Hongera TANESCO SONGEA lakini SOWASA ................

ligendayika

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,183
198
Napenda kuwapongeza Tanesco songea kwa kuboresha huduma ya umeme mjini hapa kwa kipindi cha miezi minne mfululizo umeme si tatizo tena, hakuna mgao na kama kuna tatizo taarifa hutolewa na huwa kama taarfa ilivyosema. Lakini hawa jamaa wa maji wanajiita Sowasa maji hakuna na taarifa hakuna cha kushangaza bili zipo palepale ilihali maeneo kama ya majengo hakuna maji kwa miezi miwili sasa hakuna maji sasa lakini bili ni zilezile tatizo ni nini?.
 
Hongereni watu wa Songea kwa kupata umeme wa uhakika kwa miezi minne mfululizo. Tahadhari ni kuwa, hayo majenereta yanatumia mafuta na yanatoka mbali, Dsm. Sitaona ajabu ukirudi tena humu jamvini ukitueleza kuwa umeme haupatikani mfululizo kwa ukosefu wa mafuta!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom