Elections 2010 Hongera Kikwete lkn kaul zako zitekelezwe kwa vitendo.

Jasho la Damu

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
956
120
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana ziara za kutembelea wizara mbalimbali zinazofanywa na mhe rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Nitakuwa mnafiki,mzandiki na mpinga maendeleo endapo nitachelea kumpa hongera mhe JK juu ya hoja na makosa anayotoa karibu katika kila wizara anayotembelea kasoro wizara ya kilimo chakula na ushirika hapa hakuniteka hisia zangu hata kidogo.

Mhe rais JK alinifurahisha zaidi alipoweza kuwakosoa mawaziri wa wizara za miundombinu, mifugo na uvuvi na maendeleo ya jamii. Ukiwa mwepesi w
 
1. Bandiko lako linaonyesha linaendelea, lakini kwa vile unaposti na simu ya mchina, imekata baadhi ya Maandishi na maudhui!

2.Kama unampongeza JK kwa hatua ya kuwakosoa Mawaziri, basi ungekuwa wa maana kwa kuanza na cdm, ambao ndio chanzo na chachu kuu ya JK kutembelea mawizara!

3.Kama ukosoaji ule wa Waziri wa Miundombinu unauona unafaa, basi wewe ni mfaidika wa mfumo Nyonyaji uliopo sasa.
 
Inaendelea

Ukiwa mwepesi wa kufikiri huwez kuhoji jinsi bwana magufuli alipokuwa anajinasibu kwamba wizara yake inapeleka kila mkataba wa ujenz wa miundo mbinu kwa CAG ili kupunguza ubadhirifu lkn mhe Rais JK alionyesha ukomavu kwa kuhoji je CAG anakagua VITABU VYA PAYMENT VOUCHER au VALUE OF MONEY ILIYOTUMIKA? je endapo malipo yote yakawa yamelipwa kama inavyotakiwa na ujenz haujafanyika CAG ataweza kugundua hilo.
Hakuishia hapo aliwataka pia wizara kuunda INSPECTORATE TEAM
 
Hakuna la kumpongeza, maana aliwahi kutembelea kabla na kutoa maagizo ambayo hayakutekelezwa, na haya hayatatekelezwa maana watendaji ni walewale!
 
ACHENI JAKAYA KIKWETE AISHI KWENYE MABAWA YA MIDEGE ANGANI AKICHAGUA ILMRADI GHARAMA YA KODI ZETU KUIFADHILI MIRADI HIYO HAIZIDI ROBO YA TIJA TUNAYOVUNA KWENYE MAPENZI YAKE HAYO!!!

Hivi PakaJimmy, huenda huyu mwenye bandiko lake akawa ni Rweyemamu wa Ikulu kule Magogoni, Katibu Mwenezi na Propaganda CCM au ndio tuseme Zilipendwa Mzee Tyson Wassira Waziri wa Uhusiano leo hii kaamua kutoka Ki-Doti-Komu vile nini??

Tathmini ya huu Mradi wa ziara ya Mhe Kikwete Mi-Wizarani kamwe haitofanywa na akili za kilabuni hivi; tutakwenda mbele kidogo na kutaka ripoti iliyoandaliwa baada ya kutumia vigezo vya kisayansi (Project Monitoring and Evalution) ili kubaini kwamba tangu anapanga ziara hii.

Ni sharti JK atujibu kwa mtaji wa kodi zetu anazoendelea kutumia hivi sasa katika 'Kikwete Tembelea Wizara Project' (KTWP) na wal si kutupigia kelele za kishabiki hapa; huko kwenye siasa za kishabiki Vijana hatumo bali ni kwamba TIJA tu ndio tuwekewe mezani kweupe. Washiriki wa KTWP watujibu maswali kama vile Kikwete: (1) alikua na makusudio yepi, (2) kakuta hali halisi ikoje, (3) hali hiyo inajilinganisha vipi na kipinda cha mara ya mwisho mradi kama huo ulipotendeka, (4) Wa-Tanzania tumelazimika kuwekeza kiasi gani katika hiyo Month-Long Kikwete Project na iko wapi thamani ya kodi zetu mle????

Dr Bila ripoti tunaomba tangu ziara na familia yako mbugani na kote huko mikoani. Wapinzani na wabunge wote kwa ujumla nanyi tutawabana sana juu ya jinsi gani Viongozi Waandamizi wanavyotumia kodi zetu na TIJA za wazi zinazopatikana kwenye kile watendalo tukilinganisha na gharama iliotumika. Tukizingatia nidhamu kama hii tangu ikulu hadi nyumba kumi mitaani kwetu basi wananchi tutaona ACCOUNTABILITY wa hali ya juu!! Huko nyuma JK ameripotiwa kuwa na ziara nyingi sana na hata wakati mwingine kudaiwa kuwakera walipa kodi.

Kwangu mimi sitojali ziara zake ni nyingi kiasi gani ba ni thamani ya tija iliyopatikana ukilinganisha na gharama tulizowekeza mle. Tena mimi nitamuunga mkono sana JK akiweza basi kila siku awepo tu kwenye pipa angani kila kukicha ilmradi UNPOLITICISED WATCHDOG POLITICAL GROUPS AND PARLIAMENT wanaturidhisha katika hili bila swali kubaki kichwani mwetu.

Tunasupibi ripoti bungeni juu ya matumizi kwenye mradi huu na vile vile kwenye hotuba ya mwisho wa mwezi akajikite katika TIJA zenye kugusika na kuonekana tulizozivuna kwenye KTWP. Hatutaki blaa blaa na longo longo nyingi za mwaka wa 47 ambayo ndio haswa imetunashisha kama taifa kwenye huu umasikini gundi mabegani.

Mhe Kikwete kama CEO wa Tanzania kwa sasa, kama angelikua anaongoza kampuni ya kibiashara lazima angelazimika kuridhisha Wajumbe wa Bodi (Wahe Wabunge, nchi wahisani na Asasi za Kiraia husika) na haswa wamiliki wa kampuni (sisi wananchi) juu ya kila atendalo na faida ya kuonekana bila siasa, kwa nini ishindikane kwa ngazi ya taifa endapo kweli hatukusudii kuja kupata misaaada to Rwanda au hata Kenya kutupa LIFTI KWENYE NDEGE YAO toka kwenye hatari Libya????
 
Inaendelea

Ili kufuatilia na kuchunguza wale wote wanaojenga ktk hifadhi ya barabara kuwakataza na kuwachukulia hatua mapema kabla hawawekeza kwa kiwango kikubwa na baadae kuwataka waondoke ndani ya masaa 48.

Pia mhe Rais amenifurahisha leo wakati anamhoji waziri wa mifugo na uvuvi khs mahali shamba la mifugo la KIZOTA na sehemu lilipo hapa ilionyesha wazi waziri mwenye dhamana hakuwai kufika wala halijui japo alilitaja mwenyewe kwenye taarifa.
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana ziara za kutembelea wizara mbalimbali zinazofanywa na mhe rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Nitakuwa mnafiki,mzandiki na mpinga maendeleo endapo nitachelea kumpa hongera mhe JK juu ya hoja na makosa anayotoa karibu katika kila wizara anayotembelea kasoro wizara ya kilimo chakula na ushirika hapa hakuniteka hisia zangu hata kidogo.

Mhe rais JK alinifurahisha zaidi alipoweza kuwakosoa mawaziri wa wizara za miundombinu, mifugo na uvuvi na maendeleo ya jamii. Ukiwa mwepesi w

Umenipotezea muda wangu kusoma uozo huu....alipoanza urais 2005 alitembelea hivyohivyo...Nadhani ndio alienda kuwafundisha kuiba vizuri nadhani unakumbuka uozo wa Richmond,madini nk...........sasa leo unasema unampongeza JK kwa lipi?
 
Maskin watanzania tumenyimwa uwezo wa kufikiri na tumepewa uwezo wa mawazo ya kitumwa. Kazi ya Upinzani si kila jambo kupinga bali kuifanya SERIKALI iwajibike kwa maslahi ya wananchi. CDM wamefanya mazuri tumewasifia leo kikwete akifanya zuri bado anaonekana kwa sura ile ile ya ubaya. Tusiwe wajinga SI KILA JAMBO ASEME DK SLAA AU CDM NDIO TULIKUBALI KWANI HATA CDM INAPENDA KUONA SERIKALI INAWAJIBIKA.
 
Tumekupata...
 
Hapo umenena mkuu. Mnyonge mnyongeni na haki mpeni. Kwa kweli amejitahidi sana na tumpe nafasi afanye yaliyo mema kwa waTZ.
 
Back
Top Bottom