Hospitali ya AghaKhan Dar waanza kupima kisukari bure

OkSIR

Senior Member
Jun 3, 2009
108
1
Hospitali ya AghaKhan Dar waanza kupima kisukari bure


Na Patricia Kimelemeta

HOSPITALI ya Aghakhan imeanza kupima wagonjwa wa kisukari ikiwa ni moja ya mpango wake wa kuwafikia wagonjwa katika jamii inayowazunguza.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa mpango huo, Dk Jacob Shabani alisema wananchi wengi wanapata matatizo ya magonjwa yasiyoambukiza lakini
wanashindwa kwenda hospitali kupima.

Alisema kutokana na hali hiyo mpango huo utaweza kuwafikiwa wananchi wengi ambao wanasumbuliwa na ugonjwa huo, lakini wanashindwa kujitambua kwa sababu hawajapatiwa vipimo vya kiafya.

"Tumeamua kuanzisha mpango huo ambao tunaamini tutaweza kufanikiwa kwa kuwafikiwa wananchi wengi na kuwajengea tabia ya kwenda katika vituo vya afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu, na ushauri,"alisema Dk Shabani.

Aliongeza kuwa mkakati wao ni kuwapima wagonjwa
zaidi ya 1,000 na kupatiwa ushauri nasaha juu ya kupunguza tatizo hilo. Shabani alisisitiza kuwa, mpango wao wa kuwapima wagonjwa utaendelea hadi mikoani katika hospitali zote za Agha Khan kwa ajili ya kuwapatia huduma hiyo wananchi wa mikoa hiyo.
 
Impressive, even though these procedures could be done by patients themselves, kuelimishana how to ni muhimu.

B
 
Impressive, even though these procedures could be done by patients themselves, kuelimishana how to ni muhimu.

B

But you have to know first that you are sick first ndo upime mwenyewe. Ni kitu kizuri hicho, nafikiri wao watafanya random blood sugar check up peke yake na hiyo ina false positives nyingi sana, kwa sababu inategemea yule mtu amekula saa ngapi. Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa over diagnosis ya kisukari. Ni bora wakatumia Glucose tolerelence test, au ikiwezekane watumie HbA1 ambazo kidogo ni specific.
 
Back
Top Bottom