Hosea na PHD yake

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
678
Hivi Hosea si alisema Ph.D yake alifanyia USA? Au aliacha kule na kuja kuanza upya UDSM.

Maelezo aliyoyatoa kwenye tuhuma zake huenda yana utata.

Jamaa ana Ph.D ya rushwa TZ na bado mambo ya rushwa yanamgonga, hapo tatizo sio elimu, tatizo ni watu wenyewe waliopewa hayo majukumu.

Hosea atunukiwa PhD

2007-11-25 12:38:28
Na Godfrey Monyo

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dk. Edward Hosea, ametunikiwa shahada ya juu ya udaktari (PhD) katika fani ya sheria.

Alifanya utafiti kwenye eneo hilo la mapambano dhidi ya rushwa nchini Tanzania: Nguvu ya ushahidi wa mazingira.

Dk. Hosea ni miongoni mwa wanachuo 3,739 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, waliotunukiwa shahada mbalimbali na Mkuu wa Chuo Balozi Flugence Kazaura,katika mahafali ya 37 yaliyofanyika jana chuoni hapo. Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wanawake waliohitimu walikuwa 1,376.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutunukiwa shahada hiyo Mkurugenzi wa TAKUKURU alisema elimu aliyopata itamuongezea kiwango cha ujuzi na maarifa katika utendaji kazi.

Alisema pamoja na kupanua uelewa amekuwa na zana kamilifu za kitaaluma za kupambanua mambo na kufanya kazi kwa viwango vya juu kiufanisi na kwa umahiri.

``Nashukuru kupata shahada lengo langu ni kuwatumikia wananchi kikamilifu. Lakini pia hatua hii iwe changamoto kuwa kusoma hakuna mwisho unaweza kujiendeleza hata ukiwa kazini� tusichoke kusoma,`` alisema Dk. Hosea aliyechukua miaka mitatu kukamilisha PhD yake.

Alipata shahada ya kwanza ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ya pili aliichukulia nchini Canada.

Katika shehere hiyo ya mahafali Chuo Kikuu kilitangaza mkakati wa kuboresha elimu pamoja na shughuli zinazoendeshwa na taasisi hiyo ya elimu ya juu kwa kuunda kitengo maalumu cha kuhakiki na kudumisha viwango vya ubora.

Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Rwekaza Mukandala, alisema katika hotuba yake kuwa kitengo hicho kitakachoanzishwa hivi karibuni kitadumisha viwango vya ubora katika kufundisha, kutafiti na kutoa huduma za kijamii.

``Moja ya majukumu muhimu ya kitengo ni kuhakikisha kuwa viwango vya elimu vinaboreshwa, ufundishaji unaangalia upya namna ya kuboresha programu zao mara kwa mara ili zilingane na viwango na taratibu zinazokubalika kimataifa,``alisema Makamu Mkuu wa Chuo.

Aliwaambia wahitimu na wageni mbalimbali kuwa lengo kuu la kuangalia upya progamu hizo mara kwa mara ni kuhakiki, kuboresha na kudumisha ubora wa progamu zinazofundishwa.

``Kitengo hiki kitafanya kazi bega kwa bega na wakuu wa vitivo na idara ili kuiwezesha menejimenti ya chuo kuwa na taarifa wakati wote juu ya changamoto zinazokabili ubora wa utendaji kazi kila zinapotokea ili kuchukua hatua za haraka kukabiliana nazo,\"alisema Profesa Mukandala.

Profesa Mukandala alisema Baraza la chuo hicho limeidhinisha sera mpya ya uhakiki wa ubora kwa ajili ya chuo kikuu, sera ambayo iko mbioni kutumika.

Katika tukio hilo, Makamu Mkuu wa Chuo alimtangaza Profesa Pius Yanda kuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel.

Alisema: ``Mwaka huu mmoja wetu Profesa Yanda alishiriki katika paneli juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani ambapo yeye na wenzake akiwemo Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Bw. Al-Gore wamepata Tuzo ya Nobel,``alisema Profesa Mukandala na kumpongeza kwa dhati kwa ushindi huo ulioipa heshima Tanzania.

Alizungumzia suala la udahili na kuongeza kuwa nia si kupunguza idadi ya udahili bali pia kuweka mikakati ya maendeleo ya muda mrefu.

``Mkakati huu utajumuisha kuongeza kasi ya upanuzi wa udahili katika baadhi ya programu za mafunzo na katika viwango fulani na wakati huo huo kuongeza au kupunguza idadi ya wanafunzi katika fani nyingine, `` alisema.

Alisema mjadala wa namna ya kupunguza wanafunzi katika fani fulani na kutekeleza mkakati huo yanaendelea.

Akizungumza uhaba wa walimu na jitihada za kuongeza wanataaluma wa kufundisha sekondari na shule za msingi Profesa Mukandala alisema Chuo Kikuu kitatoa kipaumbele katika programu ya shahada ya kwanza kwa kupanua udahili katika fani ya elimu na kuboresha programu nyingine zinazofungamana na ualimu.

``Pia tunahitaji kuzipa umuhimu fani za sayansi, teknolojia na biashara kutokana na umuhimu wake katika maendeleo ya nchi na uhitaji wa taaluma hizo katika soko la ajira.``

SOURCE: Nipashe
 
Nampongeza kwa dhati, na hasa eneo ambalo alifanyia utafiti....tatizo ni kwa jinsi gani ametumia hiyo elimu yake kuboresha mapambano dhidi ya rushwa ikitiliwa maanani tuhuma zilizowahi kurushwa hapa JF?

Kingine pia kama ameweza kuimaliza hiyo PhD kwa miaka 3 tu UDSM...nahisi kuwa ana 'kichwa' si cha kitoto...alikuwa full time ama part time? mechapisha kwenye majarida gani?

Ishu nyingine ni kwua inakuwaje waalimu waliopo hapo hapo baadhi yao nasikia wanapata PhD baada ya hata miaka 6, binafsi nimeshuhudia aliyepata PhD baada ya miaka kama 9 hivi ya utafiti....ama kweli tunatofautiana kiuwezo
 
Hata mimi hiyo Ph.D ya miaka mitatu huku akiwa anaendelea na kazi
full time naona hapo labda jamaa ni kichwa saaaanaaaaa au la kulikuwa na aina ya kubebwa.

Kuna sehemu nilisoma alikuwa anasoma Ph.D Marekani kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi, labda mambo mengi alifanya akiwa USA na kaja kumalizia tu mlimani.

All in all kwa kuwa na Ph.D ya mlimani kwenye masuala ya sheria na rushwa ni ishara tosha kwamba kabobea kwenye hayo maeneo. Sasa ni wakati wa kudeliver maana hana visingizio vyovyote vya kushindwa kupambana na rushwa ambayo kaisomea vizuri.
 
Nami nampongeza kwa kupata PhD nyumbani- ni funzo kwa wataalamu wetu saa ingine wasikimbilie kusoma PhD nje-(maana hupotelea huko huko saa ingine) kama kuna nafasi na capacity nzuri ya supervision hapa nyumbani -basi wasome hapa hapa! Na serikali iweke kipaumbele na kutenga pesa kuwajenga uwezo wa vyuo vyetu kutoa PhD nyingi! Sina data- kuna ntu anajua tangu UD, MU na SUA kuna PhD wametoa? Kwani kati ya wanafunzi wote, ni wangapi wanakua waliomaliza ni PhDs?

Again, hongera sana Dr. Hosea!
 
103005hoseadg4.jpg

The Chancellor of the University of Dar es Salaam, Ambassador Fulgence Kazaura, bestows on Edward Gamaya Hoseah a Ph.D. in Law degree yesterday at a graduation ceremony held at the Hill.(Photo: Omar Fungo)

Picha kwa hisani ya IPP media
 
NakuliliaTanzania:

Ph.D. baada ya miaka 9? Kwa misingi ipi?
Tafadhali angalia vizuri kumbukumbu zako; hili linatia utata hapa. Kwani sidhani kuwa Chuo Kikuu wanaoutaratibu wa muda mrefu namna hiyo wa kumaliza masomo ya aina hiyo. Itakuwa ni tofauti sana na taratibu za vyuo vingi duniani. Mwenye habari na hili atupatie ukweli.

Inavyoelekea, huyu Hosea kahamisha baadhi ya mambo aliyokuwa ameyakamilisha kule Marekani kabla ya kuitwa nyumbani ndio maana muda ukawa mfupi kiasi hicho, na hasa ukiwekea maanani kwamba alisoma huku akifanya kazi; isingekuwa rahisi hivyo.
 
Kwani tukimpongeza tu yakaisha itakuwaje??

yaani kila kitu tunahoji (negatively), akikosea MADONGO akifanya jambo zuri TUNAMTAFUTIA SABABU za kumpiga MADONGO!!!

Mzee amefanya kitu mfano, kwa hili tumpongeze ili anapoboronga tuwe watu wa hekima na ukweli!!!

Tuache kugeuza JF kijiwe cha FITNA na MAJUNGU!!!!
 
Bokassa,

Labda utuambie kwenye posts za hapo juu Majungu na Fitina yako wapi?

Uchambuzi ni kuichambua habari kama ilivyo, kupongezana au kushutumiwa ni yatokanayo na wala wala sio mwanzo wa uchambuzi.
 
Hata mimi hiyo Ph.D ya miaka mitatu huku akiwa anaendelea na kazi full time naona hapo labda jamaa ni kichwa saaaanaaaaa au la kulikuwa na aina ya kubebwa

Ungetoa hiyo nyekundu tu mzee!! Kwa mtu mwenye busara ya kawaida kijani ingetosha kaka!!
 
Ungetoa hiyo nyekundu tu mzee!! Kwa mtu mwenye busara ya kawaida kijani ingetosha kaka!!

Bokassa,

Nafikiri umeshindwa kuelewa maana ya hii thread kuwa kwenye siasa. Kama ingelikuwa na maana mtu ku graduate wala isingelikuwa hapa. Ingeweza kuwekwa sehemu nyingine na watu wakatoa pongezi wawezavyo. Hapa ilipo ni kwasababu ya cheo chake na Ph.D aliyochukua, hivyo kustahili kuchambuliwa kwa wale wanaotaka

Wewe huoni mtu anayefanya kazi full time na kumaliza Ph.D kwa miaka mitatu hapo kunaweza kuwa issue au mhusika anaweza kuwa na uwezo mkubwa sana?

Pamoja na hayo yote sidhani kama unaweza kusema hizo comments ni FITINA au MAJUNGU unless kama hujui maana haya maneno.

Kulingana na comments za wengine sasa naamini wala Hosea hajasoma hiyo Ph.D miaka mitatu na badala yake huenda sehemu alifanya akiwa USA. Lakini kama kweli kafanya miaka mitatu, tena UDSM basi anastahili sifa kubwa sana.
 
NakuliliaTanzania:

Ph.D. baada ya miaka 9? Kwa misingi ipi?
Tafadhali angalia vizuri kumbukumbu zako; hili linatia utata hapa. Kwani sidhani kuwa Chuo Kikuu wanaoutaratibu wa muda mrefu namna hiyo wa kumaliza masomo ya aina hiyo. Itakuwa ni tofauti sana na taratibu za vyuo vingi duniani. Mwenye habari na hili atupatie ukweli.

Inavyoelekea, huyu Hosea kahamisha baadhi ya mambo aliyokuwa ameyakamilisha kule Marekani kabla ya kuitwa nyumbani ndio maana muda ukawa mfupi kiasi hicho, na hasa ukiwekea maanani kwamba alisoma huku akifanya kazi; isingekuwa rahisi hivyo.

Kalamu, amini usiamini....nasikia kuna kuandika machapisho yakakubalika, au yasikubalike na vingunge kwenye majarida ya kimataifa, na pia kuna suala la kuwa umeanza kufanya juu ya topic flani, baada ya miaka 3 utafiti unagoma, unaambiwa anza upya, nk so hilo suala lipo mkubwa!
 
Bokassa,

Nafikiri umeshindwa kuelewa maana ya hii thread kuwa kwenye siasa. Kama ingelikuwa na maana mtu ku graduate wala isingelikuwa hapa. Ingeweza kuwekwa sehemu nyingine na watu wakatoa pongezi wawezavyo. Hapa ilipo ni kwasababu ya cheo chake na Ph.D aliyochukua, hivyo kustahili kuchambuliwa kwa wale wanaotaka

Wewe huoni mtu anayefanya kazi full time na kumaliza Ph.D kwa miaka mitatu hapo kunaweza kuwa issue au mhusika anaweza kuwa na uwezo mkubwa sana?

Pamoja na hayo yote sidhani kama unaweza kusema hizo comments ni FITINA au MAJUNGU unless kama hujui maana haya maneno.

Kulingana na comments za wengine sasa naamini wala Hosea hajasoma hiyo Ph.D miaka mitatu na badala yake huenda sehemu alifanya akiwa USA. Lakini kama kweli kafanya miaka mitatu, tena UDSM basi anastahili sifa kubwa sana.

Hswaa hivho ndo tunachokisema hapa na wala siona kama kuna mtu anamfitini Dk Hosea....ameshatunukiwa PhD basi yatosha...ila kuwa na shaka na kuhoji upande wa pili ndio maana hasa ya huu mjadala kuwa hapa...hasa kwa wale tunaoelewa maana ya PhD na msoto uliopo kuipata

Hongera sana Dk Hosea!
 
Kalamu, amini usiamini....nasikia kuna kuandika machapisho yakakubalika, au yasikubalike na vingunge kwenye majarida ya kimataifa, na pia kuna suala la kuwa umeanza kufanya juu ya topic flani, baada ya miaka 3 utafiti unagoma, unaambiwa anza upya, nk so hilo suala lipo mkubwa!

NakuliliaTanzania:
Hapana ndugu yangu hayo uliyoyasema ya kufanya miaka mitatu na mpaka utoe machapisho ya majarida ya kimataifa hayapo kabisa; unless hiyo university sijui niite vipi tena, kukuhakikishia kuwa taratibu za vyuo vikuu vyenye hadhi havipishani sana katika mambo ya namna hii. Sio vigumu kufuatilia taratibu hizo na kuzifahamu hata kama hujachukua Ph.D. ya aina yoyote na katika chuo chochote.

Kama chuo kinakuacha hivi hivi unasota miaka mitatu yote bila hata kuwa na habari yoyote nawe, kupitia kwa msimamizi wako au timu maalum ya wasimamizi wako, halafu mara buuu, wanakuvamia eti umekuwa ukifanya utafiti usiotakiwa na uanze upya - hilo halitawezekana kabisa. Kumbuka wewe hukai pale bure, unalipia.
 
Kalamu,

Alichoandika Nakulilia Tanzania kinawezekana ila sio njia ambayo
wanaofanya Ph.D wengi hupitia yaani ni extreme case lakini zipo. Mimi nawafahamu watu wengi tu ambao wamechukua miaka zaidi ya sita kufanya Ph.D zao na pia wale ambao walifika mahali wakadhani karibu wanamaliza, mara mizengwe mingine inajitokeza.

Sijui kwa UDSM lakini kwa chuo nilichosoma mimi (japo mimi sikusoma Ph.D), hata uwe full time bado ilikuwa hakuna uwezekano wa kumaliza Ph.D kwa miaka mitatu maana kuna mchakato wa mambo ambayo lazima uyapitie na kuyamaliza na kwa pamoja ilikuwa haiwezekani kumaliza kwa miaka mitatu. Waliojitahidi sana walikuwa wanatumia miaka minne, average ilikuwa miaka mitano na kuna wengine wengi ilikuwa inakuwa zaidi ya hapo.

Kwa kumbukumbu zangu za UDSM najua kuna mikiki mikiki mingi na ndio maana niliposikia Hosea kamaliza kwa miaka mitatu, nikajua looh! hapa tunaweza kuwa na kichwa kikali hasa, lakini tena nikagundua ilikuwa part time.

Kwa kuangalia kilichojadiliwa hapa, sidhani kama Hosea kasoma miaka mitatu. Nafikiri ni ile ile ya kuongezea chumvi kwenye jambo, huenda ni waandishi wa habari ndio wakakimbilia kuandika bila kutaka ufafanuzi. Lakini pia huenda hata yeye mwenyewe anaona ujiko kusema katumia miaka mitatu wakati anajua ukweli sio hivyo.

All in all kuongoza taasisi ngumu na yenye matatizo kama PCCB na bado kufanikiwa kumaliza Ph.D yake ni mafanikio makubwa sana. Najua sio rahisi kuchanganya shule, kazi na familia kwa pamoja.
 
Sijawai kusikia PhD ya three years, never in my life. I believe this guy was part-time. I don't care amefanya thesis au paper base. There is no way ukasoma PhD ndani ya miaka 3.
 
Mtanzania:
Sijapata kusikia Ph.D. inayofanyika kwa zaidi ya miaka saba (max.) kwa sababu yoyote ile.
 
Sijawai kusikia PhD ya three years, never in my life. I believe this guy was part-time. I don't care amefanya thesis au paper base. There is no way ukasoma PhD ndani ya miaka 3.

Mkuu Mtanganyika

Nilijaribu kuulizia suala lako nimepata taarifa kuwa kwa sheria za sasa za UDSM PhD ni miaka mitatu. Ukizidisha unaomba extension.

Vile vile kati ya watu 15 waliomaliza juzi nasikia kulikuwa na wahitimu kama wanne wameweza kumaliza kwa muda huo. Sikuweza kupata majina yao.

Hila suala pia ambalo sikupata ufafanuzi ni kuwa mweshimiwa Dr. Hosea alikuwa kwenye atachment-addendum- sikuelewa hili lilikuwa na maana gani?
 
Back
Top Bottom