Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Dailynews Reporter in Dodoma,
28th January 2010
TANZANIANS may soon witness trains moving as fast as 120 kilometres per hour as the government mulls introduction of fast moving locomotives in an effort to improve transport services.
The Minister for Infrastructure Development, Dr Shukuru Kawambwa, told the National Assembly here that the trains would be travelling at 120 kilometres per hour, unlike the existing trains which travel at 35 kilometres per hour.
"Theres nowhere in the world where trains are now travelling at 35k/h and China has just introduced trains with 350k/h, commented Dr Kawambwa.
The minister explained that the government was planning to improve rail tracks by expanding gauge from 1000 metres (Ni 1000 mm) to standard gauge of 1435 metres (ni 1435 milimetres).
I refuse to comment!! hata mnishikie bastola!!
Mwanakijiji na wengine,
Nilikuwa nataka kuanzisha thread maalumu juu ya uwezekano wa kubadilisha reli ya kati upana wake. Ila kiuvivu kikanipitia na nikasahau.
Upana wa reli ya kati wa 1000 mm (1m) kwa kweli umepitwa na wakati na duniani, reli nyingi zinatumia sasa huo upana wa 1.435m. Sina uhakika sana wa Warusi kama wamebadilisha train zao zinazokwenda Western Europe ila zamani nasika walikuwa wakibadilishia matairi ya train na ndipo train linaondoka na kuanza safari kuingia German na linaporudi mchezo unakuwa huohuo.
Upana wa 1m kwa kweli unahasara nyingi sana. Train haliwi stable linapokwenda speed kubwa na hii inaweza kuwa hata inachangia sana kuleta ajali za mara kwa mara reli ya kati. Ila cha muhimu zaidi kwangu mie ni hiki nilitaka kuandika hapo mapema.
Nchi kama German, UK, Ufaransa, Sweden, Japan nk ni watu ambao huwa standard zao ziko juu sana. Hubadilisha mabehewa kabla hayajachakaa sana. Kama tungeliweza kuwa na karakana nzuri ya kuyafanyia matengenezo hayo mabehewa yao waliyoacha kuyatumia kutokana na wenzentu kuwa na speed kubwa sana zaidi hata ya hiyo 120km/hr basi tungelifaidika sana na hii kitu. Nafikiri hawa jamaa wangelitupatia au kutuuzia kwa bei nafuu sana sana. Usiogope ufisadi maana hata kwenye mapya wanaweza kufisadi.
Pia mashine za kutengenezea reli na hata kujenga zitakuwa nyingi sana ziko katika standard hiyo ya 1.345m kuliko hii ya kwetu ya 1m.
Mwisho nafikiri nchi nyingi na makampuni mengi ya jirani wameanza kulalamika kuwa kutumia magari kusafirisha mizigo yao inawacost sana. Hivyo wameanza lobbying ili reli ziwe zinatumika kusafirisha mizigo yao. Kulikuwa na makala moja nilisoma ila sikumbuki wapi wakiweka gharama za kusafirisha mizigo kutoka Kenya hadi Uganda kwa maroli, ilikuwa inatisha. Hivyo tutake au tusitake, Umoja wa Afrika Mashariki kwa hili nina imani watatusukuma ili reli ya kati irudi. Labda ndiyo maana hata mkataba na Wahindi wameuvunja.
Siwezi kufahamu Kawambwa anasema ukweli kiasi gani na PILAU LA UCHAGUZI nalo liko kiasi gani. Ila ukweli ni kwamba reli ya kati lazima tubadilishe UPANA WAKE kama kweli na sisi tunataka kuwa karne walau ya 20. Hayo ya matrain yanayokwenda mwendo wa 120kmphr siwezi amini hadi nione kwanza reli ya kati imelala ikiwa na 1.435m upana.
NB: Upana wa reli duniani angalia hapa >> [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Rail_gauge[/ame]