ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Mimi sio daktari ila nahindwa kukubali kama kumpasua mtu kibofu ni acceptable alafu ushindwe ku repair hadi afe. Na hakufa haraka ni kweli unavyosema alikufa baada ya wiki 3, labda ni acceptable kufa pole pole in 3 weeks
Katika operation ya uzazi, kupasua kibofu ni mojawapo ya complications zinazotarajiwa. Katika nchi zilizoendelea kama Marekani na Uingereza 0,5 -1 percent ya watu wanaofanyiwa operation hii hupata madhara haya. Pia hutegemea kama operation inafanyika kwa mara ya kwanza au mgonjwa anazaa kwa operation mara ya pili na zaidi, au kama kuna opration nyingine ya tumbo alifanyiwa.
Kuchana kibofu sio complication ya kusababisha mgonjwa kufa. Dawa yake huwa ni kurepair tu. Iwapo surgeon ameshindwa kurepair anaweza kuzuia damu kumwagika halafu akafanya utaratibu wa kumpata surgeon mwenye ujuzi wa kurepair.
Kama mgonjwa alichanwa kibofu wakati wa operation ya uzazi na daktari aliyefanya hiyo operation akagundua kuwa kibofu kimechanika hakiwezi kutokea kifo chenye uhusiano wa moja kwa moja na kuchanika kwa kibofu.