Hongera Mheshimiwa "Rais" Rostam Aziz

Pokea hongera zangu mheshimiwa rais kwa kufanya haya yafuatayo kwa ufanisi mkubwa.

1. Umepigana kufa na kupona na kuhakikisha Dr. Slaa hasikii harufu ya ikulu.
2. Hukulala usiku na mchana hadi ulipohakikisha Jakaya anaingia ikulu.
3. Umetumia kila linalowezekana kuhakikisha Sitta haukwai uspika.
4. Umepandikiza spika wako umpendae mama Makinda.
5. Umetumia hila za ajabu kuua upinzani rasmi bungeni - japo hujafanikiwa sana.
6. Umesaidia rafiki na wapambe wako kushika kamati nyeti za bunge.
7. Unajipanga kumsafishia njia swahiba wako Lowassa agombee 2015.

Kazi uliyofanya ni kubwa, tunakuzawadia kifuta jasho shilingi bilioni 94!
CCM wanavyohaha kuzima soo la RACHEL na kwa kauli ya Mkama nimeanza kuamini kweli RA ni rais.
 
Maneno ya mukama mbele ya waandishi wa habari kuhusu walengwa wa slogan ya magamba, imenidhihirishia bayana kuwa mapacha watu RACHEL ni moto wa kuotea mbali, siyo mchezo. Kumbe Nnape anachofanya ni longolongo tu!
 
...8.Kubatilisha azimio la NEC la kuwatimua toka chama cha magamba.HONGERA MH. RAIS KWA USHINDI WA KISHINDO.WEWE NDIYE CCM BANA HAO KINA MKAMA NA NAPE NI VIKARAGOSI TU MBELE YAKO
 
Mie naogopa maana asiyeshindwa na jambo ni mtu hatari sana!!!!!!!! Osama alikuwa hatari kwelikweli lakini hatimaye amelala doro; sasa huyu naona ni noma!!!!!!!!!!!!!!
 
it is a very unfortunate situation...lakini ndo hapo Bongo yetu tulipoifikisha...the guy is screwing all of us! mbaya zaidi, hili tunalijua na hatuna cha kumfanya ... hilo ndo linaloniuma kuliko vyote
 
Umia peke yako sisi wengine hatutishi kwa lolote zaidi sana he will come to a shameful end and this is to happen not far from now!
 
Aliyemzawadia Rostam Bil 94 ni yule aliyetaka mkataba uvunjwe!!!!!!!!!! Can anybody remind me who that was again?
 
Pokea hongera zangu mheshimiwa rais kwa kufanya haya yafuatayo kwa ufanisi mkubwa.

1. Umepigana kufa na kupona na kuhakikisha Dr. Slaa hasikii harufu ya ikulu.
2. Hukulala usiku na mchana hadi ulipohakikisha Jakaya anaingia ikulu.
3. Umetumia kila linalowezekana kuhakikisha Sitta haukwai uspika.
4. Umepandikiza spika wako umpendae mama Makinda.
5. Umetumia hila za ajabu kuua upinzani rasmi bungeni - japo hujafanikiwa sana.
6. Umesaidia rafiki na wapambe wako kushika kamati nyeti za bunge.
7. Unajipanga kumsafishia njia swahiba wako Lowassa agombee 2015.

Kazi uliyofanya ni kubwa, tunakuzawadia kifuta jasho shilingi bilioni 94!

Big up Mr. Tanganyika!

Hii imekaa vizuri sana sina shaka wadau huyu jamaa ametafakuli nakutafakali na kutoa nondo nzito lenye tani 10. Sina shaka ndio maana hawa jamaa kufukuzwa chichim ni ngumu ndio maana wamepewa siku 90 kama viini macho ya kuwatoa RA, Viji-cent, na Lo.
 
Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko ccm -magamba kuwatosa magamba wenzao
nape, chiligati, na mkulu siku ile walitoka kwa mbwembwe sasa wananywea wenyewe hivi hawakujua kwamba mapacha watatu ndio walioshikiria ccm na ndio wanoendesha serikali ya kimtandao? Tofauti na chadema na slaa hakuna mtu mwingine mwenye ubavu wa kumtosa chenge anajua madudu mengi ten years as ag. Tofauti na chadema na slaa dr wa ukweli hakuna mwingine anaweza kumtosa mzee wmenye mvi amekamata kila kona ya ccm watavua wapi waache wapi? Amekamata hadi spika -kila konaaaaaaa ni mjanja huyu isipokuwa kwa chadema tu na dr slaa ndio maana alisema ccm iangalie sana arusha, tofauti na chadema na dr slaa nani anaweza kumnyoshea roast ni gwiji la magamba anajua kila kila kona akiguswa tu anafungulia -nape ajifunze sasa ataanza kuchukua chake mapema na kuanza kuwapamba. Kifo cha ccm hicho mbele pachungu nyuma pachungu waende wapi??????? Let them dissolve the party.
 
Mapacha watatu ni noumer hv JK km amirijesh mkuu si awapoteze tuu kama nyerere alivyowapoteza kina prof babu na kambona na tuntemeke sanga mi sielewi Kwnn asitumie nguvu aliyonayo bora lawama kuliko fedheha wanayompa hadi usawa huu
 
Kilio cha watanzania kitashinda tu ondoa shaka kwa hilo.....

Siyo lowasa wala ccm watakaoshinda 2015...

Huyu rostam miaka 30 jela inamngojea tuu wewe subiri serikali makini iingie madarakani...
 
Mapacha watatu ni noumer hv JK km amirijesh mkuu si awapoteze tuu kama nyerere alivyowapoteza kina prof babu na kambona na tuntemeke sanga mi sielewi Kwnn asitumie nguvu aliyonayo bora lawama kuliko fedheha wanayompa hadi usawa huu

hana uwezo!
 
Naomba wanachama wa jf mjiandae kurudi kwenye asili zenu,ili mtoe elimu ya uelewa kwa wazee na wadogo zetu walioko huko,ili nao wabadilike na tufanikishe mapinduzi ya kifikra, tusikae town tukipiga soga na kukosoana sisi kwa sisi, ili hali wote tunaelimu ya kuelewa.
Kunywa juice kwa mrija town,wakati wazee wetu na wadogo zetu hawaelewi kesho yao ikoje, ni dhambi kubwa, naomba jiandae ufike kwenu uwafunde kwa hili.
Jamii ikiangamia chini ya uwepo wako, ni dhambi kubwa. Grayson, 2011.
 
Rostam siyo tatizo, tatizo ni vibaraka na mbwa wake wanaomlinda. Ukiweza kuwamaliza hao vibaraka na mbwa wake hafurukuti!
 
Naomba wanachama wa jf mjiandae kurudi kwenye asili zenu,ili mtoe elimu ya uelewa kwa wazee na wadogo zetu walioko huko,ili nao wabadilike na tufanikishe mapinduzi ya kifikra, tusikae town tukipiga soga na kukosoana sisi kwa sisi, ili hali wote tunaelimu ya kuelewa.
Kunywa juice kwa mrija town,wakati wazee wetu na wadogo zetu hawaelewi kesho yao ikoje, ni dhambi kubwa, naomba jiandae ufike kwenu uwafunde kwa hili.
Jamii ikiangamia chini ya uwepo wako, ni dhambi kubwa. Grayson, 2011.

hii imenigusa sana,tatzo ni pale kwa bibi anayezani ccm hii ndo ile ya Nyerere,zungukeni kule kwa bibi watofautishie ccm ya Nyerere na hii ambayo iko chini ya lebo ya Rachel.tusiishie apo wape tumaini jipya,pipoooz power!.asanten
 
Me nnaona nchi ilishauzwa Ila Watz wa hali ya chini bado tu hatujapatwa mgao
 
Hii ni nzuri, lakini sasa hivi(kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari) maamuzi ya kumfukuza Rostam yanaelekea kuwatokea puani wakubwa wapya wa CCM. Hebu tuvute subira time will tell.nami nakuunga mkono kwa kutoa hongera hizo.
 
Back
Top Bottom