali kuanzia mapambano ya uhuru hadi leo, kama kuna hotuba yoyote ambayo unafahamu ilileta mabadiliko ya kisiasa ama kijamii tuwekee hapa.

Hotuba ambazo ziliwakugusa wananchi, viongozi ama uhalisia wa mambo. Hotuba ambazo bila hata sisi kujua zimejikita katika maongezi yetu ya kila siku kwa namna moja ama nyingine, wakati mwinginge tunatumia fikira zilizopo kwenye hotuba hizo kama nyezo za shughuli zetu.

Katika hotuba hizo naimani kunamafunzo na hamasa tunazoweza kupata kukabiliana na mazingira yetu ya leo. Unauhuru wa kuandika umuhimu wa hotuba hiyo ukipenda

Ombi: Kwa wale ambao hatuba hizo zinaweza kupatikana kwenye mtandao, tafadhali tuwekee link na maelezo mafupi kwanini unadhani hotuba hiyo ni muhimu sana.

HOTUBA MAARUFU
1. Mwalimu Nyerere
2. Horace Kolimba - (??)

WACHANGIAJI KATIKA HOTUBA ZA MWALIMU
1. Bw. Andrew Daraja
2.

WACHANGIAJI WENGINE KATIKA UANDISHI WA NYERERE
1. Bw. Benjamini Mkapa
2. Mzee. Bukuku
 
Last edited:
Hotuba ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere mara tu baada ya kuwa Waziri Mkuu kufuatia ushindi wa TANU ambao ulikipa ridhaa chama hicho kuunda Baraza la Kwanza la Mawaziri wa Serikali ya Tanganyika mwaka 1961. Hapa nitakata vipande ambavyo naona vinaweza kutumika katika mazingira yetu ya sasa. Hotuba kamili inapatikana katika MAELEZO YA KWANZA YA MWALIMU NYERERE KAMA WAZIRI MKUU WA KWANZA TANGANYIKA.

Nadhani hotuba hii ni muhimu kwani Nyerere hakuahidi mbingu, zaidi ya kuwakumbusha wananchi juu ya wajibu wao na nguvu zao katika kuleta maendeleo. Haya ndio baadhi ya maneno niyapendayo.

"Nawaelezeni jambo hili kwa unyenyekevu mkubwa, kwa sababu mimi na wenzangu, ni watumishi wenu ninyi mnaonisikiliza. Tunajua kuwa mnatuamini, nanyi tunawaamini. Na ni ninyi tu mnaotupa nguvu zetu, tunazozihitaji kwa kazi kubwa iliyo mbele yetu.

Je leo tunawaamini viongozi wetu? Je tunatambua ni sisi ndio tunawapa nguvu ya kutuongoza?

Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, na imani mliyonayo juu yetu, tunapata, na tutazidi kupata nguvu za kuendesha serikali yenu. Lakini tunawaomba msisahau, na mara nyingi sana, nimekukumbusheni jambo hili, kwamba serikali haiwezi kufanya kila kitu.

Je tumeshafanya upembuzi wa kina kipi ni wajibu wa serikali na kipi ni wajibu wetu?

Utajiri wa Tanganyika, bado uko ardhini. Hatuanzi na akiba kubwa ya fedha kama Ghana kwa mfano, iliyoanza nayo ilipopata uhuru wake. Hatuna mkononi fedha walizonazo ndugu zetu wa Nigeria. Kwa kweli, elimu yetu iko nyuma zaidi kuliko Kenya na Uganda.

Leo tunagawa ardhi kama peremende!

Kwa hiyo, tunaanza bila ya kuwa na wananchi wa kutosha, wenye elimu ya juu, tunayohitaji katika jitihada zetu za kujenga utajiri wa nchi hii.

Lakini matatizo haya, hayanitishi mimi, hayawatishi wenzangu, na wala hatuombi kwamba yawatisheni ninyi. Tunayaona kwamba ni jaribio tu. Lakini jaribio hili, na umasikini, si la serikali tu, ni la kila raia wa Tanganyika.

Unaona kibri hicho "hayanitishi mimi, na wala yasitutishe sisi"

Lakini ni ninyi tu, tunaoweza kupigana vita vya umasikini. Namuomba kila raia wa Tanganyika, aape kiapo cha kuwa adui wa umasikini. Amshambulie adui huyo mahali popote atakapoonekana.

Hamna kiongozi anayeweza kutuletea maendeleo ni nguvu kazi yetu ambayo itaendeshwa kwa uongozi dhabiti"

Ukiacha pamba yako shambani bila kuichuma, ukiwa na uwezo wa kuongeza shamba lako kwa eka moja, au nusu eka, au hata robo eka, lakini ukaacha kwa uvivu tu.
Ukaacha rutuba ya shamba lako ikaharibiwa, ikiwa shamba lako limejaa magugu na wewe hujishughulishi kuyaondoa, ukiwa unapuuza masharti unayopewa na wataalamu wa kilimo au hujishughulishi kuongeza elimu yako ya kilimo, au ukiwa unazurura tu bila kufanya kazi, ikimtegemea mjomba au shangazi, au Prime Minister wa Tanganyika akufanyie kazi, basi wewe ndugu yangu, si adui wa umasikini.

Wewe si adui wa ujinga, wewe si adui wa maradhi, wewe kwa kweli ni rafiki mkuu wa maadui hao. Wewe ni adui wa Watanganyika wote wanaofanya jitihada yao yote kumshambulia adui huyo.

Ndugu zangu, vita hivi ni vyenu, vita hivi ni vyetu wote na adui yetu ni huyo niliyemtaja. Basi, tusipoteze wakati wetu tukishambulia maadui ambao kwa sasa ni marehemu.

Tusidhani hata kidogo kwamba sifa yetu katika Afrika au sifa yetu katika Dunia nzima, itategemea ukali na ufundi wa matusi tutakayotumia kutukana ukoloni uliokufa au hata ukoloni mpya utakaojaribu kuanzishwa kwa ujanja na hila za watu wasiopenda uhuru wetu.

Leo tunakemee ufisadi! Je bila kuchukua hatua tutaleta mabadiliko kweli?

Sifa yetu, itategemea mambo tutakayofanya kuongeza na kudumisha nguvu zetu ili tuwe na uwezo wa kulinda uhuru wetu wenyewe, na pia kuwasaidia ndugu zetu wengine kupata uhuru wao na kuulinda pia.

Wala tusipoteze wakati wetu katika kugombania vyeo na fahari ya nafsi. Kilichotufikisha hapa leo, kwa upesi hivi na kwa amani hivi, ni umoja wa watu wa Tanganyika. Ninapoulizwa kwa mfano, ni nini mwezi wa Machi kwa muda wa siku mbili tu, jibu langu ni moja, umoja.

Tuweke tofauti za vyama, tupiganie maslahi ya taifa letu jamani!

Nani asiyejua kwamba msingi wa kufanikiwa kwa TANU, ni umoja wa TANU. Kadhalika katika vyama vya ushirika au vyama vya wafanyakazi wanachama wake wanaposhikana bega kwa bega, mambo yao yatawaendea vyema. Wanachama wake wakigombana na kutengana, mambo yao na mambo ya taifa zina yatakwenda tenge.
Gazeti-Mtanzania
ISSN 0856-5678
Tarehe: Ijumaa Oktoba 14, 2005.
 
Mimi nazikumbuka hotuba mbili za mwalimu J. K Nyerere, 1. Aliyoitoa Mei Mosi 1995 Pale uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Mbeya 2. na ile iliyotanguliwa nayo mwaka huo huo mwezi February aliyoitoa pale Kilimanjaro hotel kwa waandishi wa habari. Mwenye hizo hotuba azipost Jamani.
 
Yaani maisha yote ya tanzania tunazikumbuka za nyerere tu! Hii ni hatari!
 
Hotuba ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere mara tu baada ya kuwa Waziri Mkuu kufuatia ushindi wa TANU ambao ulikipa ridhaa chama hicho kuunda Baraza la Kwanza la Mawaziri wa Serikali ya Tanganyika mwaka 1961. Hapa nitakata vipande ambavyo naona vinaweza kutumika katika mazingira yetu ya sasa. Hotuba kamili inapatikana katika MAELEZO YA KWANZA YA MWALIMU NYERERE KAMA WAZIRI MKUU WA KWANZA TANGANYIKA.

.

Nakushukuru sana nadhani umefikiri kitu cha Busara na chenye maana sana. hotuba hii ya JK Nyerere inamafunzo mengi lakini sijui kama wanayashika licha ya kusema wanamuenzi. Binafsi nimewahi kusikia hotuba ya Mwalimu RTD sasa TBC akizungumzia Mwadui kubaki mashimo nakubwa ambayo hatutaweza kuyafukia licha ya kutoa almasi nyingi lakini wananchi wa Maganzo wako hoi, hotuba hii ningependa kuipata zaidi kwa kina naomba aliyenayo ama anayoifahamu ailete hapa.
 
Wale ambao mmesikiliza hotuba mbalimbali kuanzia mapambano ya uhuru hadi leo, kama kuna hotuba yoyote ambayo unafahamu ilileta mabadiliko ya kisiasa ama kijamii tuwekee hapa.

Miongoni mwa hotuba kali niliyoisoma "Nyaraka za Taifa" ni ya Mheshimiwa Kiongozi Kinjekitile Ngwao, wakati anawajenga jamaa kupigana Vita vya Maji Maji. Ni hotuba fupi, iliyokuwa na hamasa, ushawishi, ujasiri na muelekeo.
 
Authenticity ya hotuba? Kama unakumbuka mawili matatu tupe hapa tufaidi-Kinjekitile Ngwale ni shujaa wangu wa ukweli its sad hatendewi haki na historians both wazawa na wakoloni aaaaghhhhhhhhhrrrrrrr!!!!!!!
 
KINJEKITILE huyu ninayemfahamu mimi ambaye ni mheshimiwa saana au.....?
 
Asanteni kwa bidii zenu.
Naomba pia mtu anayeweza kutuwekea hapa hotuba za Adolf Hitler. Kuna maelezo kuwa Hitler alikuwa a great man of oration.
 
Yaani maisha yote ya tanzania tunazikumbuka za nyerere tu! Hii ni hatari!
Tumekuwa na viongozii wengi na wasemaji wengi lakini hawajawahi kusema kitu cha kuwafanya wakumbukwe, sisi wengine apart from Nyerere tunaweza tukakwambia Hotuba za Rais Kennedy, au Nickson, Rais Nkrumah, Martin Luther King Jr, Malcom X, Ghandi etc kama tungekuwa tunafikiria globally. Lakini ukisema kwa TZ siwezi kukumbuka kitu zaidi ya Hotuba za JKN. Kwani akina msuya, Malecela, Kawawa, sokoine, Kikwete, ben, Alhaji wote sikumbuki kitu,hii inamaana hawajwahi kuwa na hotuba ya mvuto kwangu, Kwa hiyo nadhani hatuwezi kulazimisha kukumbuka kitu ambacho siwezi kukikumbuka, labda waweke kipindi kingine RTD sijui wakiite wosia wa Ndugu wengine bwa ha ha
 
..binafsi siko interested sana na mtoa hotuba, bali mwandishi wa hotuba hiyo.

..nani alikuwa akiandika hotuba za Nyerere,Mwinyi,na Mkapa. kwa mtizamo wangu hao ndiyo waliofanya kazi kubwa zaidi.

..waandishi wa hotuba za Kennedy,Nixon,Reagan,Clinton,... wote wanajulikana na wanapewa heshima kutokana na kazi zao.

..tufike mahali wa-Tanzania tuanze kuwatunza baadhi ya watumishi wa umma ambao wako behind the scene wakilitumikia taifa kwa uzalendo wa hali ya juu kabisa.
 
Mara nyingi hotuba za mwalimu siyo za kuandikiwa kama wafanyavyo viongozi wengi.Ndo maana hotuba zake ziliwekwa kwa pamoja na kuwa vitabu k.m kitabu Binadamu na maendeleo,n.k
Na hicho ndicho kinachomtofautisha na viongozi walio wengi unapoandikiwa hotuba unacozungumza ni mawazo uliyopangiwa kuyasema.
Na si ajabu ukawa mtu wa kusema hili na kutenda lile.
 
Kahinda said:

Kahinda,

..ijulikane basi ni hotuba ni zipi Mwalimu aliandika mwenyewe na zipi aliandaliwa na wasaidizi wake. pia ijulikane wasaidizi hao ni kina nani.

..kwanini masuala kama haya yanakuwa ni siri? kuna ubaya au aibu gani kuwatunza watu kama hao hadharani?

..ninachopigania mimi ni historia yetu na michango ya wananchi mbalimbali kuwekwa wazi.
 
Kwa hiyo Penu Pale unataka ukumbukwe ufisadi na pumba za RA au?

Sisemi za RA ndio zikumbukwe, lakini sitashanganzwa kwamba ungesoma vizuri hotuba zake labda tusingeweza kushangazwa na yanayotokea leo! Hotuba mbaya au nzuri ndani yake inabebwa taswira ya huyo mwandishi!

Pili, nafahamu nyerere anahotuba zenye msimamo na ndio maana hotuba ya kwanza nimeweka ya kwakwe, lakini sitaki kuamini ndio mtu pekee tanzania ambaye alikuwa anatoa hotuba za maana. Nadhani tukijaribu kutafuta tunaweza kupata maneno ya busara nje ya nyerere!
 
Miongoni mwa hotuba kali niliyoisoma "Nyaraka za Taifa" ni ya Mheshimiwa Kiongozi Kinjekitile Ngwao, wakati anawajenga jamaa kupigana Vita vya Maji Maji. Ni hotuba fupi, iliyokuwa na hamasa, ushawishi, ujasiri na muelekeo.

Tafadhali ikumbuke hotuba hiyo, uandike mwenyewe, utuwekee hapa.
 
..binafsi siko interested sana na mtoa hotuba, bali mwandishi wa hotuba hiyo.

..nani alikuwa akiandika hotuba za Nyerere,Mwinyi,na Mkapa. kwa mtizamo wangu hao ndiyo waliofanya kazi kubwa zaidi.

..tufike mahali wa-Tanzania tuanze kuwatunza baadhi ya watumishi wa umma ambao wako behind the scene wakilitumikia taifa kwa uzalendo wa hali ya juu kabisa.

Nakubaliana na wewe kabisa, na hilo ni jambo la msingi sana!

Tafadhali mwenye ufahamu ni nani alikuwa mchangiaji mkuu katika uandishi wa hotuba za nyerere atufahamishe!

That will be very interesting!
 
Mara nyingi hotuba za mwalimu siyo za kuandikiwa kama wafanyavyo viongozi wengi.Ndo maana hotuba zake ziliwekwa kwa pamoja na kuwa vitabu k.m kitabu Binadamu na maendeleo,n.k
Na hicho ndicho kinachomtofautisha na viongozi walio wengi unapoandikiwa hotuba unacozungumza ni mawazo uliyopangiwa kuyasema.
Na si ajabu ukawa mtu wa kusema hili na kutenda lile.

Mwalimu alikuwa anatayarishiwa hotuba. Kabla ya kuhutubia anaisoma na kuiweka kichwani, hivyo alikuwa anajua atazungumzia nini. Uzuri alikuwa na kichwa cha kukumbuka na kukariri yale aliyoandikiwa ayahutubie.
 
Nakubaliana na wazo kwamba mwalimu alikuwa anaandikiwa hotuba na juu uwezo wake wa kukariri. Lakini na imani mwalimu alikuwa anakubalina na maandishi anayosema. Inakuwa vigumu sana kuamini kwamba mwalimu angeweza kukariri vitu ambavyo haviamini!

Mwandishi au waandishi wa hotuba hizo walikuwa kina nani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom