Hongera Pinda na samahani! ulikuwa sahihi!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Anusurika kifo akidhaniwa albino

* Wavuvi waliomvamia wauawa na wananchi
* Mwingine anaswa na mifupa ya binadamu

NA PETER KATULANDA, MWANZA (Uhuru)

MWANAFUNZI wa darasa la kwanza, katika Shule ya Msingi Nyamatongo, wilayani Sengerema, Martha Hussein (10), amejeruhiwa kwa kukatwa panga sehemu ya jicho, baada ya kuvamiwa akidhani albino.

Mbali na hilo, polisi mkoani Mwanza wanamshikilia mwanamke anayetuhuma kukutwa na mifupa inayodhaniwa kuwa ya binadamu.

Martha alivamiwa Machi 12, mwaka huu, saa 12.00 asubuhi, ambapo waliomvamia waliuawa na wananchi.

Tukio hilo lilithibitishwa na serikali ya kijiji cha Nyamatongo na Kaimu Kamanda wa Polisi, Elias Kalinga.

Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Nyamatongo, Lucas Mashinge, alisema Martha alikumbwa na mkasa huo, baada ya watu wawili waliodaiwa kuwa wavuvi kumvamia wakidhani ni albino kutokana na weupe wake.

Alisema wavuvi hao wakiwa na mapanga walimshambulia Martha alipokuwa akielekea shule.

Mashinge alisema Martha aliokolewa na yowe lililopigwa na wenzake wanne aliokuwa ameongozana nao.

"Kelele za wenzake zilifanya watu wajitokeze haraka kwenye eneo la tukio na kuwakimbiza hadi walipowakamata watu hao waliotambulika kuwa wavuvi, wakiwa wamemjeruhi Martha sehemu ya juu na chini ya jicho la kulia," alisema Mashinge.

Alisema Martha si albino, isipokuwa rangi yake inashabihiana nao, hivyo kwa watu wasiomfahamu, hudhani kuwa ni albino.

Mashinge alisema waliouawa na wananchi wametajwa kwa jina moja la Seleman na Method, wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 30 na 32.

Alisema kabla ya kuuawa kwa silaha za jadi, watu hao walipohojiwa na wananchi sababu za kumkamata mtoto huyo, walidai kutokana na rangi yake walidhani ni albino na kwamba, walikuwa wanataka viungo vyake.

Wakati huo huo, Suzana Sengerema (48), mkazi wa kata ya Katunguru, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na vipande vya mifupa inayosadikiwa kuwa ya binadamu.

Suzana alikamatwa Machi 15, mwaka huu saa nne usiku, katika mtaa wa Migombani, baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia mwema.

Taarifa za polisi zilisema baada ya kuhojiwa, Suzana alikiri kuwa mifupa hiyo ni ya binadamu na kwamba huisaga na kuitumia kwa matumizi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuinywa.

Kaimu Kamanda Kalinga alisema mifupa hiyo itapelekwa kwa wataalamu kuthibitisha kama ni ya binadamu au la, kabla ya kumfikisha mahakamani.


My Take:
Niseme nini, hili lawezekana kuwa suluhisho la mauaji ya Albino. I think.
 
Last edited by a moderator:
Huwa naitafakari sana kauli ya "ameuawa na wananchi wenye hasira kali".
Kwakweli kauli hii ina element za UZEMBE ndani yake!Maana in most of the time,baada ya kauli hii kutolewa(hasa na vyombo vya usalama) ujue kuwa hapo ndo suala la uchunguzi wa mauaji haupo tena,kwa kifupi wanakuwa wamejivua jukumu.
 
Ukisoma utaona kuwa jamaa waliwakamata hao jamaa wakawahoji, waliporidhika wakawauwa.
 
Huwa naitafakari sana kauli ya "ameuawa na wananchi wenye hasira kali".
Kwakweli kauli hii ina element za UZEMBE ndani yake!Maana in most of the time,baada ya kauli hii kutolewa(hasa na vyombo vya usalama) ujue kuwa hapo ndo suala la uchunguzi wa mauaji haupo tena,kwa kifupi wanakuwa wamejivua jukumu.

Unategemea nini kutoka kwa wananchi wanao jua kinaga ubaga kwamba sheria zipo ili kuwalinda wahalifu wote na kuwanyanyasa wao?
Siungi mkono jambo hili la kuchukua sheria mkononi, lakini kama ni jambo liwezalo kusaidia jamii ilopotoka kufuata kanuni na taratibu ni bora iwe hivyo.

Siku nyingine utaratibu wa kuchukua sheria mkononi utatumika dhidi ya viongozi wa kitaifa. Siku hiyo itakuwa ndiyo siku ya ukomo wa utawala dharimu na mwanzo wa machafuko makubwa kabla ya heshima kurudi.
 
Siku nyingine utaratibu wa kuchukua sheria mkononi utatumika dhidi ya viongozi wa kitaifa. Siku hiyo itakuwa ndiyo siku ya ukomo wa utawala dharimu na mwanzo wa machafuko makubwa kabla ya heshima kurudi.


we ngoja tu... hata punda hugoma kwenda akibebeshwa sana!
 
Nafikiri wanaanza kutekeleza sasa... sijui tutafika wapi baada ya hili. Yangu macho na masikio..
 
eh ua tu.ndiyo iwe dawa yao.mambo ya haki za binadamu sijui nini ni kuwadekeza tu.Ukiishi kwa upanga ufe kwa upanga vilevile.
 
Unategemea nini kutoka kwa wananchi wanao jua kinaga ubaga kwamba sheria zipo ili kuwalinda wahalifu wote na kuwanyanyasa wao?
Siungi mkono jambo hili la kuchukua sheria mkononi, lakini kama ni jambo liwezalo kusaidia jamii ilopotoka kufuata kanuni na taratibu ni bora iwe hivyo.

Siku nyingine utaratibu wa kuchukua sheria mkononi utatumika dhidi ya viongozi wa kitaifa. Siku hiyo itakuwa ndiyo siku ya ukomo wa utawala dharimu na mwanzo wa machafuko makubwa kabla ya heshima kurudi.

...and that is the best solution when other means are proven to be inefficient as applied to Albino killers and thieves....
 
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

Zamani tulikuwa tunaitana NDUGU; baadaye kukaja Waheshimiwa na Walalahoi, leo hii kila mtu kashika lake.
 
Dah hii ni mbaya sana, yaani jamaa hata ile zawadi waliotangaziwa hawaitaki!!.....haya!....tunaelekea wapi jamani?
 
naingojea kwa hamu sana siku tutakapo pata hasira na kulia na mafisadi na wanasiasa wanaowabeba na kutoa vichwa vyao huku tukiimba kwa shangwe.
 
Nachukua fursa hii kutoa pongezi zangu za dhati kwa wanakijiji wa kijiji cha Nyamatongo kwa kazi nzuri waliofanya ya kuua hawa "wakokozi" waliotaka kuua hako kabinti....way to go 'wanawane'!! Pia natoa changamoto kwa wakulu wa vijiji vingine kuanzia Kome, Buchosa, Bukokwa, Itabangumba, Nyakasungwa, Nyamizeze, Nyamazugo, Isenyi, Nyanzenda, Uzinza, Katunguru na vijiji vyote pembezoni ya ziwa Nyanza mpaka Kamanga, kazi iwe ndio hiyo hili "eneo" letu liwe huru na haya mauaji ya "kipumbavu" ya ndugu zetu albinos!!!

Againi, pongezi chungu nzima..ningekuwa nyumbani Nyakaliro ningewakaribisha chai nyumbani wanakijiji wote wa Nyamatongo, mmenifurahisha sana!!!
Wnahitaji pongezi za dhati........wamenifurahisha wamewakamata....wakawahoji wakakiri kuwa walitaka kumnyofoa binti viungo wakidhani ni albino....

......wananji wakifiria watuhumiwa wanawajua fika kuwa walitenda mauaji wako selo na kesi hakuna kinachoendelea wakaona isiwe taabu...

...nami nawapa pongezi kubwa.....hakika nawaambieni kama ikifanywa mara 2 au 3 hawa wauaji hawatarudia tena....
 
Haaaa, jamani. Nadhani hao wananchi wameamua kutekeleza agizo la Pinda la kutaka wanaoua Albino nao wauwawe papo kwa papo. Sasa lini wananchi watatekeleza pia ushauri wangu kuhusu mafisadi? Tukiwakamata tuwafanye nini hapo kwa hapo? Hebu kumbukeni nilisema nini hapa

Asha
 
hata na yule mkuu wa wilaya ya Bukoba alitembelea shule zilizofelisha, akaona walimu hawajafika hadi saa tatu asubuhi akachukua daftari la mahudhurio, akathibitisha ilikuwa hivyo jana yake na juzi yake, akawaita walimu wale, akawauliza, wakakiri...akawachapa viboko!

Wakamfuta kazi!! kwi kwi kwi!!

My take, toa adhabu kali kwa wakosaji ili mradi usijulikane!!! vinginevyo wapeleke kwenye vyombo husika!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom