Hongera star tv kwa kipindi hiki cha asubuhi show,lakini wageni hawa.............

ligendayika

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,183
198
Tunapongeza kipindi hiki cha asubuhi kwani kimesheeni habari nzuri na motomoto lakini tatizo ni baadhi ya wageni mnaowaita hapo kweli wanatuharibia hata hamu ya kuendelea kutazama wanakuja na misimamo yao na kutoa amri tu. ilihali kwa mtazamo wangu mnawaita watoe maoni na namna ya kutatua au kusuruhisha baadhi ya mambo na pengine kutoa maelezo fulani . Lakini kuna baadhi ya watu wao ni kutoa amri kuwataka watu au viongozi kuchukua hatua sasa sijui wao nao ni viongozi au Star tv mnawaita ili wawasemee viongozi wetu. Nawasilisha.
 
Mkuu.Angalia isijekuwa labda na wewe umeshindwa kuwaelewa.Bila shaka na wao ni maoni yao tu japo wewe umeyatafsiri kama amri.Jambo la msingi ni kuangalia katika hilo walisemalo lina mashiko?Kama hoja ina mantiki basi acha na iwe amri tu...!
 
Hasa hao wageni wanaokuwa studio ya Mwanza, mimi binafsi hata kama mada ni nzuri napata shida sana kuwaelewa baadhi ya hao wageni!! Kwangu mi Channel ten kwa Kibwana Dachi nawakubali sana.
 
Kipindi cha toungee asubuhi kiko fresh ila kuna siku waliwaalika wazee wawili makada wa magamba waliboa watu wengi sana.
 
Back
Top Bottom