Hongera Maua Seminari kwa matokeo ya Kidato cha IV

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,619
2,567
[h=2]Napenda kuwapongeza wanafunzi na walimu wa Maua Seminari (Moshi) kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani yenu mwaka hadi mwaka. Mumekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa wanafunzi na walimu wanaopenda mafanikio katika masomo yao.

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

CSEE 2011 EXAMINATION RESULTS
[/h] [h=3]S0130 MAUA SEMINARY:
DIV-I = 15 DIV-II = 15 DIV-III = 2 DIV-IV = 0 FLD = 0


[/h]
 
Asante kwa kutupongeza,pale atuchezi ni kitabu kwa kwenda mbele:first::first::first::first::first::first:
 
Hongereni sana uchache wa wanafunzi na kuwachuja ipasavyo ndio imepelekea wafaulu vizuri...sio kama shule zetu za uswahilili wako 350 mpaka ubaini mwanafunzi hata notice haandiki au hafanyi homework inakuwa shughuli hongeren sana///
 
Kanda ya ziwa sijafurahia matokeo ya Makoko seminary, something must be done aiseee

CSEE 2011 EXAMINATION RESULTS

S0127 MAKOKO SEMINARY SECONDARY SCHOOL
DIV-I = 9 DIV-II = 22 DIV-III = 28 DIV-IV = 11 FLD = 0
 
Kanda ya ziwa sijafurahia matokeo ya Makoko seminary, something must be done aiseee

CSEE 2011 EXAMINATION RESULTS

S0127 MAKOKO SEMINARY SECONDARY SCHOOL
DIV-I = 9 DIV-II = 22 DIV-III = 28 DIV-IV = 11 FLD = 0

nenda kawafanyie maombi..
 
Hapana, siyo seminari zote zina excel good. Zile zenye uasilia wa santa ndo hufanya vizuri zaidi, lakini zile uasilia wa Al xxxx, El xxxxx mbado hazijatilia mkazo elimu dunia, zina mkazo wake zenyewe.
hongereni mno, ila shule za seminary do excel good in their exams.
 
Tunawapongeza sana,hope kina mkulima na rombic bdo wanakaza buti!kina machorongo,yle mzee wa kidampa, na mzee wa kachumbari (dereva) sina uhakika kma bdo wapo pale!!!long time!!!daaaah
 
Ehehehe waungwana miaka ya 1991 (tulikuwa wa kwanza Tanzania) pongezi kwa kudumisha kiwango. Wakati huo huku Rector Placidus Meir,Morata,kule Henk yah ndugu yangu, mbundu kwa pembeni na discount zake,pale mashambulizi ya wakulima na Rhombic,Egfrid na biology.etc. Usisome unajitaka? sina mfano. Big up
 
Isingekuwa vyema nikapita tu bila kuonyesha furaha yangu kwa kuwapongeza Maua. Sio idadi bali ni NIDHAMU YA SHULE HIZI ndio sababu ya matokeo mazuri. Shule zote zenye lembe la nidhamu mara nyingi zitafanya vizuri hata zile za serikali.

Nidhamu sio swala la mwanafunzi ni swala la uongozi mzima wa shule. Walimu wenyewe wawe na nidhamu, waipende kazi yao, wafuatilie wanafunzi na wawe na malengo na wanafunzi wao. Nidhamu sio kupenda sifa, sio kutafuta matokeo mazuri ili shule ionekana inangara! Kusudio liwe ni wanafunzi kuelewa sio kupasi mitihani.

Pale Maua, haya yanatendeka tena tokea enzi za zamani sana. Wakati ule mapadri walimu wa kizungu hawakusita kushindania muda wa wanafunzi katika masomo yao. Kila mwalimu alitaka mwanafunzi atumie muda mwingi inavyowezekana katika somo lake, na wale wanafunzi wasio na nafasi, wasiojali walikuwa kama maadui wa walimu hawa. Walitakiwa wakalima viazi maana hawakuwa na mwelekeo wa kusoma! Walifukuzwa! Ni bora kwa yule ambaye hana mwelekeo wa elimu ya juu, akaonyeshwa njia mapema atafute namna inayomfaa ya maisha kuliko kuwa naye hadi mwisho akaambulia zero ambayo humkatisha tamaa katika maisha.

Hongera Maua, Hongera Walimu wa Maua, NINYI NI MFANO WA KUIGWA! Makobe umenena
 
Hongereni sana uchache wa wanafunzi na kuwachuja ipasavyo ndio imepelekea wafaulu vizuri...sio kama shule zetu za uswahilili wako 350 mpaka ubaini mwanafunzi hata notice haandiki au hafanyi homework inakuwa shughuli hongeren sana///

Sio uchache ni uchaguzi wa nani anastahili kusoma pale. Kuna watu nakuhakikishia hata ungewafundisha wa5 tu darasani bado wangefeli.
 

Hii ni shule ya Seminary ya Kiislamu. Tazama somo la KIISLAMU, hakuna hata mmoja aliyepata C wote ni D na F.

Kuna D moja tu ya Maths, waliobaki F

Kwa matokeo haya, na ile mizozo inayoendelea Ndanda utakubaliana na mimi kuwa kuna watu Elimu sio nia yao ila wana mambo yao na ndio maana wengine wameamua kugomea mitihani.

Kama kamati za shule zitaipa mgongo Elimu na kuchaguliwa kwa misingi ya U'maalim hamna lolote litakalofanyika kwa mmiujiza hapa​





Ni ajabu sana shule ya Kiislam halafu wamefel soma la Kiislam..kweli maajabu hayaishi duniani. Hii ina maana hata wanachoabudu labda hawakijui! Very sad indeed.
 
Kwa huku Bongo, kuwa na seminari za Kiislamu parse ni kuandaa Janga la kitaifa...labda kwa nchi zingine inawezekana!
 
Ehehehe waungwana miaka ya 1991 (tulikuwa wa kwanza Tanzania) pongezi kwa kudumisha kiwango. Wakati huo huku Rector Placidus Meir,Morata,kule Henk yah ndugu yangu, mbundu kwa pembeni na discount zake,pale mashambulizi ya wakulima na Rhombic,Egfrid na biology.etc. Usisome unajitaka? sina mfano. Big up

Nilisoma pale 1982-1988. Tulikuwa na mambo kemkem. Msosisi safi kabisa lakini kazi lo! Asubuhi bustani kabla ya breakfast. Kisha breakfast halafu class. Saa nne mapumziko + chai. Mchana lunch. Saa 9 chai kisha kazi shambani. Saa 10 michezo kwa wote bila mtu kubaki bwenini. Saa 12 prep hadi saa 1 supper. Saa 2-4 study time. Kisha taa kuzimwa madarasani hadi asubuhi.

Tulijifunza mambo mengi sana: pamoja na masomo tulijifunza pia brick making, beekeeping, useremala, namna ya ku'oparate' machines kama hizi za Kilimo kwanza, kufuga kuku wa nyama na kuku wa mayai, grafting, music (kuimba + kusoma nota za music) kupiga kinanda, kodian, piano, flute, guitar etc), English debate nk. Kwa hiyo, ilikuwa ukihitimu masomo pale ulikuwa na uelewa mpana sana wa mambo.

Wakati ule Maua ilikuwa inachua mchepuo wa Kilimo na kila mwaka tulikuwa tunatoa sample ya mazao kupeleka wizarani kama mfano kwa shule zingine na pia tulikuwa tunajitegemea kwa chakula - tulikuwa tukizalisha wenyewe. Halafu wakati wa likizo mtu akiamua kubaki shuleni alikuwa akilipwa kwa kufanya kazi mbalimbali za usafi na bustani. Hivyo, ilisaidia kwa wale ambao walikuwa wana shida ya ada maana fedha tulizokuwa tukilipwa zilikuwa zinatosha pia kulipia ada ya shule na matumizi mengine. Je, utaratibu huu bado unaendelea? Sasa hivi nasikia kuna multipurpose hall ya kisasa, ambayo ni kubwa sana. Kwa kweli Maua is great!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom