Hongera mheshimiwa Jakaya Kikwete kwa uamuzi mgumu, sasa wapinzani hawana cha kuongea!

nipende kuuangana na watanzania wenzangu kukupongeza kwa uamuzi mgumu uliouchukua wa kusafisha chama cha mapinduzi,kwa mtu yoyote aliyekomaa kisiasa na mwenye busara hawezi kushindwa kutoa pongezi zake kwani ni viongozi wachache sana katika dunia hii wanaoweza kusafisha chama tena kwa kuondoa viongozi wa juu kabisa,hili liwe fundisho kwa wapinzani hapa nchini kwamba mabadiliko ndani ya chama yanawezekana ikiwa tuu watatumia busara.
sisi vijana wako tuko pamoja katika ujenzi wa nchi hii,Mungu akubariki na akulinde siku zote.

Uamuzi mgumu ni kutaifisha mali yote ya kifisadi na kuwasweka wahusika lupango. Jifunzeni kwa hayati mwalimu na uhujumu uchumi. Kweli wa-tz ni wavivu wa kufikiri.
 
Mimi kati ya kifo na CCM mimi nitachaguwa kifo. kama kuoga ni usafi taulo lisingechafuka, CCM ni ile ile, ni chama ambacho kiu yake ni kushinda uchaguzi tu basi, hakipo kwaajili ya kuwaletea watanzania maendeleo. mpaka leo ahadi ya kikwete aliyotimiza ni baadhi ya vibajaj tu na sio vyote, kwahiyo mtu makini kama mimi huwezi kunitoa kwenye mambo ya msingi ukanieleza habari za gamba, hizo ni information za kushare na watu wajinga na sio mimi.
Mkuu Saigon huwa unanivunja mbavu kwa kicheko pindi nionapo majibu yako kwa watu kama hawa akina Kashaga....hakika unawaweza sana!
 
nipende kuuangana na watanzania wenzangu kukupongeza kwa uamuzi mgumu uliouchukua wa kusafisha chama cha mapinduzi,kwa mtu yoyote aliyekomaa kisiasa na mwenye busara hawezi kushindwa kutoa pongezi zake kwani ni viongozi wachache sana katika dunia hii wanaoweza kusafisha chama tena kwa kuondoa viongozi wa juu kabisa,hili liwe fundisho kwa wapinzani hapa nchini kwamba mabadiliko ndani ya chama yanawezekana ikiwa tuu watatumia busara.
sisi vijana wako tuko pamoja katika ujenzi wa nchi hii,Mungu akubariki na akulinde siku zote.

Hakuna maanuzi yoyote magumu yaliyofanywa , wakina makamba waliomba kujiudhuru wao wenyewe ,ingekuwa yeye ndiyo kawafukuza tungesema kafanya maamuzi magumu,

sijui ni maamuzi gani magumu unayosifia ????
maamuzi ya kuvua gamba na kuvaa manyoya? we kweli kilaza

tunataka afanye maamuzi yafuatayo
Atumbie kagoda ni akina nani?
IPTL, Rich mond, meremeta, busyagi n.k

pia atuambie Rz1 anapata wapi pesa za kununua majumba.
maamuzi magumu unayajua wewe? ebo
 
CCM haitakiwa kufanyiwa madiliko ya mwili(physical change) inahitajika kufanya mabadiliko yanayofanana na mabadiliko ya kikemikali (chemical change) kwa sababu kulinganihwa na kujivua gamba ni kwamba wanahitaji kutoa uzee wa ngozi ndani ya miili yao hivi uzee wa ngozi ndani ya chama chao ni tatitizo kwa watanzania au ufisadi? hivi alitumia neno magamba kwa kuogopa kuingia kwenye mtego wa kutumia neno ufisadi? ingawa kivitendo chama chake kinatumia neno mafisadi, wenzetu wanaelemewa na matatizo makuu matatu moja ni kukwepa dunia ya wasema kweli eti kwa sababu uwazi unakijeruhi chama pili wenzetu wanafikiri pesa ni kila kitu sisi cdm tunasema utu kwanza na tatu ni kujiweka katika ushindani wa kutumia fursa ya wingi kuwa ndio busara, hata pale wanapogundua kuwa wingi wao hasa katika bunge ni mzigo kwa umma kwa sababu wakati wote wengi wao wanalikizo ya kutofikiri, kaeni mkao wa kupiga kamera muone hoja ya kupongezana kuvua gamba mkiani itakavyopamba moto lakini tunaweza kumpongeza JK kwa sababu ya uungwana wa kukubali kushindwa na kupokea ilani ya cdm aitekeleze kwa ahadi zake hazina suluhu kwa matatizo ya kijamii na kiuchumi ya watanzania
 
JK ni zumbukuku anaendeshwa na rimoti kila mtu anaweza kubonyeza anavyotaka. Sijawahi ona kikwete amèfanya uamuzi mgumu peke yake bila shinikizo. Kujiuzulu el alishinikizwa, kupunguza baraza la mawaziri shinikizo, kuwapanga akina sitta, mwakyembe, na magufuli ni shinikizo. He cant concentrate coz anasikiliza sauti kibao zinamjia mpaka anapoteza concentration. Tunamlinganisha na mgönjwa wa akili anaposikia sauti zikimwita, nyingine zinamtishia, nyingine zinasema aue, nyingine zinasema akimbie mwisho wa siku anabaki kaduwaa au anamute. Ndicho ambacho anakifanya either afanye kutimiza sauti inayosikika sana au anauchuna kila mmoja aongee anavyotaka. Jk hana jipya na wala hastahili kupongezwa ila wapongezwe wananchi, na Cdm walioinitiate ishu ya ufisadi. Huwa natamani nitende tukio ili nimshuti na bastola jk kwan sitaman hata kumwona. Lakin any way Mungu anisamehe wacha amalize na atuachie katba nzuri.
 
Kwa hakika JK anastahili pongezi za kila anayeamini "Bila CCM imara (chama dola), Nchi inakwenda mrama". Kwa hatua iliyofikiwa, tumpongeze ila tusiichie hapo. Tumwongezee msukumo kuona azimio la kuwaondoa mafisadi katika nyadhifa zao ndani ya chama linatimia katika muda uliowekwa. Ikitokea ukaidi wowote au mabadiliko yoyote kuwabakiza hao mafisadi; anguko la imani inayoanza kurejea kwa ccm na M/Kiti wake litakuwa kubwa zaidi kuliko ilivyo sasa. Na ukaidi huo unaweza kupelekea misuguano ndani ya chama kuwa ya Ki-Mafia zaidi kiasi cha hata kumwondoa M/Kiti kwa stahili ya AKUANZAE, MMALIZE!

Naomba fisadi aliyetolewa CCM......usiwe unaongea tu...
 
Ccm ndo inakufa kifo cha mende hivyo..miguu juu...miaka hamsini wameshindwa kuinua hali ya maisha ya mtanzania wa kawaida wanakalia kujinufaisha wao tu na familia zao kwa kusaini mikataba feki na kupata ten percent...wanafail kusoma alama za nyakati na kuchange strategy za kuinua uchumi hasa zama hizi za globalization wategemee anguko la maana. ..hivi kwel mimi na akili zangu nisupport chama failure ka ccm...
 
UFISADI UPO NDANI YA KILA SEHEMU KTK CCM KUJIVUA GAMBA KWA CC NI KM TONE LA SUKARI BAHARINI go chadema.co.tz and find list of shame wapo kumi.
 
mi nahisi wewe hujielewi na hutufai jamii forums, cz una danganywa kama watanzania wa karne zilizopita, cz ccm inavunja kamati kuu eti inatoa mafisadi wakati mafisadi haohao wapo nec na ndio inayo chagua kamati kuuu,
 
Hivi huyu mtoa mada anaishi hapa Tanzania kweli!?,gamba lipi au maamuzi yapi magumu aliyoyacchukua Jk!?,au UMETUMWA!?,kawaambie waliokutuma kuwa sie tupo macho.Hivi ulitumia muda kufikiri juu ya ulichokiandika!?,hautufai JF labda ingekua enzi zileee!!!!.
 
Kutumia gharama kwa ajili ya maziko, ilhali haikutumika wakati wa kuuguza sioni maana yake.
Jk anachofanya ni mbinu ya kukiokoa chama na si watanzania. Kupongeza jambo hilo lazima uwe na maslahi binafsi na ccm.
 
Hii ndio kazi ya wenye akili nyingi. Ngoja uone ccm yenu itakavyosambaratika kwa kivuli cha gamba. Wamecheza ngoma ya cdm bila kujua. Pipo
 
napita tu jamani ila sioni sababu ya kumpongeza raisi asiyejua wamiliki wa dowans kampuni tata nchini...
 
nipende kuuangana na watanzania wenzangu kukupongeza kwa uamuzi mgumu uliouchukua wa kusafisha chama cha mapinduzi,kwa mtu yoyote aliyekomaa kisiasa na mwenye busara hawezi kushindwa kutoa pongezi zake kwani ni viongozi wachache sana katika dunia hii wanaoweza kusafisha chama tena kwa kuondoa viongozi wa juu kabisa,hili liwe fundisho kwa wapinzani hapa nchini kwamba mabadiliko ndani ya chama yanawezekana ikiwa tuu watatumia busara.
sisi vijana wako tuko pamoja katika ujenzi wa nchi hii,Mungu akubariki na akulinde siku zote.

Uamuzi gani mgumu hapo kubadilisha sura za viongozi ndio ugumu? Uamuzi mgumu ungekuwa kwa Kikwete mwenyewe kujiuzuru kwasababu kama CC, NEC na sekretariet ya chama vimeshindwa kazi maana yake mwenyekiti ndio ameshindwa kazi. Pia yeye ndio fisadi nambari 1 kwahiyo angejiuzuru pia kwa hilo tungemuona muungwana na jasiri na kwamba amechukua uamuzi mgumu. Kashfa zote za akina RA, EL na AC Kikwete anahusika. Kama ni kujivua gamba yeye ndio angevuliwa kwanza sio kuleta usani sani tu! Na nyie mnajifanya kumpongeza mnajipendekeza sijui ndio kutaka U-DC au U-RC!!
 
Mkuu hivi kile kidude cha groan mnacho tu nyie premium members eeh? Nakitafuta ile mbaya! Hawa jamaa si ndo wamerudi kutoka dodoma...kila mara ushuzi tuu...watu tusitulie jamvini jamanii!

Wakuu wamekiondoa hiki ni cha kubumba tu hata we unaweza kukiweka ni kuandika tu na kupost kile natural jamaa walilalamika na mods wakakitoa!
 
Kashaga mambo vipi? utaukabali tu mziki wa CDM leo hii unapongeza JK kwa kuvua gamba kwa hiyo unakuri ndani ya ccm kuna mafisadi na viongozi wasio waadilifu au wenye uwezo mdogo katika utendaji wao.
umechoka kutumia ile baiskeli yako unajikomba ili JK akupe vx
 
Back
Top Bottom