Hoteli iliyozunduliwa na JK yavunjwa!

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Sijui kama hii ipo hapa.
Ile Hoteli ya kitalii ya Snow Crest iliyozinduliwa Ijumaa iliyopita mjini Arusha na JK, imevunjwa leo alfajiri na maofisa wa Tanroads kwa maelezo kuwa sehemu ya majengo yake yalikuwa katika hifadhi ya barabara. Vitu vilivyovunjwa ni pamoja na geti kuu la kuingilia hotelini, sehemu ya fensi na kibanda cha walinzi.
 
Hizi ndiyo nchi zetu. na ndiyo maana hazi-hishiki! Ni lazima hawa nao wameona kuwa waonyeshe ubabe wakavunja. Masikini hajui thamani ya pesa. yeye ni vunja vunja tu!
 
Visirani tuu,kiwanja alipataje na hao wana road reserve walikuwa wapi?
Mnadiscourage wawekezaji uhuni huo
The same ilitokea Yombo kisiwani Makamba akiwa DSM RC aliwaambia TAZARA mlikuwa wapi wakati wananchi wanajenga!
Hawakubomoa
 
Tamaa ya pesa. Kama Tanroads wamevunja si washitakiwe tu ili tuone nani mwenye makosa. Lakini vile vile hapa kuna mushkeli kubwa sana ilikuwaje JK aende kufungua Hoteli ambayo inaelekea ilijengwa kwa mizengwe.
 
Knowing my country and my fellow countrymen and women, sitashangaa kuona huyu bwana alipata pesa akawa na kiburi.

Tatizo wengi wetu ni shule. We get money wakati hatuna uwezo wa kupambanua namna ya kuzi invest. Inawezekana jamaa alitumia pesa kuhonga, wakati ameshaambiwa hilo eneo ni la bara bara. Infact mimi nilivyoona amemleta JK kuifungua nimeshtukia..naona kama ni jamaa anayependa misifa.

TANROADS siyo wajinga hivyo. Huyu atakuwa alitumia ubabe wa "connection" na wakubwa kuamua kujenga bila kufuata utaratibu.

I will be pleasantly surprised kama jamaa alionewa.

NB: KAMA JAMAA YUKO WRONG..SIONI HAJA YA KUMUHURUMIA ETI ALIWEKA PESA NYINGI...NI LAZIMA AJIFUNZE KWAMBA TUNAPOIMBA KILA SIKU RULE OF LAW..TUNATAKA WATU WAFUATE SHERIA. Sasa kwa vile anafahamiana na JK...ndo alidhani kwamba he can do whatever he pleases....I have the feeling jamaa alitumia ubabe wa connection kuwadharau Tanroads.
 
Sio mchezo na haya ndiyo yanachezea credibility ya ofisi hizi kubwa.wanachezeana patapotea kama wanacheza sandakarawe vile.Haiingi akili hoteli iliyofunguliwa na rais, barely 4 days, geti linapunguzwa kwa kutofuata sheria
 
wakati inajengwa walikuwa wapi? Yaani sisi sijui tukoje!

Tatizo hapa siyo wavunjaji yaani Tanroads au wamiliki wa Hotel, tatizo ni huyu rais wetu kufungua kitu then kesho yake kinavunjwa anajisikiaje? na si tuelewe nini?, haya ndiyo mambo tulikuwa tuna discuss the other day kabla ya ufunguzi yaani - priority zake- mi naona kajitakia mwenyewe.

Ningemsifu zaidi angeenda kwao chalinze akague wakulima wa mananasi ambao hata hawana soko la uhakika, juzi nimepita pale minanasi inajiozea tu barabarani.

wana JF mnaonenda Moshi / Arusha Xmas, angalieni minanasi pale chalinze innavyooza na hali ya kiuchumi ya wananchi wa eneo analotoka mkulu wetu.

Wakati huo huo mi juice kibao ya kutoka SA imejazana kwenye supermaket za wadosi, wakati miembe, michungwa na minanasi inatuozea. ha ha ha - heko Tanzaniaaaaa

We have long way to go....
 
Sijui kama hii ipo hapa.
Ile Hoteli ya kitalii ya Snow Crest iliyozinduliwa Ijumaa iliyopita mjini Arusha na JK, imevunjwa leo alfajiri na maofisa wa Tanroads kwa maelezo kuwa sehemu ya majengo yake yalikuwa katika hifadhi ya barabara. Vitu vilivyovunjwa ni pamoja na geti kuu la kuingilia hotelini, sehemu ya fensi na kibanda cha walinzi.

Agizo nafikiri limetoka kwa Mkuu mfunguzi wa hotel
 
Tamaa ya pesa. Kama Tanroads wamevunja si washitakiwe tu ili tuone nani mwenye makosa. Lakini vile vile hapa kuna mushkeli kubwa sana ilikuwaje JK aende kufungua Hoteli ambayo inaelekea ilijengwa kwa mizengwe.

Hawa jamaa waliambiwa siku nyingi kuwa wamevunja sheria kwa kujenga uzio kwenye road reserve sasa kuonesha jeuri ya pesa yao na kutaka kuwatisha waliowapa tahadhali hiyo ndio wakaja na mbinu ya kumualika Rais ili aje afungue hiyo hotel kuhalalisha makosa yao!! Wamevunjiwa kwa uhalali kabisa ili liwe fundisho kwa wakola wengi wanaojenga hovyo hovyo mijini!
 
Sijui kama hii ipo hapa.
Ile Hoteli ya kitalii ya Snow Crest iliyozinduliwa Ijumaa iliyopita mjini Arusha na JK, imevunjwa leo alfajiri na maofisa wa Tanroads kwa maelezo kuwa sehemu ya majengo yake yalikuwa katika hifadhi ya barabara. Vitu vilivyovunjwa ni pamoja na geti kuu la kuingilia hotelini, sehemu ya fensi na kibanda cha walinzi.
...Mi nadhani kuna watu ambao sehemu fulani za ubongo wao zinahitilafu unless kama hao wamiliki wa hotel waliambiwa tangu mwanzo kuwa wasijenge kwenye hifadhi ya barabara wakapuuza otherwise ni uhuni kwenda kuvunja fence wakati gharama zimetumika nyingi tu. Ndio kukomoana?
 
siku zote hapa bongo watu hawatakai kuona maendeleo ya wengine, sasa toka msingi unachimbwa mpaka jengo kuzinduliwa ninyi mlikua wapi? wacheni hizo jamani, sasa mkibomoa je mmewalipa?
 
...Mi nadhani kuna watu ambao sehemu fulani za ubongo wao zinahitilafu unless kama hao wamiliki wa hotel waliambiwa tangu mwanzo kuwa wasijenge kwenye hifadhi ya barabara wakapuuza otherwise ni uhuni kwenda kuvunja fence wakati gharama zimetumika nyingi tu. Ndio kukomoana?

Refer post ya Bulesi hapo juu
 
inawezekana kabisa hayo ni maagizo kutoka kwa mwenye nchi ukizingatia tunaelekea uchaguzi mkuu jamaa akaona itamuaribia.
 
as I always say, inji hii haina uongozi, mambo mengi ya kujiuliza, ilikuwaje mwekezaji akapewa kibali cha kujenga hotel ktk hifadhi ya barabara? ......mlolongo mrefu mpaka kufikia watu walioprocess mwaliko wa rais kwenda kuzindua hotel iliyojengwa barabarani.
Too shame!!!!!!!!!
 
MOD tayari kuna thread nyingine inayofanana na hii tafadhali ziunganishwe ili kuleta mtiririko mzuri.
 
hii ni aibu pia kwa raisi ambae mpaka anaenda kuzindua hiyo hotel alitakiwa awe na full information kuhusiana na uhalali wa hoteli hiyo......ss tuone kama hao TANROADS watashitakiwa,inafurahisha kuona owner wa hotel analalamika eti hizo ni harakati za wabaya wake(competetitors)ama kweli kazi tunayo
 
Namwamini mate Kakoko kwamba atakuwa hajakurupuka na amechukua maamuzi kwa kufuata sheria za nchi.

Kakoko ni yue aliyekuwa moto wa kuotea mbali alipokuwa mlimani miaka ya 1986 -1991.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom