Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,728
- 2,259
Matukio ya wiki hii, hasa hili la CCM "kujivua Gamba" linastahili pongezi .
Kwa muda mrefu sasa waanzishi wa malumbano ndani na nje ya JF wamekuwa wakiifuatilia kwa makini sana muelekeo wa CCM kama chama tawala na JK akiwa mweyekiti wake.
Wengi wamelaumu ufisadi wa waziwazi uliofanyika baada ya JK na "mtandao" kuingia madarakani.
Wengi zaidi wamelaumu kushindwa kwa CCM kuchukua hatua kudhibiti ufisadi baada ya JK kuingia madarakani mwaka 2005.
Na wengine wengi zaidi wamemlaumu JK binafsi kwa kutowachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi.
Wapo walio hoji ukaribu wa JK na watuhumiwa hawa, hasa Edward Lowassa, Rostam Aziz na Chenge.
Mara nyingi JK amekuwa akiwapoza wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuwahukumu moja kwa moja watuhumiwa hawa wa ufisadi, na TAKUKURU pia imeshindwa kupata ushahidi juu ya hilo.
Wananchi hawakufanya ajizi, na hapa navipongeza vyama vya upinzani kwa elimu waliyoitoa kwa wananchi.
Ufisadi ni mbaya , ufisadi ni kuingiza umaskini katika nchi,ufisadi unahujumu uchumi wa nchi.
Tumeona mikataba inayoumiza nchi(Richmond na sekta ya madini), tumeona madeni yanayotokana na mikataba feki kama ya Dowans(94bil),tumeona ununuzi wa vifaa vibovu(radar).
Kwa ujumla wananchi wamejionea madhara ya ufisadi katika muda huu wa kipindi kisichozidi miaka 10.
Chama kilikuwa katika wakati mbovu pengine kuliko wakati wowote katika uhai wake kikiwa chini ya katibu Mkuu wake Makamba ambaye hakuwa na ubavu, upeo wala mbinu za kudhibiti ufisadi.
Kwa bahati mbaya sana wahusika wakuu ndio hao hao walioko katika ngazi za juu katika uongozi wa chama, na ni marafiki wa karibu wa mwenyekiti wa chama tawala CCM.
Kampeni na uchaguzi wa mwaka 2010 ni kama umekizindua chama kutoka katika usingizi mzito wa kufikiri kitatawala milele Tanzania.
Kupungua kwa kiwango kikubwa kwa watu wanao muunga mkono mkuu wa nchi kutoka 82% mwaka 2005 hadi 61% mwaka 2010 ni mstuko tosha kwa chama tawala.
Pongezi zangu kwa JK na CCM ni kuelewa maana ya mstuko huo na madhara yake kwa CCM.
Kitendo cha kudhibiti kundi lile la watu watatu(EL, RA na Mzee wa Vijisenti) si tu imeleta muamko mpya wa watu kuona kuwa chama hakijatekwa na mafisadi bali pia kuona kuwa chama bado kinawasikiliza wanachama wake na wananchi kwa ujumla.
Kwa staili ya kuwaengua hawa mafisadi katika nafasi za juu za chama, chama kimeonyesha uwezo mkubwa wa kujirekebisha-kitu ambacho vyama vingi vya upinzani haviwezi kukifanya kwa ufanisi.
Pongezi zangu kwa JK , CC na NEC yake kwa kuondoa kwa sasa mada za ufisadi zilizo wapa wapinzani nguvu ya kuishambulia CCM. Ni wazi kuwa wapinzani wa CCM sasa watachanganyikiwa kwa kukosa mada za kuwaunganisha.
Ilifika wakati mwana CCM wa kweli aliona aibu kusimama hadharani na kujitambulisha , kwa kuogopa kuzomewa!
Kukidumisha chama ni jambo la muhimu sana na tukumbuke kuwa hata Mao Tse Tung alihalalisha wanachama wake wa Communist Party kuishambulia Makao Makuu pale alipoona inaanza kutekwa na watu wachache wenye malengo yao binafsi.
Baada ya "kujivua gamba", pengine naweza kusema kuwa JK amejitengenezea uhalali wa kukumbukwa kwa kutoruhusu chama kutekwa myara na watu wenye malengo binafsi ya kujinuafaisha-kwa hili anastahili pongezi.
Kwa hili vile vile ameweka msimamo(precedence) ya kutambua kuwa chama kina wenyewe, nawenyewe ni wananchi na sio wafadhili.
Hongera CCM!