Hongera Manispaa ya Kinondoni kwa daraja la Goba na Makongo

Sendeu

Member
Jun 29, 2009
59
2
Wadau pale panapostahili pongezi lazima tutoe na hii inakwenda kwa manispaa ya kinondoni kwa kuanza ujenzi wa daraja la mto mbezi la kuunganisha goba na makongo hongereni sana na tunaomba muimarishe barabara yote toka goba stend hadi makongo juu hadi survey ili hata daladala ziwe zinafanya route hiyo sisi wakazi wa goba hakika tumepata ukombozi asante sana
 
ni ccm wanajenga nini?nimeona uzinduzi wa ujenzi kijani tupu halafu hata mbunge hajahusishwa ili mwaka 2015 waseme ccm imejenga si halmashauri
 
Acha wajenge tu mkuu sisi ndo tutakaopima ila cha msingi tupate daraja bila kujali ccm au cdm yote heri tuuuu
 
Je panapitika hapo kwa gari kwa sasa? Huwa napita hapo kwa mishemishe zangu ila sijapita muda. Nilipaogopa palichimbika sana. Naombeni mnijuze wadau.
 
Je panapitika hapo kwa gari kwa sasa? Huwa napita hapo kwa mishemishe zangu ila sijapita muda. Nilipaogopa palichimbika sana. Naombeni mnijuze wadau.
<br />
<br />
Panapitika ndugu ila lazima uwe na gari ya juu sio saloon yenye 4wd vinginevyo kuna kamvua Kamenyesha pameharibika sana kaka
 
Hivi ni ccm ndio wanaotoa pesa za ujenzi au ni serikali? Ujenzi huo upo katika mpango wa sera ipi?
 
Hivi ni ccm ndio wanaotoa pesa za ujenzi au ni serikali? Ujenzi huo upo katika mpango wa sera ipi?

Hiyo ni kodi yetu wananchi na imerudi kutekeleza shughuli za maendeleo ya wananchi, magamba hawana cha kujivunia hapo kwani fedha haijatoka kwenye vitega uchumi vyao.
 
CCM wana childish politics wa nilivyoona jana wale madiwani na Mwenyekiti CCM wilaya nilicheka sana. Inaonyesha kweli CDM imewabana sana CCM maana matendo ya wana CCM hayaingii akilini kama yanafanywa na watu wazima n a wasomi--------------------aibu sana inaonyesha bado tunafanya siasa za ujima.

CCM hebu badilikeni fanyeni siasa za kisasa......mnatuangusha
 
Hiyo barabara ingekarabiwa ifike mivumoni kupitia goba - kulangwa na iende hadi madale na msakuzi.
 
Sasa wakuu hapo daraja linajengwa msifurahie sana,daraja litakapokamilika ukiwachunguza viongozi wa halmashauri wote utawaona wamejenga magorofa na kununua magari ya kifahari kwa hiyo project moja ya kujenga hilo daraja,ulizia limegharimu shilingi ngapi ukiambiwa utazimia.gharama yake ni sawasawa na kujenga madaraja kama hayo matano marekani.Kwa hiyo unaposikia kuna mradi fulani wa maendeleo umeanzishwa usirukeruke sana ujue ni deal imepigwa ya maana.Kwa hiyo wakuu ulipowaona pale viongozi wa CCM usifikiri ni wajinga ni kuwa walikua wanasherekea ulaji,nyie mnafikiri walikua wananadi sera hakuna hiyo.
 
Back
Top Bottom