Hotel ya Sea Cliff inawaka moto sasa hivi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,484
54,855
Habari nilizopata hivi punde ni kwamba hotel ya seacliff inawaka moto sasa hivi. Na moto ni mkubwa sana. so wenye access nafikiri watafuatilia kwa karibu hili swala. Mia
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wana JF

Nimepata taarifa kuwa moto mkubwa unawaka katika hoteli ya Sea Cliff iliyoko masaki Dar es salaam.

Ikumbukwe hii ni mara ya pili hoteli hii kuungua moto. Jitihada za kuuzima bado zinaendelea lakini moto bado ni mkubwa sana kwa sasa
 
Habari nilizopata hivi punde ni kwamba hotel ya seacliff inawaka moto sasa hivi. Na moto ni mkubwa sana. so wenye access nafikiri watafuatilia kwa karibu hili swala. Mia

Asante kwa info japo bado ni tetesi. Mia
 
sijui kama watawahi coz hii ni mara ya pili hii hotel inaungua. Hii inaonyesha hatujifunzi kutokana na makosa. Mia
 
Kwa mara nyingine tena!!! Dah! naona huu umeshakuwa mchezo wa hawa wahindi labda kuna kitita cha bima maana haiwezekani katika miaka michache baadaye moto mwingine utokee katika hotel ile.

we kweli GT nakuongeza like lingine mkuu...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
moto ulitokea Jumapili, September 23, 2007 karibu miaka mitano baadaye moto mwingine!!!! Hapa kutakuwa na namna si bure.
 
Hata mimi nimeisikia juu juu, vp hakuna aliyepoteza maisha lakini?
 
Wanajua wenyewe Mkuu lakini moto mwingine baada ya miaka mitano inatia shaka labda wanaiunguza hata ule moto wa 2007 kuna watu walidai wameiunguza. Inataka uchunguzi wa kina na watu waliobobea katika maswala ya uchunguzi wa moto ili kuweza kulithibisha hili, na Tanzania sidhani kama tuna wataalam kama hao.

inaunguwa au wanaiunguza?
 
Kwa mara nyingine tena!!! Dah! naona huu umeshakuwa mchezo wa hawa wahindi labda kuna kitita cha bima maana haiwezekani katika miaka michache baadaye moto mwingine utokee katika hotel ile.

Mkuu BAK, hata mimi nimeshangaa. Hawa wahindi huenda wanaendeleza huu mchezo wao. Mara ya kwanza ilipoungua wakalipwa na bima na jamaa walisikika wakitamba kuwa "baada ya kuungua tutakuja na kitu kikali zaidi". Naona tena wanataka kuja na kitu kingine kikali zaidi, lol! Nimewahi kusikia story ya mhindi mmoja huko Arusha aliyekuwa na kawaida ya kuchoma nyumba zake moto halafu analipwa na bima. Walipoona amezidi wakamfanyia ujasusi wakakamata mawasiliano yake ya simu na watu waliokuwa wanapanga nao huo mchezo mchafu, nasikia aliishia kunywa sumu wakati akingojea kesi yake.
Halafu nasikia pia mh. Ali Hassani Mwinyi ana hisa hapo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa matukio planned, haiwezekani akafa mtu hapo. Tusubiri kusikia tathmini ya uharibifu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom