Elections 2010 Hongera ITV kujiondoa CCM

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Hongera ITV kujiondoa CCM
Ni wengi wetu walioona uzi nilioweka hapa JF uliokuwa na kichwa cha “tangu lini ITV ikawa CCM” ambapo ITV walikuwa wanarusha taarifa za habari za CCM pekee. Baada ya uzi huo na wanaJF wengi kuchangia, kumekuwa na mabadiliko makubwa mpaka sasa.
  1. kwanza habari zake zinacover karibia wagombea wote ambao wapo kwa nia ya kushindana
  2. Pili muda hautofautiani sana wakati habari zikirushwa.
  3. Inaonesha kuwa chombo hiki ni cha kijamii zaidi badala ya kuegemea chama fulani

Hii ni nzuri. Lakini angalieni.. Tembo akisifiwa …..
 
Haya ni mabadiliko mazuri kwa future ya Tanzania. I hope siku ya kutangaza matokeo watapeleka waandishi wao all over the country. TV za kenya zilipeleka (ziliajiri hata temps) watangazaji wao kila mahali wakati wa uchaguzi uliopita (wa kupitisha katiba) ili kuhakikisha kuwa michezo michafu haifanyiki.

Nategemea ITV na wengine wafanye the same mwaka huu.
 
Hongereni sana ITV. Cheers. Mmesikia maombi ya wadau.
 
AAAAh! hivyo ndivyo vigezo nyako kwa kituo cha tv au redio kukiainisha na chama fulani, hivyo saSA hivi ITV imejiunga na chadema,
StaR Tv wako chama gani, QUALITY tusaidie kujua??
 
Na pia nafikiri baada ya mafisadi kutaka kutupa tena karata ya kumhusisha Mengi na dawa za kulevya huku Jk akiendelea kuyasifia majimboni yanakogombea, Imemlazimu Mengi kufikiri mara mbili maana hajajua nia ya mkwere ndani ya chama chao ccm.
 
nadhani tumekosa kumbukumbu hivi mnakumbuka humu humu ndani ya jamvi mliwahi kulalamikia mkutano mmoja wa dk slaa coverage ilikuwa ya kinafiki kwa kutoonysha waliohudhuria na badala yake kumuonyesha mgombea pekee na baadaye kuisifia itv,je mnakumbuka coverage ya slaa kupokelewa kwao karatu ilirusha na itv tu ? kwa mimi ambaye naangalia itv kila siku si kweli itv imebadilika bali tangu kampeni zinaanza imekuwa ikitoa air time sawa kwa wagombea,jk yuko na mwandishi vedasto msungu na slaa yuko na ufoo salo huku lipumba akifanyiwa kazi na waandishi wao walioko mikoani,habari ndiyo hiyo
 
[QUOTE .......................... Hii ni nzuri. Lakini angalieni.. Tembo akisifiwa ….. [/SIZE][/FONT][/QUOTE] Mkuu usemi ueugeuza kichwa chini miguu juu. Kama nakumbuka vizuri unasema "Mgema akisifiwa Tembo ulitia maji".
 
Back
Top Bottom