Hongera mh Kigwangala kwa kuipinga CCM Nzega!

Zyansiku

Member
Jul 27, 2009
49
10
Mbunge wa jimbo la Nzega Mh Kigwangala ameonyesha ukomavu wa kisiasa, moyo wa kujiamini na kujitambua kama Mwakilishi wa wananchi na siyo mwakilishi wa chama chake kwa maana ya CCM!

Mh Kigwangala ameandaa maandamano makubwa ya amani kwa kuwashirikisha wananchi wote wapenda maendeleo aidha maandamano haya yameahidiwa kufanyika siku japo amekuwa akipata upinzani mkali toka kwa ccm kwa sababu ccm isingependa kumuona Mbunge wake akiandaa maandamano ya kupinga jambo ambalo linasimamiwa na serikali iliyopo madarakani kwa maana ya ccm yenyewe.

Mh kigwangala baada ya kutangaza kuandaa maandamano hayo amepata upinzani mkali kutoka kwa uongozi wa ccm wa wilaya yake juu ya kuyazuia maandamano hayo hali iliyofikia kumita Mh Kigwangala kwenye kikao cha kamati ya Maadili ya ccm kitu ambacho Mh Mbunge aliona kuwa hatendewi haki na kugoma kutokea mbele ya kamati hiyo.

Katibu wa ccm wilaya ya nzega baada ya kuona kuwa amedharauliwa akaamua kumuandikia Mh Mbunge barua ya kumzuia kufanya maandamano hayo barua ambayo baadae imeonekana kwenye mtandao wa kijamii wa facebook unaotumiwa na Mh Kigwangala japo hadi dakika ya mwisho Mh Mbunge amesisitiza kufanya maandamano hayo.

Nimeamua kumpongeza Mh kigwangala kwa maamuzi yake hayo ili kuwafundisha wabunge wengine wote wanapaswa kuwajibika kwa wapiga kura wao na si kwa chama kilichowapeleka Bungeni na hapa naanza kupata ladha ya kuwa na wagombea binafsi kwani inamfanya mchaguliwa kuwajibika zaidi kwa wananchi na si kwa chama cha siasa, kigwangala kaonyesha njia nadhani na wabunge wengine watafuata wachache walionyesha njia safi ya uwajibikaji kwa wananchi ni pamoja na Mh Fulikunjombe, kangi Lugola na wengineo.

Kwa mara nyingine tena hongera sana Mh Kigwangala kwa kuipinga CCM kwa maslahi wana Nzeoga wakiwemo wana CCM wanaokuzuia kufanya maandamano hayo.

Ifuatayo na nakala ya barua aliyoandikiwa Mh kigwangala inayopatikana kwenye mtandao wa Mh Kigwangala.

attachment.php

attachment.php
 
Huyu hatakiwi kupewa misifa. Huo ni utovu wa nidhamu kwenda kinyume na matakwa ya chama. Nakushangaa leo Kigwangwala unamsifia WAKATI Shibuda unamkandia
 
Saini ya kutokuwa na imani na pinda ni mtihani tosha.
Je alithubutu kutia saini?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
namtakia yote mema amaliza ungwe hii salama, kwasababu nina uhakika hatakuja achaguliwe tena kuwa mbunge wa nzega...
 
Ameshasoma alama za nyakati. Ameona mpaka 2015 CCM inaweza ikawa imebaki jina tu kwa jinsi wanavyoendelea kupukutika. Ule woga unaelekea kumwisha maana kwa sasa ukigombea kwa tiketi ya Magamba uwezekano wa kushinda ni 20%. Vijana na walioelimika wameongezeka na hawataki kabisa kusikia Magamba. Ndo maana akina Membe wameanza kuhasi mapema.
 
Ya kuchaguliwa tutakutana nayo 2015 na hapo ni kama nitaamua kugombea tena , Leo tunafanya kazi iliyo mbele yetu
mkuu mlifanikiwa kufanya maandamano ?? marar ya mwisho nilisikia kuwa mumeruhusiwa kuaandamana 1/2 km tu hadi uwanjani tupe up date japo kidogo tu

HONGERA SANA KWA USHUJAA UNAO ONYESHA
 
hakuna ushujaa hapo nikujisafisha tu.kenge ni kenge hawezi kuwa mamba
 
Ya kuchaguliwa tutakutana nayo 2015 na hapo ni kama nitaamua kugombea tena , Leo tunafanya kazi iliyo mbele yetu

wewe ni mnafiki tu, ulijua utapewa uwaziri ndiyo maana ukaongopa kuwa mmoja ya walio tia sahihi kumuondosha pinda..
 
Ameshasoma alama za nyakati. Ameona mpaka 2015 CCM inaweza ikawa imebaki jina tu kwa jinsi wanavyoendelea kupukutika. Ule woga unaelekea kumwisha maana kwa sasa ukigombea kwa tiketi ya Magamba uwezekano wa kushinda ni 20%. Vijana na walioelimika wameongezeka na hawataki kabisa kusikia Magamba. Ndo maana akina Membe wameanza kuhasi mapema.

...watu km hawa hatuwataki cdm watatuletea matatizo
 
Mbunge wa jimbo la Nzega Mh Kigwangala ameonyesha ukomavu wa kisiasa, moyo wa kujiamini na kujitambua kama Mwakilishi wa wananchi na siyo mwakilishi wa chama chake kwa maana ya CCM!

Mh Kigwangala ameandaa maandamano makubwa ya amani kwa kuwashirikisha wananchi wote wapenda maendeleo aidha maandamano haya yameahidiwa kufanyika siku japo amekuwa akipata upinzani mkali toka kwa ccm kwa sababu ccm isingependa kumuona Mbunge wake akiandaa maandamano ya kupinga jambo ambalo linasimamiwa na serikali iliyopo madarakani kwa maana ya ccm yenyewe.

Mh kigwangala baada ya kutangaza kuandaa maandamano hayo amepata upinzani mkali kutoka kwa uongozi wa ccm wa wilaya yake juu ya kuyazuia maandamano hayo hali iliyofikia kumita Mh Kigwangala kwenye kikao cha kamati ya Maadili ya ccm kitu ambacho Mh Mbunge aliona kuwa hatendewi haki na kugoma kutokea mbele ya kamati hiyo.

Katibu wa ccm wilaya ya nzega baada ya kuona kuwa amedharauliwa akaamua kumuandikia Mh Mbunge barua ya kumzuia kufanya maandamano hayo barua ambayo baadae imeonekana kwenye mtandao wa kijamii wa facebook unaotumiwa na Mh Kigwangala japo hadi dakika ya mwisho Mh Mbunge amesisitiza kufanya maandamano hayo.

Nimeamua kumpongeza Mh kigwangala kwa maamuzi yake hayo ili kuwafundisha wabunge wengine wote wanapaswa kuwajibika kwa wapiga kura wao na si kwa chama kilichowapeleka Bungeni na hapa naanza kupata ladha ya kuwa na wagombea binafsi kwani inamfanya mchaguliwa kuwajibika zaidi kwa wananchi na si kwa chama cha siasa, kigwangala kaonyesha njia nadhani na wabunge wengine watafuata wachache walionyesha njia safi ya uwajibikaji kwa wananchi ni pamoja na Mh Fulikunjombe, kangi Lugola na wengineo.

Kwa mara nyingine tena hongera sana Mh Kigwangala kwa kuipinga CCM kwa maslahi wana Nzeoga wakiwemo wana CCM wanaokuzuia kufanya maandamano hayo.

Ifuatayo na nakala ya barua aliyoandikiwa Mh kigwangala inayopatikana kwenye mtandao wa Mh Kigwangala.

attachment.php

attachment.php

Mkuu Nzyansiku big up sana kwa thread iliyojitosheleza maana ukisoma huna haja ya maswali
 
Ya kuchaguliwa tutakutana nayo 2015 na hapo ni kama nitaamua kugombea tena , Leo tunafanya kazi iliyo mbele yetu

Angalau sasa mheshimiwa unaona wazi kwamba mipango ya kifisadi yenye lengo la kuwadhulumu wananchi wa nchi hii inasimamiwa kwa nguvu na Serikali ya chama chako! Vita hii unayopigana utapata mafanikio kidogo sana ukiwa ndani ya hilo dubwana linaloitwa ccm! Nakushauri tafakari kwa makini!
 
Back
Top Bottom