Hosea ondoka kabla ya fedheha!

Mkukuti

Member
Feb 8, 2008
20
3
Hosea mchezo unaotaka kuucheza ni wa hatari kubwa na gharama yake hatuko tayari kuibeba. Ulilikoroga kwa kuwasafisha Richmond, ni jukumu lako kuwajibika!. Kuwasakama wapinga ufisadi ili ionekane wanalipiza kisasi watakapochadili mapendekezo ya serikali juu ya utekelezaji wa maazimio ya bunge, ni utoto ambao utatugharimu sote, sio tu hatuko tayari kubeba gharama ya utoto wako, lakini tunapaza sauti kwa kiwango cha juu...Jiuzulu, Jiuzulu Jiuzulu, kabla Bunge halijajadili upuuzi wa taasisi yako kuwasafisha wezi.
 
Edward Hoseah ateuliwa mjumbe UNDP

Na Mwandishi Wetu;
Tarehe: 30th October 2009

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, ameteuliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kuanzia mwaka jana hadi 2011.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Takukuru kwa vyombo vya habari, uteuzi wa Mkurugenzi huyo ni kwa mujibu wa barua ya shirika hilo ya Oktoba 9 mwaka huu iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Geraldine Fraser-Moleketi.

Taarifa hiyo ilisema Bodi hiyo inahusika na masuala ya utawala bora na rushwa chini ya Mpango wa Maendeleo wa Kimataifa wa UNDP.

Pia taarifa hiyo ilisema majukumu ya wajumbe wa Bodi hiyo ni kutoa na kupokea michango ya mataifa mbalimbali, kuimarisha ushirikiano na uhusiano mzuri kati yao na kufuatilia utekelezaji wa mikakati ya utawala bora katika nchi wanachama.

Tanzania ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa ambaye anafaidika na mipango ya UNDP ambapo Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa (NACSAP) ni moja ya miradi inayofadhiliwa na shirika hilo.

big paradox of our times!
 
Back
Top Bottom