Hongera twiga stars

saitama_kein

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
981
99
Twiga Stars... imefanya mauaji kwa kuifunga Timu ya Eritrea mabao 8-1 katika mchezo uliomalizika jioni hii katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Kila kipindi kiliwapatia Twiga mabao manne
 
Kwa kweli nilijisikia raha sana jana........asante sana kwa kutupa burudani. Nawatakia ushindi mwingi ktk mechi zenu zinazofata.
 
JAmani wadada wanatandaza kabumbu yaani walinifurahisha sana jana. Hongera zenu wadada kwa mabao hayo nane kwa kweli ulikuwa ni ushindi wa kujivunia. Eritria yule mchezaji nambari 13 alikuwa anajitahidi sana angekuwa ana support nzuri nafikiri wao pia wangefanya vizuri kiasi. But Hongera Twiga
 
Dah hongera sana dada zetu,
Hawa wafadhiri waiiangalie hii timu kwa macho yote wamekazana kumwaga pesa kwenye timu ya Maskio Max lakini hatuoni kitu si bora ya hawa ambao wanachangia pesa kiduchu lakini kandanda wanasakata kiukweli wadau waangalie hii timu.
 
BRAVO! Dada zangu wa Twiga Stars. Kweli mmetufanya tujisikie fahari. Nakutuondolea mawazo juu ya timu ya wanaume ambayo ipo njiani kutolewa na Wanyarwanda! Maksimo aige mfano huu wa timu ya dada
 
Back
Top Bottom