Hongera wanaharakati na wasomi juhudi zenu bado zinahitajika kulinusuru taifa katika

Jan 16, 2007
721
176
HONGERA WANAHARAKATI NA WASOMI JUHUDI ZENU BADO ZINAHITAJIKA KULINUSURU TAIFA KATIKA JANGA WAKATI NI HUUUUU!!!!!.
Ningelipenda nitumie nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa wanaharakati,wasomi na wadau mbalimbali kwa juhudi zao bila ya woga kulinusuru taifa kutoka katika janga.Kwa kutoa ushauri kwa watawala,serikali na chama cha ccm na vyama vya kisiasa na taasisi mbalimbali katika mstakabala na masilahi ya Taifa.Ni wazi ya kwamba katika kipindi kirefu taifa letu limekua likiongozwa kama ilivyo kua ikitakiwa kuongozwa na kusababisha taifa letu kupiga maktaimu na kutosogea hatua yoyoyote na kama ni hatua au maendeleo basi ni kwa watawala na si walalahoi.
Hali hii imesababishwa na mambo kadhaa.kuongoza kwa mazoea bila kufata mishale ya wakati na mabadiliko na watawaliwa wakiendelea kuwaamimini kwa mazoea vilelevile,ubinasi na tamaa ya kijilimbikizia mali na familia zao,ufisadi na kukosa maadili ya uongozi n.k kuyataja machache.Wanaharakati wasomi na wadau wengine haya matendo waliyakemea kwa kuwashauri watawala kwa njia za kirafiki kama rafiki kumshauri kumshauri rafiki,lakini watawala waliyaliwapuuza.Waliendea kuwakilisha ushauri wao kwa njia mbalimbali kwao na mojakwa moja kwa jamiii na kutoa ushauri laikini bado watawala kwa ulevi wa madaraka bado waliendelea kuyapuuza na kutafuna rasilimali za walalahoi!Kitendo hambacho kimetufisha hapa tulipo wakati pengo kati ya watawala na watawaliwa ni kubwa na kusababisha mgawanyiko mkubwa na kuzaa matabaka ya walionacho na wasionacho.Katika hali kama hii vurugu na machafuko hayahepukiki.
Pamoja na jitihada za watawala kwa kutumia fedha na madaraka kuwaziba midomo na kutoa vitisho kwa wanaharakati,wasomi na wadau juhudi zao hazikufanikiwa .JUHUDI za wanaharakati,wasomi na wadau wengine zimeanza kueleweka kwa walalahoi na lugha yao wameanza kuielewa na kuzaa matunda.WANAHARAKATI,WASOMI NA WADAU ZIENDELEZENI JUHUDI HIZI KWA MAKINI NA AMAMANI BILA UMWAGAJI DAMU KUFIKIA UKOMBOZI!UKOMBOZI NA NURU YA UKOMBOZI IKO HATUA MOJA KUTOKA TULIPO.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Wanaharakati tunawategemea pia muda utakapofika wa kuondoa CCM madarakani kwa njia ya maandamano.Ya Misri lazima yatokee kwani ni wind of change
 
Back
Top Bottom