Hoseah: Chenge ana kesi ya kujibu

Chenge ambaye wakati wa ununuzi huo alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) anatuhumiwa kuwa kiungo muhimu katika ununuzi wa rada kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya BAE Systems. .

Asisitiza hana kesi ya rada
Kuhusu kuhusika kwa Chenge katika kashfa ya rada baada ya Mahakama Kuu Uingereza kuamuru BAE Systems kurejesha sehemu ya fedha kwa Tanzania kutokana na kubaini upotevu wa nyaraka muhimu za manunuzi halali, Dk Hoseah, alisema, mbunge huyo hahusiki na kwamba hakuna ushahidi wowote wa kumtia hatiani.

“Nashangaa kuona Watanzania wakishikilia kuwa Chenge ashtakiwe kwa kitu ambacho hakina ushahidi, lakini wanasahau kuwaeleza Waingereza kuwa ndio wahusika,” alifafanua Dk Hoseah,
Kuhusu Kagoda
Akizungumzia kashfa nyingine inayotikisa Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited inayodaiwa kuchota Sh 40 bilioni kutoka Akaunti ya Madeni Nje (EPA) katika Benki Kuu Tanzania (BoT), alisema taasisi yake imeanzisha upya uchunguzi, licha ya kamati ya Rais Kikwete, kuwabana wahusika wakarudisha kitita hicho.

Dk Hoseah alisema kwa kutambua hilo, ndiyo maana amewaomba Watanzania wote wenye ushahidi wauwasilishe ofisini kwake ili kuwezesha kuendelea kwa mchakato huo wa kuwafikisha mahakamani wahusika wote. Mkuuu huyo wa Takukuru, alisema kwa sasa kumbukumbu katika jalada la usajili wa kampuni hiyo kwa Msajili wa Makampuni (Brela), zinaonyesha wamiliki wake wote wawili ni marehemu.

Mwananchi
Huo ndio usanii wa Tanzania na takukuru yake.
Yaani chenge alikuwa kiungo muhimu kati ya tanzania na BAE kwenye ununuzi wa rada; na imeshabainika kuwa ununuzi ule uligubikwa na rushwa, halafu hicho kiungo kiwe hakiusiki? Inashangaza na inatia mashaka.
Kama hana kesi ya kujibu juu ya suala zima la rada, kwanini sasa mnamshitaki. Mimi nadhani mnamshtaki si wa kuwa na mali bali ni kwa kuwa mali ni nyingi na mna wasiwasi na namna alivyozipata, na mojawapo ya njia hizo ni rushwa katika rada.
Isitoshe chenge hakujuliana leo kuwa ana mali nyingi, mlimjua tangu aliposema kuwa hizo dola 1.2m ni vijisenti - mbona hamkuchukua hatua wakati huo?.
Hosea tunakushangaa sana - ulishakataa kumshitaki chenge kwa masuala hayo tangu zamani, leo umesukumwa na nini?. Kuna sababu mbili
Ya kwanza ni kuwa serikali imeona inanyimwa hela za rada kwa kuwa inatuhumiwa kuwalinda mafisadi wa rada, sasa inaona ijitutumue. Wakishalipwa, yanaishia hapo.
Pili ni suala zima la kujivua gamba. Wameona chenge hataki kujizuru toka uongozi wa ccm hivyo wameona wamuundie kesi.
Kuhusu suala la kagoda
Hosea anasema watuhumiwa walibanwa wakarusha kitita, bado anataka ushahidi. Ushahidi gani zaidi ya huo?
Eti wenye ushahidi waulete na wakati huohuo eti wahusika wameshakufa!
Walirudisha fedha wakiwa hai hamkuwakamata, wamekufa ndipo mnataka ushahidi!!!!!
 
Hivyo ndivyo anavyoogopa kuwakata wala rushwa wa ccm kuogopa wataandamana pia, we huoni kashindwa kuwakata, mapacha watatu, Jairo, Kamati ya madini bungeni, na wengi wa namna hiyo. Kwanza yeye mwenyewe mna rushwa, nafikri taasisi inayoongoza kwa rushwa namba 2 ni Takukuru, ya kwanza ni police (trafic). Na kama ameamu kusema hadharani kwamba ALISHINDWA KUWAKAMATA ina maana ameshindwa kazi, sijui kwanini JK hajamwajibisha hadi sasa! au ndo mambo ya USWAHIBA HAYA MHESHIMIWA MSIKIVU JK !!!!!!!!!!!
 
sasa na wewe kinachokushangaza hapo ni nini? ulitegemea aseme nini? kama sio chadema angewezaje kusema ccm wametoa rushwa na wakati yeye ameteuliwa na rais mwenyekiti wa ccm kuwa hiyo nafasi aliyonayo unataka akale wapi? police? hakuna hosea bila ccm hakuna ccm bila hosea.

Pia hosea ni janga la taifa kama yalivyo majanga mengine..ukimwi, umeme, wizi, ufisadi kibaya zaidi bado anaendelea kumsafisha chenge..mimi naona hapa si bure itakuwa na yeye anamaslahi kwenye ishu ya rada..hivi nani anaweza kumchunguza hosea? Au nguvu ya umma tufanye kazi yetu?i yetu?
 
This individual should be investigated for the role he played in the Valambhia case, which is to date considered the longest running, the most epic, the most expensive legal case in the history of Tanzania. He was the AG from 1995-2005, in all those years he dragged Mr. Valambhia to court, in fact to three courts. The Valambhia case was at one time in all the three courts of Dar es Salaam-the High Court, the Court of Appeal & Kisutu court. Even when Mr. Valambhia and his attorney Mr. Maira triumphed over 14 times in the courts, Mr. Valambhia was always dragged back to court. Why was the Judgement from the Court of Appeal, the highest court of the land never obeyed? It is a fact that after winning a final & conclusive Judgement from the COA in March 2003, the AG dragged Mr. Valambhia back to court on september 2003 on an issue that was res judicata. Why? Did he have no respect for the rule of law, for good governance in his own country? In fact, its almost absurd to read that the TZ gvt. is "demanding" their compensation money from Bae as directed by a British Judge-why is the TZ gvt. so eager that the British gvt. follow the rule of law when some officials of the TZ gvt. blatantly have ignored the rule of law in matters concerning their own courts? In the Valambhia matter, in 1992 when Mr. Valambhia's decree was sitting on the desk of every TZ gvt. official & when the case was subjudice still his money was released to his partner through drafting of what is called an "instrument". This act was wrong, as the case was still subjudice and one partner had won his entitlement, the money belonged to the company. Who is responsible in the tZ gvt. to draft legal documents? The Valambhia case was a civil suit between two business partners and when the gvt. intervened one case gave birth to 14 cases. Mr. Valambhia died in complete financial destitution. He was in the courts every single day of his life. When he was crying out in the newspapers articles during those days, that a daylite robbery was taking place in broad daylite. It was and continues to be the truth today. The case is still in the courts after the death of Mr. Valambhia, and in fact, it is a "personal" project of the mighty few, to keep the Valambhia case in courts keeps billing and invoicing to the BoT flowing consistently. There is a report conducted by an independent person on this matter, it was commissioned by the BoT, the report is the "Maregesi" report. AND there is an excellent investigative article on this matter written by Richard Mgamba of the Guardian newspaper, dated June 2009, titled " The most expensive legal suit in Dar's history". Its not available online, the link doesn't work, its suppressed by the gvt. But its available in the archives of the Guardian newspaper. There is another excellent article also, dated oct 28-nov.3, 2003, titled "Chenge faces imprisonment, says counsel" by Timothy Kahoho which appeared in the Family Mirror. Also, an article titled "Dar Officials 'Abetting Money Laundering'" by Faustine Rwambali which appeared in the East African. Please note that this case has cost the country more than the decretal amount. & Prominent lawyers from the BoT have been paid near the decretal amount. The accounting method that is used for billing and invoicing of this case for the BoT lawyers fees in very interesting. Suffice it to conclude that to deny Mr. Valambhia Justice by manufacturing cases against him was to the "benefit" of certain individuals. As stated in the Richard Mgamba article that the Valambhia case which is still languishing in the High Court today is a "personal" project of the mighty few. It has nothing to do with the law. There is no case, its just "fiction" being created so that money flows out of the BoT-billing/invoicing. The case was decided in the final/conclusive COA Judgement & yet the AG of that time 2003 did not obey a Judgement from the Highest court of the land, the COA.
Ibuntu, I this Valambia case deserves its own thread haswa ukizingatia 1.Valambia mwenyewe katangulia mbele ya haki bila kutendewa haki.2.Wakili wake Maira naye katangulia bila kuvuna mavuno ya jasho lake.3.Bot wameuza ng'ombe kwa kesi us kuku kwa kumlipa wakili wake Mkono a fortune kisha kumtosa na kumchukua wakili Wa EPA Dr.Ringo Tenga kuendeleza ulaji mpaka kesho. Etc.
 
lazima tuwe tunareason...Hosea kateleza kwa kuvunja sheria anazozisimamia lakini kiutendaji walichofanya ndio kilpaswa kufanyika. kiongozi bora ni yule anayeweza kuelewa afanya maamuzi gani, kwa nani , na wakati gani... under no way lolote litakalo fanyika against Chadema lazima hisia za uonevu zitaamushwa... wanacha tumekuwa nao hofu ya kuonewa.. pia kipindi cha uchaguzi asingeweza kuwakamata.. siasa zetu Chaedma ni vurugu hilo hatupingi
 
Chenge ni msukuma,Hosea ni msukuma, DPP Feleshi ni msukuma na DCI Manumba ni msukuma. Hapo lazima yatapelekwa mashitaka dhaifu ili hatimaye mahakama imsafishe mzee wa vijisenti. Hiyo ni karata tatu.

This is a very important observation.
Lazima Chenge ashinde tu!!!!!!!!!!!!!!!!!. Unajua inategemea umepeleka counts zipi mahakamani. Ukipeleka legelege atashinda tu. watanzania subiri mtaona namna charge zitakavyokuwa framed, lazima ziwe dhaifu tu. Bwana tusidanganyane, ukabila upo mkubwa Tanzania, ila tunafunika kombe mwana haramu apite. Hawawezi kumtosa msukuma mwenzao.
 
Chenge ni msukuma,Hosea ni msukuma, DPP Feleshi ni msukuma na DCI Manumba ni msukuma. Hapo lazima yatapelekwa mashitaka dhaifu ili hatimaye mahakama imsafishe mzee wa vijisenti. Hiyo ni karata tatu.
In addition all of them have worked under Chenge and Have a lot of respect ON him as many of Ministry of Justice Leaders. The Name of the game that is now being played is "MAHEPE"
 
chenge21.jpg

Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge

SAKATA la kumiliki dola 1.2 milioni za Kimarekani (zaidi ya Sh1.2bilioni) katika kisiwa cha Jersey, Uingereza, linalomkabili mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, limeingia katika hatua mpya baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kutangaza kukamilisha uchunguzi na kukabidhi jalada kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kwa hatua zaidi za kisheria. Chenge alikutwa na kiasi hicho cha fedha mwaka 2008, kufuatia uchunguzi wa kashfa ya ununuzi wa rada uliofanywa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO).

Chenge ambaye wakati wa ununuzi huo alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) anatuhumiwa kuwa kiungo muhimu katika ununuzi wa rada kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya BAE Systems. Hata hivyo, kufuatia Chenge kukutwa na kiasi hicho kikubwa cha fedha zenye utata ambacho alikiita vijisenti, kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa watu wa kada tofauti nchini wakitaka ashitakiwe, na jana Mkurugenzi wa Takukuru Dk Edward Hoseah, alitangaza hadharani mjini Arusha kwamba mtuhumiwa huyo wa ufisadi atashtakiwa chini ya kifungu cha 27 Sheria ya Takukuru ya mwaka 2007.

Sehemu yakifungu hicho cha sheria, kinaainisha kuwa mtu akiwa na mali ambazo hazilingani na kipato chake alichokipata akiwa madarakani au baada ya kuondoka, ni kosa kisheria. “Mtu ambaye atafanya kosa akiwa au akishikilia madaraka ya umma, kwa kuishi kwa kipato ambacho hakilingani na kipato cha sasa au kile alichopata…Au anayemiliki mali ambazo hazilingani na kipato chake kisheria, atakuwa akitenda kosa.” Kifungu hicho kinaeleza.

Dk Hoseah alifafanua zaidi kwamba, kama DPP atalipitisha jalada hilo la Chenge, mbunge huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote. Kashfa ya kuwa na fedha hizo katika akaunti ya nje, ndiyo ilimwondoa Chenge katika wadhifa wa Uwaziri wa Miundombinu mwaka 2008, baada ya gazeti la Guardian la Uingereza kufichua kuwa Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali wa zamani, alikuwa akimiliki kiasi hicho cha fedha. Hata hivyo, alipoulizwa na waandishi Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere baada ya kuachana na msafara wa Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa akitoka naye ziarani nchini China, Chenge alikiri kumiliki akiba hiyo ya fedha, lakini akiziita ni vijisenti, jambo ambalo liliwashangaza watu wengi nchini na kuibua hasira zaidi.

Lakini, Dk Hoseah akifafanua zaidi mchakato huo mzito wa kisheria, alisema ni Watanzania wachache mno wanaoweza kuwa na akiba ya fedha kiasi kama hicho nje ya nchi au mahali kokote, jambo ambalo aliongeza kuwa ndilo lililowasukuma kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo za Chenge.

Asisitiza hana kesi ya rada
Kuhusu kuhusika kwa Chenge katika kashfa ya rada baada ya Mahakama Kuu Uingereza kuamuru BAE Systems kurejesha sehemu ya fedha kwa Tanzania kutokana na kubaini upotevu wa nyaraka muhimu za manunuzi halali, Dk Hoseah, alisema, mbunge huyo hahusiki na kwamba hakuna ushahidi wowote wa kumtia hatiani.

Kwa mujibu wa Dk Hoseah, waliohusika na kashfa hiyo tayari wameshatajwa na hata washiriki wao wanajulikana wakiwamo raia wa Uingereza. “Nashangaa kuona Watanzania wakishikilia kuwa Chenge ashtakiwe kwa kitu ambacho hakina ushahidi, lakini wanasahau kuwaeleza Waingereza kuwa ndio wahusika,” alifafanua Dk Hoseah, akirejea mchakato wa kesi hiyo ambayo Chenge alikuwa akiwakilishwa na mwanasheria wake wa Kimarekani, JJ Madorsky. “Ingekuwa sio kweli, Waingereza hawangekaa kimya, wangesema,” alisema Dk Hoseah.

Kuhusu Kagoda
Akizungumzia kashfa nyingine inayotikisa Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited inayodaiwa kuchota Sh 40 bilioni kutoka Akaunti ya Madeni Nje (EPA) katika Benki Kuu Tanzania (BoT), alisema taasisi yake imeanzisha upya uchunguzi, licha ya kamati ya Rais Kikwete, kuwabana wahusika wakarudisha kitita hicho.

Dk Hoseah alisema kwa kutambua hilo, ndiyo maana amewaomba Watanzania wote wenye ushahidi wauwasilishe ofisini kwake ili kuwezesha kuendelea kwa mchakato huo wa kuwafikisha mahakamani wahusika wote. Mkuuu huyo wa Takukuru, alisema kwa sasa kumbukumbu katika jalada la usajili wa kampuni hiyo kwa Msajili wa Makampuni (Brela), zinaonyesha wamiliki wake wote wawili ni marehemu.

Kesi ya Mwakalebela
Wakati huo huo, Dk Hoseah amebainisha kwamba taasisi yake imekamilisha marekebisho ya mashtaka katika kesi inayomhusu, aliyewa katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela. Alisema Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Iringa ilikataa mashtaka ya awali ya Takukuru dhidi ya Mwakalebela kwa maelezo kuwa yafunguliwe kwa kutumia sheria mbili tofauti ambazo ni ile ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na ile ya Takukuru ya mwaka 2007.

Dk Hoseah alisema; “Tumekamilisha marekebisho ya mashtaka dhidi ya Mwakalebela na tumeyafikisha mahakamani, ingawa tunasikia kuwa naye amefungua kesi Mahakama Kuu, tunasubiri, lakini kesi yake isingeweza kumalizika bila ya kusikilizwa.”Aliongeza kesi hiyo inafanya idadi ya kesi zote za Uchaguzi Mkuu uliopita kufikia 18 hadi sasa na kwamba zote zitashughulikiwa na taasisi yake.

Kesi hiyo dhidi ya Chenge inatarajiwa kuwa moja ya kati ya kesi nzito nchini, kutokana na nafasi yake ya uongozi kama Mwanasheria Mkuu.

Mwananchi

Huu wote ni usanii tu. Mbona hoseah anababaikababaika. Hivi ulivyokuwa unamsafisha hukujua kuwa alikuwa na hela ambazo hawezi kuwa na maelezo amezipataje?? Mbona mnatufanya hatuna akili. Kazi imekushinda upo ulipo kwa ajili ya kulinda viongozi wako mafisadi. Wewe mwenyewe ni fisadi mzuri tu na rushwa kama kazi. Any way, we don't expect anything positive from chenge's saga and the other mafisadis as long as you hoseah hold that office. Only God will know your fate.
 
Back
Top Bottom