Hongera TvT lakini...

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,414
Naam,

Televisheni ya Taifa imemaliza kuuonyesha mchezo ama tamthilia ya "The Long wait". Ama kweli tamthilia hii imetugusa tulio wengi.

Yani imekaa vema sana. Binafsi niliipenda namna ilivyokuwa kwa Red Butterfly ambaye amecheza sehemu mbili akionekana watu wawili tofauti.

TvT hawa hawa ndio walituletea tamthilia ya zamani ambako tuliwaona kina Angelo na Yna wakifanya mambo yao. Ama kweli tamthilia hiyo pia iliigusa jamii.

Kifupi tamthilia hizi mbili zimeiongezea watazamaji TvT kuliko kawaida. Watu tulikuwa tukiona w/end imefika tunanuna huku tukitegeshea ifike J3 tuwaone wale wakali wetu kwenye tamthilia hizi. Shukrani sana TvT kwa tamthilia hizi.

LAKINI


Mmechemka vibaya sana kuleta tamthilia ya "Stolen moments" ambayo nawahakikishia haitaweza kufikia viwango vya tamthilia zilizopita.

Kwanini:
Waigizaji ni walewale ambao tumewazoea, ni heri mngetafuta mbadala mwingine kuliko kufanya makosa kama ya Star Tv. Yasomeni mazingira waandaaji wa vipindi. Ni udhaifu nauona lakini huenda ni mtizamo usio sahihi, sijui wadau mnasemaje?
 
Ukija ITV enzi hizo kuna secreto De amor....kina rehandro na maria clara wanakimbiza mbaya....yani zote zilikuwa konki
 
Huu Uzi uliwekwa 2007

Kipindi icho naugulia matokeo ya kidato cha nne...aiseee
 
Back
Top Bottom