Hotpot nalo sanduku la kura?

dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,725
255
Ndugu wana Jf tumeshuhudia maneno mengi toka kwa wapinzani wakati wa kampeni na baada ya kupiga kura juu ya mbinu chafu zinazofanywa na CCM kwa kuingia katika vyumba vya kupigia kura na ma hotpot ya vyakula kwa kisingizio cha kuwapelekea mawakala wao vyakula. Hii ilikuja thibitika kuwa huwa sio chakula bali ni kura zilizopigwa tayari ili kuongeza kura kwa mgombea wao. Wana JF, leo hii CCM imekuwa ikijitapa kuwa inapambana na wezi wa mali ya UMMA wakati wa kutafuta kukaa madarakani inatumia mbinu za wizi. Je huu wizi utaisha? Lakini pia, je ni vizuri kujisifu kuwa nawe ni mwizi na utatawala daima na milele? Kwa kipindi cha uchaguzi wapinzani hubakia mita mia toka eneo la kupigia kura kwa kuhofia kuibiwa na CCM kura zao. Je, hili nalo ni suala jema kwa CCM kwa kusifika kuwa wao ni wezi wa kura?
 
ccm hawana chao hakuna mwizi aliyedumu kwani haki siku zote lazima itashinda uovu tuu
mfumo wanaoutumia CDM wa piga kura linda kura ni muhimu sana kutumiwa dhidi ya hawa magamba
 
Back
Top Bottom