Hongera Kikwete; Hongera CCM kwa mpango huu

Hiyo miundo yenyewe ipo jamani au ndo hii hii aliyokuja kimalizia kabisa mhindi? Tusije tukashuhudia maafa. Sidhani kama hiko kitu kipo na kinawezekana kwa sasa kama kawaida uchaguzi unakuja kwahiyo muda wa ahadi hewa na porojo ndo huu. Wameshindwa wa mabasi sembuse na train bwana? Hawa vijana wa bagamoyo wantaka kutufanya mazezeta sasa
 
Dailynews Reporter in Dodoma,
28th January 2010

TANZANIANS may soon witness trains moving as fast as 120 kilometres per hour as the government mulls introduction of fast moving locomotives in an effort to improve transport services.

Hebu niwahi Zero Pub pale kaunta tukajadili hili maana soon and very soon treni kutoka DAR - MZA inaondoka asubuhi saa kumi na mbili mpo ROCK CITY!

Nani ameturoga? wTF???????
 
Hata ile kauli mbiu ya uchaguzi huu ujao, "Kilimo Kwanza" ilipotangazwa rasmi nikaandika hapa ukumbini kwamba hii ni bora ibadilishwe na kuwa "Mafisadi Kwanza" na sikukosea kabisa maana sasa yale mapapa ya mafisadi Jeetu Patel na Yusuf Manji yanaugombea mradi huo ili wapate mkataba wa kuyaleta matrekta toka India na ugomvi wao umesababisha mradi "kukwama", Na mkuu wa nchi alisema nini kuhusu ugomvi huo wa mapapa wa mafisadi...."anasikitishwa sana na hali hiyo"

Hatujarogwa na yoyote bali ni kuwachagua viongozi ambao hawastahili kabisa kutuongoza na tunayarudia makosa hayo kila wakati. Mpaka hapo tutakapojifunza kwamba kuna haja ya kuchagua viongozi wenye sifa na mapenzi ya kweli na Tanzania na ambao wataweka mbele maslahi ya nchi yetu. Kauli kama hizi na ahadi za kisanii tutaendelea kuzisikia sana na kamwe hazitazaa matunda yoyote.
 
Wow interesting...way to go yaani!...na juzi kwenye speech ya Obama nilisikia anasema kuwa wanataka kuweka fast train kama zile za China huko Florida....

Hiyo project ya kiwkete italeta kazi nyingi sana,.....hope siyo maneno tuu zile ahadi hewa kuwaweka sawa wananchi ili aweze kuchaguliwa tena term ya pili....bali watafanya kweli....
 

Hivi ile project ya mabasi ya kasi Dar imeishia wapi??

Ukiendelea kuuliza most likely utaambiwa....Bado inafanyiwa feasibility study, pesa zimeisha ndiyo maana study haijamamilika, zilizotengea US 10ml hazikutosha kwa ajili ya feasibility study.
 
Kama kuna kitu kinanikera kwa wanasiasa ni lugha yao ya kusema yajao siku zote... ni wanasiasa wachache sana kama wapo wanaosema tumefanya, nimefanya... I have accomplished etc...

Lugha zao nyingi ni tunampango, tumeunda tume, kikosi kazi, tunajadili, tunafanya feasibility study, tunatafuta wafazili... blaaa blaaa blaaa....
 
Jibu mnalo acheni kulalamika .....fanyeni kweli kwenye chaguzi, msiirudishe madarakani CCM. Tuanze upya
 
Nadhani bado wanaandaa mpango wa kutafuta uwezekano wa kupata mkakati wa kuunda tume itakayochunguza uwezekano wa kuanzisha mradi huo kwa ufanisi mkubwa. Kabla mpango kabambe wa kutafuta uwezekano wa kupata pesa za kuuanzisha.

Baada ya maandalizi hayo kukamilika, ndipo mchakato wa kisera utakapoanza ili kuunda tume huru itakayotafuta mawazo ya wananchi kuhusu utaratibu utakaofaa wa kusimamia mradi huo.

Na baada ya hilo kukamilika ndipo mpango mwingine na mwingine utakapoanza

Fantastic!!!!
 
Hawa vijana wa Bagamoyo ni wasanii si watendaji ; ushirikina umewaharibu wanafikiri kila kitu ni tunguli hata kujenga reli!!
 
Hiyo ya 35kph haipo na ilipokuwepo ilikuwa ni mtambo wa vifo. Je hii ya kufikirika ya l20kph si itakuwa kiama chetu? Ok mwaka wa uchaguzi huu tutuambiwa mengi maana mshipa wa aibu hawana.tusubiri
 
Kawambwa kaniacha hoi. Kaacha uengineer kawa mwanasiasa kachara kwa miaka mitatu tu. Hana tofauti na Chemponda aliyeahidi kuunganisha Tanga na Chakechake kwa barabara ya lami.
 
Nafikiri hizi ahadi zisizo na mwisho ndio ingekuwa kazi rasmi ya vyama vya upinzani bungeni. Kwa maana kwamba kila mwanzo wa kikao cha bunge kungekuwa na rejea ya yote yaliyoahidiwa na yaliyofanyika mwaka uliyopita ili kuangalia kama mipango iliyopangwa mwaka uliopita imefanyika kulingana na time frame ya serikali.
 
Kama kuna kitu kinanikera kwa wanasiasa ni lugha yao ya kusema yajao siku zote... ni wanasiasa wachache sana kama wapo wanaosema tumefanya, nimefanya... I have accomplished etc...

Lugha zao nyingi ni tunampango, tumeunda tume, kikosi kazi, tunajadili, tunafanya feasibility study, tunatafuta wafazili... blaaa blaaa blaaa....

Kikwete hana cha kusema kuhusu nime... au tume....maana hakuna lolote lile alilofanikisha, labda aseme nimefanya usanii au tumefanya usanii hili tutamuelewa lakini vinginevyo hana jipya la kujifagilia.
 
kwa nini wasijenge Barabara za lami kwanza wakamaliza?investment ya kujeng HSR ni kubwa sana.
 
Jakaya alipokuwa London aliwaacha watanzania solemba na kwenda kuangalia mechi ya Spurs na ka timu gani sijui vile, hicho ndicho kilikuwa kipau mbele chake pamoja na kupewa uanachama wa kudumu na hicho kilabu, Aliahidi kurudi na mara aliporudi alianza na majigambo kwamba barabara kutoka Songea hadi Mwanza itakuwa ya lami kabla ya kipindi cha miaka mitano hakijaisha. Je ametimiza hilo? Vile vile aliahidi kurekebisha mikataba ya madini Je, amefika wapi?

Alipokubali wahindi kuchukua TRL na sasa iko taabani anataka tumuamini kwamba ataleta fast trains? Je anaweza kujisifia kitu gani tangu alipochukua madaraka kabla hajaanza hadithi za Pwagu na Pwaguzi? Je ni kiasi gani cha pesa ya walipa kodi anatapanya? Mbona hatujamsikia kukemea au kuwawajibisha wanaoshindwa katika nyadhifa zao?
 
izi ndio ahadi za prof jay kwenye wimbo wa ndio mzee, kawambwa anasahau kikwete juzi katutukanisha uko libya kwa kudai tz ni maskini sana kukarabati reli kwa bil.15 sasa uyo kawambwa anadhani lokomotive ( kichwa cha treni ) cha iyo treni ya kasi naweza kua sh ngapi? for your record huge engine za lokomotice ziko kwenye 5bil. ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya ......................


Prices vary greatly depending on type (AC or DC power); electronics; power distribution systems; the load rating; and with the number of locomotives purchased. A single AC locomotive with options can cost $2.3 million, while a large railroad recently purchased 200 'bare bones' units for $1.75 million each. Low-end AC units can be had for a little as $1.4 million. Modern locomotives are good for about a million miles before major overhaul. At this point they are often traded in on new ones, and the manufacturer will rebuild the old unit and sell it to a smaller railroad for about half of what a new one costs.
In addition to the purchase price, the average locomotive costs about $35,000 a year for fuel and preventative maintenance.


http://wiki.answers.com/Q/How_much_does_a_real_locomotive_cost

Kama sikosei, vichwa vya train na zile mashine za kufulia umeme, bei zake zinakwenda sawa. Hii inatokana na sababu kuwa Engine tunazohitaji sisi yaani za diesel, huwa si engine hasa kama gari ila generator ya umeme. Umeme ukizalishwa ndiyo unakwenda kuendesha motor zilizowekwa kwenye matairi tayari na faida yake ni hakuna energy kubwa kupotea kama kwenye magari. Hivyo basi mara nyingi huwa wanaweka Li-generator na baadaye kulijengea Body na matari na mwisho sehemu ya dereva na mchezo unakwisha. Hivyo bei ya engine za train na za kuzalisha umeme, bei inakuwa haipishani sana.

Ila huo utunzaji wake na jinsi linavyokunywa mafuta kwa kweli INATISHA.
 
Marehemu Shaaban Robert hakukosea alipozungumzia nchi ya KUSADIKIKA na KUFIKIRIKA ... kina Kawambwa & Company wanaishi kwenye nchi hiyo ya njozi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom