Hongera Mzee Aboud Jumbe kutimiza miaka 92 [Happy Birthday]

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Anaitwa Aboud Jumbe. Yeye ni Rais wa zamani wa Zanzibar. Ndiye aliyekuwa Makamu wa Rais Nyerere kwa kipindi kirefu yaani miaka 12 wakati Karume alikuwa makamu kwa mia minane tu.

Aboud Jumbe amezaliwa huko Mkamasini mjini Unguja tarehe June 14, 1920 Hivyo, leo mzee Jumbe anatimiza umri wa miaka 92. HAPPY BIRTHDAY MZEE ABOUD JUMBE.

Ifuatayo ni historia yake fupi kama nilivyoitoa kwenye kitabu hiki: {Zanzibar hadi mwaka 2000: ISBN: 9789987898015, pg. 284-287, by Ali Shaaban Juma}.

******************
Mzee Jumbe alianza elimu ya msingi katika shule ya wavulana ya Mnazi Mmoja mwaka 1930 hadi mwaka 1937 alipomaliza darasa la nane. Akajiunga na Sekondari ya Mnazi Mmoja (Ben Bela) hapo mwaka 1938 hadi 1942 na alifaulu sana katika masomo ya kiingereza, Historia, Kiswahili, Elementary Maths na Geography.

Katika mwaka 1943-1945 alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere huko Uganda kwa masomo ya miaka miwili ya stashahada ya Ualimu Diploma in Education. Baadhi ya wanafunzi aliosoma nao huko Makerere ni Julius Nyerere na Hamza Kibwana Mwapachu.

Mzee Jumbe alirudi Zanzibar na alianza rasmi kazi ya ualimu January 01, 1949. Wakati huo alikuwa mwalimu wa Biology pale Mnazi Mmoja (Ben Bela).

Katika uchaguzi wa mwaka 1957 Jumbe alijiandikisha katika jimbo la Ng'ambo, kituo namba 84 cha Old Shimoni. Katika uchaguzi wa Zanzibar wa Juni 1961 aliwania jimbo la Fuoni na akashinda. Alichaguliwa kuwa Kiongozi wa Upinzani katika Baraza la Kutunga Sheria (kama alivyo Freeman Mbowe sasa hivi) hadi mwaka 1964.

Mara baada ya Mapinduzi ya 1964, Jumbe alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri wa ndani wa Zanzibar na baadaye alikuwa Waziri wa Afya na Ujenzi.

Baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Jumbe alikuwa Waziri wa nchi katika Ofisi ya Makamo wa Rais katika Serikali ya Muungano kuanzia April 1964 hadi 1972.

Kufuatiwa kuuawa kwa Abeid Karume hapo April 7, 1972, Aboud Jumbe aliteuliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Rais wa ASP na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Vyama vya TANU na ASP viliungana February 05, 1977 na kuzaliwa CCM. Ndipo Jumbe akateuliwa kuwa Makamo wa Mwenyekiti wa CCM hadi alipolazimika kujiuzuru nyadhifa zote January 30, 1984.

Baada ya kujiuzuru mambo ya siasa Jumbe aliamua kuhamia nyumbani kwake Mji_Mwema mjini Dar na kujishughulisha na kilimo na kueneza dini ya kiislam. Kufuatia kuanzishwa Chuo Kikuu cha Al-Zahra cha Tunguu Zanzibar, Aboud Jumbe aliteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini wa chuo hicho.

Aboud Jumbe ametunga kitabu kiitwacho: The Partner-ship, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Miaka 30 ya Dhoruba.

******************

Tuifanye Jamii Forum iwavute hata wasioipenda kwa kuwaonyesha kuwa hapa ni kisima cha uelewa na upende usipende ama utakuja au utakopi thread humu na kuzipelekea mtandao wako ambao bila kufanya hivyo haupati watu.


Wiki jana Lawrence Masha Waziri wa zamani wa Mambo ya ndani alitoa hoja kwamba hatuna rekodi ya mambo mengi ya nchi. Akatoa mfano kuwa ukiwa Kenye ukitaka history ya Kenyatta au Moi utaipata. Hapa ukitaka history haupati.

Mwambieni Masha asijenge chuki na mitando kama Jamii Forum aje achungulie tunavyoshuka na history. Tuwaambie na wakubwa kwamba Jamii Forum ndiyo imekuwa ya kwanza kukumbuka birthday ya Jumbe wakati mwenzake Nyerere alipata birthday ya Kitaifa 1997 alipotimiza miaka 75.

Hongera Jumbe kwa kuishi miaka 92. Hongera kwa kuwaona marais wote wa Tanzania na Zanzibar hadi leo.

Mzee Jumbe Tahadari ni kwamba baada ya post hii unaweza kupata simu nyingi. Usishangae maana inaweza kuwa ndiyo kazi ya Jamii Forum, inawezekana kuna wakubwa hata walikuwa hawana hilo wazo lakini kwa vile JF imekusabahi basi sasa na wao wamekumbushwa.

HAPPY BIRTHDAY TOKA KWANGU. HAPPY BIRTHDAY TOKA KWA JAMII FORUM.
 
hongera sana mzee nikupateje kwa makala murua, good work

Baba wa taifa la Zanzibar, aliye hai. Hebu apewe vipindi maalimu, hasa kuhusu Muungano. Atatusaidia huyu mzee mwenye roho nzuri. Happy Birthday Dear Dad.
 
jamani huyu mzee mbona yuko kimya kiasi hiki? long time sijapata kumsikia.
 
Mzanzibari kweli kweli hana hila ndani yake mzee wa watu. Happy birthday
 
Anaitwa Aboud Jumbe. Yeye ni Rais wa zamani wa Zanzibar. Ndiye aliyekuwa Makamu wa Rais Nyerere kwa kipindi kirefu yaani miaka 12 wakati Karume alikuwa makamu kwa mia minane tu...
I see! Kumbe Mwalimu Nyerere alikuwa mzee hivyo-miaka 1975!!
 
jamani huyu mzee mbona yuko kimya kiasi hiki? long time sijapata kumsikia.

Aliambiwa asiongee milele!!! Na Kigamboni ndimo alimolazimishwa kuishi kama Tumtemeke !!! But he is innocent and adorable grandpa. Have many more years to witness the death of Muungano!!! Your dreams will come true!!
 
duh.! Babu hongera sana mimi nilijua mola alishakuchukua.! Kumbe na sisi tuna mandela wetu.!
 
Huyu mzee kwanini anang'ang'ania kukaa kigamboni na hataki kurudi kwao Zenj miaka yote hii?
 
Jumbe hakuna shaka kwamba wewe ni mmoja wa viongozi bora Duniani na ambaye huna shutuma yoyote kwenye nchi yako have a long life father of the nation
 
Huyu mzee kwanini anang'ang'ania kukaa kigamboni na hataki kurudi kwao Zenj miaka yote hii?

Mzee Aboud Jumbe alifungwa kifungo cha kisiasa, hakutakiwa kusafiri nje ya nchi wala kuzungumzia siasa.Na Serikali zote zinazokuja zinaheshimu hukumu hiyo!Hawawezi kumzungumzia kabisa!!
 
Back
Top Bottom