Hotel ya Lamada inaiba Maji

NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
559
26
KAMPUNI ya Usambazaji Maji kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, Dawasco, imekata maji katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam kwa kujiunganishia maji kiholela.

Hoteli hiyo imekuwa ikitumia maji ya DAWASCO bila kulipa Ankara toka kuanzishwa kwa kampuni hiyo baada ya serikali kuvunja mkataba na kampuni ya city water.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo jana, Mkurugenzi Mkuu wa Biashara wa Dawasco, Raymond Mndolwa alisema wanaidai hoteli hiyo zaidi ya Sh96 milioni.

"Kwa kawaida tukiwakamata hawa watu wanaojiunganishia maji kinyamela huwa tunawapelekea Ankara ya miezi 24, na kwahoteli kama hii tunaikadiria inatakiwa ilipe milioni nne kila mwezi" alisema Mndolwa Pia alisema mbali na hoteli hiyo kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha, wataifikisha mahakamani kwa kosa la kuiujumu Dawasco.

Alisema wamekuwa wakifika hotelini hapo mara kwa mara kufuatilia chanzo cha maji yanayotumiwa na hoteli hiyo lakini uongozi wa Lamada ulikuwa ukijibu kuwa maji yanayo tumika ni yakisima.

Mndolwa alisema kuwa mbali na kusambaza maji katika hoteli hiyo, pia wamejenga kisima ambacho uhifadhi maji ya kampuni hiyo baada ya kuyateka kutoka kwenye bomba la upana wa nchi tatu ambalo linaingiza maji hotelini hapo.

Alisema habari za kujiunganishia maji kiholela katika hoteli hiyo walipata kutoka kwa wasamaria wema.
Juhudi za kumpata msemaji wa hoteli hiyo hazikuzaa matunda baada ya mtu wa mapokezi kusema hamjui mkuu wake wa kazi na kuwa yeye nimgeni hotelini hapo

Source:Mwananchi

Hii hoteli wamiliki wake inasemekana ni Mrs A Mkapa akishirikiana na Bwana Kishimba tena huyu jamaa anatafutwa na polisi kwa ufisadi. Hivi kwanini wafanyabiashara wa Kitanzania wanapenda kuiba na dezo ya huduma za maji na umeme kila mara utasikia biashara zao mara wanatumia vishoka maji wanajiungia kiwizi halafu wanatamba wao ni wafanyabiashara wakubwa why?
 
Yaani aibu tupu! Wizi kuanzia Juu, Katikati hadi chini kabisa. Nadhani tuonaolipa maji na umeme kihalali ni walalahoi pekee. Hawa Lamada Hotel wakabwe hadi mwisho bila kuzingatia kama ni Mama Mkapa au Baba Mkapa.
 
Back
Top Bottom