Hongera Mnadhimu LISSU

Mar 1, 2012
29
10
Pendekezo la LISU kuwa kuna haja ya kumchukulia waziri Mkuu hatua na hatimaye likaafikiwa na ZITO kwenye Majumuisho ni zuri linapaswa liungwe mkono na WABUNGE wote wenye MAPENZI mema na NCHI hii bila kutanguliza maslahi ya vyama vyetu.

Najua WAZIRI MKUU SI FISADI ila WASAIDIZI WAKE Lakini kitendo cha yeye kutowawajibisha hakikubaliki hivyo MAWAZIRI WALE WABOVU Waachie ngazi au yeye WAZIRI MKUU abebe dhamana hiyo.

TUMECHOKA KUSIKIA, KUSOMA KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WIZI NA UFISADI SERIKALINI.Viongozi kumbukeni ninyi tumewachagua tukawapa dhamana ya kutuongoza tuongozeni vizuri mkishindwa turudishieni NCHI yetu.

TAMBUENI NINYI NI WATUMISHI WETU NA SISI NI MABOSS MLIKUJA KUOMBA KURA SASA MNAFANYA NINI?Kuondoka kwa NYERERE NA SOKOINE ndo NCHI imekuwa haina mwenyewe?!!!
 
Uwezi kuwa msafi katikati ya wezi. Kama unakubaliana nao kwa matendo yao pia wewe unalamba utamu wa asali.
 
Mh.Lowasa kama ikishindikana either mawaziri wenye kashfa kujiuzuru au waziri mkuu kujiuzuru basi wewe na akina Karamagi lalamikeni kuwa mlionewa. Mbona wengine wanalindwa ninyi mlitupiliwa mbali?
 
Hebu nisaidieni, hivi waziri mkuu anaweza kuchukua hatua gani za kinidhamu dhidi ya waziri yeyote? Maana wote ni wateule wa Rais, na bila shaka Rais ndiye mwenye mamlaka ya kumwondosha waziri. Wasiwasi wangu; adhabu tunayotaka kumpa Pinda pengine si yake.
 
Nina mashaka na wabunge wa ccm kwani wamelivaa vazi la woga na hilo limeshuhudiwa ktk masuala mbalimbali.
Sasa kama wabunge wa magamba ni watanzania kwanza kabla ya kuwa wanaccm basi,waungane na upinzani kuiwajibisha serikali.
Mungu uwabariki wabunge wa chadema na uwape nguvu baadhi ya wabunge wa ccm;WALIO WAZALENDO
 
Ni kweli mkuu na kwa taarifa yako PINDA ANANGUVU HATA YEYE MWENYEWE HAJIJUI TU!
Aauwezo wa kumfukauza kazi mtendaji yeyote mbovu ikiwemo pamoja na mawaziri!
 
Kumbe mkuu hapo hujaelewa! ni hivi kama wabunge wa CCM wangekuwa na big heart ingepigwa kura ya kutokuwa na imani na Rais, kwakuwa kwa asilimia kubwa hawawezi aultenative nyingine inatafutwa kutoa uchafu serikalini
 
Nina mashaka na wabunge wa ccm kwani wamelivaa vazi la woga na hilo limeshuhudiwa ktk masuala mbalimbali.
Sasa kama wabunge wa magamba ni watanzania kwanza kabla ya kuwa wanaccm basi,waungane na upinzani kuiwajibisha serikali.
Mungu uwabariki wabunge wa chadema na uwape nguvu baadhi ya wabunge wa ccm;WALIO WAZALENDO

Laiti wangejua kuwa sasa hakuna haja ya kuogopa kwani ccm sio ya kuogopwa tena. Kama ni mkweli simama ili uhesabiwe, kwani mwisho wa wanafiki na waoga unakaribia. Ukitoka ccm kwa ajili ya kutetea wananchi wal usiwe na woga, wananchi hao watakurudisha mjengoni kupitia CDM
 
In fact aliyelianzisha ni Tundu Lissu, akamalizia Zitto Kabwe baada ya kuona kuwa serekali isingeweza kuwajibika kirahisi. Hoja ya Zitto inalenga utekelezaji. Kimsingi, wabunge hawana mamlaka juu ya mawaziri, lakini wanaweza kumtoa waziri mkuu ambaye ameshindwa kuwajibisha mawaziri wake. Hapa ni kuweka muundo sawa. Nadhani katiba inayokuja italiangalia hilo pia
 
Mh.Lowasa kama ikishindikana either mawaziri wenye kashfa kujiuzuru au waziri mkuu kujiuzuru basi wewe na akina Karamagi lalamikeni kuwa mlionewa. Mbona wengine wanalindwa ninyi mlitupiliwa mbali?
Hivi Lowasa alijiuzuru au alistaafu. wataalam wa kiswahili watujulishe maana kuna mkanganyiko hapo. inawezekana kabisa naye anapokea mafao yote ya uPM mstaafu baada ya kutumikia nchi kifisadi kwa miaka miwili tu kama PM.
 
lowassa alijiuzuru tbccm ndo huwa wanadai alistaafu
 
Hebu nisaidieni, hivi waziri mkuu anaweza kuchukua hatua gani za kinidhamu dhidi ya waziri yeyote? Maana wote ni wateule wa Rais, na bila shaka Rais ndiye mwenye mamlaka ya kumwondosha waziri. Wasiwasi wangu; adhabu tunayotaka kumpa Pinda pengine si yake.

Wazo zuri. Tutalizingatia kwenye katiba mpya. Kwa sasa ni ama yeye au mawaziri wajiwajibishe wenyewe au Rais awawajibishe. Sasa imetosha
 
Hebu nisaidieni, hivi waziri mkuu anaweza kuchukua hatua gani za kinidhamu dhidi ya waziri yeyote? Maana wote ni wateule wa Rais, na bila shaka Rais ndiye mwenye mamlaka ya kumwondosha waziri. Wasiwasi wangu; adhabu tunayotaka kumpa Pinda pengine si yake.

Hukusikia uafafanuzi wa Zitto nini? Katiba haiwapi wabunge nguvu kufukuza Mawaziri:

  1. Either wajiuzulu wenyewe(jambo ambalo hawataki)
  2. Or wabunge wampigie kura ya kutokuwa na imani na PM(Katiba inaruhusu hili) amabayo itasababisha Rais kuvunja baraza
 
Back
Top Bottom