Hongera Star tv kwa usawa kuhusu mauaji kata ya Ngado Singida

Dawa ni kuwa na jf tv and redio huo ndio utakuwa muarobani wa habari za uhakika hapa Bongo. Mimi nimeamua kuangalia Citizen ya kenya. Wako juu kuliko kituo chochote ukanda wa Afrika mashariki nikitaka habari na matukio ya nyumbani kwa vile hiyo startv haiko kwenye king'amuzi nazama zangu Jf tu.

Wakuu mimi tangu mdogo mpaka sasa sioni kama Itv inakuwa na kuimprove kwa maana ya utoaji bora wa habari zenye urari na Independent kama jina lao.

Tupigeni jaramba wakuu tuchangie jf tv kulalamika hakutufikishi popote.

mkuu itabidi ununue king'amuz cha TING hbar za stat tv usiwe unazimiss
 
Huu wako ni unazi na uchochezi mtupu, habari imekuwa balanced kwasababu tu imemuonyesha Mwita Mutabe akimtuhumu Mwigulu Chadema kazi mnayo!! Chama Gongo la mboto DSM

habari imekua balanced kwasababu baada ya mwita mutabe kumtuhumu Mwigulu Nchemba muandishi akampigia simu Mwigulu Nchemba kudhibitisha habari hii.
Acheni uoga, waTZ wamesanuka.
 
we jamaa ni kilaza sana
sikila m2 ni mwanachama wa chadema humu? swala ni ku balance na kupata full information ndo wa2 tunacho kitaka! acha uccm! hata siye ni wanachama ila penye upuuzi sema usiogope
 
Majembe ambao wapo star tv + radio free afrika ya ukweli mbaya mimi tangu uchaguzi wa MERU ni star tv tu na radio free afrika
 
Star TV niliwakubali kitambo sanaa, walianza niteka na habari zao za michezo, ziko deep.

Habari za kawaida vile vile ziko kwa kina, unaelewa kabisa chanzo na unaweza kuona au kutabiri mwisho.

Siasa hawaegemei popote iwe Mabwepande, CDM, Sau, CUF, TLP, NCCR etc. Wanasema ukweli kwa kusikiza pande zote na kuchunguza.

Kweli Star brightens my Day.
 
Star TV niliwakubali kitambo sanaa, walianza niteka na habari zao za michezo, ziko deep.

Habari za kawaida vile vile ziko kwa kina, unaelewa kabisa chanzo na unaweza kuona au kutabiri mwisho.

Siasa hawaegemei popote iwe Mabwepande, CDM, Sau, CUF, TLP, NCCR etc. Wanasema ukweli kwa kusikiza pande zote na kuchunguza.

Kweli Star brightens my Day.

Inabidi waendelee na msimamo huo ili watanzania wazidi kuiamini.
 
Leo nimeangalia taarifa ya habari ya chanel 10 na ya ITV lakini vituo hivyo vyote viwili vimetoa habari ya upande mmoja kwa kumuonyesha katibu wa UVCCM akilaani mauaji yaliyotokea bila kuonyesha upande wa pili.

Lakini kituo cha Star tv pekee ndo kimebalance habari kwa kumuonyesha Mwita Mwikabe wa CHADEMA akimtuhumu Mwigulu Nchemba kutuma watu kuja kufanya fujo na pia mwandishi wa star tv alimpigia Mwigulu kuhusu tuhuma zinazomkabili na akazikanusha.

Tunaomba vituo vingine vya runinga kuiga mfano wa star tv kwa kutoa habari zilizokamilika na kuwa na pande mbili sio kutupatia habari zilizo za upande mmoja.Fuateni maadili ya uandishi wa habari sio mnakuwa kama TBCCCM.
Na vituo hivyo ni: Mlimani TV ya jijini Dsm, pamoja na Clouds Tv.
 
Naona ITV wanataka tuwasuse kama TBC-CCM.

Jamani lakini naona ITV afadhali, TBC kwa kweli ni matope. TBC wanaishi kwa kodi ya mtanzania, hivyo wanatakiwa kuripoti habari kwa maslahi ya watanzania wote bila kujali itikadi zao za kisiasa, kidini, ukanda au ukabila. Nchi imebadilika, siyo ya chama kimoja tena, hivyo TBC waondokane na ukiritimba wa chama kimoja, hausaidii nchi yetu. Unabomoa, wasikilizaji na watazamaji wa chombo hiki kikubwa wanazidi kupungua. Ushindani unazidi kuongezeka na yule atakayehimili ni yule ambaye anajiweka (positioning) kuhudumia jamii mtambuka. Huwezi kuwaghilibu tena watanzania wa leo. Watu watapenda kuangalia habari na michanganuo (analysis) inayozingatia ukweli na hali halisi ya nchi yetu.

Upinzani na CCM sasa ngoma droo tena kwa wastani upinzani unapendwa zaidi na watanzania walio wengi. Kuudhalilisha upinzani kwa kuto-kuripoti kihalali mambo yao kunavunja heshima ya vyombo husika. TBC ifanye maamuzi ya haraka na ITV warekebishe kidogo tu watakuwa sawa.

ITV waangalie vipindi vyao vifuatavyo:

1. Dk 45: It has to be real. Yaani mahojiano yawe ya ukweli, kuna a lot of staging currently - yaani inaonyesha kuna maandalizi na uchakachuaji unafanyika kwanza kabla ya kurusha kipindi. Muendasha kipindi awe anasoma na kujielimisha mambo ya ndani kumhusu mgeni na mada husika. Asome habari za sasa (current issues), utafiti kwenye nyanja husika na aulize maswali yanayogusa jamii. Hapo siyo bungeni, unaweza kumpa maswali makuu lakini maswali fuatizi aulizwe na atoe majibu. Kujikanyaga siyo aibu au jambo baya kila wakati, ndiyo uhalisia wa binadamu. Hakuna msikilizaji atakayemwona mtu fulani wa ajabu sana eti tu kwa sababu ameshindwa kujibu swali moja au mawili kati ya ishirini, labda ukishindwa kuanzia matano kati ya ishirini tutahoji, huyu waziri vipi.

2. Malumbano ya hoja: hiki kipindi ni tatizo kubwa. Waendeshaji wako mbele mno kumlinda kiongozi fulani au serikali hadi inakuwa too much waswahili husema. Saa zingine waendeshaji wanatia maneno mdomoni mwa msemaji. Na watanzania hawa walivyo waoga ukiwatisha tu ndo kabisaaaa hawasemi. Tuwaache watu wawe huru. Kuna mzee mmoja huwa wanamwita kipindi cha Pima Joto chini ya mzee Masako, mbona huachwa tu awe huru. Kitu cha kuwasaidia wasemeje wakimsema kiongozi, wawe tu na takwimu au ushahidi. Msiwaingilie sana. Kipindi kisiwe student-ish sana. Ni vizuri kuwafundisha vijana wetu kujenga hoja na kuzitetea kwenye public lakini isiewe tu ni kama debate ya wanafunzi. Audience/wageni msiwaalike kwa kuwachambua, mruhusu tu hata wageni nasibu. Itachangamsha mjadala zaidi.

Huu ni ushauri wa bure kwa dada yangu Joyce Mhaville. Jaribuni kuwa na ulinganifu badala ya kuikingia kifua serikali kana kwamba nyie ni wasemaji wake. Wapeni nafasi watu wa serilika na vyama, wasije wakasema wananyimwa nafasi, lakini hali halisi ya wananchi iwekwe wazi pia. Hakuna tunayemsaidia kwa kujaribu kuwaridhisha viongozi. Wao wamesharidhika tayari, wananchi ndo wenye matatizo tuwape nafasi.
 
Nilikua mpenzi wa itv kwa habari hii itabidi nijikite star tv huenda nilikua napishana na mambo mengi.!

Mkuu mimi nikiwa nyumbani huwa sikosi kuangalia taarifa ya habari ya StarTV. Ni wazuri kuliko TV station zote za TZ hasa kwenye habari za kimataifa na michezo. Kwenye habari za kimataifa wana jamaa mmoja aliyebobea katika uchambuzi wa habari za kimataifa anaitwa Samadu Hassani. Nafikiri huyu jamaa atakuwa na mshahara special ili asitoke hapo.
 
Ninapenda kuaangalia ITV lakini kwa habari hii itabidi niamie star tv maana inawezekana napitwa na mambo mengi kwenye habari.
 
Huu wako ni unazi na uchochezi mtupu, habari imekuwa balanced kwasababu tu imemuonyesha Mwita Mutabe akimtuhumu Mwigulu Chadema kazi mnayo!!

Chama
Gongo la mboto DSM

Ukiachana na ushabiki wa chama chako cha mabwepande, habari iliyobalance ni ipi?
 
Star tv siku za J2 inanipa challenge sana, hasa nikisikia kuna kipindi sijui wanaiita Tuongee siasa, nikijua tu mwongoza kipindi ni Yahya M naamua kwenda ibada ya mchana. Yahya yupo fair sana kwenye kazi yake, halalii upande wowote!
tunataka watangazaji wa aina yake!
 
Last edited by a moderator:
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom