Hosea na PHD yake

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dk. Edward Hosea, ametunikiwa shahada ya juu ya udaktari (PhD) katika fani ya sheria.


Asalaam Aleykum waungwana.
Nadhani pamoja na uhuru wa kusema, bado sheria in nafasi yake katika kulidanganya Taifa. Ni dhahiri watu wengi hujenga hoja ikiwa kuna mtu anatajataja tu madarasa pasipo ukweli, hasa ikiwa mtu huyo ana dhamana ya Taifa letu!!

Nimeshawishika kuandika ili kama kuna mtu mwenye uhakika na matamshi yake ya awali, basi abainishe watu tuingie kazini!! kwani hata nukuu ya hapo juu, inakwepa kueleza lolote husika la historia yake kuhusu PhD.

Inshallah tutadanganywa mno!! ikiwa hatuamki ati!!
 
drax:
Mbona unatuweka kwenye mduara?

....."bado sheria ina nafasi yake katika kulidanganya Taifa?"

...."umeshawishika kuandika ili kama kuna mtu mwenye uhakika na matamshi (yake? nani? Mkurugenzi?)

....ni ipi historia yake kuhusu Ph.D.?

Kama unayo mambo ya uhakika kuhusu jambo hili ni kwa vipi usitumwagie tu hapa tuzidi kulichambua?
 
Aise watu kama wewe wamekua adimu sana katika kufichua hawa wenye vyeti bandia.. Tumwagie data mzee utufumbue macho,, Na kuna PhD nyingi sana za wakubwa na wenye madaraka serikalini zimekua zitajwa kuwa na uwalakini,, so naunga mkono mzee kwamba......................Tupe details......One!
 
Sijawai kusikia PhD ya three years, never in my life. I believe this guy was part-time. I don't care amefanya thesis au paper base. There is no way ukasoma PhD ndani ya miaka 3.

...mkuu inawezehana na nimeona watu ninaowafahmu kwa karibu sana tena vyuo vya maana sana sio vya ubabaishaji....ila ni kazi kweli kweli.
 
Mkuu Mtanganyika

Nilijaribu kuulizia suala lako nimepata taarifa kuwa kwa sheria za sasa za UDSM PhD ni miaka mitatu. Ukizidisha unaomba extension.

Vile vile kati ya watu 15 waliomaliza juzi nasikia kulikuwa na wahitimu kama wanne wameweza kumaliza kwa muda huo. Sikuweza kupata majina yao.

Hila suala pia ambalo sikupata ufafanuzi ni kuwa mweshimiwa Dr. Hosea alikuwa kwenye atachment-addendum- sikuelewa hili lilikuwa na maana gani?

Kakindomaster,
Asante Mkuu kwa taarifa.

Kama UDSM wanafanya miaka mitatu basi hapo safi. Nijuavyo mimi
huku nje pia kikawaida wanatoa sponsorship miaka mitatu lakini sehemu kubwa ni kwa ajili ya kuhakikisha wale ambao hawafanyi kitu baada ya miaka mitatu wanakatiwa scholarship. Baada ya hapo huombwa extension na wengi wanamaliza kati ya miaka minne na sita.

Kalamu, usishangae ya Musa, utaona ya Firauni, wapo mkuu wanaosoma miaka mingi sana. Tena ukiwakuta kazini vitu wanaviona ipasavyo. Kuna factors nyingi zinaweza kuchangia. Nitakutafutia mifano kama nitaipata online.
 
Nimejitahidi kusoma thread zote ili nigundue tatizo liko wapi mpaka watu wanaanza mjadala kuhusu PHD ya miaka mitatu au kusoma full time na part time!! Labda nianze kwa kutoa mwangaza PHD ni nini kwa lugha nyepesi.

PHD ni masomo ya udaktari wa falsafa katika fani ambayo tayari unaijua kwa undani ila unataka kufanya utafiti ili kuletea ujuzi mpya wa kuelewa kwa ukaribu na kwa undani matatizo mbalimbali yanayoisumbua hiyo kategoria uliyosomea. Mara nyingi katika PHD watu wanaongeza maarifa mapya!!

Baada ya kusema haya naomba nitamke kuwa kumaliza PHD kwa miaka 3ni standard procedure ya vyuo vingi duniani (ukipenda soma prospectus ziko mtandaoni). Mtu yeyote ambaye hatamaliza ndani ya muda anaweza kuomba kuongezewa muda!!

mara nyingi hii hutokea pale ambapo wataalamu wenzako waliobobea wanaokusimamia wanapohisi huo utafiti wako siyo kitu kipya na tayari kinajulikana!!

Cha muhimu kuelewa ni kwamba huo utafiti mpya ni lazima uwe mpya kiasi kwamba hata huyo msimamizi wako (ambaye ni expert katika hilo somo) anakuwa haujui kwa undani kwa hiyo unachofanya ni kumkonvince!!

PHD ni research based kwa hiyo haifanywi kwa kusoma darasani. Kwa hiyo mtu anapokuwa full time haina maana anahudhuria darasani bali ina maana anakuwa chuoni akifanya research katika maktaba, kusoma vitabu na article mbalimbali na kutafsiri utafiti uliopatikana katika field!!

Sasa turudi kwa hosea. Kwake kufanya PHD kuhusu rushwa ni kazi rahisi mno hata kama ni part time. Amefanya kwenye field anayoielewa na ambayo amekuwa akiifanyia kazi kama mkuu kwa muda mrefu. Kama ni data za utafiti atakuwa nazo za kutosha tena nyingine ni za siri ambazo mtu wa kawaida ambaye hayupo PCCB hatoweza kuzipata!!

Mimi naamini kama chuo kikuu wangekubali angemaliza kabla ya miaka hata mitatu!!

Siwezi kusema kwa hakika kama hosea alianza PHD yake marekani ila ninavyojua mwaka 2005 alikuwa UDSM akisoma huku akifundisha.

Nakumbuka wakati mimi naenda kufundisha wanafunzi wangu nilikuwa nakutana naye pale lecture rooms za yombo akiwafundisha wanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria (akiwamo Ridhwani Kikwete).

Kuhusu kutoa machapisho nafikiri huko ni kuongelea swala la kuwa professor. Maana hapo ndio utatakiwa kuwa na machapisho. Ila sidhani kama kwa hosea hilo litakuwa taabu maana ametoa lectures na paper za kutosha kuhusu mapambano ya rushwa nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 10.

Natumaini nimetoa mwangaza wa kuwezesha wana JF kufanya mjadala wenye afya tukiwa na ufahamu wa kutosha.

Naomba kuwakilisha!!!!!!
 
Kalamu, usishangae ya Musa, utaona ya Firauni, wapo mkuu wanaosoma miaka mingi sana. Tena ukiwakuta kazini vitu wanaviona ipasavyo. Kuna factors nyingi zinaweza kuchangia. Nitakutafutia mifano kama nitaipata online.

PhD watu wengine nasikia walisoma miaka kumi na ushehe.

Pia nasikia hata UDSM kuna wanafunzi professionals ktk PhD ambao wana miaka saba/nane na bado hawajui lini watamaliza.

Hata USA nafikiri wapo(kuna watu nasikia kila wakati wanasoma PhD miaka inapiata) hata ujerumani nilikuwa na rafiki yangu mmoja alikula miaka kama sita PhD mpaka akakata tamaa hila mwisho alipata.
 
Hata mimi ningependa kuona Defence yake kabla ya kupata hiyo PhD, maana kama ame-research kuhusu Rushwa ya Tanzania halafu madudu anayofanya kwenye ile ofisi mimi kama ndio Profesa kwenye kamati lazima ningempiga chini.
 
....huyu nahisi alikuwa na majeshi hawezi kumaliza Phd na stress zote za bongo....namkumbuka Sumaye ambaye masters yake nina wasiwasi nayo mno...itakuwa tu backup kwa kwenda mbele...ni mtazamo tu!!
 
Research topic yake kama wadau wengine walivyoonyesha ilikuwa within his sphere of operation. Nina hakika surbodinates wake aliwapa kigwaride cha kutosha kama anahitaji information fulani au data on the topic. Kabla ya kumpongeza je tunaweza kupata angalau abstract ya hiyo ropic yake?
 
Back
Top Bottom